1.   ARSENAL

Waliowasili

Yaya Sanogo (Auxerre, huru), Mathieu Flamini (AC Milan, huru), Mesut Ozil (Real Madrid, ada ya Pauni Mil. 42.5), Emiliano Viviano (Palermo, kwa mkopo)

Walioondoka

Gervinho (Roma, ada pauni mil. 8), Vito Mannone (Sunderland, ada Pauni Mil. 2), Martin Angha (Nuremberg, ada haijulikani), Andrey Arshavin (Zenit, Huru), Denilson (Sao Paulo, Huru), Sebastian Squillaci (Bastia, Huru),  Marouane Chamakh (Crystal Palace, Huru), Andre Santos (Flamengo, Huru), Craig Eastmond (Colchester, Huru), Jernade Meade (Swansea, Huru), Sanchez Watt (Colchester, Huru), Conor Henderson (ameachwa), Johan Djourou (Hamburg, kwa mkopo wa msimu mzima), Francis Coquelin (Freiburg, kwa mkopo wa msimu mzima), Joel Campbell (Olympiacos, kwa mkopo wa msimu mzima), Ignasi Miquel (Leicester, kwa mkopo wa msimu mzima), Wellington (Real Murcia, kwa mkopo wa msimu mzima), Chuks Aneke (Crewe, kwa mkopo wa miezi sita)

2.   ASTON VILLA

Waliowasili

Aleksandar Tonev (Lech Poznan ada Pauni Mil.2.5), Jores Okore (Nordsjaelland, ada haijulikani), Leandro Bacuna (Groningen, ada haijulikani), Nicklas Helenius (Aalborg, ada haijulikani), Antonio Luna (Sevilla, ada haijulikani), Jed Steer (Norwich,huru), Libor Kozak (Lazio, ada Pauni Mil.7)

Walioondoka

Jean Makoun (Rennes, ada haijulikani), Richard Dunne (QPR, huru), Eric Lichaj (Nottingham Forest, huru),  Andy Marshall (Millwall, huru), Derrick Williams (Bristol City, huru), Brett Holman (Al Nasr, huru), Darren Bent (Fulham, kwa mkopo wa msimu mzima), Nathan Delfouneso (Blackpool, kwa mkopo wa miezi sita), Samir Carruthers (MK Dons, kwa mkopo wa miezi mitano), Graham Burke (Shrewsbury, kwa mkopo wa miezi mitano), Stiliyan Petrov (ameachwa), Stephen Ireland (Stoke, kwa mkopo wa msimu mzima, Barry Bannan (Crystal Palace, ada haijulikani).

3.   CARDIFF

Waliowasili
Gary Medel (Sevilla, ada ya Pauni Mil. 11), Steven Caulker (Tottenham, ada Mil.9), Andreas Cornelius (FC Copenhagen, ada ya Pauni Mil. 8.5), John Brayford (Derby, ada ya Pauni Mil. 1.5), Simon Moore (Brentford, ada haijulikani), Maximiliano Amondarain (Nacional, ada haijulikani), Kevin Théophile-Catherine (Rennes, ada ya Pauni  Mil. 2.1), Peter Odemwingie (West Brom, ada ya Pauni Mil 2.5).

Walioondoka

Robert Earnshaw (Toronto, huru), Stephen McPhail (ameachwa), Heidar Helguson (huru), Nat Jarvis (ameachwa), Ben Nugent (Brentford, kwa mkopo miezi mitano), Joe Ralls (Yeovil, kwa mkopo miezi mitano).



4.    CHELSEA

Waliowasili

Andre Schurrle (Bayer Leverkusen, ada pauni Mil. 18), Marco van Ginkel (Vitesse Arnhem ada ya Pauni Mil 9), Cristian Cuevas (O'Higgins, ada ya Pauni Mil. 3), Mark Schwarzer (Chelsea, huru), Willian (Anzhi, ada pauni Mil. 32), Samuel Eto'o (Anzhi, huru), Christian Atsu (Porto, ada pauni Mil. 3.5).


Walioondoka

Jeffrey Bruma (PSV,ada Pauni Mil.2.5), Florent Malouda (Trabzonspor, huru), Ross Turnbull (Doncaster, huru), Yossi Benayoun (released), Thibaut Courtois (Atletico Madrid, kwa mkopo wa msimu mzima), Patrick van Aanholt (Vitesse Arnhem, kwa mkopo wa msimu mzima), Oriol Romeu (Valencia, kwa mkopo wa msimu mzima), Cristian Cuevas (Vitesse Arnhem, kwa mkopo wa msimu mzima), Lucas Piazon (Vitesse Arnhem, kwa mkopo), Todd Kane (Blackburn,  kwa mkopo msimu mzima), Marko Marin (Sevilla, kwa mkopo msimu mzima), Gael Kakuta (Vitesse, kwa mkopo msimu mzima), Wallace (Inter Milan, kwa mkopo msimu mzima), Patrick Bamford (MK Dons, mkopo wa miezi mitano), Paulo Ferreira (ameachwa), Christian Atsu (Vitesse Arnhem, kwa mkopo msimu mzima), Victor Moses (Liverpool, kwa mkopo msimu mzima), Romelu Lukaku (Chelsea, kwa mkopo msimu mzima).

5.   CRYSTAL PALACE

Waliowasili

Dwight Gayle (Peterborough, ada Pauni Mil.8.5), Jose Campana (Sevilla, ada Pauni Mil.1.75), Stephen Dobbie (Brighton, ada haijulikani), Jerome Thomas (West Brom, huru), Kevin Phillips (Blackpool, huru), Elliot Grandin (Blackpool, huru), Marouane Chamakh (Arsenal, huru), Florian Marange (Bordeaux, huru), Neil Alexander (Rangers, huru), Jason Puncheon (Southampton, kwa mkopo wa msimu mzima), Jimmy Kebe (Reading, ada haijulikani), Jack Hunt (Huddersfield, ada haijulikani), Adrian Mariappa (Reading, ada haijulikani), Barry Bannan (Aston Villa, ada haijulikani)

Walioondoka
Alex Marrow (Blackburn, ada haijulikani), Andre Moritz (Bolton, huru), Jermaine Easter (Millwall, huru), Jason Banton (MK Dons, kwa mkopo wa miezi mitano), Ryan Inniss (Cheltenham, kwa mkopo wa mwezi mmoja), Peter Ramage (Barnsley, kwa mkopo wa msimu mzima)


6.   EVERTON

Waliowasili

Arouna Kone (Wigan, ada Pauni Mil.5), Joel Robles (Atletico Madrid, ada haijulikani), Antolin Alcaraz (Wigan,huru), Gerard Deulofeu (Barcelona, kwa mkopo wa msimu mzima), James McCarthy (Wigan, ada haijulikani), Romelu Lukaku (Chelsea, kwa mkopo wa msimu mzima), Gareth Barry (Manchester City, kwa mkopo wa msimu mzima)


Walioondoka
Jake Bidwell (Brentford, ada haijulikani), Jan Mucha (Krylia Sovetov,huru), Thomas Hitzlsperger (ameachwa), Conor McAleny (Brentford, kwa mkopo wa msimu mzima), Phil Neville (ameachwa), Marouane Fellaini (Manchester United ada ya Pauni Mil. 27.5), Victor Anichebe (West Brom, pauni mil. 6).


7.   FULHAM

Waliowasili

Sascha Riether (Cologne, ada Pauni Mil.1.3), Derek Boateng (Dnipro, ada haijulikani), Fernando Amorebieta (Athletic Bilbao, huru), Maarten Stekelenburg (Roma, ada haijulikani), Ange-Freddy Plumain (Lens, huru), Adel Taarabt (QPR, kwa mkopo wa msimu mzima), Darren Bent (Aston Villa, kwa mkopo wa misumu mzima), Scott Parker (Tottenham, ada haijulikani)

Walioondoka

Chris Baird (ameacha), Simon Davies (ameachwa) Mahamadou Diarra (ameachwa), Csaba Somogyi (released), Mladen Petric (ameaacha), Mark Schwarzer (Chelsea,huru), Tom Donegan (ameachwa), Alex Smith (Swindon,huru), Dan Burn (Birmingham, mkopo wa msimu mzima), Marcelo Trotta (Brentford, kwa mkopo), Cauley Woodrow (Southend, kwa mkopo).



8.   HULL

Waliowasili

Tom Huddlestone (Tottenham,ada Pauni Mil.5.25), George Boyd (Peterborough,huru), Maynor Figueroa (Wigan, huru), Curtis Davies (Birmingham, ada haijulikani), Ahmed Elmohamady (Sunderland, ada Pauni Mil.2), Allan McGregor (Besiktas,ada Pauni Mil.1.8), Steve Harper (Newcastle, huru), Danny Graham (Sunderland, mkopo kwa msimu mzima), Yannick Sagbo (Evian, ada Pouni Mil.3), Jake Livermore (Tottenham, mkopo kwa msimu mzima)

Walioondoka

Corry Evans (Blackburn, ada Pauni Mil.700,000), Sonny Bradley (Portsmouth, huru), Danny East (Portsmouth,huru), Mark Cullen (Luton,huru), Andy Dawson (Scunthorpe, huru), Jamie Devitt (Chesterfield, huru), Paul McKenna (ameachwa), Seyi Olofinjana (ameachwa), Jay Simpson (ameachwa), Jack Hobbs (Nottingham Forest, mkopo kwa msimu mzima), Tom Cairney (Blackburn, mkopo kwa miezi mitano), Cameron Stewart (Charlton, mkopo kwa msimu mzima).


9.    LIVERPOOL

Waliowasili

Kolo Toure (Manchester City, huru), Luis Alberto (Seville, ada Pouni Mil.6.8), Iago Aspas (Celta Vigo, ada Pauni Mil 7.5), Simon Mignolet (Sunderland, ada Pauni Mil. 9), Aly Cissokho (Valencia, kwa mkopo wa nsimu mzima), Tiago Ilori (Sporting Lisbon, ada haijulikani), Mamadou Sakho (Paris Saint-Germain, ada haijulikani), Victor Moses (Chelsea, kwa mkopo wa msimu mzima).

Walioondoka

Andy Carroll (West Ham ada Pauni Mil.15.5), Danny Wilson (Hearts,huru), Jamie Carragher (ameachwa), Jonjo Shelvey (Swansea,ada Pouni Mil.6), Stewart Downing (West Ham,ada Pouni Mil.6) Jay Spearing (Bolton, ada Pauni Mil.1.4) Suso (Almeria, kwa mkopo wa msimu mzima), Conor Coady (Sheffield United, kwa mkopo wa miezi mitano), Pepe Reina (Napoli, kwa mkopo wa msimu mzima), Jack Robinson (Blackpool, kwa mkopo wa misimu mzima), Oussama Assaidi (Stoke, kwa mkopo wa msimu mzima), Fabio Borini (Sunderland, kwa mkopo wa msimu mzima), Daniel Pacheco (AD Alcorcon, ada haijulikani).

10.               MANCHESTER CITY

Waliowasili

Fernandinho (Shakhtar Donetsk, ada Pouni Mil.30), Jesus Navas (Sevilla, ada Pauni Mil. 15), Alvaro Negredo (Sevilla, ada Pauni Mil. 20.6), Stevan Jovetic (Fiorentina, ada Pauni Mil. 25.8), Martin Demichelis (Atletico Madrid, ada Pauni Mil. 3.5)

Walioondoka
Carlos Tevez (Juventus, ada Pauni Mil. 10), Kolo Toure (Liverpool, huru), Wayne Bridge (Reading, huru), Ryan McGivern (Hibernian, huru), Roque Santa Cruz (Malaga, huru), Karim Rekik (PSV, kwa mkopo wa msimu mzima), Jeremy Helan (Sheffield Wednesday, ada haijulikani), Maicon (Roma, huru), Reece Wabara (Doncaster, kwa mkopo wa mwezi mmoja), Scott Sinclair (West Brom, kwa mkopo wa msimu mzima), Denis Suarez (Barcelona, ada Pauni Mil. 1), Abdul Razak (Anzhi, kwa mkopo wa msimu mzima), Harry Bunn (Sheffield United, kwa mkopo), Gareth Barry (Everton, kwa mkopo wa msimu mzima).

11.               MANCHESTER UNITED

Waliowasili
Guillermo Varela (Penarol, ada ya Pauni Mil.1), Marouane Fellaini (Everton, ada ya Pauni Mil.27.5), Fabio Coentrao (Real Madrid, kwa mkopo)

Walioondoka
Paul Scholes (ameachwa), Scott Wootton (Leeds, ada Pauni Mil. 1), Ryan Tunnicliffe (Ipswich, kwa mkopo wa miezi mitano), Frederic Veseli (Ipswich, huru), John Cofie (Barnsley, huru), Reece Brown (Watford, huru), Sean McGinty (Sheffield United, huru), Nick Powell (Wigan, kwa mkopo wa msimu mzima), Bebe (Pacos de Ferreira, kwa mkopo wa msimu mzima).

12.               NEWCASTLE

Waliowasili

Loic Remy (QPR, kwa mkopo wa msimu mzima), Olivier Kemen (Metz, ada haijulikani)

Walioondoka
James Perch (Wigan, ada ya Pauni Mil. 700,000), Danny Simpson (QPR, huru), Steve Harper (Hull, huru), Shane Ferguson (Birmingham, kwa mkopo wa msimu mzima), James Tavernier (Shrewsbury, kwa mkopo wa mwezi mmoja, Mehdi Abeid (Panathinaikos, kwa mkopo wa msimu mzima, Adam Campbell (Carlisle, kwa mkopo wa miezi mitano)

13.               NORWICH

Waliowasili

Ricky van Wolfswinkel (Sporting Lisbon, ada ya Pauni Mil. 8.6), Javier Garrido (Lazio, ada haijulikani), Nathan Redmond (Birmingham), Martin Olsson (Blackburn, ada haijulikani), Carlo Nash (Stoke, huru), Leroy Fer (FC Twente, ada haijulikani), Gary Hooper (Celtic, ada ya Pauni Mil.5), Johan Elmander (Galatasaray, kwa mkopo wa msimu mzima)

Walioondoka

Grant Holt (Wigan, ada ya Pauni Mil.4), James Vaughan (Huddersfield, ada haijulikani), Leon Barnett (Wigan, ada ya Pauni Mil. 500,000), Jed Steer (Aston Villa, huru), Chris Martin (Derby, huru), Marc Tierney (Bolton, huru), Simeon Jackson (Eintracht Braunschweig, huru), Korey Smith (Oldham, huru), Elliott Ward (Bournemouth, huru), Tom Adeyemi (Birmingham, huru), George Francomb (AFC Wimbledon, huru), Lee Camp (ameachwa), Declan Rudd (Preston, kwa mkopo wa msimu mzima), Andrew Surman (Bournemouth, kwa mkopo wa msimu mzima), Lee Camp (West Brom, kwa mkopo wa msimu mzima)

14.               SOUTHAMPTON 

Waliowasili

Dejan Lovren (Lyon, ada ya Pauni Mil.8.5), Victor Wanyama (Celtic, ada ya Pauni Mil.12), Daniel Osvaldo (Roma, ada ya Pauni Mil.15)

Walioondoka

Vegard Forren (Molde, ada haijajulikani), Frazer Richardson (Middlesbrough, huru), Danny Butterfield (Carlisle, huru), Danny Seaborne (Yeovil, huru), Ryan Dickson (Colchester, huru), Ben Reeves (MK Dons, huru), Sam Hoskins (Yeovil, huru), Richard Chaplow (Millwall, huru), Steve De Ridder (FC Utrecht, huru), Jason Puncheon (Crystal Palace, mkopo wa msimu mzima), Emmanuel Mayuka (Sochaux, kwa mkopo wa msimu mzima).

15. STOKE CITY



Waliowasili
Erik Pieters (PSV, ada ya Pauni Mil. 3), Marc Muniesa (Barcelona, huru), Juan Agueldo (New England Revolution, huru)Oussama Assaidi (Liverpool, kwa mkopo wa msimu mzima), Marko Arnautovic (Werder Bremen, ada ya Pauni Mil.4), Stephen Ireland (Aston Villa, kwa mkopo wa msimu mzima).


Waliondoka
Dean Whitehead (Middlesbrough, huru), Carlo Nash (Norwich, huru), Matthew Upson (Brighton, huru), Rory Delap (Burton, huru), Matthew Lund (Rochdale, huru), Mamady Sidibe (CSKA, huru), Michael Owen (ameachwa), Florent Cuvelier (Sheffield United, ada haijulikani)

16. SUNDERLAND

Waliowasili

Modibo Diakite (Lazio, huru), Duncan Watmore (Altrincham, ada haijulikani), Valentin Roberge (Maritimo, huru), Cabral (Basle, huru), David Moberg Karlsson (IFK Gothenburg, huru), Vito Mannone (Arsenal, ada ya Pauni Mil.2), Jozy Altidore (AZ Alkmaar, ada ya Pauni Mil 6), El Hadji Ba (Le Havre, ada haijulikani), Emanuele Giaccherini (Juventus, ada Pauni Mil. 8.6), Ondrej Celustka (Trabzonspor, kwa mkopo wa msimu mzima), Charis Mavrias (Panathinaikos, ada Pauni Mil. 2.5), Ki Sung-yueng (Swansea, kwa mkopo wa msimu mzima), Fabio Borini (Liverpool, kwa mkopo wa msimu mzima), Andrea Dossena (Napoli, kwa mkopo wa msimu mzima).


Walioondoka

Ahmed Elmohamady (Hull, ada Pauni Mil. 2), James McClean (Wigan, ada Pauni Mil. 2), Titus Bramble (ameachwa), Matthew Kilgallon (Blackburn, huru), Ryan Noble (Burnley, huru), Alfred N'Diaye (Eskisehirspor, kwa mkopo wa msimu mzima), Danny Graham (Hull, kwa mkopo wa msimu mzima), Billy Knott (Wycombe, kwa mkopo wa mwezi mmoja), Stephane Sessegnon (West Brom, ada ya Pauni Mil. 6)

17.               SWANSEA


Waliowasili

Wilfried Bony (Vitesse Arnhem, ada ya Pauni Mil. 12), Jose Canas (Real Betis, huru), Jordi Amat (Espanyol, ada ya Pauni Mil. 2.5), Jonathan De Guzman (Villarreal, kwa mkopo wa msimu mzima), Alejandro Pozuelo (Real Betis, ada Pauni Mil. 425,000), Jonjo Shelvey (Liverpool, ada Pauni Mil. 6), Gregor Zabret (NK Domzale, ada haijulikani), Alex Gogic (Olympiacos, huru), Jernade Meade (Arsenal, huru), Alvaro Vazquez (Getafe, kwa mkopo wa msimu mzima).

Walioondoka

Kemy Agustien (Brighton, huru), Mark Gower (Charlton, huru), David Cornell (St Mirren, kwa mkopo wa msimu mzima), Kyle Bartley (Birmingham, kwa mkopo wa msimu mzima), Alan Tate (Yeovil, kwa mkopo wa miezi mitano), Dwight Tiendalli (ameachwa), Ki Sung-yueng (Sunderland, kwa mkopo wa msimu mzima)

18.               TOTTENHAM

Waliowasili

Paulinho (Corinthians, ada Pauni Mil.17m), Nacer Chadli (FC Twente, ada Pauni Mil.6), Roberto Soldado (Valencia, ada Pauni Mil. 26), Etienne Capoue (Toulouse ada Pauni Mil. 8.6), Vlad Chiriches (Steaua Bucharest ada Pauni Mil. 8.5), Erik Lamela (Roma, ada Pauni Mil. 30), Christian Eriksen (Ajax, ada Pauni Mil. 11.5m)

Walioondoka

Steven Caulker (Cardiff, ada ya Pauni Mil.9), Clint Dempsey (Seattle Sounders, ada haijulikani), Tom Huddlestone (Hull, ada ya Pauni Mil.5.25), William Gallas (ameachwa), John Bostock (Royal Antwerp, huru), David Bentley (ameachwa), Jake Nicholson (ameacha), Jake Livermore (Hull, kwa mkopo wa msimu mzima) Massimo Luongo (Swindon, kwa mkopo wa msimu mzima), Adam Smith (Derby, kwa mkopo wa msimu mziam), Ryan Mason (Swindon, kwa mkopo), Bongani Khumalo (Doncaster, kwa mkopo), Alex Pritchard (Swindon, kwa mkopo), Ryan Mason (Swindon, kwa mkopo wa msimu mzima), Grant Hall (Swindon, kwa mkopo wa msimu mzima), Scott Parker (Fulham,ada haijulikani), Iago Falque (Rayo Vallecano, kwa mkopo wa msimu mzima), Gareth Bale (Real Madrid,ada ya Pauni Mil.86), Benoit Assou-Ekotto (QPR, kwa mkopo wa msimu mzima), Tom Carroll (QPR, kwa mkopo wa msimu mzima)

19.               WEST BROMWICH ALBION


Waliowasili

Diego Lugano (PSG, ada haijulikani), Nicolas Anelka (huru), Matej Vydra (Udinese, kwa mkopo wa msimu mzima), Scott Sinclair (Manchester City, kwa mkopo wa msimu mzima), Goran Popov (Dynamo Kiev, kwa mkopo wa msimu mzima), Morgan Amalfitano (Marseille, kwa mkopo wa mzimu mzima), Stephane Sessegnon (Sunderland ada ya Pauni Mil.6), Victor Anichebe (Everton, ada ya Pauni Mil.6).

Walioondoka

Jerome Thomas (Crystal Palace, huru), Gonzalo Jara (Nottingham Forest,huru), Marc-Antoine Fortune (Wigan, huru), Scott Allan (Birmingham,kwa mkopo wa msimu mzima), James Hurst (Crawley, huru), Lee Camp (huru), Peter Odemwingie (Cardiff, ada ya Pauni Mil.2.5).

20.               WEST HAM


Waliowasili

Andy Carroll (Liverpool, ada ya Pauni Mil. 15.5), Stewart Downing (Liverpool, ada ya Pauni Mil.6), Razvan Rat (Shakhtar Donetsk, huru), Adrian (Real Betis, ada haijulikani), Danny Whitehead (Stockport County, ada haijulikani)

Walioondoka
Rob Hall (Bolton, huru), Carlton Cole (ameachwa), Gary O'Neil (QPR, huru)

An Ivy League-educated marriage counselor who gives marital advice but finds it difficult to address issues with her own marriage. 
 click for larger (if applicable)
Jurnee Smollett plays the central character in the film. Her character is caught between Lance Gross and Robbie Jones. Smollett’s Judith is an Ivy League educated relationship expert who gives marital advice for a living, yet can't seem to follow that advice in her own marriage to Bryce (Gross). Bored with her life, she breaks her professional code and begins an affair with a smooth talking client (Jones). 
 click for larger (if applicable)
After the initial excitement of their torrid relationship wears off, Judith realizes that she's made a grave mistake. It will take every ounce of courage and forgiveness for Judith to escape the dangerous situation she finds herself in.Rounding out the cast are Vanessa Williams in the role of Janice, the owner of the firm where Judith practices, and Kim Kardashian as Ava, Judith’s sassy co-worker. Accomplished singer and actress Brandy Norwood, better known to some as simply Brandy, will play Melinda, Bryce’s co-worker, whose personal life ends up intersecting with Judith’s in an unexpected twist. 

Licha ya harakati mbalimbali za kumkomboa mwanamke, bado kuna mabosi nchini wanawanyanyasa wanawake kwa kuwalazimisha kufanya nao ngono.
Wapo wanaonyanyaswa au hata kuteswa ikiwemo kusemwa maneno machafu au kutishiwa kufukuzwa kazi kwa sababu tu wamekataa kutoa penzi kwa bosi.

Wale wanaokubali, wengine wanaishia kupewa ahadi hewa za kufundishwa magari, kupelekewa kozi mbalimbali. Hata hivyo mbaya zaidi ni kwamba mabosi wengine hata kama wameoa, hupenda kuwamiliki wanawake hao kana kwamba ni wake zao kwa kuwafuatilia sana nyendo zao.

Ukahaba wa mabosi hufanywaje?

Baadhi ya wanaume kwa mwonekano ni vigumu kuamini kama ndiyo wanaofanya vitendo vichafu kwa wafanyakazi wao. Wanaposimama kwenye vikao, utasema mtu huyu, lakini wafanyakazi wa kike wamekuwa ni wenye kuwanyanyasa mno.

Baadhi ya mabosi wamekuwa wakitoa vitisho kuwa ‘kama hunipi penzi nitakuporomosha cheo au hata kukufanyia visa vyovyote hadi uhame’.

Katika baadhi ya ofisi badala ya mabosi kutumika kama washauri wa  wafanyakazi wao kuzipenda ndoa na nyumba zao, ndio wamekuwa wakitumia fedha zao kuwahonga wanawake hata magari, huku makatibu muhtasi wakidaiwa kuwa ndio wanaosumbuliwa zaidi.

Wapo mabosi huwaingia wanawake wakiwemo wake za watu kwa kuwapangia safari za mikoani au nje ya nchi hasa wanapoona hawana wepesi wa kukubaliana na matakwa yao.

“Nakumbuka kuna bosi mmoja katika ofisi moja nyeti aliwahi kudaiwa kumnunulia gari mke wa mtu kabla ya kuhama chombo hicho,” anasema mkazi mmoja wa Kimara.

Bosi aliweza kumpa safari ya nje mwanamke na kisha kumnunulia gari zuri kuliko la mumewe.

Hii ni moja ya kati ya matukio mengi ya mabosi kuwaingiza wafanyakazi wao katika ngono badala ya kuwa ndio washauri wema kwa wafanyakazi ili waweze kuziheshimu ndoa zao.

Sifa zifaazo kwa mabosi
Kwa mujibu wa msomi maarufu katika tansia ya uongozi, Christopher Rocchio wa Marekani, katika chapisho lake la ‘Secret Millionaire’, mabosi wanapaswa kutoa miongozo mizuri ya namna ya kuishi vema ndani na nje ya sehemu za kazi, kwa bahati mbaya, baadhi yao wamekuwa sababu ya kuharibika kwa ndoa za wafanyakazi wao.
 
Wataalamu wengine katika masuala ya uongozi na utawala, Ruth Faulkner katika chapisho lake la “Viridor boss’ na Fernandez, Maria-Elena katika gazeti la Los Angeles Times, mabosi wanaweza kuchangia kuharibu au kujenga ndoa za wafanyakazi wao kutokana na mafundisho au namna wanavyoendesha mambo sehemu za kazi.
 
Je, wewe ni bosi wa namna gani au ofisini kwenu mabosi wenu wakoje? Kila mtu aliyeko kwenye ajira analo jibu lake. Hata hivyo kwa vyovyote inavyokuwa ni suala la msingi kila bosi kutafakari kwamba dhamana aliyonayo si kufanya ngono wala kutongoza wafanyakazi na kuwatisha, bali kushirikiana nao kuongeza mafanikio katika eneo la kazi.
Simulizi ya mmoja wa wanawake  
 
Mwajuma Sabuni (sio jina lake halisi), ni mfanyakazi  katika kiwanda kimoja jijini Dar es Salaam (jina linahifadhiwa) analalamikia unyanyasaji wa kijinsia kutoka kwa wenye vyeo vya juu yao.
 
“Nimefanya kazi katika kiwanda hiki kwa miaka saba sasa. Sisi wafanyakazi wa kike imekuwa ni kawaida kulazimishwa kufanya ngono.Baadhi ya wasimamizi wa vitengo ndio wahusika wakuu wa kulazimisha wapewe ngono, ukiwakataa ajira yako inakuwa hatarini”.
Haya ni baadhi ya mambo mabaya wanayofanyiwa wanawake sehemu za kazi.
 
Baadhi yao hulazimika kujiingiza kwenye ngono zisizo salama kwa sababu tu wanaogopa kuwaambia mabosi wao watumia kinga kwa hofu kwamba itaonekana kama ni kuwadhalilisha kuwa huenda wana Ukimwi. 
 
Katika mkutano wa wadau wa kupambana na ugonjwa wa Ukimwi hivi karibuni jijini Dar es Salaam, wanawake wako kwenye hatari zaidi ya kuathirika na ugonjwa huo kwa sababu baadhi ya hao mabosi hawatumii kinga na huwa hawako tayari kupima, kwa bahati mbaya zaidi wale wanaofanya nao baadhi yao huogopa kuhoji chochote hivyo mabosi hufanya watakavyo ikiwemo kutotumia kinga.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi nchini (Tacaids), Dk Fatma Mrisho anasema, “Hatari ya wanawake  kuathirika na Ukimwi ni kubwa mno. Pia ni changamoto kubwa inayohitaji jitihada za kila mmoja wetu.”
Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta), Hezron Kaaya anapendekeza mifuko ya hifadhi ya jamii kuanzisha mfuko wa kuwasaidia wanawake na wasichana.
Mkurugenzi wa Sera na Utetezi wa Chama cha Waajiri nchini (ATE), Justina Lyela ambaye amewataka waajiri nchini kuepuka kuwapunja wafanyakazi wa kike ukilinganisha na wanaume ili kuwawezesha kiuchumi.
Tamwa na unyanyasaji
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake  (Tamwa), katika moja ya mpango mkakati wake wa miaka mitano 2010-2014, pamoja na mambo mengine kimepanga kufanya shughuli ambazo zitaimarisha elimu kwa mtoto wa kike kwa kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia.
 
Unyanyasaji wa kijinsia
 
Unyanyasaji wa kijinsia ni tendo baya kwa haki za binadamu na linasababisha maumivu kwa wahusika. Vilevile, linahusisha kumlazimisha mtu kufanya nae mapenzi bila ridhaa yake. Lakini kufanya mapenzi na watu kama baba, mama, kaka, dada, babu au bibi ni aina nyingine ya unyanyasaji wa jinsia.
 
Unyanyasaji wa kijinsia ni kosa la jinai. Unyanyasaji huo ni pamoja na kutumia maneno kwa mfano baadhi ya mabosi huwatishia wafanyakazi wa kike kwamba wasipokubali kufanya nao ngono watawafukuza kazi.
 
Unyanyasaji sio unahusisha sauti, ishara au maonyesho ya sehemu za mwili kwa makusudi kinyume na matakwa ya mtu, kwamba kwa mfano mtu anaweza kukuonyesha sehemu za siri au kukuvamia kwa kugusa sehemu zako za siri kama njia ya kukushawishi mfanye ngono.
Kanuni za adhabu (sura ya 16) kama zilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, zipo wazi kwamba hakuna mtu anayeruhusiwa kujamiiana na mtu mwingine bila ya ridhaa yakeÖ.anayefanya hivi maana yake ni sawa na  ubakaji.
 
Ni kosa kupigwa busu bila ridhaa
Sheria ziko wazi kuwa hakuna mtu anayeruhusiwa kushika viungo vya siri vya uzazi, au kukupiga busu bila ya ridhaa ya mhusika.
 
Hivi karibuni, Tamwa  ilizindua ripoti ya utafiti wa unyanyasaji wa kijinsia uliofanyika Aprili mwaka huu katika wilaya 10 za Tanzania Bara na Zanzibar.
 
Mkurugenzi wake, Valery Msoka anasema  waafiti waliwahoji watu mbalimbali katika ngazi za familia na kupata ukweli wa hali halisi ya unyanyasaji wa kijinsia.
 
W i l a y a zilizofanyiwa utafiti ni Wete (Pemba Kaskazini),  Mjini Magharibi (Unguja Magharibi), Unguja Kusini,  Kisarawe (Pwani), Newala (Mtwara), Mvomero (Morogoro),  Lindi vijijini na Ruangwa (Lindi), Kinondoni na Ilala, Dar es Salaam.
 
Kwa mujibu wa Tamwa matendo haya ya unyanyasaji wa kijinsia kwa ujumla yameshamiri nchini, na  kwamba zaidi ya asilimia 39 ya wanawake nchini wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili.
 
Watuhumiwa wa unyanyasaji huu kwa kiwango kikubwa ni wanaume, huku sheria zikionekana kushindwa kuchukua mkondo wake ipasavyo.
 
Mfano halisi ni ripoti ya Polisi Zanzibar, ambayo inasema  katika mwaka 2011, yalikuwapo matukio 268 ya unyanyasaji yaliyoripotiwa, kesi zilizofikishwa mahakamani ni 55, hata hivyo ni kesi moja ndiyo iliyomtia mtuhumiwa hatiani.
 
Je, nini kifanyike kuepusha mateso wanayofanyiwa wanawake maofisini? Ni changamoto ambayo inapaswa kuendelea kufanyiwa kazi ili kuepusha mabosi viwembe wanaoendelea kuwanyanyasa wanawake wakitumia madaraka yao.
 
Waziri Sophia Simba wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, ametaka kuwepo usawa wa fursa kama vile elimu na rasilimali za uchumi hasa kwa wanawake.
Waziri Simba anaamini kwamba kwa jitihada ambazo Serikali inaendelea nazo nchini, tatizo la unyanyasaji wa kijinsia litaendelea kupungua.
 
Baadhi ya mikakati hiyo ni pamoja na uwepo wa sheria mbalimbali ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaonekana kushawishi watu kujali haki za kijinsia.

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.