Staa wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, Thierry Henry, ametangazwa rasmi kuwa balozi mpya wa kimataifa wa kampuni ya michezo ya kubashiri mtandaoni, Betway, wakati huu ambapo ligi kuu za barani Ulaya zinarudi dimbani kwa msimu mpya.
Katika
nafasi yake hiyo mpya, Henry anatarajiwa kuwa kiungo muhimu kati ya mashabiki
wa soka na mchezo wenyewe, kupitia maudhui maalum na mitazamo ya kitaalamu
atakayoshiriki kwa ushirikiano na kampuni hiyo.
Henry
alianza soka lake la kulipwa nchini Ufaransa akiwa na AS Monaco, kabla ya
kujiunga na Juventus kwa kipindi kifupi na kisha kutua Arsenal mwaka 1999,
ambako alijizolea umaarufu mkubwa kwa kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu
hiyo. Aliisaidia Arsenal kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu England (EPL), ikiwemo
msimu wa ‘Invincibles’ mwaka 2003/04, na mataji matatu ya FA Cup.
Katika ngazi ya kimataifa, Henry alikuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa kilichoshinda Kombe la Dunia mwaka 1998, na pia alitwaa taji la Euro 2000. Tangu astaafu soka, amekuwa kocha na mchambuzi maarufu wa soka katika vituo vya runinga mbalimbali.
“Soka
siku zote limekuwa mchezo wa kasi na msisimko, na hayo ndiyo mambo ambayo
Betway huwapatia mashabiki kwa namna ya kipekee,” alisema Henry. “Ninatarajia
kushiriki kwenye kitu kikubwa kinachowaunganisha watu na mchezo wanaoupenda.”
Tangazo
hilo limetolewa wakati ambapo Ligi Kuu England (EPL), La Liga na ligi nyingine
kubwa barani Ulaya zinarejea, kipindi ambacho huwa na ushawishi mkubwa kwa
mashabiki na wadau wa soka duniani kote.
Kwa
mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo, uteuzi wa Henry unaonesha dhamira ya
kuendelea kuwekeza kwenye soka la kimataifa. Betway tayari ni mshirika wa klabu
kadhaa maarufu ikiwemo Arsenal, na inaendesha shughuli zake katika masoko
mbalimbali ya Afrika, Ulaya na Amerika.
Mwisho
Post a Comment