June 2025

Serikali yazindua mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini Nyamongo kwa udhamini wa Barrick

 Na Mwandishi Wetu, Nyamongo,

Serikali imezindua mafunzo ya siku 14 ya kuvijengea uwezo vikundi 48 vya vijana wachimbaji wadogo wa madini kutoka ukanda wa Nyamongo wilayani Tarime, mkoani Mara.

Mafunzo hayo yataanza kesho Juni 21, 2025, chini ya udhamini wa Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara kwa kushirikiana na North Mara Trust Fund.

Vikundi hivyo vyenye wanachama 2,736 vilikabidhiwa leseni 96 za uchimbaji madini bure na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, mwanzoni mwa Mei 2025.

Hafla ya uzinduzi wa mafunzo hayo imefanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Ingwe - Nyamongo leo, mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Chikoka, ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Chikoka (kulia), Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, Francis Uhadi na viongozi wengine wakifurahia uzinduzi wa mafunzo kwa wachimbaji wadago wa madini uliofanyika Nyamongo wilayani Tarime, Mara leo Juni 20, 2025.

Katika hotuba yake, Chikoka amewahimiza vijana hao kuhudhuria mafunzo hayo kikamilifu na kuyazingatia ili yawe muongozo na dira ya shughuli zao cha uchimbaji madini.Sambamba na hayo, amewataka kuepuka migogoro katika vikundi vyao na kutokubali kukatishwa tamaa katika hatua hiyo ambayo aliita safari ya mafanikio.“Kupitia kwenu tunatarajia kuona mabilionea wapya ndani ya Nyamongo. Serikali itakuwa nanyi bega kwa bega, mkiwa na shida pigeni hodi mtafunguliwa na kusikilizwa,” Chikoka amewambia wachimbaji hao.Aidha, ameishukuru Barrick kwa kuridhia kutoa baadhi ya maeneo yake kwa ajili ya wachimbaji hao, akisema hatua hiyo itasaidia kukomesha tatizo la vijana kuvamia mgodi wa North Mara kwa kisingizio cha kukosa maeneo ya kuchimba madini.

 

Sehemu ya wachimbaji wadogo wa madini waliohudhuria uzinduzi wa mafunzo yao.

Kwa upande wake, Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, Francis Uhadi, amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa anazofanya kuboresha sekta ya madini nchini.Uhadi ambaye amemwakilisha Meneja Mkuu wa Mgodi huo, Apolinary Lyambiko, amesema wataendelea kuunga mkono jitihada hizo, na kwamba mafanikio katika mradi huo wa wachimbaji wadogo wa madini yanahitaji ushirikiano kati ya serikali na wadau.

 

Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo, Dkt. Elisante Mshiu, amesema Serikali ya Tanzania inastahili pongezi kubwa kwa kuwa ya kwanza duniani kuanzisha hatua ya kurasimisha wachimbaji wadogo wa madini.Dkt. Mshiu amesema mafunzo hayo yatahusu elimu ya uchimbaji na uchenjuaji madini, biashara, tabia ya fedha, afya na utunzaji wa mazingira, ushirikiano katika vikundi, sheria na miongozo mbalimbali ya uchimbaji madini.

 

Nao baadhi ya wachimbaji wadogo wanaokwenda kunufaika na mafunzo hayo, wakiwemo Dominic Daniel, Bedi Elias, Careen John na Ester Max, wameeleza kupokea hatua hiyo kwa furaha, huku wakiomba hatua zilizobaki ziharakishwe ili waanze uchimbaji. “Tunaishukuru serikali kwa kutuletea mafunzo haya lakini tunaiomba isitucheleweshee hatua zinazofuata ikiwa ni pamoja na kutuonesha maeneo ya kuchimba na kusaidia vitendea kazi vya kisasa,” amesema Ester.

 

Sehemu ya wachimbaji wadogo wa madini waliohudhuria uzinduzi wa mafunzo yao.

Mafunzo hayo yatafanyika kwa makundi na siku tofauti kwenye kumbi za shule za sekondari Bwirege, Ingwe, Nyamongo, Nkenge, Kemambo na Julius Kambarage Nyerere zilizopo tarafa ya Ingwe.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Chikoka (aliyesimama) akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mafunzo hayo.

Picha ya pamoja ya viongozi walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa mafunzo hayo.


Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini (mbele) wakiwakilisha wenzao katika picha ya pamoja na viongozi.


 ...Ambapo Tsh 1.2 trilioni ilikwenda kwa makampuni ya wazawa

...Yawaasa watanzania kuchangamkia fursa migodini

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Kampuni ya Barrick Twiga imethibitisha kwa vitendo utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini kwa kufanya manunuzi Tsh 1.5 trillioni ambapo Tsh 1.2 trilioni 75% ilikwenda kwa makampuni ya watanzania wazawa kupitia kanuni ya maudhui ya ndani (Local Content).

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde akifungua rasmi Jukwaa la nne la utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini.

Akitoa salamu kwa niaba ya wadhamini wa Jukwaa la nne la utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini nchini unaofanyika jijini Mwanza, Mkuu wa Kitengo cha Ugavi wa Barick North Mara, Enock Otieno alisema kwamba kwa ushirikiano wa Wizara ya Madini, Tume ya Madini na wadau wengine wamefanikiwa kutekeleza kwa vitendo kanuni ya maudhui ya ndani (Local Content).

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde akipata maelezo jinsi ya utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Ugavi, Barrick North Mara, Enock Otieno (mwenye miwani) kwenye Jukwaa la nne la utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta hiyo.

“Kwa kushirikiana na Wizara, Tume na wadau wengine tumefanya mikutano, warsha na makongamano kadhaa ili kuhamasisha na kukuza uelewa wa watanzania katika kushiriki kwenye shughuli za uchumi katika sekta ya madini ili kuchochea mabadiliko Chanya ndani ya nchini,” alisema Otieno

Aliongeza kwamba kampuni ya Barrick Twiga kwa kutambua madini ni maisha na utajiri wanatekeleza mradi wa barabara kutoka Kahama hadi kakola kilomita 73 kwa kutoa Tsh 83.36 billioni kwa minajili ya kuboresha miundombinu.

Mgodi wa Barrick North Mara umesisitiza kwamba ipo tayari kupokea na kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini lakini muhimu ziwe na viwango vinavyohitajika,

Otieno alisema kwamba mgodi wa Barrick North Mara una fursa nyingi kwa ajili ya watanzania wazawa ili waweze kushiriki kwenye sekta ya madini.

“tupo tayari kupokea bidhaa zinazotokana na viwanda vya ndani ili umuhimu watanzania wajue mahitaji na ubora wa bidhaa kwa sababu usalama na afya za wafanyakazi ndani migodi ni kipaumbele cha kampuni ya Barrick katika migodi yake hapa nchini,” aliongeza

Otieno alisema kwamba tuna fursa nyingine ni uhitaji wa chuma kwenye mgodi wa Barrick North Mara na hii ni fursa kwa watanzania kuchangamkia kwa sababu pia kuna upatikanaji wa malighafi ya chuma kutoka Liganga.

Afisa Mawasiliano wa kampuni ya Barrick nchini, Neema Ndossi akipokea tuzo na cheti cha udhamini wa Jukwaa la nne la utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini nchini kwa niaba ya kampuni, unaofanyika jijini Mwanza.

Alifafanua kwamba ni muhimu watanzania kuzingatia weledi na kuunganisha nguvu zao ili kuweza kuanzisha viwanda vya chuma kwa sababu mahitaji ya malighafi hiyo migodini ni kubwa mno na fursa ya kipekee kwa watanzania wazawa kuanza kukua katika ukandarasi na huduma za migodini hapa nchini.

“Hii ni fursa ya kipekee kwa watanzania wazawa kuanza kuingia kwenye sekta ya madini kwa sababu fursa zinapatikana mpaka kwenye ya uchongaji miamba kwenye mashimo ya chini bado kuna hitajika bidhaa na mitambo kwa ajili ya shughuli za uchimbaji na cementi ,” alifafanua Otieno.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde akipata maelezo jinsi ya utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Ugavi, Barrick North Mara, Enock Otieno (mwenye miwani) kwenye Jukwaa la nne la utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta hiyo.

Alisema kwamba umuhimu kwa watanzania wazawa kuzingatia ubora wa bidhaa na uendelevu wa usambazaji wa huduma husika ili kuweza kujenga uaminifu na uwezo kwa wakandarasi wa ndani kwenye sekta ya madini hapa nchini.

Naye , Meneja Mahusiano ya Jamii,wa Barrick North Mara, Franscis Uhadi kupitia alisema kwamba kampuni hiyo ya Barrick ambayo inamiliki migodi ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi ambao huo katika hatua za mwisho za ufugaji inaendelea kutekeleza kanuni zote za Maudhui ya Ndani (Local Content) na Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).

“Kampuni ya Barrick inatekeleza kwa vitendo ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini kwa kufanya kazi na makampuni ya wazawa na kuendelea kuwajengea,”

“Jumla ya makampuni ya ndani 706 imefanya kazi na migodi ya barrick na kuna makampuni 603 ni kampuni za wazawa na bado tutaendelea kufanya kazi na makampuni ya kitanzania kama sehemu ya kuwajengea uwezo,” aliongeza

Kwa upande wake, Mgeni rasmi wa Jukwaa hilo la nne la ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini, Waziri wa Madini, ,  Anthony Mavunde  alisema kwamba sekta ya madini imeweza kuchangia 9.0 % ya pato la taifa mwaka jana.

“mafanikio katika sekta ya madini ni makubwa na mpaka sasa ninavyozungumza sekta hii ya madini imechangia Tsh 985 billioni kwenye mfuko mkuu wa serikali haya ni mafanikio makubwa sana kwenye sekta ya madini,” alisema Mavunde.

Aliongeza kwamba serikali ya awamu ya sita chini Dkt Samia Suluhu Hassan ilitoa maelekezo ya kuweka akiba ya dhahabu na ndani ya miezi nane Benki kuu ya Taifa (BOT) ina akiba ya dhahabu ya Tani 5.2.

“Sekta hii ya madini inakua kwa kasi kubwa pamoja na mambo mengine kuna viwanda tisa vinajengwa vya kuchakata na kusafisha dhahabu ili kukuza mnyororo wa dhamani,” aliongeza Waziri Mavunde.

Waziri Mavunde alisema kwamba katika utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini kupitia kanuni ya maudhui ya ndani (Local content) ambapo kuna watanzania 16,874 ambao wameajiriwa kwenye sekta ya madini hapa nchini.

Alifafanua zaidi kwamba ni muhimu watanzania ambao ni watoa huduma wazingatie weledi kwenye kazi ya utaoji huduma migodini (compliance) na kujenga utamaduni wa kushirikiana kwa kushikana mikono ili wafanye kazi kwa ufanisi zaidi.

“ndugu zangu watanzania changamkieni hizi fursa kwenye sekta ya madini kwa kushirikiana na serikali itaendelea kutengeneza mazingira mazuri kwa wazawa kuweza kufanya kazi kwenye migodi na kuwajengewa uwezo pamoja na kuhakikisha kwamba taasisi za fedha zinawakopesha,” alisisitiza

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo alisema kwamba sekta ya madini imeendelea kuchangia mapato ya serikali, kutoa fursa za ajira kwa watanzania kupitia maudhui ya ndani (Local content), kukuza ujuzi kwa wazawa na kuvutia uwekezaji wa ndani na nje.

“Malengo ya sera ya madini 2009 pamoja mambo mengine ila muhimu wa kuifunganisha na sekta zingine za kiuchumi ili kuchochea ukuaji wa sekta zingine na kuchangia maendeleo ya taifa, alisema Mbibo

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Madini na Biashara kutoka Tume ya Madini, CPA, Dkt Venance Kasiki, alisema kwamba watanzania wanayo fursa ya kwenda kwenye mgodi wa Buzwagi ambao upo kwenye hatua za mwisho za ufugaji.

“Hii ni fursa ya kipekee kwa watanzania wazawa kwenda kwenye eneo la Buzwagi ambapo kuna miundombinu bora na ya kisasa kama vile maji, umeme na Barabara kwa ajili ya kufanya uwekezaji,” alisema Dkt CPA Kasiki

Alisema kwamba eneo la mgodi wa Buzwagi watanzania wanaweza kuanzisha viwanda vya bidhaa kwa ajili ya kuhudumia migodi kadhaa ya hapa nchini na kutokana na eneo la Buzwagi ambalo lina Hecta

Alisema kwamba pamoja na mambo mengine eneo la Buzwagi lenye hecta 3365 ambalo ni maalum kama Kongani ya uwekezaji na viwanda (BSEZ) ina fursa ya zaidi ya kujengwa sio tu viwanda vya bidhaa kwa ajili ya migodini hata viwanda vya vipuri kwa ajili ya mitambo ya migodini.

Alisema kwamba hii ni fursa ya kipekee kwa watanzania kuendelea kuunganisha nguvu zao kutokana na miundombinu mizuri na bora kwenye eneo la Buzwagi ni kuharakisha uanzishwaji wa viwanda na kutoa na kutoa bidhaa zenye ubora na viwango.

Dkt CPA Kasiki alisema kwamba Tume hiyo imeendelea kutoa mafunzo na elimu kwenye makampuni, taasisi za elimu mbalimbali na jamii kwa ujumla ili uelewa wa Maudhui ya Ndani (Local Content) ili watanzania wapate uelewa zaidi kuhusu kanuni hiyo.

“Serikali kupitia Tume ya Madini imejikita na ina wataalamu wa kutosha wa kutoa elimu kuhusu Maudhui ya Ndani (Local Content) ili watanzania waweze kupata uelewa na kuingia kwenye sekta ya madini kwa ajili ya kupata kazi za kutoa huduma, ajira na ukandarasi wa shughuli mbalimbali kwenye migodi ambayo ipo hapa nchini,” aliongeza Dkt CPA Kasiki

Aliongea kwamba ni umuhimu kwenye hii ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini moja ya nyenzo muhimu ni ya kuungana (Joint venture) kwa maana ya kutunisha mtaji ili kuweza kupata kazi kwenye migodi iliyopo hapa nchini.

Dkt CPA Kasiki alifafanua kwamba serikali iliamua kuja na kanuni ya Maudhui ya Ndani (Local Content) baada ya kilio cha umma (Public Outcry) kuhusu kwa watanzania hususani jamii inayozunguka migodi kutokunufaika na uwepo wa rasilimali madini.

“Baada ya kilio hicho cha muda mrefu na baadaye kuja kwa sera ya madini ya mwaka 2009 ya kuwawezesha watanzania wazawa kushiriki katika uchimbaji wa madini, kupata kazi za ukandarasi, zabuni na kutoa huduma mbalimbali,” alisema Dkt Kasiki

Dkt CPA Kasiki aliongeza kwamba pamoja na mambo mengine sheria ya madini 2019 na 2022 ili kuja ili kutatua matatizo na kero za ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini ili kupanua wigo na utatuzi wa changamoto hizo.

Aliongeza kwamba fursa za kukuza mnyororo wa thamani kwa watanzania kupitia sekta ya madini ni kubwa na pamoja mambo mengine fursa za kazi kama vile, mitambo ya migodini, Tehama, ujenzi wa viwanda vya kutoa bidhaa kwenye migodi, usafi na ufuaji wa nguo, famasi na tiba na huduma ya chakula. 

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt Janet Lekashigo alitoa wito kwa wadau kuendelea kushiriki kwenye Jukwaa la madini ili kuleta na kuchochea fikra za nafasi ya ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini nchini.

Dkt Lekashigo alisema kwamba jukwaa hilo ni kuchochea fikra mpya na majadiliano ya kitaaluma ili kuweza kusaidia watanzania kushiriki kwenye uchumi wa sekta ya madini.

“Jukwaa hili la nne ni la majadiliano, mawazo na kuleta fikra Chanya ili kuchochea mabadiliko ya ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini ili waweze kunufaika na rasilimali za madini hayo kwenye maeneo yao,” alisema Dkt Lekashigo

Aliongeza kwamba umuhimu wa Jukwaa hilo ni kuja pia na mapendekezo mbalimbali ya namna bora ya kuwawezesha na kufungua milango ya watanzania wazawa kufanya kazi zaidi za ukandarasi na zabuni kwenye migodi hapa nchini.

Dkt Legashiko alisema kwamba Tume hiyo itaendelea kushirikiana na wadau wote kwenye sekta ya madini hususani sekta binafsi kupitia Maudhui ya Ndani (Local content) kuhakikisha dira ya madini ni maisha ni utajiri inakamilishwa kikamilifu kwa kuwashirikisha watanzania wazawa kwenye sekta ya madini nchini.

Mwisho

Na Mwandishi Wetu, Mwanza 

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt Janet Lekashigo ametoa wito kwa wadau kuendelea kushiriki kwenye Jukwaa la madini ili kuleta na kuchochea fikra za nafasi ya ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini nchini.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt Janet Lekashigo akitoa neno la ufunguzi kwenye Jukwaa la nne la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa wattanzania katika sekta ya madini , mkutano huo uliondaliwa na Tume ya Madini nchini, unafanyika kwa siku tatu jijni Mwanza.

Akizungumza kwenye Jukwaa la nne la utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini unaofanyika jijni Mwanza, Dkt Lekashigo alisema kwamba jukwaa hilo ni kuchochea fikra mpya na majadiliano ya kitaaluma ili kuweza kusaidia watanzania kushiriki kwenye uchumi wa sekta ya madini.

“Jukwaa hili la nne ni la majadiliano , mawazo na kuleta fikra Chanya ili kuchochea mabadiliko ya ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini ili waweze kunufaika na rasilimali za madini hayo kwenye maeneo yao,” alisema Dkt Lekashigo 

Aliongeza kwamba umuhimu wa Jukwaa hilo ni kuja pia na mapendekezo mbalimbali ya namna bora ya kuwawezesha na kufungua milango ya watanzania wazawa kufanya kazi zaidi za ukandarasi na zabuni kwenye migodi hapa nchini.

Dkt Legashiko alisema kwamba Tume hiyo itaendelea kushirikiana na wadau wote kwenye sekta ya madini hususani sekta binafsi kupitia Maudhui ya Ndani (Local content) kuhakikisha dira ya madini ni maisha ni utajiri inakamilishwa kikamilifu kwa kuwashirikisha watanzania wazawa kwenye sekta ya madini nchini. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Madini na Biashara kutoka Tume ya Madini, CPA, Dkt Venance Kasiki, alisema kwamba Tume hiyo imeendelea kutoa mafunzo na elimu kwenye makampuni, taasisi  za elimu mbalimbali na jamii kwa ujumla ili uelewa wa Maudhui ya Ndani (Local Content) ili watanzania wapate uelewa zaidi kuhusu kanuni hiyo.

“Serikali kupitia Tume ya Madini imejikita na ina wataalamu wa kutosha wa kutoa elimu kuhusu Maudhui ya Ndani (Local Content) ili watanzania waweze kupata uelewa na kuingia kwenye sekta ya madini kwa ajili ya kupata kazi za kutoa huduma , ajira na ukandarasi wa shughuli mbalimbali kwenye migodi ambayo ipo hapa nchini,” aliongeza Dkt CPA Kasiki 

Alisema kwamba ni umuhimu kwenye hii ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini moja ya nyenzo muhimu ni ya kuungana (Joint venture ) kwa maana ya kutunisha mtaji ili kuweza kupata kazi kwenye migodi iliyopo hapa nchini.

Dkt CPA Kasiki alifafanua kwamba serikali iliamua kuja na kanuni ya Maudhui ya Ndani (Local Content)  baada ya kilio cha umma (Public Outcry) kuhusu kwa watanzania hususani jamii inayozunguka migodi kutokunufaika na uwepo wa rasilimali madini.

“Baada ya kilio hicho cha muda mrefu na baadaye kuja kwa sera ya madini ya mwaka 2009 ya kuwawezesha watanzania wazawa kushiriki katika uchimbaji wa madini , kupata kazi za ukandarasi, zabuni na kutoa huduma mbalimbali,” alisema Dkt Kasiki

Dkt CPA Kasiki aliongeza kwamba pamoja na mambo mengine sheria ya madini 2019 na 2022 ili kuja ili kutatua matatizo na kero za ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini ili kupanua wigo na utatuzi wa changamoto hizo.

Aliongeza kwamba fursa za kukuza mnyororo wa thamani kwa watanzania kupitia sekta ya madini ni kubwa na pamoja mambo mengine fursa za kazi kama vile , mitambo ya migodini , Tehama , ujenzi wa viwanda vya kutoa bidhaa kwenye migodi, usafi na ufuaji wa nguo , famasi na tiba na huduma ya chakula.  

 Mwisho 

Katika mwendelezo wa dhamira yake ya kuendeleza  vipaji na kukuza utafiti nchini, kampuni ya Barrick nchini imekuwa mmoja wa wadhamini wa maadhimisho ya kumi ya wiki ya Utafiti na Uvumbuzi uliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo imetunukiwa cheti cha tuzo kutokana na udhamini huo.

Meneja wa Barrick nchini Dk.Melkiory Ngido akipokea cheti cha udhamini  kwa niaba ya kampuni.

Katika maadhimisho ya mwaka huu Barrick imetoa shilingi milioni 10  kwa mmoja wa washindi katika utafiti Dkt. Juma Mmongoyo, kutoka   Mkwawa University College of Education (MUCE) kwa mradi wake wa utafiti kuhusu “Mbinu za kudhibiti mdudu mharibifu wa nyanya kwa ajili ya ukuaji wa zao la nyanya mkoani Iringa.

Mmoja wa washindi wa utafiti katika maadhimisho haya akipokea hundi ya zawadi kutoka Barrick.

Barrick mbali na udhamini huo imekuwa imekuwa ikidhamini programu mbalimbali za  utafiti ,uvumbuzi,na  inazo programu za mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu na vya kati kwenye migodi yake nchini ya North Mara na Bulyanhulu ambayo inaiendesha kwa ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals pia imekuwa kila mwaka ikifadhili semina za kuwajengea wanafunzi wa vyuo vikuu uwezo kupitia taasisi ya AIESEC Tanzania.

Meneja wa Barrick nchini, Dkt Melkiory Ngido akiuliza swali kutoka kwa vijana wa Chuo Kikuu kuhusu uvumbuzi na utafiti kwenye moja ya mabanda kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwenye maadhimisho ya kumi ya wiki ya utafiti na uvumbuzi ulimalizika jana , kushoto ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia , Profesa peter Msoffe.
Semina za Aiesec zinazoendelea katika vyuo vikuu mbalimbali nchini zinazidi kuwapatia Wanafunzi utambuzi wa kujua fursa zilizopo nchini na jinsi ya kuzitumia kuendeleza maisha yao,kupata ajira, kujiajiiri na kutengeneza fursa za ajira.


Meneja wa Barrick nchini, Dkt Melkiory Ngido akisisitiza jambo kuhusu tafiti na ufumbuzi kwenye maadhimisho ya kumi ya tafiti na ubunifu yalioandaliwa na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kwa viongozi waandamizi wa Wizara ya Elimu   Sayansi na Teknolojia na wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Yatoa kiasi cha shilingi bilioni 93.6...

Na Damas Makangale.

KATIKA kudhihirisha kuwa ubia kati ya kampuni ya Barrick Gold Corporation na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals Corporation unaendelea kunufaisha pande zote mbili,  Migodi ya Barrick nchini imetoa gawio la shilingi bilioni 93.6 kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutunukiwa tuzo ya nafasi ya Kwanza katika makundi ambayo Serikali ina hisa chache kwa mwaka huu.

Hundi ya gawio hilo (Dummy cheque) imekabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt Samia Suluhu Hassan  na Meneja wa Barrick nchini, Dkt  Melkiory Ngido, katika hafla ya Serikali kupokea Gawio na  michango kutoka kwa taasisi na mashirika ya umma (Gawio Day 2025)  iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Barrick  nchini, Dk.Melkiory Ngido akimkabidhi mfano wa hundi shilingi billioni Tsh 93.6  kwa mheshimiwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye hafla ya siku ya gawio iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam, wengine pichani ni Waziri wa Nchini Ofisi ya Rais (Uwekezaji ) Profesa Kitilla Mkumbo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Twiga Andrew Mwangakala .

Mwaka wa fedha wa2022/23 kampuni ya Barrick nchini pia ilishika nafasi ya kwanza kutoa gawio kwa Serikali ya kiasi cha shilingi bilioni 84 ambapo mwaka jana ilishika nafasi ya pili kwa kutoa gawio ya kiasi cha shilingi bilioni bilioni 53,482,072,393.

Migodi iliyopo chini ya kampuni ya Barrick na Twiga Minerals nchini ni North Mara na Bulyanhulu na Buzwagi ambao upo katika mchakato wa kufungwa.

Akiongea juu ya mafanikio haya, Meneja wa Barrick  nchini,Dk.Melkiory Ngido alisema Barrick na Twiga Minerals mbali na kutoa gawio nono kwa Serikali pia imekuwa ikichangia pato la Serikali kupitia malipo ya tozo mbalimbali  katika maeneo yenye shughuli za migodi yake sambamba na kuchangia kukuza uchumi wa Taifa kupitia kodi, ushuru, magawio, mishahara na malipo kwa wazabuni wa ndani .

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania , Dkt Samia Suluhu Hassan akikabidhi tuzo kwa mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Kampuni ya Twiga Minerals , Andrew Mwangakala na Meneja wa Barrick  nchini,Dk.Melkiory Ngido na wa kwanza kushoto ni Waziri wa Nchini Ofisi ya Rais (Uwekezaj ) Profesa Kitilla Mkumbo.

Aliongeza mbali na kutoa gawio la kuchangia pato la Serikali,uwekezaji wa kampuni ya Barrick nchini unaendelea kuboresha maisha ya wananchi kupitia miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yanayozunguka migodi yake kwa fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) zinazotolewa na migodi inayoimiliki ya North Mara na Bulyanhulu.

Kwa upande wake . Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu  akiongea katika hafla hiyo alisema kampuni ya Twiga Minerals imekuwa ikifanya vizuri kwenye sekta ya uchimbaji wa madini nchini kwa kadri siku zinavyozidi kusonga mbele.

Mchechu alisema kwamba kwa mwaka huu serikali imepata Tsh 1.28 Trillioni kama gawio , michango na makusanyo mengineo ambazo zinakwenda kuboresha sekta ya elimu , afya , miundombinu na sekta zingine mtambuka kwenye uchumi wa nchini.

Mwisho 

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.