June 2014

Na Happiness Katabazi

JAJI Shabani Lila wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, Aliyekuwa amepangwa kusikiliza rufaa iliyokuwa imekatwa na Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu , Sheikh Ponda Issa Ponda, amejitoa kusikiliza rufaa hiyo  kwa maelezo Kuwa Dhamira yake inamfanya ajione hawezi kusikiliza rufaa hiyo.

Jaji Lila alitoa uamuzi huo mwishoni mwa wiki ambapo alisema Dhamira yake haimtumi kusikiliza rufaa hiyo namba 89/2013 iliyokatwa na Mwomba rufaa (Ponda) dhidi ya jamhuri inayo omba Mahakama Kuu itengue hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya Mei 9 Mwaka 2013, ambayo ilimtia hatiani kwa kosa Moja la kuingia kwa jinai Katika Kiwanja Cha Chang'ombe Markaz ambapo ilimfunga Kifungo Cha Mwaka mmoja nje na kumtaka  awe mtunza Amani na raia mwema lakini Agosti Mwaka na alikamatwa na kufunguliwa Kesi ya uchochezi kwa Madai ametenda makosa ya uchochezi wakati Akiwa ndani ya Maandalizi ya hukumu hiyo.

"Kwa Dhamira yangu hainitumi kusikiliza rufaa ya Ponda, nimerudisha jarada la rufaa hii  kwa Jaji Mfawidhi ili aweze kumpanga  jaji mwingine wa kusikiliza .....na pia nimelikataa ombi la Wakili wa Ponda, Juma Nassor lilokuwa Linaomba Mahakama hii impange Jaji mmoja atayesikiliza rufaa hiyo ya Ponda na ombi lilonalooamba Mahakama hiyo itoe amri ya Kuzuia Kesi ya uchochezi iliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya Ponda  Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro isimame hadi rufaa iliyokatwa na Ponda Katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, itakaposikilizwa kuamriwa.

Ponda aliwasilisha mahakamani hapo ombi la Kuomba Mahakama hiyo itoe amri ya Kuzuia Kesi ya uchochezi inayomkabili Morogoro ,isiendelee kusikilizwa hadi pale rufaa yake aliyoikata mapema Mwaka Jana ya Kapinga hukumu iliyotolewa Na Mahakama ya Kisutu Mei 9 Mwaka Jana, ambayo ilimtia hatiani Kwa kosa la kuingia Kwa jinai Katika Kiwanja Cha Markas Chang' ombe, ambapo Mahakama hiyo ilimfunga Kifungo Cha nje Cha Mwaka mmoja, lakini Agosti Mwaka Jana, alifikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro akikabiliwa na Kesi mpya ya uchochezi na kutenda kosa wakati yupo chini ya uangalizi wa Kifungo Cha Mwaka mmoja nje.

Hata hivyo Wakili wa Ponda ,Nassor alimwambia waandishi wa Habari Kuwa licha Jaji Lilla alikataa ombi lake la kuomba Maombi mawili ya mteja wake yapangwe wa jaji mmoja lakini Jaji Mfawidhi ameyapanga Maombi hayo mawili ya Ponda yaani rufaa iliyokatwa na Ponda na ombi la kuomba Kesi ya Uchochezi inayomkabili mTeja wake mkoani Morogoro, yamepangwa kusikilizwa kwa jaji Mmoja aitwaye Lawrnce  Kaduri ombi la kuomba Kesi ya uchochezi iliyofunguliwa Morogoro dhidi ya Ponda itaanza kusikilizwa Agosti 4 mwaka huu na rufaa yake Ponda itakuja kutajwa tarehe hiyo hiyo.

Mapema Juni Mwaka huu, Wakili Mwandamizi wa serikali Bernad Kongora aliwasilisha pingamizi la awali mahakamani Linaomba Mahakama hiyo itupilie Mbali maombi  hayo ya Ponda yanayo omba Mahakama itoe amri ya usikilizwaji wa Kesi ya uchochezi iliyofunguliwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro ya simama hadi rufaa yake itakapoamriwa kwasababu ombi Hilo linalengo ya kuaribu muda wa Mahakama na halina Msingi.

Chanzo: Gazeti La Tanzania Daima la Jumatatu, Juni 30 Mwaka 2014.


Redio za jamii nchini zimeaswa kutumika vizuri katika kuelimisha kamii juu ya kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kupitia vipindi vya redio.
DSC_0125
Meneja wa kituo cha Sengerema FM Redio, Ndg. Felician Ncheye, akitoa nasaha za ukaribisho kwa washiriki wa mradi wa SHUGA na mgeni rasmi. Katikati ni Mgeni rasmi Mratibu wa UKIMWI halmashauri ya Sengerema mkoa wa Mwanza kupitia mradi wa TACAIDS, Ndg. Geofrey Mabu na Kulia ni Afisa Mipango VVU/UKIMWI  UNESCO, Ndg. Herman Mathias.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog)

Hamasa hiyo imetolewa na Ndg Geofrey Mabu ambaye ni mratibu wa UKIMWI halmashauri ya Sengerema mkoa wa Mwanza kupitia mradi wa TACAIDS wakati akifungua warsha ya siku tatu ya mradi mpya ujulikanao kama SHUGA, unaotekelezwa na shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana  Shirika la Mfuko wa Watoto (UNICEF) inayofanyika katika kituo cha Redio Jamii Sengerema mkoani Mwanza.
DSC_0129
Mgeni rasmi Mratibu wa UKIMWI halmashauri ya Sengerema mkoa wa Mwanza kupitia mradi wa TACAIDS, Ndg. Geofrey Mabu akifungua warsha ya siku tatu ya mradi mpya kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi mapya ya VVU ujulikanao kama SHUGA.

Mabu amesema kuwa mradi huo umekuja wakati muafaka ambapo malengo yake yakizingatiwa na kutekelezwa kama ilivyopangwa utasaidia kufikia malengo ya serikali ya kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI hadi Zero.





Amesema kuwa redio za jamii ni kiungo muhimu katika kuelimisha jamii na kuwa kama zitatumika vizuri kusambaza elimu ya UKIMWI kupitia vipindi vyake zitasaidia kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali kupitia TACAIDS.

Vile vile ameziomba redio zitakazoshiriki katika mradi huu, kutumia vizuri fursa hii waliyoipata kuhakikisha wanafanikisha malengo ya mradi kwa kiwango cha juu kwa kufanya hivyo pia watakuwa wamelinusuru taifa na janga hili la UKIMWI.

Awali Mkufunzi wa Radio za jamii kutoka shirika la UNESCO Bi Rose Mwalimu akitoa ufafanuzi wa malengo ya semina hiyo, amesema kuwa mradi huu wa SHUGA unalenga kupambana na maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI kwa vijana hapa nchini kupitia vipindi vya mchezo wa redio kubadili tabia.

Amezitaja redio 10 zinazoshiriki katika mradi huu nchini Tanzania kuwa ni FADECO Redio ya Karagwe mkoani Kagera, ORS ya Manyara, Sengerema FM mkoani Mwanza, Pangani FM ya mkoani Tanga na Kahama FM kutoka Shinyanga.  

Nyingine ni Kitulo FM ya Makete Njombe, Kyela FM ya Mbeya, Nuru FM kutoka Iringa, Pambazuko FM Ifakara na Kwanza Jamii Redio FM kutoka Njombe.


DSC_0069
Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu akitoa maelezo kuhusu madhumuni ya warsha inayohusisha mradi wa SHUGA


DSC_0269
Afisa Mipango VVU/UKIMWI  UNESCO, Ndg. Herman Mathias akitoa mada kuhusu VIjana, Balehe na Mahusiano ya Ngono wakati warsha ya siku tatu ya mradi mpya kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi mapya ya VVU ujulikanao kama SHUGA.



DSC_0103
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa umakini mada zilizokuwa zikitolewa na wakufunzi.



DSC_0238


DSC_0261
Mshiriki kutoka Kahama FM Redio, Makunga Peter akiuliza jambo kutoka kwa mkufunzi (hayuko pichani).



DSC_0192





DSC_0212
Picha juu na Chini ni Afisa Mipango VVU/UKIMWI kutoka UNICEF, Bi. Alice Ijumbe akitoa mada kuhusu kiwango cha Maambukizi ya VVU kwa Vijana na hali ya Afya ya Uzazi Salama wakati wa mafunzo hayo



DSC_0251
Mshiriki wa warsha ya siku tatu ya mradi mpya kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi mapya ya VVU ujulikanao kama SHUGA kutoka  Sengerema FM Redio, Peter Marlesa akijenga hoja kuhusu viashiria hatarishi vya maambukizi ya VVU kwa vijana


DSC_0279
Pichani juu na chini washiriki wa warsha ya siku tatu ya mradi wa SHUGA wakiwa katika vikundi kazi.



DSC_0289




DSC_0169
Mgeni rasmi Ndg Geofrey Mabu wa TACAIDS, wakufunzi wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya siku tatu ya mradi mpya kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi mapya ya VVU ujulikanao kama SHUGA.


chanzo cha habari na Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog



















































Diamond Platnumz mwanamuziki wa bongo fleva asiyeshikika sasa hivi akifanya show kali jijini Los Angeles, California siku ya Jumamosi Juni 28, 2014 ikiwa pia akijiandaa kwenye BET Awards 14 inayofanyika leo jijini humo.

Wimbo wake wa my number one aliyeshirikiana na Davido wa Nigeria umechaguliwa kwenye category ya international collaboration. 
Mgeni wa heshima alikuwa Mhe. Ahmed Issa ambaye ni Balozi wa Heshima wa Tanzania-California



Mashabiki wa Diamond kwenye showa ya Diamond Platnumz iliyofanyika Los Angeles, California nchini Marekan



Diamond Platnumz aka Rais wa Wasafi akifanya vitu vyake California.


Kushoto ni Balozi wa Heshima, Mhe. Ahmed Issa akiwasili ukumbini hapo akiongozana na wanajumuiya wa California.


Picha na: Abdul Majid, mwakilishi wa Vijimambo Los Angeles California. Kuona picha zaidi bofya hapa.


Source by www.wavuti.com














































































You can now learn at your own pace and at your own convenience using state of the art an online supportive learning system with the University of Cyprus.  With increasing tasks and responsibilities at work or in the family, it becomes a challenge to attend a full time classroom and so this solution is specially geared towards helping you.  

To add to this fabulous facility, you can complete your higher degrees at less than half the cost and still receive an internationally accredited qualification.  Move on in your career with better qualifications today, contact us in Dar es Salaam on 0716 921751 or 0755 276750 today.

MAHAKAMA Kuu Kanda Ya Dar es Salaam, leo itaanza kusikiliza kesi  iliyofunguliwa na wanachama wa tatu wa  Timu ya Soka ya Simba,  ambao wanakomba mahakama hiyo  itoe amri ya Muda  ya Kuzuia  kufanyika  kwa uchaguzi Mkuu wa Timu  hiyo ambao umepangwa  kufanyika Juni 29 Mwaka huu.
Akizungumza na Tanzania Daima Jana mchana, Wakili wa wanachama  Hao,  Revocatus Kuuli alisema  uongozi wa Mahakama umempatia Jaji Augustine Mwarija kuisikiliza na inaanza kusikilizwa kusikilizwa Leo.

Endapo Jaji Mwarija atasikiliza Kesi hii Na.291/2014  Kama ilivyopangwa, itakuwa ni Mara yake ya pili kusikiliza Kesi ya aina hiyo. Mara ya Kwanza ilikuwa ni Mei 8 Mwaka  2010 ambapo Jaji  Mwarija akiwa na wa Mahakama hiyo alitoa amri ya  kubatirisha amri ya muda ya kuzuia uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba uliofanyika Mei 9 mwaka 2010.

Amri ya kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa simba iliyotenguliwa na jaji huyo ilitolewa Mei 6 mwaka 2010 na aliyekuwa Hakimu Mkazi Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Amiceth Wambura ambapo Jaji Mwarija Alisema Amefikia uamuzi wa kutengua amri hiyo baada ya kubaini kuwepo Kwa dosari Katika amri ile ya Mahakama ya Kisutu.

Amri hiyo ilitolewa  saa 1:10 jioni na Jaji Agustine Mwarija baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili zilizokuwa zinavutana katika kesi iliyokuwa imefunguliwa na Michael Wambura dhidi ya mwenyekiti wa klabu ya Simba, wa wakati huo, Hassan Dalali, kuruhusu uchaguzi huo kuingiliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Juni 23 mwaka huu, wananchama Hao watatu kupitia Wakili wao Kuuli walifungua   mahakamani hapo Maombi hayo madogo, Na.291/2014  Josephat Waryoba, Said Lly Monero na Hassan Hassan, ambao wanamshitaki Rais wa Timu ya Simba, Ismail Aden Rage na Bodi ya Udhamini ya Timu  hiyo.

Kwa mujibu wa hati hiyo inayonyesha walalamikaji wana jumla ya Madai matatu ambayo dai la kwanza wakiomba Mahakama hiyo itoe amri ya kuwazuia wadaiwa kuitisha uchaguzi Mkuu uliofangwa kufanyika Juni 29 Mwaka huu.

Wakili Kuuli analitaja ombi la pili ni wanaomba jumla ya wanachama 66 waunganishwe Kwenye Kesi hiyo ili nao wawe walalamikaji dhidi ya wadaiwa   kwasababu wadaiwa ambao Rage na Bodi ya Wadhamini wamevunja   Katiba ya Simba , taratibu za uchaguzi na  na maadili ya uchaguzi , kadi za uanachama za wanachama hao zimearibiwa.

Wakili Kuuli alidai kuwa mdaiwa wa kwanza Kamati ya Utendaji ya Simba walishindwa kuweka sawa Kamati ya Maadili  ya simba  Kama inavyotakiwa  na Katiba ya Timu  hiyo na Kanuni za uchaguzi za TFF.

Alidai Kwa  vitendo hivyo wadaiwa hao  wamevunja taratibu  zote  za uchaguzi  na kwamba Hakuna Chombo Cha klabu ya Simba  ambacho kimepewa madaraka ya kusimama a masuala ya rufaa ya Maadili ya wanachama wake  na kwamba rufaa zote zote zinazohusu Maadili zinasimamiwa na mdaiwa wa pili(Bodi ya wadhamini ya simba),  nakwasababu hiyo wanaiomba Mahakama hiyo itafsiri Hilo.

" Japo Kuwa maelekezo toka TFF  kwenda mdaiwa wa kwanza (rage) ya
Yaliyomtaka Rage aweke  sehemu ya  Kamati ya Maadili , Rage  alishindwa kutekeleza maelekezo hayo KWA Madai Kuwa  robo  Tatu ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa Timu hiyo , wanatuhumiwa KWA makosa ya utovu wa Maadili .

" Barua ya TTF kwenda KWA Rage  ya Mei   29 Mwaka huu ,na barua ya Mwenyekiti wa Simbaya Juni 17 Mwaka huu ambayo alikuwa akimjibu Rais wa  TFF, Jamal Malinzi ni  ambazo tumeziambatanisha katika hati yetu ya madai kama vielelezo ili mahakama itoe tafsiri ya sheria " alidai wakili huyo.

Aidha walalamikaji hao wanadai Kuwa Kamati ya Uchaguzi ya Simba ipo kinyume na Katiba ya Timu ya Simba Kwani Kamati hiyo Ina baadhi ya wanachama ambao walioteuliwa Na Kamati ya Utendaji  na waliondolewa na Rais wa Timu hiyo  Katika Kamati hiyo kinyume Cha Sheria .

Pia wamedai Kuwa Kamati ya uchaguzi ya simba  haina mamlaka ya Kamati ya Maadili  ya kuwandoa  baadhi ya wagombea Katika mchakato wa uchaguzi Mkuu Kwani Kamati ya uchaguzi wa kuwachuja wagombea  pekee na suala la utovu wa Maadili  na nidhamu ya mgombea jukumu Hilo limekabidhiwa  Kwenye Kamati ya Maadili peke na siyo Kamati ya Uchaguzi .

"Kwa Sababu hiyo tunaimba Mahala hii itamke Kuwa utaratibu wote wa kuendesha uchaguzi ndani Timu  ya Simba  ni batiri  kwasababu umekiuka Katiba ya Simba" Alidai Wakili  Kuuli.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Juni 25 Mwaka 2014.

The people's Bank of Zanzibar Limited (PBZ Ltd) which is one among the oldest commercial banks in Tanzania and the only indigenous bank in Zanzibar wholly owned by the people of Zanzibar has today expanded its online remittance services to Tanzania from abroad by launching a new service for mobile phone subscribers in the country.

The new service enables members of Tanzanian Diasporic communities to transfer money to their loved ones in Tanzania directly to their mobile phones. Thus, anyone with a mobile phone in Tanzania can now receive money securely and promptly from overseas regardless of his/her location in the country. Similar service is already enjoyed by other East African countries.

The service is carried-out in collaboration with a widely renowned and an award-winning London-based financial services institution calledWorld Remit

The People's Bank of Zanzibar couldn't have planned a better timing for the launch of this new service than at the moment when the local Tanzanian mobile networks just signed the 'interoperability agreement' which allows mobile money customers to transfer cash to each other regardless of whether they are using Tigo Pesa, Airtel Money or Ezy Pesa on their mobile handsets.

With such an agreement in place, many families in the Diaspora will now be enticed to send e-money back home to the e-wallet accounts of their relatives even if the relatives live in remote villages. This will definitely promote a nascent ‘cashless’ economy in Tanzania and will help to drive forward e-commerce and socio-economic development in the country.
According to the People’s Bank of Zanzibar, from January 31st, 2013, when the first remittance worth only TShs 31,252.00 was sent from Toronto, Canada, up to date around one billion Tanzanian Shillings have already been remitted to Tanzania from different Diaspora communities through the People’s Bank of Zanzibar using cash pickup at the counter, bank deposit and airtime top-up services.

Visiting any branch of the bank in Tanzania today one would not fail to notice queues of customers beaming with smiles as they happily wait to pick up their cash sent by their relatives and friends from Europe. These queues are now part of the history of the People's Bank of Zanzibar, as no one would from
tomorrow go to stand on a queue when he knows quite well that he can receive cash from abroad directly in the palm of his/her hand.

Monthly records of the People's Bank of Zanzibar show that the number of remittances from different Diaspora communities are increasing month after month with Canada leading. Of late, UK which has the largest population of Tanzanians abroad has also caught up with the spirit after lagging behind for sometime and if it continues with the same tempo might soon surpass Canada.

The remittance services provided by the People’s Bank of Zanzibar were originally destined only for the recipients of those cities where the bank had its branches, viz, Pemba, Zanzibar and Dar Es Salaam. But, with the launching of this new service today, a new window has been thrown open for more than 27 million Tanzanians who own mobile phones in the country.

According to the officials of the bank in Zanzibar, the system has begun today to transfer funds to Tigo mobile phone numbers only (Tigo Pesa accounts), while the process of finalizing agreements with the other 3-BIG mobile providers in the country goes on.

Recipients are required to pre-register for mobile money service with their mobile phone providers prior to the usage of the service.

Remittance services through the People’s Bank of Zanzibar from USA to Tanzania are expected to start by the end of the year.

To all those who toiled, moiled and operated as one high performing team for the successful launching of the service today, we say it loud to them - AHSANTENI SANA!


Source: Zanzibar Ni Kwetu

COMESA ANNOUNCES MEDIA AWARDS
The Common Market for Eastern and Southern Africa (COMESA) has announced the launch of its annual media awards for 2014. The COMESA Media Awards 2014 are open for published and broadcasted works in the fields of Print, Radio, Television, and online media that focus on programmes and activities relating to regional economic integration in Eastern and Southern Africa.

The objective of the Awards is to promote reporting of COMESA regional integration activities and recognize journalists whose works contribute to the integration agenda. The awards are open to journalists from the 19 COMESA Member States. Eligible entries are for works published/broadcast between January and December 2014

Selection of the best works will be decided upon by an adjudication panel identified by COMESA Secretariat from Member States. Winners shall be announced and prizes awarded during the COMESA Heads of State and Government Summit in Addis Ababa expected to take place in the first half of 2015. The first prize in each category carries a monetary award, a trophy and a certificate.

Winners for COMESA Media Awards 2013 were Julius Barigaba of the EastAfrican Newspaper and Xavier Ahabyona of the Uganda Broadcasting Corporation. The duo was presented with certificates of merit by President Joseph Kabila Kabange of D R Congo during the COMESA Heads of State Summit in Kinshasa in February this year. They also received cash awards of $2000 each.

Each year since 2009, COMESA invites media practitioners from the region to submit published articles and audio/visual productions relevant to the regional integration agenda for consideration for awards.
Details for entry are published in the COMESA website www.comesa.int


KTH the School of Computer Science and Communication (KTH CSC) invites applications for a PhD position in verification of low-level software.

We are seeking a PhD student in computer science with specialization in software security to join the PROSPER project on provably secure execution platforms for embedded systems.

The objective of the project is to build and verify low-level virtualization solutions.
 
To realize this we work with formal verification tools (theorem provers, low level program analysis tools), we build hardware models, we develop the virtualization platforms and integrate them with existing operating systems (Linux), and we apply the provers and tools to high performance code at assembly or C level.

The specific role of the PhD student we are looking forward here is to be determined, but will likely involve theory and tool development for multicore processors.

The successful candidate is expected to have a strong foundational background in computer science (program logics and program verification, machine architecture, operating systems, programming) and mathematics (areas such as discrete mathematics, formal logic).

Application deadline: July, 6, 2014
Start date: September 2014

Details of the application procedure can be found on our website at:


For individual questions, the interested candidate is welcome to contact Mads Dam (mfd@kth.se) or Roberto Guanciale (robertog@kth.se).

Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka 2014 ambao waliomaliza kidato cha nne mwaka 2013
Wanafunzi waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti kwenye shule walizopangiwa kuanzia tarehe 10 Julai 2014 na mwisho wa kuripoti ni tarehe 30 Julai 2014. Aidha, hakutakuwa na mabadiliko ya wanafunzi kubadilishiwa shule walizopangiwa, hivyo wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangiwa kama inavyoonekana katika matokeo haya.
SOMA TAARIFA YA UCHAGUZI WA WANAFUNZI KUINGIA KIDATO CHA TANO HAPA
MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO MWAKA 2014


Wasichana Shule Zote

Wavulana Shule Herufi A-L

Wavulana Shule Herufi M-Z

Source by www.pmoralg.go.tz



2.0 WATAHINIWA WALIOFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE, MWAKA 2013

Jumla ya watahiniwa 427,679 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2013, wakiwemo wasichana 199,123 sawa na asilimia 46.56 na wavulana 228,556sawa na asilimia 53.44. Kati yao watahiniwa 404,083 sawa na asilimia 94.48 walifanya mtihani na watahiniwa 23,596 sawa na asilimia 5.52 hawakufanya mtihani huo.

2.1 Watahiniwa wa Shule (School Candidates)

Kwa Watahiniwa wa Shule, watahiniwa 367,163 walisajiliwa kufanya mithanikati yao wavulana
ni 198,099 na wasichana ni 169,064. ambapo watahiniwa 352,614sawa na asilimia 96.04 walifanya mtihani; kati yao wasichana walikuwa 162,412 sawa na asilimia 96.07 na wavulana 190,202 sawa na asilimia 96.01. Watahiniwa14,549 sawa na asilimia 3.96 hawakufanya mtihani kwa sababu mbalimbali.

2.2 Watahiniwa wa Kujitegemea (Private Candidates)

Kati ya watahiniwa60,516 wa kujitegemea waliosajiliwa kufanya mtihani, watahiniwa 51,469 sawa na asilimia 85.05 walifanya mtihani na watahiniwa 9,047 sawa naasilimia 14.95 hawakufanya mtihani kwa sababu mbalimbali.

Jumla ya watahiniwa 235,227 sawa na asilimia 58.21 ya watahiniwa waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2013 walifaulu. Mwaka 2012 watahiniwa waliofaulu walikuwa 185,940 kati ya 431,650 waliofanya mitihani; hii ni sawa na asilimia 43.08. Matokeo haya yanaonesha kuwa mwaka 2013 ufaulu umeongezeka kwa asilimia 15.13.

3.1 Ufaulu wa Watahiniwa wa Shule

Mwaka 2013 Watahiniwa wa Shule waliofaulu ni 201,152 sawa na asilimia 57.05 ya watahiniwa 352,614 waliofanya mtihani. Kwa mwaka 2013 kuna ongezeko la ufaulu wa watahiniwa 41,405, sawa na asilimia 25.91 ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2012 ambapo watahiniwa 159,747 walifaulu.

3.2 Ufaulu wa Watahiniwa wa Kujitegemea

Takwimu zimeonesha kuwa kumekuwa na ongezeko la ufaulu kwa watahiniwa wa kujitegemea kutoka 26,193, sawa na asilimia 43.07 mwaka 2012 hadi kufikia watahiniwa 34,075, sawa na asilimia 66.21 kwa mwaka 2013; Kwa kulinganisha na mwaka 2012 lipo ongezeko la asilimia 30.09 kwa ufaulu wa watahiniwa wa kujitegemea.

Ufaulu wa watahiniwa wa shule kwa mwaka 2013 katika madaraja ya I -III umefikia watahiniwa 71,527 sawa na asilimia 20.28 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara.Hivyo kuna ongezeko la ufaulu wa asilimia 106.73 ikilinganishwa na matokeo ya ufaulu kwa mwaka 2012, kwa kuwa watahiniwa wa shule waliofaulu katika madaraja I-III kwa mwaka huo walikuwa 34,599 sawa na asilimia 9.67 ya watahiniwa waliofanya mtihani.

5.0TARATIBU ZA UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO 2014.

Kulingana na utaratibu uliowekwa na Serikali, mwanafunzi anayeomba kuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari kidato cha tano na vyuo vya Ufundi, hulazimika kujaza ‘Selform’ ambayo ndiyo fomu rasmi ya maombi. Kwa kutumia fomu hiyo, mwanafunzi huchagua maombi matano ya tahasusi (Combinations)za masomo anayotaka kusoma na shule anayotarajia kujiunga nayo kwa kila chaguo.
Kamati ya uchaguzi humpanga mwanafunzi katika machaguo yake ya masomo na shule kwa kuanzia na chaguo la kwanza. Kama mwanafunzi atakuwa hana sifa katika machaguo yote aliyoomba, mwanafunzi husika hupangiwa chaguo la somo alilofaulu zaidi na katika shule iliyopo karibu na wilaya yake ya makazi kulingana na tahasusi na nafasi zilizopo katika shule husika.

6.0 IDADI YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUINGIA KIDATO CHA TANO

Jumla ya Wanafunzi 54,085 sawa na asilimia 75.61 ya wanafunzi 71,527 waliostahili kuingia Kidato cha Tano Tanzania Bara kwa mwaka 2014 wamechaguliwa; hilo ni ongezeko la wanafunzi 20,402 kwa kulinganisha na wanafunzi 33,683 waliochaguliwa mwaka 2013. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 2014 wavulana ni 31,352na wasichana ni 22,733.

Wanafunzi wamechaguliwa kujiunga kidato cha Tano katika jumla ya shule 241 zikiwemo shule 33 zilizopangiwa wanafunzi kwa mara ya kwanza mwaka 2014.

Nawashukuru sana wadau wote wa elimu katika Halmashauri mbalimbali kwa kuimarisha miundombinu ya shule hizo, ikiwemo maabara.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha Tano 2014 ni kutoka shule za serikali na zisizo za serikali. Kati yao wavulana 14,826 sawa na asilimia27.41wamechaguliwa kusoma masomo ya sayansi na wavulana 16,526 sawa na asilimia 30.56 wamechaguliwa kusoma masomo ya sayansi ya Jamii. Aidha,wasichana 7,859 sawa na asilimia 14.53wamechaguliwa kusoma masomo ya sayansi na wasichana 14,874 sawa na asilimia 27.50 wamepangwa kusoma masomo ya Sayansi ya Jamii.

Nawapongeza walimu wote kwa juhudi walizozifanya katika ufundishaji kwa kuzingatia mbinu za ufundishaji walizopata kupitia mpango wa mafunzo kazini (INSET)kwa walimu wa sayansi na lugha (Kiswahili na Kiingereza) unaosimamiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Ofisi ya WaziriMkuu, Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa. Aidha nawapongeza wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi. Hali hiyo inaonesha kuwa jitihada za Serikali za kuhamasisha vijana kusoma masomo ya Sayansi zimeanza kuzaa matunda.

Natoa wito kwa wanafunzi wa jinsi zote kujisomea kwa bidii masomo yote, yakiwemo ya Sayansi na Sayansi ya Jamii, kwani yanategemeana. Walimu wa masomo ya Sayansi, Sayansi ya Jamii na Hisabati wanakumbushwa kutumia mbinu shirikishi za kitaalam na kisaikolojia katika kufundisha ili kuwavutia wanafunzi wengi zaidi kusoma na kufaulu mitihani yao. Aidha walimu wa masomo ya Sayansi, waendelee kuwahamasisha wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi wakiwemo wanafunzi wa kike. Aidha, wanafunzi wa kike wanapaswa kujiamini kuwa wanaweza masomo yote yakiwemo ya Sayansi, kwani siri ya kujifunza ni utayari.

7.0 WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VYA UFUNDI, MWAKA 2014

Jumla ya wanafunzi 472wakiwemo wavulana 355na wasichana 117
wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Ufundi. Idadiya wanafunzi hao imepungua kutoka 530 mwaka 2013 hadi 472 mwaka 2014 kwa sababu kwa sasa vyuo hivyo vimeanza kuchukua wanachuo wa shahada ya kwanza. Aidha, kutokana na ufaulu kuongezeka idadi ya wanafunzi wa kike waliochaguliwa kujiunga na vyuo hivyo imeongezeka kutoka wanafunzi 114 mwaka 2013 hadi wanafunzi 117mwaka 2014 sawa na ongezeko la asilimia 2.63.

Natoa wito kwa wanafunzi kuendelea kusoma kwa bidii masomo ya sayansi ili mwakani idadi ya wanafunzi wanaojiunga na mafunzo ya ufundi iongezeke ili Taifa lipate wataalam wa kutosha wa ngazi zote.

8.0 SABABU ZA WANAFUNZI KUKOSA KUCHAGULIWA KUINGIA KIDATO CHA TANO
Jumla ya wanafunzi 16,800 wakiwemo watahiniwa wa kujitegemea 10 waliokuwa na sifa za msingi hawakuchaguliwa kwa sababu mbalimbali zikiwemo: ufinyu wa nafasi za shule za Kidato cha Tano (wanafunzi 16,400) na kukosa tahasusi - Combination (wanafunzi 400).

Serikali inatarajia kufanya uchaguzi wa awamu ya pili baada ya kubaini nafasi zitakazokuwa wazi zinazotokana na wanafunzi ambao hawakuripoti awamu ya kwanza. Aidha, Serikali imeweka utaratibu wa kuwapatia nafasi ya kusoma kidato cha Tano na cha Sita kwa pamoja na shahada ya Ualimu wanafunzi wenye sifa.

Shule za Kidato cha Tano na Sita zinatakiwa kuwa na mahitaji ya msingi, ikiwemo miundombinu yenye uwiano sahihi wa vyoo, bafu, vyumba vya madarasa, bweni, jiko, bwalo, maktaba, maabara, chumba cha Jiografia; pamoja na samani kulingana na idadi ya wanafunzi.

Shule zenye Kidato cha Kwanza mpaka cha Nne ambazo zinahitaji kuanzisha kidato cha Tano, zinatakiwa kuwa na miundombinu na mahitaji kamilifu yanayotosheleza kidato cha Kwanza hadi cha Nne kabla ya kuanza kujenga miundombinu ya Kidato cha Tano na Sita.

Natoa wito kwa Makatibu Tawala Mikoa wawaelekeze Wakurugenzi wa Halmashauri, Miji na Majiji kuhakikisha azma ya Serikali ya kila Tarafa kuwa na shule ya Kidato cha Tano inatekelezwa ili kupunguza idadi ya wanafunzi wanaokosa nafasi. Kutokana na ongezeko la ufaulu wa masomo ya sayansi tunahimiza shule zitakazoanza Kidato cha Tano ziwe na maabara ili kuongeza idadi ya wanafunzi wa tahasusi za sayansi.

Aidha, shule ambazo hazikupangiwa wanafunzi kutokana na mapungufu mbalimbali, Makatibu Tawala wa Mikoa husika wanahimizwa kuwaelekeza Wakurugenzi kusimamia kwa karibu ukamilishwaji wa shule hizo ili ziweze kupokea wanafunzi wa chaguo la pili (Second selection).

Natumia nafasi hii kuwahimiza wadau wote wa Elimu kuhakikisha kuwa shule zote zinazoanzishwa kwa ajili ya kidato cha Tano ziwe za bweni kwa kuwa wanafunzi wa kutwa ni wachache na ni lazima watoke eneo husika. Kwa mfano, mwaka huu shule ya sekondari Buswelu ya mjini Mwanza imekosa wanafunzi kwa kuwa ni ya kutwa na Mwanza kuna shule 3 za kutwa. Hivyo ilikuwa vigumu kupata wanafunzi wa eneo hilo wa kutosheleza shule hizo.

Wakuu wa Shule wahakikishe kuwa wanafunzi wa kidato cha nne wote wanajaza ‘Selforms’ kwa umakini na kwa usahihi ili kurahisisha zoezi la uchaguzi. Aidha, wazazi kwa kushirikiana na walimu wawaelekeze watoto wao kuwa na dira, kuwasaidia kusoma kwa malengo na kufanya machaguo ya tahasusi kulingana na dira walizonazo.

10.0 WANAFUNZI KURIPOTI KATIKA SHULE WALIZOPANGWA

Muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano mwaka huu 2014,utaanza mwezi Julai tarehe 10. Wanafunzi wamepangwa katika shule zenye miundombinu na walimu kwa masomo husika. Aidha, iwapo baadae mapungufu yatajitokeza, wakuu wa shule wameelekezwa kutoa taarifa kwa uongozi wa Halmashauri husika kuhusu upungufu huo.

Uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano umefanyika kwa kutumia mfumo wa kompyuta kwa kuzingatia machaguo ya wanafunzi pamoja na ufaulu hivyo hakutakuwa na mabadiliko yoyote.
Kwa nafasi hii, naagiza wanafunzi wote kuripoti katika shule walizopangwa tarehe 10 Julai, 2014. Wanafunzi ambao watashindwa kuripoti shuleni hadi tarehe30 Julai, 2014 nafasi zao zitajazwa na wanafunzi ambao wamekosa nafasi.

Mwisho ninachukua nafasi hii kuwapongeza wanafunzi waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi mwaka 2014, walimu, wazazi, Bodi za Shule, viongozi, jamii na wadau wote wa elimu kwa jitihada za kuwaandaa wanafunzi, na kufanikiwa kuingia Kidato cha Tano. Ushirikiano wa wadau wote unatakiwa ili kuboresha elimu hapa nchini.

Wataalam wa elimu kuanzia ngazi ya shule wawe na utaratibu endelevu wa kuelimisha wadau katika utekelezaji wa malengo yanayopimika. Katika utaratibu wa ”Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now)”; kila mmoja anatakiwa kuacha utendaji wa mazoea na afanye kazi kwa malengo na viwango, kuwa na mipango inayotekelezeka ya muda mfupi na muda mrefu na kuwa na vipindi vya tathmini kwa kila lengo kabla, kati na mwisho wa utekelezaji. Ni matumaini yangu kuwa wakuu wa shule na viongozi wote wa elimu wakizingatia taratibu hizi, elimu inayotolewa hapa nchini itaendelea kuwa bora zaidi.

Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2014 inapatikana katika tovuti zifuatazo: -

Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Mhe. Kassim M. Majaliwa (MB)
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAMISEMI






































Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.