Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda, amempandisha cheo Alphonce Simbu kutoka Sajini kuwa Sajinitaji katika hafla iliyofanyika ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi Upanga Jijini Dar es Salaam leo Septemba 25, 2025 baada ya kupata mafanikio ya Mbio za Marathon Tokyo, Japan.

Jenerali Mkunda amesema ushindi wa Simbu wa kutwaa medali ya dhahabu katika Mashindano ya Mbio za Marathon ya Dunia Kilomita 42, zilizofanyika Toyo Japan ni kwa Watanzania wote na Afrika kwa ujumla na kwamba michezo ni sehemu ya kazi jeshini, hivyo Sajinitaji Alphonce Simbu amefanya kazi nzuri na kuwataka Maafisa na Askari wote jeshini kuiga mfano wa Sajinitaji Simbu.


Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.