March 2015



BENKI YA TAIFA YA BIASHARA (NBC) imezindua huduma mpya ya NBC BENKI NILIPO ambapo mteja anaweza kupata huduma zote za kibenki kupitia simu yake ya mkononi, kompyuta mpakato kama kulipia bili na huduma zingine popote pale alipo.
 
Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Maria Alina Kimaryo (katikati), Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala cha benki hiyo, Raymond Mutagahywa (kushoto) na Mshauri wa Bidhaa wa benki hiyo, Canicius Joseph wakizindua huduma mpya  ya NBC Benki Nilipo jijini Dar es Salaam leo. Wateja wa benki hiyo sasa wanaweza kupata huduma za kibenki kwa kutumia program maalum ya NBC katika ‘play store’ hivyo kupata huduma za kibenki kupitia laptop zao, tablets na simu za mkononi za smartphones.
Akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa huduma hizo jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Masoko wa Benki hiyo, Maria Alina Kimaryo alisema kwamba huduma hizo mpya ni rahisi kutumia na kurahisisha shughuli za mteja kwa kupitia simu yake ya mkononi na kompyuta mpakato kwa njia ya intaneti kwa kutoa na kulipa bili zake za luku, dawasco, dstv na huduma zingine.

“Watu wengi wanaangalia ni njia gani rahisi ya kuangalia akaunti zao kwa masaa 24 kwa siku kwa kutizama salio kulipa bili kupitia simu zao za mkononi ili kuweza kuokoa muda na ndipo benki ya NBC ilipoamua kuja na huduma hizi za kipekee nchini ya BENKI NILIPO ili kurahisisha shughuli za biashara na za kijamii nchini,” aliongeza

Aliongeza kwamba huduma hizo mpya zimetengenezwa kwa ajili ya kwenda na wakati wa mazingira ya sasa ya jamii yenye sayansi na  teknolojia ambapo mteja anaweza kufanya shughuli zote za kibenki bila kulazimika kwenda benki au kuwa na akaunti na benki ya NBC,

Kimaryo alisema kwamba ndani ya huduma hiyo mteja anaweza kupata taarifa za akaunti yake, kuhamisha fedha kwenda kwenye akaunti yake mwenyewe na akaunti nyingine za NBC kwa watu wengine na kuendesha akaunti yake akiwa ndani au nje ya nchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala za Kibenki, Raymond Mutagahywa alifafanua kwamba benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora na bunifu kwa ajili ya wateja wao huku wakienda sambamba na maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa kuboresha huduma za kibenki nchini.

Alisema kwamba uzinduzi wa huduma hiyo mpya nchini ni kiashiria tosha kwamba benki hiyo imejipanga kuendelea kutoa huduma na bidhaa bora kabisa za kibenki hapa nchini na kuwarahisishia watanzania kwenye huduma za kibenki nchini.

Mutagahywa aliongeza kwamba kupitia huduma hiyo ya kipekee nchini wateja wa benki hiyo wanaweza kutuma fedha kwa wapendwa wao ambao pia watakuwa hawana akaunti na benki hiyo na wateja wa NBC wanaweza pia kuweka fedha kwenye ATMs mahali popote.



Mshauri wa Bidhaa wa Benki ya NBC, Canisius Joseph (kulia), akionyesha jinsi huduma mpya ya NBC Benki Nilipo inavyofanya kazi wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Meneja Masoko wa NBC, Maria Alina Kimaryo, Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala cha benki hiyo, Raymond Mutagahywa na Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe.

Meneja wa ATM na Kadi wa Benki ya NBC, Wambura John (katikati) akimwonyesha mmoja wa mteja, Nusra John (kulia) jinsi anavyoweza kutoa pesa katika ATM ya benki hiyo bila ya kuwa na kadi kwa kutumia huduma ya NBC Cash Popote katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya NBC Benki Nilipo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Huduma za Jamii wa benki hiyo, Irene Peter.


Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala cha benki hiyo, Raymond Mutagahywa  (Kkushoto), akizungumza wakati  wa uzinduzi wa huduma mpya ya  NBC Benki Nilipo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Meneja Masoko wa NBC, Maria Alina Kimaryo na Mshauri wa Bidhaa wa benki hiyo, Canisius Joseph.


Meneja Mahusino wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto) akiweka mambo sawa katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.

Add caption

Baadhi ya maofisa wa benki hiyo waliohudhuria uzinduzi wa huduma mpya ya NBC Benki Nilipo jijini ar es Salaam le
























Dar es Salaam. Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema, amemsamehe Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye hivi karibuni alimtolea maneno makali kutokana na kutofautiana naye juu ya msimamo wa viongozi wa Kikristo kuhusu Katiba Inayopendekezwa.
“Natumia nafasi hii kueleza juu ya maneno ambayo yalitolewa na mchungaji fulani, sikumbuki anaitwa nani… nasema nimemsamehe kutoka ndani ya moyo wangu wote anaweza kuwa na sababu zake ila nimemsamehe kabisa” Kardinal Pengo
Kardinali Pengo alitoa msamaha huo mbele ya waumini katika Kanisa la St Joseph, Dar es Salaam jana, siku mbili baada ya Askofu Gwajima kuhojiwa na Polisi kwa madai ya kumkashifu kiongozi huyo, mbele ya hadhara.
Askofu Gwajima anadaiwa kutoa kauli za kumkashifu kiongozi huyo kwamba amewasaliti wa viongozi wenzake wa Kikristo kwa kuwataka waumini wa dini hiyo kuamua wenyewe suala la Katiba Inayopendekezwa kinyume na msimamo wa waraka wa kupinga katiba hiyo uliotolewa na Jukwaa la Wakristo Tanzania (CCT).
Baada ya kutolewa kwa waraka huo ulioagiza waumini kuipigia kura ya hapana katiba hiyo, Askofu Pengo alinukuliwa akisema viongozi wa dini hawana mamlaka ya kuzuia wananchi kuikubali Katiba hiyo huku akisisitiza waachiwe uhuru wao wa kuamua.
Akizungumza jana wakati wa ibada ya Jumapili ya Matawi, inayoadhimishwa wiki moja kabla ya Sikukuu ya Pasaka, Kardinali Pengo, bila ya kumtaja jina alisema: “Natumia nafasi hii kueleza juu ya maneno ambayo yalitolewa na mchungaji fulani, sikumbuki anaitwa nani… nasema nimemsamehe kutoka ndani ya moyo wangu wote, anaweza kuwa na sababu zake ila nimemsamehe kabisa.
“Sina ghadhabu wala chuki ila kinyume chake, naomba tumwombee yeye na watu wote waliokuwa wamehusika pengine nyuma yake ili Mungu aweze kutulinda na kutudumisha katika hali ya amani ya Taifa letu.”
Alisema hatua ya Polisi kumkamata ni sehemu ya kutekeleza utaratibu wa jeshi hilo tu, lakini yeye kwa nafsi yake ameshamsamehe.
Atolewa ICU, wafuasi wakamatwa
Katika hatua nyingine, Askofu Gwajima ametolewa kwenye chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) na kuhamishwa katika wodi ya kawaida  baada ya afya yake kuendelea vizuri.
Askofu huyo alikuwa ICU kwenye Hospitali ya TMJ, Mikocheni, alikofikishwa usiku wa Ijumaa baada ya hali yake kubadilika ghafla alipokuwa akihojiwa Kituo Kikuu cha Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Askofu huyo alijisalimisha kituoni hapo akiitikia wito wa polisi uliomtaka kufanya hivyo kutokana na tuhuma za kutoa lugha chafu dhidi ya Kardinali Pengo.
Akizungumza jana, mke wa Askofu huyo, Grace Gwajima alisema baada ya madaktari kumuona anaendelea vizuri, wameamua kumtoa ICU na kumpeleka kwenye wodi ya kawaida.

“Tunamshukuru Mungu sasa hivi anaendelea vizuri tofauti na alivyokuwa jana (juzi) alikuwa hawezi kula chakula na kuongea lakini sasa hivi anaongea na anakula chakula,” alisema na kuongeza:
“Tunashangazwa ni nini kimetokea Polisi wakati akihojiwa. Alitoka nyumbani akiwa mzima na ametolewa polisi akiwa amebebwa hajitambui.”
Mke wa Askofu huyo alisema wakiwa hospitalini hapo usiku wa kuamkia leo, walikuja askari polisi na kuwakamata baadhi ya viongozi na walinzi wa kanisa hilo na kuchukua magari yao.
Akizungumzia suala hilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema inawashikilia na kuwahoji watu 15 ambao wanatuhumiwa kwa makosa ya kula njama pamoja na kujaribu kumtorosha Askofu Gwajima.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Kamanda Kova alisema jana saa 9.30 usiku watu hao 15, katika hali isiyo ya kawaida walifika hospitalini hapo wakidai kwamba walikuwa wanataka kwenda kumuona mgonjwa huyo.
“Askari ambao wapo katika lindo hilo waliwatilia shaka hivyo waliwakatalia kuingia. Kundi hilo la watu 15 lilijaribu kutumia nguvu kuingia katika chumba alicholazwa Askofu Gwajima lakini walikamatwa na kikosi maalumu cha Polisi ambacho kabla ya tukio hilo kilikuwa kinafuatilia mwenendo wa kundi hilo.”
Alisema baada ya kukamatwa, watuhumiwa hao walipekuliwa hapohapo TMJ na kukutwa na begi ambalo lilikuwa na vitu mbalimbali mojawapo vikiwa ni bastola aina ya Berreta ikiwa na risasi tatu, risasi 17 za bunduki aina ya Shortgun, vitabu viwili vya hundi na hati ya kusafiria yenye jina la Gwajima Josephat Mathias.
Alisema baada ya upekuzi kukamilika, watuhumiwa walifikishwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa mahojiano zaidi ikiwa ni pamoja na kupata uhalali wa wao kumiliki silaha hizo na risasi.
“Upelelezi wa shauri hilo unaendelea kwa madhumuni ya kubaini sababu za njama hizo sambamba na kujua mbinu zote zilizotumika kutaka kufanikisha jaribio la kumtorosha Askofu Gwajima.”

Chanzo cha habari na gazeti la kila siku la Mwananchi






















































DSC_0035
Mwanamuziki Lady Jay Dee akitoa burudani na Machozi Band Ijumaa ya tarehe 27 mwezi huu ndani ya kiota chake cha Mog Bar & Restaurant (Nyumbani Lounge) katika show anazofanya mara moja kwa mwezi kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ambapo Ijumaa hiyo alimualika Msanii machachari wa Bongo Flava Ali Kiba kwa ajili ya kukonga nyoyo za mashabiki wake ndani ya kiota hicho.
DSC_0033
DSC_0058
Vijana watanashati wenye vipaji vya aina yake wa Machozi Band wakipiga Back Vocal kumpa sapoti Lady Jay Dee a.k.a Komando Binti Machozi. Kutoka kushoto ni Faraja, Omirady pamoja na Chiqitita.
DSC_0089
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Machozi Band wakimtunza manoti Lady Jay Dee.
DSC_0083
DSC_0078
DSC_0046
Umati wa mashabiki wa Machozi Band wakipata burudani kutoka kwa band hiyo inayoongozwa na Lady Jay Dee.
DSC_0048
DSC_0065
DSC_0066
DSC_0204
Msanii nyota nchini, Ali Kiba akitoa burudani ya aina yake ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant baada ya kutikia mualiko wa msanii mwezake Lady Jay Dee na kufanya Live Music bila kutumia CD na kuwafanya mashabiki kupagawa zaidi.
DSC_0217
Ali Kiba akiendelea kuwaburudisha mashabiki wake Machozi Band.
DSC_0219
Warembo walipagawajem sasa.
DSC_0248
Twende kazi hapo sasa.
DSC_0253
Mrembo akijinafasi kwa Ali Kiba.
DSC_0275
#ChekechaCheketua.......Wadada wakichizika na mauno ya Ali Kiba na style yake mpya.
DSC_0283
Mwanadada hakukubali kabisa na kuamua kupanda jukwaani kulipiza mauno ya Ali Kiba.
DSC_0284
Picha inajieleza jinsi Ali Kiba alivyokonga nyoyo za mashabiki wake.
DSC_0296
Lady Jay Dee: Nimemkuta analia, kajilaza, sababu amechoka.....Mengi amevumilia, yalomkwaza, anataka kuondoka....ana siku ya pili sasa, hajarudi nyumbani kulala,...namuonea huruma sana, haya....mapenzi hayana maana
Lady Jay Dee: who the single girl.....who the single boy, Ali Kiba: i am a single boy.......Ali Kiba: who the single girl, .......Lady Jay Dee: i am a single girl.......Lady Jay Dee: who the single boy, Lady Jay Dee na Ali Kiba:....mi na we single boy.
DSC_0300
Tumefunika mbaya mtu wangu....ndio ishara waliyokuwa wakipeana Ali Kiba na Lady Jay Dee.
DSC_0281
DSC_0256
DSC_0010
Binti mrembo binti kwenye kipaji Faraja wa Machozi Band akiwapa raha mashabiki wa Band hiyo Ijumaa ya mwisho wa mwezi huu ndani kiota cha Mog Bar & Restaurant (Nyumbani Lounge).
DSC_0142
Mkali wa Reggae na Dance Hall nchini Double D akiwarusha mashabiki wake ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant.
DSC_0158
Mkali wa Reggae na Dance Hall nchini Double D katika hisia kali za kuwapa raha mashabiki wake.
DSC_0144
Vijana wakijiachia vilivyo baada ya Reggae za Double D kuwakolea ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant.
DSC_0170
Omirady wa Machozi Band akitoa burudani kwa mashabiki wa Band hiyo katika show inayopigwa mara moja kwa mwezi na kuwateka mashabiki wengi ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant.
DSC_0015
Msanii Chiqitita wa Machozi Band akitoa burudani kwa mashabiki wa band hiyo (hawapo pichani).
DSC_0059
Mashabiki wa machozi band wakipata Ukodak.
DSC_0193
Sehemu ya umati wa mashabiki wa Live Band uliofurika Ijumaa ya mwisho wa mwezi huu ndani ya M.O.G Bar & Restaurant kushuhudia show ya wakali wa muziki nchini Lady Jay Dee na Ali Kiba.
DSC_0001
Hawa jamaa ndio wanaohakikisha Lady Jay Dee anakuwa salama siku zote.

Habari na Picha kwa msaada wa Zainul Mzige

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.