July 2014


.wamepokea shilingi 80 bilioni katika mpango wa makazi kwa watumishi wa umma

Na Damas Makangale, Makangale Satellite 

Kwa watumishi wa umma uanzishwaji wa Watumishi Housing Company (WHC) ambao ni mpango wa makazi kwa watumishi wa umma ni mkombozi wa kweli kwa ustawi wa maisha ya mfanyakazi wa serikali, asante kwa serikali ya awamu ya nne kwa kuanzisha taasisi hii muhimu kwa ujenzi wa taifa.
 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Watumishi Housing Company (WHC), Dakta Fred Msemwa akiwa amepozi ofisini kwake baada ya mahojiano.
WHC ni taasisi inayojihusisha na uendelezaji miliki na usimamizi wa uwekezaji katika miliki. Kampuni hii ya umma imepewa jukumu la kuwa mtekelezaji mkuu wa mpango wa taifa wa makazi kwa watumishi wa umma na ina jukumu la kujenga nyumba 50,000 nchi nzima.
Akizungumza na Makangale Satellite mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji mkuu wa WHC, Dkt Fred Msemwa amesema kuwa nyumba hizo zitauzwa kwa mkopo nafuu wa muda mrefu kwa watumishi wa umma.

“Baada ya Benki Kuu kulegeza masharti ya mikopo ya nyumba kwa hiyo sasa mtumishi wa umma haihitaji fedha ya kutanguliza (deposit) ambayo ni tofauti na masharti yaliyopo sasa katika uuzaji wa nyumba kwa mikopo ambayo yanamtaka mnunuzi atoe asilimia 10 mpaka 20 kama fedha ya utangulizi,” amesema Dkt Msemwa 

Amesema kwamba WHC ni taasisi ya umma yenye jukumu la uendeleza makazi yaliyo bora kwa watumishi wa umma nchini na ilianzishwa mwaka 2013 na jukumu kubwa ni kuboresha na kujenga makazi ya watumishi wa umma nchi nzima.

Dkt Msemwa alisisitiza kwamba serikali iliamua kuja na utaratibu huo wa makazi kwa watumishi wake baada ya kuona kwamba kwenye nguvu ya soko la makazi watumishi wachache wanaweza kumudu nyumba zinazouzwa na taasisi za fedha kwa sababu ya riba kuwa juu.

Amesema kwamba mkopo katika nyumba hizi ni kwa miaka hadi 25 na riba ya nyumba hizi ni asilimia 10 hadi 13 ukilinganisha na hali ilivyo kwenye soko la sasa la nyumba nchini Tanzania.

Dkt Msemwa amesema kwamba ujenzi rasmi wa nyumba hizi za watumishi wa umma zitaanza kujengwa mwezi oktoba mwaka huu sehemu mbalimbali za nchi kama vile Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Arusha, Shinyanga, Mwanza, Tabora, Dodoma, Morogoro, Mbeya, Lindi na Mtwara.

Amesema kwamba inakadiriwa kwamba kuna wafanyakazi 650,000 wanaofanya kazi kwenye mashirika na sekta ya umma ambapo wafanyakazi 10,000 sawa sawa na asilimia 2 tu tu waliopata mikopo ya nyumba.

Aliongeza pia WHC wameweza kufika hapo walipo baada ya kupata Baraka ya kuwa chini ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo ni Mfuko wa PPF, National Social Security Fund (NSSF), Mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa Umma (PSPF), LAPF, Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Serikali (GEPF), Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Amesema pia kwamba kampuni hiyo ina jukumu la kusimamia vipande vya uwekezaji katika miliki (Real Estate Investment Trusts –REITs).

“kila mtumishi wa umma atanunua nyumba kwa kupitia mkopo kwa kuangalia kiwango chake cha mshahara kama mtumishi wa umma,” alisisitiza
Dkt Msemwa alifafanua kwamba tofauti kati ya WHC ni mabenki na kampuni zingine ni kwamba wengine wanafanya biashara kwa kuangalia faida ila taasisi wana malengo ya kuhakikisha mtumishi wa serikali anapata makazi bora ya kuishi kabla na baada ya kustaafu.

Amesema kwamba kuanzia katika mkoa wa Dar es Salaam nyumba zitajengwa Mabwepande, Magomeni na Kigamboni baada ya kukamilisha taratibu zote kwa kushirikiana na serikali za mitaa na wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi ili kuhakikisha maeneo yote yanakuwa na hati miliki (title deeds).

Dira ya WHC ni “Makazi Bora kwa Watumishi wa Umma” na Dhima kuwezesha watumishi wa umma kumiliki nyumba kwa njia ya mikopo nafuu na kufaidi matunda ya uwekezaji katika miliki kwa kutumia wafanyakazi wenye weledi katika usimamizi wa uwekezaji na uendelezaji miliki.

Mwisho.



IMEGUNDULIKA kwamba Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM) ndiye mfadhili mkuu na mpanga mikakati mkuu wa kundi linalomfuata Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ambalo limeanzisha chama kipya cha siasa, Allaince for Change and Transparency (ACT-Tanzania).

Lowassa aibukia ACT
Mbunge wa Monduli, Mh Edward Lowassa
Kwa wiki kadhaa za hivi karibuni, makundi ya wanachama, washauri na wapanga mikakati wa Lowassa na Zitto wamekuwa wakikutana katika maeneo kadhaa jijini Dar es Salaam na kupeana mbinu, lengo kuu likiwa ni jinsi ya kumega Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika mapande ili kidhoofike kabla ya uchaguzi mkuu 2015.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, Lowassa amejiaminisha kwamba ndiye atakayekuwa mgombea urais kupitia CCM. Kazi kubwa anayoona mbele yake ni kuanza mapema kusambaratisha CHADEMA ili kupunguza upinzani wakati wa kampeni utakapofika.
Zitto naye, ambaye uanachama wake kwa CHADEMA umebaki kwenye makaratasi tu, anatajwa kuwa ndiye mwasisi mwenza wa ACT, na amekuwa na uhusiano wa “kikazi” na Lowassa, hata kabla hajaingia kwenye matata ya wazi na chama chake, ambacho mwishoni mwa mwaka jana kilimvua vyeo vyake vyote vya uteuzi ndani ya CHADEMA kwa tuhuma mbalimbali.
Katika hatua mojawapo, chanzo kimoja kilicho karibu na Lowassa kimesema kwamba mapema mwaka juzi, Zitto alimwendea Lowassa na kumwambia kuwa mustakabali wake kisiasa ndani ya CHADEMA si mzuri, na kwamba alikuwa tayari kumsaidia Lowassa kufanikisha malengo yake, lakini kwa sharti kwamba iwapo mbunge huyo wa Monduli atafanikiwa kupata urais, basi amteue kuwa Waziri Mkuu.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, kauli hiyo kwanza ilimstua Lowassa kwa sababu ilimuonesha Zitto kama kiongozi asiye mwaminifu, ambaye yupo tayari kufanya hujuma dhidi ya chama chake, jambo ambalo lilimfanya Lowassa atilie shaka lengo la ombi hilo.
Jambo la pili lililomshtua Lowassa ni cheo kilichopendekezwa na Zitto, maana kwa mujibu wa Katiba ya sasa, Waziri Mkuu lazima atokane na wabunge wa majimbo, na awe kwenye chama chenye wabunge wengi.
Kwa kuwa hoja hiyo ilitolewa katika mazingira ya Katiba ya sasa, na kwa kuwa haikujulikana wakati ule kama Zitto alikuwa bado ni mwanachama na kiongozi wa CHADEMA, Lowassa hakuipata nafasi kauli hiyo, lakini amekuwa anaitumia kujadili sura halisi ya Zitto.
Hata hivyo, taarifa zinasema uhusiano wao umeimarika baada ya Zitto kuchukuliwa hatua na CHADEMA, huku wapambe wa Lowassa wakipita huku na kule kusambaza propaganda kuwa CHADEMA bila Zitto inakufa.
Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema Zitto anatarajiwa kujiunga rasmi na ACT mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, na timu ya Lowassa imedhamiria kumfadhili ili kujenga taswira ya mpasuko ndani ya CHADEMA, na kuipa CHADEMA mpinzani mpya ambaye ataifanya ishindwe kumfuatilia na kumshambulia Lowassa.
Katika kikao cha mwisho kilichofanyika kati ya timu ya Lowassa na “Vijana wa Zitto” kilijumuisha baadhi ya wapambe wakuu wa Lowassa wenye kauli ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM, watu wa karibu kifamilia na Lowassa na washauri wa karibu wa Zitto, akiwamo Mhadhiri mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Ajenda zao nje nje 
Moja ya ajenda zao kuu ni kufadhili na kupandikiza watu ndani ya mfumo wa CHADEMA ambacho kinaendelea na uchaguzi wa ndani, ili wapate nafasi za uongozi, wazitumie kupata taarifa na mipango ya chama, na baadaye wajivue nafasi hizo na kukimbilia ACT, na kuleta msisimko wa kitaifa.
Gazeti hili lina taarifa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa sasa wa CHADEMA ambao “Vijana wa Zitto” wamekuwa wakiwapigia simu na wakati mwingine kuwatembelea na kuwashawishi ahadi ya fedha na vyeo ili wajiondoe CHADEMA.
Baadhi hao ni viongozi wa majimbo na mikoa ambao katika uchaguzi unaoendelea ndani ya chama hawana uhakika wa kuchaguliwa kutokana na upinzani mkubwa unaojitokeza baada ya chama kukua na kuvutia wasomi na wafanyabaishara wenye mvuto katika maneo yao.
Baadhi ya viongozi walioendewa au kupigwa simu wamechukua tahadhari, na wametoa taarifa panapohusika ndani na nje ya chama.
Mbinu mojawapo ambayo imekuwa inatumiwa na “Vijana wa Zitto” kujaribu kuvunja ngome za CHADEMA ni kuwatangazia viongozi hao kwamba ipo idadi kubwa ya wabunge wa CHADEMA wanaotarajia kujiunga na ACT. Wanawataja majina kama njia ya kujenga ushawishi.
Hata hivyo, baadhi ya viongozi hao wameliambia gazeti hili kuwa wanajua hizo ni mbinu za kipropaganda. Na baadhi ya wabunge wanaotajwa wamesema hizo ni mbinu za Zitto kutaka kuwagombanisha na chama chao na kujitafutia njia mpya kwa kutumia majina yao.
Mmoja wao alisema, “Zitto mwenyewe ameshalikoroga. Sasa hii ni tabia ya kututaja baadhi yetu, mimi na wenzangu kadhaa tumeshasikia, ni ile ile roho mbaya ya tukose wote. Kwa kuwa yeye amekosana na chama, anatafuta watu wa kufa naye.”
Mbali na kupandikiza wagombea nafasi za uongozi na kuvizia viongozi wanaoogopa joto la uchaguzi ndani ya chama, wamekuwa pia na mbinu ya kushawishi baadhi ya “wagombea watarajiwa” katika baadhi ya majimbo, wanaotajwa kuweka nia ya kugombea nafasi za uongozi kupitia CHADEMA.
Makada kadhaa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wamezungumza na gazeti hili na kutumia kauli zijazofanana. Kwa mfano, makada sita walioweka nia ya kugombea ubunge katika majimbo kadhaa ya kanda ya Ziwa Mashariki na Magharibi, wamekiri kwamba kila wanapojadili mkakati huu na “Vijana wa Zitto,” kila mmoja wa nafasi yake anapewa ahadi ya kupewa pesa zote za kufanyia kampeni.
Vile vile, baadhi yao wamesema kuwa wanaambiwa kwamba iwapo watakubaliana na mpango huo wa ACT, moja kwa moja watakuwa wamepitishwa, maana chama hicho hakina mpango wa kupata wagombea kwa kutumia kura za maoni.
Taarifa zinasema sehemu ya malengo ya vikao ya Zitto na Lowassa ni kutafuta pesa kwa ajili ya mradi huu.
Zipo taarifa zisizothibitishwa kwamba mwezi uliopita Lowassa aliambatana na Zitto katika ziara ya kimya kimya ya Mkoa mmoja wa kanda ya Ziwa ambako anasemekana anataka kujenga ngome nzito ya ACT.
“Ninachojua ni kwamba iwapo ACT itafanikiwa kupunguza makali ya CHADEMA, Mzee atapita kirahisi, maana kikwazo kikubwa alichonacho hadi sasa hakipo ndani ya CCM, bali CHADEMA,” alisema mtoa taarifa wetu aliye karibu na Lowassa, ambaye hakutaka kuthibitisha kama wawili hao walisafiri pamoja kwenda Kanda ya Ziwa.
Mkono mrefu wa CCM ndani ya ACT
Mbali na ufadhili wa Lowassa, imebainika pia kwamba makada wengi wa CCM wamewekeza raslimali zao katika kuinua ACT na kudidimiza CHADEMA.
Uchunguzi wetu umeonyesha kuwa mbali na Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, mmoja wanaoratibu kazi ya Zitto ni kada wa CCM, ambaye ni mdogo wa mmoja wa mawaziri waliojiuzulu katika sakata la Operesheni Tokomeza, anayetokea kanda ya Kusini.
Wengine wanaotuhumiwa kujihusisha na mradi huu wa Tokomeza CHADEMA ni Naibu Waziri mmoja ambaye ni bingwa wa propaganda za CCM, na ambaye amewahi kutangaza hadharani kuwa ifikapo 2015 CHADEMA kitakuwa kimekufa. Wamo pia wabunge na viongozi kadhaa waandamizi wa CCM, ambao licha ya kwamba hawamuungi mkono Lowassa, wanafurahia msukosuko wowote utakaokipata CHADEMA kuelekea 2015.
Mwingine ambaye anadaiwa kufadhili ACT ni mtoto wa kigogo, ambaye katika miaka ya karibuni ameingia kwenye kashfa nyingi, kabla ya kukwaa ubunge hivi karibuni.
Madiwani waliohama waomba radhi warejeshwe
Wakati huo huo, madiwani wawili waliohamia CCM kutoka CHADEMA, katika kata za Ngokolo na Masekelo, Shinyanga, Sebastian Peter na Zacharia Machafuko, wameibuka na kusema wanajutia uamuzi wao, na sasa wanafanya jitihada za kuomba warejeshewe uanachama wa CHADEMA baada ya kukerwa na hila za CCM na ACT.
Madiwani hao wanadai kuwa walihamia CCM kwa muda  kwani waliambiwa kuwa ACT kitakapokuwa kimepata usajili wa kudumu wangejiunga nacho ili kuimarisha upinzani nchini.
Madiwani hao walijiunga na CCM Februari mwaka huu na kupokelewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye. Baadaye, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Wilbroad Slaa alikituhumu CCM kwa mchezo mchafu.
“Tukishawishiwa kuhamia CCM kwa muda kwa lengo la kuhamia ACT ili kikipata usajili wa kudumu tuhamie huko pamoja na baadhi ya wanachama wa CCM.
“Tuliambiwa tufanye siasa za harakati, lakini tulichobaini ni kuwa tangu tukubali mawazo hayo ya viongozi wa ACT tukijua tunaimarisha upinzani imekuwa tofauti. Mkakati huo ulianza kuratibiwa na Mwenyekiti wa UVCCM, Abbakari Gulam ambaye ni mtoto wa Meya wa Shinyanga, wakiwa na Habib Mchange, kisha tuliona mkakati unatekelezwa na mbunge wa Shinyanga mjini, Stephen Masele, Nape Nauye, Januari Makamba, Mwigulu Nchemba na Ridhiwani Kikwete,” walisema katika taarifa yao mbele ya waandishi wa habari jijini Mwanza.
Wakisimulia mkakati huo walisema walifikishwa Tinde na kiongozi huyo wa UVCCM kisha wakiwa huko walipigiwa simu na Stephen Masele na kuzungumza Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA aliyewahakikishia kuwa baada ya kuondoka CHADEMA watajiunga na ACT ili iwawezeshe kupata nafasi za uongozi wa kitaifa katika chama hicho kipya, pamoja na kupatiwa kitita kikubwa cha fedha.
Chanzo chetu cha habari kutoka Shinyanga kimeelezwa kuwa baada ya kuhamia walipatiwa kiasi kikubwa cha pesa bandia, na katika kitita hicho waliambulia laki mbili ndio zilikuwa halali, pesa hizo zimetajwa kuwa zilikuwa ziwe milioni kumi na mbili lakini bada ya kuhesabu zilipatikana halali laki mbili tu, na zinadaiwa kutolewana na msaidizi wa Masele akiwa na Mchange katika hoteli ya Karena iliyopo Shinyanga, kabla ya madiwani hao kuondolewa na gari hadi Mwanza na kusafiri kwa ndege hadi Dar es Salaam kwa maelekezo ya Nape.
Tamko hilo linaongeza kuwa “kwa kipindi chote cha kudanganywa tulidhani Zitto anaonewa, hivyo tukaamua kujiunga na Chama chake ambacho alituhakikishia lakini tumebani kuwa ACT na CCM hawana tofauti, mikakati inatengenezwa na ACT ila watekelezaji ni CCM, baada ya kubaini ghiliba hizi tumeshindwa tumetafakari kuwa hata barua zetu tuliandika zikiwa na makosa ya kikanuni hivyo sasa tumemwandikia tena Meya kumuuliza ni kwanini hajatualika kwenye vikao viwili kwa kuwa tulikuwa hatujajiuzulu kisheria.
“Ili mtu kujiuzulu udiwani, kanuni zinasema kuwa diwani anaandika barua kwa Meya, unaambatanisha na kitambulisho cha udiwani, na hati ya ushindi ya udiwani ambayo hatujawapa wala vitambulisho vyetu, tulichokifanya ni kama kuandikiana barua za kawaida tu, na mtu kutangaza kujiunga na Chama kiingine bila kuchukua kadi yao sisi sio wanachama wao na kwa kuwa Chama chetu hakijachukua hatua zozote dhidi yetu basi tunarejea kwetu upinzani kushindana na CCM,” alisema Sebastian mbele ya waandishi wa habari.
Walisema CCM na ACT waendelee na kamari zao kuhadaa watanzania, “jamaa hao wana umakini kidogo ndio maana hawakubaliani kuwa bado hatujajiuzulu kisheria wakakimbilia kutupeleka jukwaani kushangilia, sasa sisi tunarudi kutumikia wananchi wetu kwani hatujavunja sheria, hatukukiuka kanuni za kujiuzulu furaha ya CCM na ACT ni ya muda tu, tulionda huko tumewabaini.
Kufuatia hali hiyo,madiwani hao waliandika kuwa “tunapenda kuomba radhi viongozi wote wa CHADEMA, wanachama na watanzania wote watusamehe, watupokee tukapambane kufanya kazi ya siasa za upinzani wa kweli kuleta ukombozi wa kweli kwa nchi yetu, tulichokiona huku tumekijua, tunawatahahadharisha wengine wakionga inafaa wajiunge huko kwa hasara yao ya maisha yao kisiasa na kufanya kazi ya kujenga CCM.”
Mkakati huu unaratibiwa na mmoja wa wabunge wa upinzani mwenye mahusiano ya karibu na viongozi wa CCM na serikali anayedaiwa hadi sasa kuifadhili ACT mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kujiimarisha mikoani kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.
Kazi ya wanazi wa ACT waliofukuzwa CHADEMA
Kwa sehemu kubwa, imebainika pia kwamba nguzo kuu za ACT ni makada wa zamani wa CHADEMA ambao kwa sababu kadhaa walipata misukosuko ndani ya chama hicho na kuchukuliwa hatua kali au kufukuzwa katika maeneo kadhaa ya nchi.
“Sisi hapa Mwanza tunatambua fika kwamba. Meya Henry Matata, Diwani Adam Chagulani wa Igoma, na Mushumbusi ndio vinara wa ACT wanaotumika kujaribu kusambaza ACT kanda ya Ziwa, na kujaribu kupenya na kubomoa ngome ya CHADEMA. Kwa sasa hata Habib Mchange wa Pwani, yupo  Mwanza anaratibu mipango ya uzinduzi wa chama chao utakaofanyika mapema mwezi ujao.
“Lakini hapa kuna ukweli ambao haupingiki, kwamba watu hawa walishafukuzwa CHADEMA, na sasa wanafanya siasa za chuki na visasi, wakiajribu kurubuni wanaCHADEMA. Pili, ni ukweli kwamba CHADEMA ni imara kuliko wanavyodhani. Haiwezi kubomolewa na wanachama wake wa zamani waliaoamua kuwekeza katika Siasa za usaliti. Hata huko waendako watasalitiana tu,” alisema kada mmoja wa CHADEMA mkazi wa Mwanza, ambaye hakutaka kutajwa jina kwa kuwa si msemaji.
Alipotafutwa John Nchimbi kwa simu alisema jina lake litakuwa linachanganywa kwani yeye hajishughulishi na siasa bali ni mdau wa michezo ambaye historia yake iko Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), huku Dk. Kitila naye akikana kushiriki mpango wowote wa kuhujumu CHADEMA.
Alisema kuwa yeye ni mwanataaluma ambaye hajihusishi na siasa za vyama na kwamba kama wako viongozi wa CHADEMA wanarubuniwa na kukubali badi chama kinapaswa kujiuliza walipataje uongozi.
Fred Lowassa, Mwigulu Nchemba, Nape Nnauye, Mshumbusi simu zao ziliita bila kupokelewa.


AJALI za barabarani limekuwa ni tatizo kubwa na sugu nchini na tumeendelea kushuhudia ajali nyingi zikitokea na kupoteza maisha ya watu na kuacha maelfu wakiwa majeruhi na wengine kuachwa vilema wa maisha.

Tatizo la ajali nyingi nchini ni kutokana na uzembe wa madereva kunakosababishwa na kutokutii sheria za usalama barabarani kwa kiwango ambacho hakivumiliki kwa mustakabali wa taifa letu.

Huko nyuma mtaalamu mmoja kutoka Chuo cha Usafirishaji nchini (NIT) aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari kwamba ajali nyingi hapa nchini zinasababishwa na binadamu yaani (Human Errors) na ni chache zinatokana na tatizo la miundombinu.

Kwa hiyo sisi kwenye blog ya Makangale Satellite tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi nchini, kikosi cha usalama barabarani kusimamia sheria, kanuni na taratibu kwenye usimamizi wa vyombo vya moto ili kupunguza ajali zinazoepukika na kunusuru maisha ya watu na mali.

Kwa sababu tunajua fika kwamba tatizo la rushwa nchini hasa katika sekta ya usafiri ni kichocheo kikubwa katika kuongezeka kwa ajali za barabarani.

Pamoja na mambo mengine madereva wasiotii sheria za barabarani wanafanya hivyo kwa sababu wanajua watatoa rushwa kwa askari wa usalama barabarani lakini ni muhimu kwa serikali kupitia Jeshi la Polisi nchini kutazama upya sheria hizi ili ikiwezekana kutoa adhabu kali ikiwemo ya kifungo cha angalau mwaka mmoja kwa makosa ya uzembe barabarani achilia mbali faini.

Hivi majuzi tumeshuhudia ajali kati ya bari la abiria na lori na takribani watu kumi na saba kupoteza maisha yao na wengine kadhaa kupata majeraha makubwa.
Wenzetu wa Afrika ya kusini wamebuni mfumo ujulikanao kama “Road Buddy” uliobuniwa na mjasiriamali anayejulikana kama Werner Van Der Westhuizen kwa kutumia teknolojia ya Cloud Computing.

Utendaji kazi wa mfumo huu ulibuniwa na Bwana Werner almaarufu kama “Road Buddy” ni kwamba mara hawa watumiaji wakuu wa barabara wanapokuwa wanakaribia magari kuna viashiria vinavyotoa ujumbe kuelezea hali hiyo nah ii ni kutokana na teknlogia iliyotumika katika mifumo hii ya Cloud Computing.

Kulingana na hali ilivyo katika nchi ambapo watu wengi wanajiuliza nini kifanyike ili kuliepusha taifa na madhara makumbwa yanayosababishwa na ajali hizi ambapo wengine wanashauri jeshi la Polisi kuziangalia sheria zake za barabari ambazo zimepitwa na wakati kulingana na mahitaji ya sasa ilikuendana na hali halisi iliyopo lakini pia kuna haja pia ya kuboresha miundo mbinu mingine kama  uufungwaji wa Camera za barabari (CCTV) na hivyo kurekodi matukio yote ya barabari na kuwanasa wale wote wanaouvunhja sheria za barabari.

Kwa wenzetu hali hii ya kusema kuna tatizola maofisa wasio waamininfu katika kupokea Rushwa litakuwa limetattuliwa kwa kiasi kwa kuwa endapo camera hizi zitafungwa na mtumiaji wa barabara akawa amevunja rekodi ni kuwa voucher ya faini itapelekwa kwenye akaunti yake na kutakiwa kulipa faini na kadhalika.

Pia ni muda muafaka pia kuangalia na technologia nyingine kama za Bwana Werner ambapo ni uhakika hadi kufikia huku ni kutokana na madhara mmbalimbali yaliyokuwa yanasabishwa na watumiaji wa barabara na waendesha vyombo vya moto ambapo vilisababisha hadi watu kama kufikiria mbinu kama hizi ili kujaribu kupunguza ajali  hizi za barabarani.

Basi la Morobest lenye na namba za usajili T 258 AHV lilipopata ajali ya kugongana uso kwa uso na Lori
na kuua Watu 17 katika eneo la Pandambili Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma, Basi lilikuwa likitoka Mpwapwa kwenda Dar es salaam.

Swali kubwa linaloacha vinywa pasipo kujibiwa ni hatua gani zichukuliwe ili kukomesha ajali hizi pamoja na jitahidi mbalimbali zinazofuatwa na vyombo vya usalama barabarani lakini hali hii inakuwa bado haikomeshe tatizo hilo
Lori lenye namba za usajili T 820 CKU na tela yenye namba za usajili T 390 CKT lililokuwa likiendeshwa na Dereva wake Gilbart Lemanya na Tingo wake Mikidadi Zubery Omary ambao wote walifariki papo hapo
linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na basi la Morobest katika eneo la Pandambili Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma

Ajali iliyotokea siku ya jumamosi katika milima ya Kitonga Barabara kuu kuelekea mikoa ya Iringa na Mbeya


































































































































Mpigie Kura Miss Tanzania USA, Joy Kalemera anayeshiriki kinyang'ayiro cha kumtafuta Miss Africa USA. Mtangazaji wa Mimi Na Tanzania Hoyce Temu ambaye pia ni Miss Tanzania 1999 yupo nchini Marekani na amefanya mahojiano na mrembo huyo.
IMG-20140727-WA0011
Pichani ni  Miss Tanzania USA 2014, Joy Kalemera katika pozi kabla ya mahojiano na Mtangazaji wa kipindi cha "Mimi na Tanzania" Hoyce Temu nchin Marekani.

Usikose kuangalia marudio ya mahojiano hayo kwenye kipindi cha "Mimi na Tanzania" Jumamosi  ya tarehe 2 August ,2014 Saa saba mchana katika kituo cha Televisheni cha Channel Ten.

Namna ya kushiriki kumpigia kura moja kwa moja kwenye profile yake Bonyeza hapa utakuwa umeingia kwenye profile ya Joy Kalemera na bonyeza kitufe chenye alama ya mkono (sehemu iliyozungushiwa duara na wino mweusi) na moja kwa moja utakuwa umempigia kura Mtanzania mwenzetu anayeiwakilisha vyema nchini yetu kwenye kinyan'ganyito hicho.

 http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2014/07/Joy-Kelemera.jpg
NOTE: Unaweza kupiga kura mara nyingi uwezavyo kila baada ya dakika mbili kwa kubofya sehemu ile ile.




IMG-20140727-WA0013
Miss Tanzania 1999 ambaye pia ni Mtangazaji wa kipindi cha "Mimi na Tanzania" Hoyce Temu akipata ukodak na Miss Tanzania USA, Joy Kelemera baada ya mahojiano maalum nchini Marekani.


IMG-20140727-WA0014
Pichani ni Hoyce Temu, Joy Kalemera na camera crew/IskaJojo studios (katikati) aliyefanikisha kukerokodi maojiano hayo.



IMG-20140727-WA0015
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu na Miss Tanzania USA 2014, Joy Kalemera katika pozi za madaha.






































































TAASISI ya Hawzat-Imam-Swadiq (A.S), iliyopo Kigogo Post, jijini Dar es Salaam, imepanga kufanya maandamano kesho kupinga mauaji yanayoendelea Mashariki ya Kati dhidi ya Wapalestina.
Profesa Abdul Shariff (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo kuhusu maandamano ya amani ya kupinga ukandamizaji wa vikosi vya Israel dhidi ya Wapalestina vinavyoendelea jijini Gaza, Maandamano hayo yatakayofanyika kesho yataanzia Ilala Boma hadi Kigogo jirani na kituo kidogo cha polisi. Maandamano hayo ya kupinga mashambulizi ya kijeshi ya Israel dhidi ya Palestina yameandaliwa na Taasisi ya Kiislamu ya Hawzat-Imam Swadig (AS).Kulia ni Sheikh Hemedi Jalala.

Mkuu wa taasisi hiyo, Hemed Jalala, akizungumza jijini Dar es Salaam jana, alisema wanapinga vikali mauaji yanayofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina na kuamua kufanya maandamano yataanzia katika kituo cha daladala cha Ilala Boma hadi Kigogo uwanja wa Bibo kuanzia saa tatu asubuhi hadi sita mchana.

“Hadi sasa maelfu ya Wapalestina wamepoteza maisha, hivyo jamii na taifa kwa ujumla tunapaswa kushirikana na kuonyesha kuguswa na mauaji hayo, kwani waathirika ni
watu wa dini zote.
“Kutokana na mauaji yanayoendelea nchini humo, watu wanashindwa kwenda misikitini na makanisani kufanya ibada na hata kushindwa kufanya shughuli zao za kila siku.” 
Jalala alisema maandamano hayo yatahusisha watu wa dini zote na yana kibali kutoka Jeshi la Polisi na kuiomba jamii kujitokeza na kushirikiana kuonesha hali ya umoja kupinga mauaji hayo kwa kuwa kunyamazia tatizo hilo ni kufanya kosa kwani hakuna hata dini moja inaruhusu mauaji ya binadamu mwingine.

Msemaji wa Taasisi hiyo Profesa Abdul Shariff, amesema kuwa wameamua kupaza sauti zao kulaani baada ya kuona Jumuiya mbalimbali za Kimataifa ikiwa imenyamaza huku mamia ya watu wakizidi kupoteza maisha.

Amesema kuwa inasikitisha kuona hata vyombo vya habari hasa vya Magharibi havitoi nafasi kubwa kwa mauaji hayo ukilinganisha na mauaji yaliyotokea kwa kulipuliwa kwa ndege Malyasia.

Viongozi na Mabalozi wa nchi mbalimbali wamealikwa ili nao waweze kushiriki katika kupaza sauti zao pamoja na Watanzania kulaani vitendo vinavyofanywa na Israel vya kuua watu wasio na hatia.

Chanzo cha habari na mtandao wa www.wavuti.com


Tafiti zimebaini kwamba Vijana hawatumii Kondomu na hutoa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na kutopata ladha wakati wa tendo la ndoa na kwamba inapunguza nguvu na visingizio vingine vingi vinavyopelekea kuashiria hatari ya maambukizi.
DSC_0084
Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias akizungumza na washauri wa Vikundi vya Vijana wasikilizaji juu ya masuala muhimu kuhusiana na kuzuia maambukizi ya VVU na Afya ya Uzazi kwa Vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 katika warsha ya kuwajengea uwezo washiriki hao katika matumizi ya mwongozo wa ufuatiliaji wa vipindi kwa wasikilizaji walengwa wa Mradi wa SHUGA Redio inayofanyika kwenye kituo cha Redio Nuru FM mjini Iringa

Hayo yameelezwa na Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias wakati akizungumza na washauri wa Vikundi vya Vijana wasikilizaji juu ya masuala muhimu kuhusiana na kuzuia maambukizi ya VVU na Afya ya Uzazi kwa Vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 katika warsha ya kuwajengea uwezo washiriki hao katika matumizi ya mwongozo wa ufuatiliaji wa vipindi kwa wasikilizaji walengwa wa Mradi wa SHUGA Redio.

 “Asilimia 40 ya Wasichana na Asilimia 47 ya Wavulana ndio wenye ufahamu wa kina juu ya maambukizi ya VVU huku asilimia kubwa wakiwa hawana elimu ya kutosha na hawajui afya zao kwa kuwa hawana utamaduni wa kupima VVU”, amesema Bw. Mathias.

Katika warsha hiyo ya siku mbili inayoendeshwa na UNESCO kwa kushirikiana na UNICEF katika kituo cha Redio cha Nuru FM Iringa, Bw. Mathias amesema kuna umuhimu mkubwa wa kutoa elimu sahihi kwa Vijana ya kujikinga na maambukizi ya VVU na Mimba kutokana na uelewa mdogo wa Vijana katika matumizi sahihi ya Kondomu.

Wakichangia mada kuhusu masuala muhimu yanayowahusu vijana katika maambukizi ya VVU vijana wamesikitishwa na mimba za utotoni kwa wasichana zinazochangia vifo vya Mama na Watoto na wasichana kuacha masomo.

Washiriki wa warsha hiyo wametaka hatua za haraka zichukuliwe kuhakikisha kuwa sheria za mtoto zinazoruhusu mtoto wa kike kuolewa katika umri mdogo zinafanyiwa marekebisho ya haraka kulinda haki ya mtoto wa kike.

Wakijadili mada hiyo washiriki wamesema mila na tamaduni pia zinachangia kwa kiasi kikubwa kumkandamiza mtoto wa kike katika masuala mbalimbali ya maendeleo yake.
Wakitoa mifano ya baadhi ya mila zilizowafanya wapaze sauti kuhusu mabadiliko ya sheria za mtoto ni ile sheria ya ndoa na mila inayoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 kwa ridhaa ya wazazi. Umri huo unakinzana na haki za mtoto kufurahia maisha yake na kupata elimu.

Mifano mingine ya kitamaduni ni pale mwanamume anapochumbia mimba wakati akijua wazi mtoto ana haki zake za msingi za kuishi.

Wamezitaja pia asasi za dini kutoa elimu kwa vijana ili kusaidia hali iliyojitokeza ya wazazi kutokuwa na muda na watoto wao kuwaelimisha kuhusu mabadiliko ya miili na afya zao.
Akitoa mada kuhusu mbinu mbalimbali za kuwezesha majadiliano katika vikundi vya wasikilizaji, Meneja Mawasiliano kutoka Pangani FM, Bw. Abdul Mfuruki amewataka wawezeshaji kutotumia nafasi walizonazo ili kuendesha mjadala wenye tija.

Amesema washauri wa vikundi hawana budi kuweka mizania kutumia busara, kusoma mazingira na kutoingiza imani au itikadi itakayopelekea kuharibu mjadala unaoendeshwa wa kufuatilia vipindi vya SHUGA Redio, kuwa wavumilivu, kusoma na kuheshimu mawazo ya wengine na kutofungamana na upande wowote ili kumweleza mshiriki wa majadiliano kufunguka zaidi.

Bw. Mfuruki amesema vijana wa vikundi vya wasikilizaji kuwaza mambo mengi ni vyema kuwasikiliza kwa uvumilivu, kupata ushauri wa wengi kwa lengo la kufanya maamuzi sahihi bila kulazimishana na vile vile kuwa wabunifu kwa kutumia mbinu mbadala ili kupata habari iliyojificha.


DSC_0184
Mkufunzi wa warsha hiyo Meneja Mawasiliano kutoka Pangani FM, Bw. Abdullah Mfuruki akiwapiga msasa washauri wa Vikundi vya Vijana kwenye warsha ya siku mbili inayoendelea mjini Iringa.


DSC_0139
Mmoja wa washiriki akihoji jambo kwa mkufunzi wakati wa mafunzo hayo.


DSC_0089
Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias akifafanua jambo kwa washiriki.


 DSC_0114

 DSC_0075

 DSC_0091

DSC_0120
Pichani juu na chini ni Washiriki wakijidiliana kwenye vikundi kazi wakati wa warsha hiyo.

 DSC_0124


DSC_0182
Mkufunzi wa warsha hiyo Meneja Mawasiliano kutoka Pangani FM, Bw. Abdullah Mfuruki akitoa mwongozo wa kazi za vikundi kwa staili ya aina yake kwa washiriki wa warsha ya siku mbili katika utekelezaji wa Mradi mpya wa SHUGA Redio.

DSC_0203
Pichani juu na chini washiriki akitolea maelezo ya picha aliyoichora ikimaanisha nini wakati wa warsha hiyo ya siku mbili inayoendelea mjini Iringa.


 DSC_0221










































Advertisement
Evening hands-on course in electronics at the Physics Department, University of Dar es Salaam

Objectives: To enable the participants to design and fabricate electronic gadgets.
To enable participants to organize and run their own workshops in electronics.
Minimum Qualifications: Form four (IV) with interest in Applied electronics.
Mode of delivery: Hands-on, practical, self tailored in modular form.
Module 1: Basic electronics (for all participants) 1 week.
Module 2: Domestics and entertainment (inverters, chargers, power supplies, TV/Video, public address, HiFi systems) 4 weeks (Fee Tshs 200,000.00)
Module 3: Basic Industrial and instrumentation, power control, and switching devices; 4 weeks (Fee Tshs 200,000.00)
Module 4: PC installation procedures, repair and maintenance; 4 weeks (Fee Tshs 300,000.00)
Module 5: Service of office equipment (photocopy, printers and scanners); 4 weeks (Fee Tshs 400,000.00)
.Venue: Physics Department, University of Dar es Salaam
Duration: Five (5) weeks, Two (2) hours each working day (1400-1600) starting from 1st August 2014
Awards: Certificate of Completion of the course.
For further information contact:
Head, Physics Department, University of Dar es Salaam, P. O. Box 35063 Dar es
Salaam. Tel: 0222410258, Email: physics@udsm.ac.tz;
Visit: www.udsm.ac.tz/conas

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.