Articles by "Siasa"

Showing posts with label Siasa. Show all posts


Na Mwandishi Wetu 

Lazima tukubali tukatae, kilichomtokea Zitto jana, kufukuzwa CHADEMA, it is a shock kwa wengi, ila wale makini wachache na yeye mwenyewe akiwemo, walijua fika kuwa kuna siku hii siku ingefika!.
Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge la Tanzania, ya Kamati ya Mashirika ya Umma (PAC) Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe

Tangu Zitto Zuberi Kabwe (ZZK) alipotangaza wazi nia yake ya kugombea urais wa 2015 kupitia Chadema, nimenote humu jf, watu wanatetemeke, kuweweseka na hata kutishika eti ZZK ni mamluki na kitendo cha kuitangaza nia hiyo, kuna lengo la kukisambaratisha Chadema!. 

Maudhui ya mada hii ni kuwachambau makundi 10 yanayomsupport au kumpinga ZZK na uamuzi wake huu. Naomba nikiri, kichocheo kilichonifanya kuanzisha uzi huu ni mada ya Mchambuzi ...

Kwa kuanzia, naomba kwanza ku declare my interest!. Namsupport ZZK kuonyesha nia na sio kutangaza rasmi nia hiyo!.

Tofauti ya kuonyesha nia mapema na kutangaza rasmi nia mapema ni hizi zifuatazo!.

Kuonyesha nia: Kubehave ki "presidential hopeful" ili kujenga nia "will" utakayoitumia kama "power" ili kukipata unachokitaka. (Where there is a will, there is a way!"). Faida ya kuonyesha nia mapema ni kukipa chama na sisi wananchi fursa ya kukupima ili muda muafaka ukifika, Chama ndicho kikushauri kijana chukua fomu gombea, unaonekana unatufaa.

Kutangaza rasmi nia: Ni kitendo cha kujitangaza rasmi nia kuwa mtu utagombea urais wa Tanzania mwaka 2015. Kwa utaratibu wa sasa, mtu huwezi kutangaza utagombea urais, ten a ukatangaza wazi mchana kweupe kwenye kadamnasi ya watu!,
kwa sababu, wagombea ni wa vyama!. ZZK hakupaswa kutangaza wazi ki vile, this was a mistake, mimi ZZK ni rafiki yangu, na pia nimeshamwambia maoni yangu kwenye hili. Kwa jinsi alivyotangaza is as if alishafikia uamuzi hivyo kutishia kuwa Chadema isipomsimamisha yeye, patachimbika!. Hili nimelieza wazi katika mada yangu ya Urais wa ZZK 2015: Ngoma Ikivuma Sana....

Baada ya kutoa utangulizi huo, sasa naomba nije kwenye hoja yangu haya makundi 10 ya watu wanao muunga mkono ZZK na wanaompinga ZZK wako wenye busara, wako waoga, wako wadini, wako wa wakabila, wako wa ukanda, wako wanafiki, wako waumini, wakowafuasi, wako washabiki, wako wakweli.

Waoga; Hili ni kundi la kwanza na ndilo kundi kubwa, hawa wanampinga ZZK kwa uoga tuu usio na sababu zozote za msingi. Hawa ni wale waliozoea mazoea, hivyo hiogopa mabadiliko yoyote yawe positive au negative, kwao ni uoga tuu!. Kwa vile ZZK ni mwana Chadema, na mwana chama yoyote anayo haki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama na ndani ya nchi. 

ZZK ameitumia haki hiyo kuelezea nia yake bila kuvunja sheria, tararibu wala kanununi yoyote ya chama. Natoa mwito kwenu nyie enyi waoga, open up be ready for changes for the better!. Ukombozi wa nchi hii utaletwa na wele tuu wenye kukubali mabadiliko na sio ving'ang'anizi!.

Wadini;Kama ilivyo kwa Tanzania, nchi kama nchi haina dini, ila watu wake wa na dini zao!. Wadini ni wale ambao, wanajiona dini zao ni bora zaidi ya dini za wengine, hivyo yoyof refence hivyo huweza kuteau mtu yoyote kutoka positio yoyote na kumgeuza kuwa ni mtu wa top office bila reference yoyote. 

Wale wanaotaza ma kwa jicho la udini, wakijuiliza kwa nini fulani kapewa nafasi fulani kwa sifa zipi na vigezo vipi, wakifikosa na kuja kuangalia dini ya mhusika, basi watamlebo JK ni mdini, hata kama bte asiye dini yao, wao wanamuona huyo sio!.
JK ni Muislamu, appointment powers zake hazina any terms baadhi ya wateule hawa wanaso sifa na wangestahili nafasi his regardless wao ni dini gani!

Ndio maana kwa baadhi ya teuzi za JK tukubali tukatae anatea as he pleases lakini kwa wengine, dini ni kigezo!. Chadema nacho kama chama hakina dini, ila wanachama, wafuasi wake na washabiki wake wote wana dini zao. Kwa hao wadini wa Chadema kwao,nafasi za juu kabisa za uongozi wa Chadema, lazima zishikwe na watu wa dini fulani!, ZZK alipogombea uenyekiti kiliwaka na mwenyewe akanywea!

Uchaguzi unakuja tena na this time tutamchagiza Prof. Safari kugombea Uenyekiti, nashauri subirini muone kitakachotokea!. `Vivyo hizo wako wanaompinga ZZK kwa dini yake, hawa watampinga Mkandara, Watampinga Arfi na Watampinga Prof. Safari kugombea top position yoyote kwa sababu tuu ya dini zao.

Hawa wapo, tukubali tukatae!. Dawa yao hawa sio kuwabadilisha, bali kuyalazimisha mabadiliko, ili hayo mabadiliko ndiyo yawabadilishe na huo udini wao uwawashe kama koti la chawa na kujikuta wanalazimika kulivua!

Wakabila; Hili nalo ni kama lile la udini, Tanzania kama nchi, haina kabila, ila wananchi wake makabila yao, viongozi nao wana makabila yao. Ukabila ni ile hali ya kuona mtu wa kabila lako ndio bora zaidi. 

Enzi za Nyerere, kwa vile alitoka Musoma, watu wa Musoma, wakajikuta wana upper hand Ikulu na kwenye Majeshi ndio maana tuliwashuhudia kina Musuguri, Mwita Marwa, Waitara etc, huku kule Ikulu kina Apiyo etc. Waziri fulani akiwa wizara fulani, inatokea wengi wa wakuu wa taasisi za wizara hiyo ni kabila lake!.
Hata JK baada ya kuingia ikulu, wako watu fulani wa kabila lake, ndugu au jamaa zake, wamefika hapo walipo kwa kubebwa tuu!, tena angalau wengine baada ya kubebwa, "ukibebwa bebeka" wamebebeka na ku perform!. Wako waliobebwa, lakini hawabebeki, they are non performers kabisa, lakini wanaendelea kuwepo tuu na sana sana ni kuhamishwa tuu huku wakiendelea ama kuto perform, au kuborongo ila wapo!. Chadema nacho kama chama, hakina kabila, ila wanachama na viongozi wake wana makabila yao!. Hakuna asiyejua kuwa kuna viongozi wenu wakuu wamefikaje hapo walipo!.
Hakuna asiyejua kuna mtu yuko bungeni na bintiye na mkwewe kwa sababu tuu ya kabila na nasaba!. Sasa kuna wanaompinga ZZK kwa sababu tuu ya kabila lake!. Wangwe alipotamka kugombea uenyekiti, kilichofuatia sote tunakijua!

Chadema ni chama cha kitaifa, kiko over and above ukabila, hivyo tutahakikisha nafasi za juu za uomgozi, zinashikwa na wenye sifa regardless ni wa makabila gani, ndio maana nitamchagiza tena ZZK agombeaa sio tuu urais, bali aanzie Uenyekiti wa Chadema ambao unautangulia urais na hauna kizingiti cha umri!

Na kuna ukabila mbaya kabisa usiotamkwa wazi, lakini umo mioyoni mwa wenye ukabila,"eti watu wa makabila fulani fulani, kamwe hawawezi kushika urais wa nchi hii!". Tutaukomesha!

Ukanda; Huu ni kama ulivyo udini, na ukabila, Tanzania kama nchi, haina kanda fulani ambazo ni preferencial, maeneo yote ni sawa mbele ya taifa!. Ila lazima tukubali, tukatae, kuna maeneo fulani, watu wake wameneemeka zaidi kuliko maeneo mengine!.
Sasa kuna baadhi ya watu wa maeneo haya yaliyoneemeka, hujiona wao ni bora zaidi kuloko watu wa maeneo mengine, hivyo kufikia stage ya kujiona wao wanastahili preferential treatment kwenye kila kitu, hali inayopelekea wale watu wa maeneo ambayo hayajaneemeka sana, kujiona wako sidelined au marginalized!.
Ili kujionyesha na wao wapo, ndio hivi sasa wanajitutumua!. Hakuna ubishi Kaskazini kuna neema kuliko kwingine kote!. Chadema nayo ime gain stronger momentum maeneo kuliko maeneo mengine ambayo its gaining now!

Hili limewapelekea baadhi ya manazi kujidhania nafasi fulani za uongozi its their rightful kutokana na kanda yao!, ndio maana utasikia safari hii rais lazima atoke kanda fulani!. Kwa vile ZZK hatoka Kaskazini, kuna wanaompinga kwa hilo tuu na hawa wakanda, hata akiibuka Prof. Mwesiga Baregu au Prof. Safari ambao wanazo sifa zote kugombea uenyekiti au urais, nao watapingwa tuu!

Ili kuiondoa hii dhana potofu ya ukanda, tunataka kushuhudia nafasi za juu zikishikwa na watu wenye sifa, regarless wanatoka kanda gani sambamba na haki za kugombea, na hata ikitokea top positions zote zikashikwa na watu wa kabila moja kanda moja, lakini watakuwa wamezipata kwa merits za sifa na uwezo, na sio kwa ukanda na ukabila wao!

Wanafiki; Hawa ni watu wanaujua uwezo wa kiukweli wa ZZK kma rais na amiri jeshi mkuu, lakini kwa sababu, wamezoe kujikomba komba kwa watu wao, wanajifanya kumpinga tuu ili wasionekane watovu wa nidhamu!

Vivyo hivyo kwa wanamsupport ZZK, kuna wale wanaomsupport na kumchagiza ili kuona Chadema inasambaratika. Wengi wa hawa hawana nia ya dhati ya mageuzi, bali wanataka ZZK apunguze kitisho cha lanss;ide victory ya Chadema come 2015 (if it will change!).

Washabiki; Miongoni mwa wanaomsupport ZZK, wako wanaomsupport au kumpinga kwa ushabiki tuu, kama walivyo mashabiki wa simba na yanga. Hata ZZK aboronge vipi, wao kama mashabiki, watamchagiza tuu na kumshagilia mpaka mwisho. 

Na kwa wasio mashabiki, hata afanye mema vipi hawa watambeza tuu. Uzuri wa ushabiki ni mapenzi tuu na sometimes hauna sababu zozote za msingi za kupenda au kuchukia!. Mfano kuna wanaoipenda yanga kwa sababu fulani na kuna wanaipenda yanga kwa bila sababu yoyote!.

Kuna mashabiki wa Yanga ambao wao hawaimaind Simba lakini kuna mashabiki wa yanga wanaichukia Simba bila sababu yoyote!. 

Mfano mimi siipendi kabisa rangi yoyote ya kijani na manjano!, kitu chochote chenye kijani na manjano kinanichefua, hivyo kujikuta naichukia Yanga kwa sababu tuu ya rangi hizo, kama yanga wangebadili rangi na kuwa blue na nyeupe, nisinge ichukia Yanga!. Vivyo hivyo ZZK ana washabiki wake na wengine wana mashabiki wao wengine, hivyo kuna wanaimpinga ZZK kwa ushabiki tuu lakini hawana hoja zozote valid ni kwa nini ZZK or why not ZZK!.

Waumini; Waumini ni stage ya juu zaidi ya washabiki, hawa wana muaminia na kumkubali. Kuna watu wanamuaminia ZZK na kumkubali hivyo kumuunga mkono!.
Katika kumuaminia na kumkubali, pia kuna watu wana waaminia na kuwakubali wengine wote wenye uwezo wa urais. Miongoni mwa waumini hawa, wale ambao wanawaaminia wengine ambao sio ZZK, watampinga ZZK kwa uwezo wao wote na hiyo upinzani wao ni justified kwa wanachokiamimni.

Wafuasi; Hawa ni zaidi ya washabiki na waumini, hawa ni followers wa ZZK ambao watamfuata popote atakapokuwepo ndipo nao watakuwepo. Followers mwanzo walikuwa washabiki, waka graduate na kuwa waamini, waka pata masters kwa kumfuata na kujiunga Chadema. 

Kwao hawa ZZK ndio everything!. Sambamba na hao, pia figures nyingine za Chadema, nao wanao wale wanaowafuatilia, hawa ambao sio wafuasi wa ZZK, hawa kwa vyovyote vile, watampinga ZZK au mwingine yoyote atakayejitokeza.

Huu ufuasi ukivuka mipaka unageuka kuabudu!. Wako wafuasi wanao waabudu wale viongozi wao na kuwaona kama miungu!. Sasa ikitokea mtu akajitokeza kuwapinga hawa miungu watu ndani ya Chadema, mtu huyo atachukiwa na kubatizwa kila aina ya jina "katumwa", "msaliti", "pandikizi" etc, etc!. Baada ya uchaguzi wa 2010, kuna watu waliaminishwa mgombea wa Chadema alishinda, NEC wakauchakachua ushindi ule na kumtangaza mgombea wa CCM!.
Sasa wengi wa hawa mashabiki, waumini na wafuasi, wanaamini na waabudu, tayari wanaye mgombea wao kwa 2015 na sio ZZK!, kitendo cha ZZK kutangaza nia, kimawatetemesha, wanatishika na kuweweseka humu jukwaani kila kukicha!. Mimi nilibahatika kuzungumza off-the record na mgombea fulani hivyo naujua msimamo wake, ndio maana nikawashauri.
Wenye Busara: Hawa ni wale ambao wanazo akili za kiutu uzima, hawa wanaelewa ushindi wowote, hupatikana kwa team work na sio individual ambitions za kuitwa rais!. Hawa wanapiga mwenendo wa ZZK kutangaza kugombea kwa sababu baadhi ya matamshi na maamuzi ya ZZK, yanaongozwa na feelings, emotions na ego, sio kwa critical thinking na tafakuri makini, hivyo huwa ni maamuzi ya papara na yasiyo na tija yoyote kwa mustakabali wa Chadema.

Hawa wanampinga ZZK bila chuki, wanaamini ni ujana na utoto, akikua atatulia. Wengi katika kundi hili ni ma great thinkers, ZZK kama ana masikio, atakuwa amewasikia!.

Wakweli;Hili ndilo kundi la mwisho na lina watu wachache. Hawa ni wale ambao wanampinga ZZK kwa sababu za ukweli au wanamsupport ZZK kwa sababu za ukweli. Ukweli daima huwa ni mchungu, ukweli huwa unauma, ukiwa mkweli daima utachukiwa na sometimes you may pay the price!.
Sometimes ukiwe mkweli mno, hili ni kosa kwa siasa zetu zilizogubikwa unafiki, majungu, fitna na mambo kibao ya kiajabu ajabu!. Kosa kubwa la ZZK ni kuwa mkweli daima!.
Mimi pia niko kwenye kundi hili, nafahamu kwa sasa ZZK ndie mtaji mkubwa zaidi Chadema kuliko mtu mwingine yoyote!. Nahisi hata ushindi wa wale vijana wa Kigoma, he has a hand!. Yako mambo mengi huwa ninayaandika humu, huwa naishia kupingwa!. Sifa kuu ya ukweli siku zote husimama!.

Kwa vile Chadema wamejipanga kushinda 2015, ziko hoja ambazo ni za ukweli na lazima Chadema wasimame nazo ikiwemo ya kutompuuza ZZK hata kidogo na kuendelea kumwacha akipayuka payuka, he needs to be contained more kuliko hivi alivyo let loose!. Chadema ndiyo inayomuhitaji zaidi ZZK kuliko ZZK anavyoihitaji Chadema!.

2015 inakuja, kuna vyama vinajipanga kuchukua nchi huku vingine vinajipanga kutetea viti vyao. Katika kutimiza azma hiyo, viko vyama vinajipanga kimipango mkakati huku vikieleza vitafanya nini, na kuna vyama vinaendeleza mahubiri, kucheza makida makida na kuchezea shilingi chooni!. 

Siku ya siku ikifika, hatutaki watu waje kutulilia tena humu as if hawakuambiwa!. ZZK ametangaza tuu nia, msitetemeke, msiweweseke wala msitishike, just do the right thing and and in doing that right thing, make sure you do it

Makala ni kwa msaada wa Jamii Forums

Mwisho.

















Uganda President Yoweri Museveni sgns a paper
Mmoja wa Marais toka katika ukanda wa Afrika Mashariki waliokaa madarakani kwa kipindi kirefu, Yoweri Kaguta Museveni amekaa madarakani takribani miaka 28
Habari  kubwa hivi sasa barani Afrika ni mapinduzi ya umma yaliyofanyika Burkinafaso, makala haya ni mtazamo wangu kuhusu kitakachojiri kusini mwa jangwa la sahara kuelekea 2030, mtazamo huu umejikita katika kutathimini matukio yanayoendelea kusini mwa jangwa la sahara na hali ya kisiasa kwa ujumla, fuatana nami katika maandishi haya ya kusisimua;

Kusini mwa jangwa la Afrika si salama

Dalili za wazi zinaonyesha kuwa nchi nyingi za kusini  mwa jangwa la Sahara zipo katika hali mbaya zaidi ya nchi za kiarabu zilizopinduliwa kama Misri na Tunisia , halikadhalika kwenye mataifa hayo ya kusini mwa jangwa la sahara kuna ukosefu mkubwa zaidi wa ajira hivyo kufanya idadi kubwa ya vijana kuwa wazururaji kuliko Burkinafaso ambayo imepinduliwa hivi karibuni. Sasa ikiwa hali iko hivi kwanini viongozi wa mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara hawachukui tahadhari?


Kwanini wanazidi kujisahau?

Viongozi wengi wa kusini mwa jangwa la sahara wanategemea kuudhibiti upinzani kwa msaada wa vyombo vya dola mfano mzuri ni hujuma kubwa dhidi ya viongozi wa upinzani kwenye baadhi ya mataifa yanayounda jumuiya ya Afrika Mashariki. Tatizo kubwa la marais hawa nikule kudhani kuwa vyombo vya dola vinaweza kuudhibiti umma, wanapaswa kujifunza kwa makini maana halisi ya nguvu za umma na athari zake kwa muktadha wa siasa za taifa lolote ulimwenguni, yatosha kuzingatia kuwa umma haujawahi kushindwa.

Vyama vingi tawala vitakataliwa

Kutokana na kushindwa kutimiza wajibu wake kwa wananchi vyama vingi tawala vitakataliwa katika mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara. Kuanzia miaka ya 1990 vuguvugu la vyama vya upinzani limeweza kuving’oa vyama tawala kadha wa kadha mifano ya UNIP Zambia, KANU Kenya na PDS Senegal hapa pia usisahau kuangushwa kwa chama cha UMD cha Fredrick Chiluba huko Zambia kilipopoteza kwa Michael Satta wa PF.

Angukohili la vyama tawala halikwepeki hasa kwa kuzingatia udhaifu wa vyama hivyo katika kushughulikia shida za wanyonge ikiwamo bei za mazao, ajira na kupanda kwa gharama za maisha, utegemezi mkubwa wa nchi za kiafrika kwa wawekezaji kutoka nje ,uwekezaji ambao umeshindwa kuondoa umasikini una kila dalili mbaya kwa vyama vya ANC Afrika Kusini, FRELIMO Msumbiji na CCM Tanzania, kuelekea 2030 vyma hivi vimezidi kupunguza idadi ya kura huku upinzani ukizidi kushika kasi kwenye nchi zao.

Marais ving’ang’anizi watang’olewa kabla ya 2030

Mwanahistoria Jovitus Mwijage katika kitabu chake “Major Events in African History” akielezea  kushindwa kwa viongozi wengi waliotwaa madaraka kwa njia za mapinduzi mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzano mwa miaka ya 1990 , katika ukurasa wa 308 anasema “Under the auspices of the constitutions made by them (African dictators), the ballots could not change the existing leadership; therefore, the barrel of the gun eventually became answer to those political puzzles. Even the constitutions made after the coups could not attend to the interests
of the masses.The leaders of the coups made the constitutions, which were to ensure that their evil interests were fulfilled. Such constitutions appeared in Uganda, Sudan, Angola, Congo, Zimbabwe, Gabon, Togo and Rwanda”.

Hali hii ya viongozi kadhaa wa kiafrika ambao awali walionekana kuwa wawakilishi wa kweli wa wananchi lakini polepole wakazivunja miguu katika za nchi zao ili waendelee kutawala hivyo kugeuka ving’ang’anizini sababu nyingine itakayopelekea mapinduzi kwa nchi hizo. Iwe ni mapinduzi ya umma ama vinginevyo lakini marais ng’ang’anizi kama Yoweri Museveni wa Uganda na mwenzake Paul Kagame wa Rwanda wamekalia kuti kavu kwani wananchi hawataki ufalme ama usultani bali wanataka demokrasia inayozingatia ukomo wa madaraka. Ikiwa
watawala wa mataifa haya wataendelea kukaa madarakani basi joto kisiasa halitawaacha salama, wimbi la mabadiliko litawafagia mmoja baada ya mwingine kuelekea 2030.


Nova Kambota ni mchambuzi na mwandishi wa siasa, hii ni sehemu ya maoni yake ya hivi karibuni kuhusu mapinduzi ya umma na mwelekeo wa siasa katika mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara.
Nova Kambota anapatikana jijini Dar es salaam, simu +255712 544237, barua pepe;



Raia Mwema: Unazungumziaje suala la Katiba mpya?

Jaji Warioba: Sina hakika kama viongozi wetu wanaelewa ni kitu gani kilicho muhimu. Nadhani tunaingia katika tatizo hili la kila mmoja anatazama manufaa yake.

Katiba hii msingi wake ulikuwa ni chama kimoja. Tumefanya mabadiliko kuna mambo ambayo yametokana na chama kimoja lakini ni ya msingi katika kuendesha nchi. Ni muhimu tuyatazame na kati ya hayo ni Tanzania ya aina gani tunayotaka kuijenga.

Moja ambalo limetokana na mfumo wa chama kimoja ni kwamba TANU, ASP na CCM vilikuwa na itikadi ambayo ilikuwa inafafanua tunataka Tanzania ya aina gani na wananchi wakaielewa.
Bila kujali ulikuwa unakubaliana na Ujamaa na Kujitegemea ulijua huu ndio mwelekeo wetu tunataka Tanzania ya Ujamaa na Kujitegemea. Ni Ujamaa na Kujitegemea na miiko yake ilikuwa inaeleweka nchi nzima. Wananchi walikuwa wanatoa uamuzi kulingana na itikadi.

Sasa hakuna. Hatujui ni Tanzania gani tunayotaka kuijenga na hapo nadhani tunapokwenda kwa wananchi tutarajie hilo kwamba kubwa tunalotaka kutoka kwa wanannchi ni Tanzania gani wanataka tuijenge.

Tusiende kwamba kulazimisha kuyazungumza haya tunayoona ni makubwa kwa sababu watazungumza kwa jinsi wanavyoona mambo yao. Unaweza kwenda sehemu ukakuta tatizo lao ni ardhi. Wengine wanaweza kuzungumzia madini. Tuyasikilize yote haya na kutokana na hayo utaona Watanzania wanataka Tanzania ya aina gani.
Katika kile kifungu cha malengo muhimu ya Taifa haya yaelezwe ndani ya Katiba kwamba Watanzania malengo waliyonayo ni haya.

Kwa hiyo, kwangu hili ni muhimu la sivyo tutabaki katika yale yale ya kujidanganya kwamba Tanzania ni nchi ya Ujamaa na Kujitegemea wakati ile misingi haipo. Lazima tujipange kuhakikisha tunajenga Tanzania tunayotaka. Katiba ni wananchi na wananchi waachwe waamue mambo yao muhimu.

Tusipofafanua Tanzania tunayoitaka bado tutakuwa na mgogoro kwa sababu hapatakuwa na yard stick ya kuwapima viongozi na Tanzania tunayotaka kuijenga.

Kuna suala la msingi kuwa wananchi ndiyo wenye madaraka. Lazima tueleze ni madaraka gani yako kwa wananchi, kwamba wana uwezo upi wa kukataa viongozi.

Saa hivi kuna kujichanganya, unakuta tunasema madaraka yako kwa wananchi lakini tumeyahamisha kwa kiwango kikubwa kwenda kwenye dola au kwenye vyama vya siasa.

Serikali utakuta imepewa madaraka makubwa lakini wanasema ni kwa niaba ya wananchi. Vyama vya siasa navyo ni hivyo, vimepewa madaraka makubwa nao wanasema ni kwa manufaa ya wananchi.

Sasa hivi pamoja na Katiba kusema kwamba msingi wa madaraka ni wananchi kwa hiyo wanachagua wawakilishi lakini bado msingi huo unabanwa kwamba unawaambia kama unataka mwakilishi lazima ufuate taratibu hizi. Kama wewe si mwanachama wa chama cha siasa basi huna nafasi hiyo.

Kwamba watu wanaweza kumchagua mwakilishi lakini chama cha siasa kinaweza kumfukuza huyu mwakilishi. Wanakorofishana ndani ya chama wanamfukuza na anapoteza mandate ya wananchi kama vile mwakilishi huyo alichaguliwa na chama. Lazima mipaka iwekwe ndani ya Katiba.

Baada ya hapo tuangalie zile taasisi muhimu, Bunge, Serikali na Mahakama tuangalie upya mgawanyo wa madaraka haya, ile separation of powers iwepo lakini pia lazima kuwapo checks and balances.

Sasa hivi nadhani itabidi tuimarishe Mahakama. Iwe na uhuru wa kifedha, wasitegemee hisani ya Katibu Mkuu wa Hazina.

Kama tumefika mahali unasema Bunge litapata bajeti kiwango fulani na vyama vya siasa vinapata bajeti fulani, Mahakama nayo lazima tuseme wanapata asilimia fulani.

Tuingie kwenye utendaji, tuangalie mgawanyo wa madaraka kati ya Rais na taasisi za utendaji. Najua Rais lazima atakuwa na madaraka lakini kuna mahali pengine ama madaraka haya yanaweza kwenda kwenye taasisi au utendaji wake Rais lazima ashauriwe.

Inawezekana tukaamua, je, kuna umuhimu wa kumpa Rais madaraka ya kuteua mawaziri lakini wawe wanathibitishwa mahali? Ateue majaji lakini wathibitishwe mahali.
Sasa hivi naona kuna watu hawataki Rais awe na madaraka makubwa lakini mimi nafikiri Rais lazima awe na madaraka isipokuwa tuangalie yale mengine awe nayo lakini kwa kushauriwa. Lazima katika Taifa kuwe na mtu mnasema lazima awe na madaraka haya, isipokuwa ni kutengeneza utaratibu.

Hata kama tunataka Rais wa kikatiba tu ingawa sioni hilo kama ni zuri katika nchi, kama tunataka awe waziri mkuu sawa. Lakini suala la madaraka ni muhimu.

Katika mabadiliko ya mwaka 1984 nia ilikuwa kupunguza madaraka ya Rais, Waziri Mkuu asimamie zaidi utendaji lakini sasa hivi unaona kama Waziri Mkuu hana madaraka ya kusimamia utendaji.

Imejitokeza Rais anasimamia utendaji, anakwenda wizara kwa wizara, anatoa maagizo ya utendaji, Katiba haijamzuia lakini imemuwekea mtu wa kumsaidia, nimeona kwenye Bunge Waziri Mkuu anaulizwa maswali ya papo kwa papo anazumgumzia sera. Sera si ya kwake, iko chini ya Rais.

Kwa hiyo tutakapozungumza Katiba ni lazima hapa tufafanue nini kazi za waziri mkuu au kama kuna sababu ya kuwa na waziri mkuu. Tuzungumze, je, mawaziri wawe kama walivyo kutokana na Bunge?
Bunge nalo liangaliwe, madaraka yake yafafanuliwe. Unajua wakati mwingine Bunge limeingilia mambo ya utendaji, lazima sasa iwepo mipaka kati ya Serikali na Bunge na tujue nani anastahili kuchaguliwa kwenda bungeni, tujue utaratibu wa kupiga kura.

Sasa hivi wanazungumzia sana Tume ya Uchaguzi. Tuzungumzie hili. Kuna watu wanafikiri lazima iwakilishe makundi fulani fulani. Zanzibar wanazungumzia uwakilishi wa vyama. Kwingine, Afrika Kusini wanaye kamishna. Ghana wanayo tume ambayo mwenyekiti ni yule yule, amekuwapo kwa muda kwa sababu yuko huru.

Naamini Tume yetu ikiwa na wajumbe kutoka vyama vya siasa haitakuwa huru. Nadhani utaratibu wa Katiba mpya utuwezeshe kupata maoni ya wananchi.

Ninachokiona sasa ni kila kundi kwa maslahi yake linatumia hoja ya wananchi kuwa wanataka utaratibu fulani. Vivyo hivyo, Serikali nayo inataka kuweka mipaka fulani kwa maslahi ya wananchi.

Tusiweke mipaka. Wananchi watoe mawazo yao.

 Kuna vyama vya siasa vinasema kwa manufaa ya wananchi tuwe na Bunge la Katiba ambalo litachagua Tume na kutoa hadidu za rejea na kusimamia mchakato na baada ya kupitisha watakwenda kwa wananchi.

Sikubaliani na hilo. Wananchi waachwe wazungumze yote wanayotaka, Katiba yao iweje. Wakishakuzungumza, hiyo tume itengeneze muswada wa katiba urudi kwa wananchi. Wazungumze, kusiwe na kikundi hapa katikati kinasema kwa manufaa ya wananchi. Hapana.

Wananchi wazungumze muswada na chombo cha kupitisha kipitishe baadaye. Wasilete vikao hapa katikati huku wanajitafutia nafasi. Mchakato huu uende moja kwa moja kwa wananchi. Tusiwawekee mawazo.
Kuna wanaharakati wanataka kuleta mambo ya kuwajaza wananchi. Nina hakika wananchi wakiachiwa uhuru, watasema na wataalamu watapanga vizuri. Nasisitiza la msingi ni kuwaacha wananchi waseme wanataka nchi ya namna gani.

Suala la Muungano pia liwe katika Katiba. Tusipokuwa makini kwa maneno yanayozungumswa sasa tutavunja Muungano.

Muungano huu una misingi yake na upo kwa manufaa ya wananchi. Tufafanue manufaa hayo ni nini kwa mwananchi wa kawaida.

Wakati wote kwa mwananchi wa kawaida, kumekuwa hakuna matatizo ya Muungano. Matatizo yanatoka kwenye midomo ya viongozi.

Shughuli za wananchi wa kawaida haziangalii orodha ya mambo ya Muungano, bali haki yao kama raia. Wanajiona ni raia katika shughuli zao za kibiashara au nyingine. Mwananchi wa kawaida anaona anayo haki ya kufanya biashara mahali popote.

Wananchi wamezoa hivyo. Msiwafikishe mahali wakajiona kuwa kwenda Zanzibar au kuja Bara inabidi wafuate taratibu za kwenda Kenya au Uganda.

Tunayo matatizo ya madaraka, kwamba unazo Serikali mbili kwa hiyo yale yaliyomo kwenye orodha ya Muungano ni kuonyesha Serikali hii ina madaraka gani. Wanagombania madaraka.

Kama suala ni mafuta au mengine tuzungumze. Inategemea mnavyokubaliana, tusije kuongeza au kupunguza kwenye orodha mambo ambayo yatakuja kuwatenganisha wananchi. Kama kwa mfano, kuna watu wanafikiri kuimarisha Muungano ni kuwa na serikali tatu, unaimarishaje?

Sasa hivi kiini ni ugomvi wa madaraka kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar.

Hivi ukileta serikali tatu, ugomvi huu hautakuwapo? Ukileta Serikali ya Tanganyika yenyewe haitadai madaraka? Mwisho wataomba madaraka hadi Serikali ya Muungano isiwe na chochote.

Hivi Serikali ya Tanganyika kwa mfano ikawapo, ikataka iwe na wimbo wake wa Taifa, bendera yake, nembo yake, kisha inadai ifanye biashara ya nje, unafikiri tutakuwa tumefika wapi?

Ni kwamba tutakuwa tunaondoa Muungano na kurudisha Tanganyika na Zanzibar. Lakini kama wananchi wanataka hivyo, sawa.

Lakini tukivunja Muungano madhara yake ni makubwa sana kwa pande zote mbili. 

Mimi naamini wale wanaotaka serikali tatu wanajua nia yao ni kuvunja Muungano na huu ndio ukweli. Ukianzisha serikali tatu, maana yake unavunja Muungan


Ndoto ya Watanzania kupata katiba mpya inazidi kufifia kadri siku zinavyokwenda. Wachambuzi wengi wanatabiri kuwa itakuwa ni vigumu sana kwa Tanzania kupata katiba mpya kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015. 

Tulidhani tungeweza kupata katiba mpaya, lakini hali ilivyo sasa hilo linaonekana ni sawa na ngamia kupita katika tundu ya sindano. Labda hatukufikiria kwa makini, tulijidanganya na tulidhani kuwa zoezi hili ni rahisi sana. Ukweli ni kuwa zoezi hili ni gumu na tumekwishaonyesha kila dalili za kushindwa mtihani huu. 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba

Mchakato wa kuandika katiba mpya unakabiliwa na changamoto nyingi, baadhi ya vikwazo vinavyokwamisha mchakato huu ni ukweli kuwa kuandika katiba mpya haijawahi kuwa ni agenda ya chama kilichopo madarakani. Suala hili hawalikubali na hawaliungi mkono kwa dhati na hakuna dhamira ya kweli katika kuwapatia Watanzania katiba mpya. Suala la kuandika katiba mpya halipo katika maandiko yoyote ya chama tawala ikiwa pamoja na ilani ya uchaguzi. 

Hakuna mahali popote ambapo kiongozi wa ngazi yoyote amewahi kulisemea kuwa wangependa kuandika katiba mpya.

Harakati za kudai katiba mpya hazikuanza leo, zilianza toka miaka ya 1980. Na juhudi za kupinga kuandika katiba mpya, nazo hazikuanza leo. Viongozi wa chama Tawala walipinga kwa nguvu zao zote. Katika miaka hiyo, walisikika wakihoji: “Ni kipengele kipi katika katiba kina mapungufu?” Aidha walidiriki kuwaambia wanasiasa kutoka vyama vya ushindani kuwa, hawana ridhaa ya wananchi, hawajachaguliwa, hivyo hawawezi kuwasemea wananchi.

 Ila wao ndio waliochaguliwa na wana ridhaa ya wananchi. Hoja hizi zilionekana kuwa na mashiko hasa ukizingatia kuwa vyama vya ushindani vilikuwa havina wabunge wala madiwani.

Tume ya Nyalali pamoja na mambo mengine ilipendekeza iundwe Tume ya Katiba (Constitutional Commission) ili iweze kuandika katiba mpya itakayokidhi mazingira mapya ya kisiasa. Tume pia ilipendekeza kufutwa kwa sheria kandamizi 40. Ilipendekeza kutolewa kwa elimu ya mfumo wa vyama vingi; pia ilipendekeza mali zote ambazo chama tawala kilizipata kwa nguvu za wananchi wote zirejeshwe Serikali. 

Mapendekezo haya na mengine, pamoja na pendekezo muhimu la kuandika katiba mpya yalikataliwa na serikali. Pendekezo moja tu ambalo lilikubaliwa nalo ni kuingia katika mfumo wa vyama vingi.

Mwaka 1992, Tanzania tuliingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa. Bunge la Chama kimoja lilifanya mabadiliko kwa kuweka kiraka na kuruhusu mfumo wa vyama vingi. Madai ya katiba mpya yaliendelea na chama kilichoko madarakani kilijibu madai haya kwa kuunda Tume iliyojulikana kama Tume ya Jaji Kisanga mwaka 1998. Tume ya Jaji Kisanga ilipendekeza muundo wa muungano wa serikali tatu; kupunguza madaraka ya Rais; matokeo ya Urais yaweze kupingwa mahakamani, wagombea binafsi waruhusiwe. Kwa mara nyingine tena, mapendekezo haya yalikataliwa.

Wakati wa uchaguzi wa 2010, chama kikuu cha upinzani, Chadema, kiliwaahidi wananchi kuwa kitaanzisha mchakato wa kupata katiba mpya ndani ya siku 100, na si kama inavyopotoshwa na baadhi ya wanasiasa kuwa eti waliahidi kupatikana kwa katiba mpya ndani ya siku 100.

 Ilani ya Chadema ilisema kuanzisha mchakato ndani ya siku 100, jambo ambalo linawezekana kabisa, kwani unaweza kuanzisha mchakato hata ndani ya siku kumi tu. Suala hapa ni kuanzisha mchakato na si kupatikana katiba.

Vuguvugu la kudai katiba mpya lilizidi kuongezeka na hasa kutoka kwa Chama kikuu cha upinzani, asasi za kiraia, baadhi ya vyombo makini vya habari,  taasisi za elimu ya juu, wasomi na mashirika yasiyo ya kiserikali. 

Chama kikuu cha upinzani kiliyakataa matokeo ya Urais na kueleza masikitiko yao kuwa kwa mujibu wa katiba iliyopo hakiwezi kuyapinga matokeo ya Urais katika chombo chochote kile. Pia walitoka nje ya ukumbi wa Bunge wakati Rais alipokuwa akilizindua Bunge jipya na wakaweka wazi msimamo wao kuwa agenda yao ni kuandika katiba mpya.

Mwanasheria mkuu wa serikali alijitokeza hadharani na kupinga kwa kusema kuwa hatutaandika katiba mpya bali itafanyiwa marekebishao katiba iliyopo. Siku zote chama tawala kimekuwa kikiamini kuwa hakuna haja ya kuandika katiba mpya bali kuendelea kuifanyia marekebisho katiba iliyopo.

 Ndio maana hadi sasa kuna mabadiliko 14 yamekwishafanyika. Waziri wa Sheria na Katiba naye akasema kuwa hakuna fedha za kuendesha zoezio hili. Haya yote yanadhihirisha kukosekana utashi wa kisiasa wa kuandika katiba mpya. Licha ya majibu haya, wadau mbalimbali wakaendelea kushinikiza, wasomi wakaanda makongamo na mijadala kujadili kwa nini tunataka katiba mpya? Je katiba iliyopo ina mapungufu gani? Pia wakaanza kujadali mchakato utakaofaa katika kuandika katiba mpya.

Baadae, tukashuhudia serikali ikisalimu amri na kukubali madai ya wadau mbalimbali juu ya umhimu wa kuandika katiba mpya. Hii ilikuwa ni mabadiliko makubwa ya msimamo wa serikali (Big U-turn).

 December 31, 2010, Rais, alilihutubia Taifa katika hotuba yake ya mwaka na akawaambia Watanzania kuwa Serikali imedhamiria kuwapa fursa Watanzania kuandika katiba mpya. Aliahidi kuwa katiba mpya itakuwa tayari kufikia tarehe 26 April 2014, tukio ambalo litaambatana na sherehe za kutimiza miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Watanzania waliahidiwa kuwa na katiba mpya kabla ya uchaguzi wa 2015.

Ni muhimu tujiulize je, Kwa nini serikali ilibadili msimamo wake ghafla namna hii? Baadhi ya sababu zilizosababisha u-turn hii kwa maoni yangu ni kama zifuatazo: Kwanza, haikuwezekana kabisa, kuendelea kukipuuza chama kikuu cha upinzani, kwani kimekuwa kikipata mafanikio kwa kuongeza idadi ya Wabunge na Madiwani; Pia, Kimekuwa kikiongeza kukubalika kwake na kupata wafuasi wengi wengi zaidi; Mfumo wa vyama vingi umekuwa ukizidi kueleweka miongoni mwa Watanzania wengi na hasa vijana; 

Nchi majirani nazo zilikamilisha zoezi la kuandika katiba mpya na kuachana na katiba zilizoachwa na wakoloni. Nchi hizo ni kama vile Uganda, Kenya, Rwanda, Ghana.  Hivyo basi, Tanzania haikuweza kuwa kama kisiwa wakati jirani zake wamekamilisha zoezi hilo. Tulikuwa tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa majirani zetu na hasa Kenya; Sababu nyingine, ni ukweli kuwa Chama Tawala kilipoteza viti kadhaa katika uchaguzi uliopita na pia umaarufu wake na kukubalika kwake kunaendelea kushuka siku hadi siku kutokana na kuandamwa na kashfa mbalimbali, matumizi mabaya ya ofisi, ufisadi, rushwa na minyukano ndani ya chama. 

Aidha mitandao ya kijamii nayo imechangia kwa kuongeza wigo wa majadiliano na kubadilishana taarifa juu ya masuala mbalimbali; Zanzibar ilikuwa imefanya mabadiliko ya Katiba kuruhusu serikali ya umoja wa kitaifa na pia kuitambua Zanzibar kama nchi, ina bendera yake, vikosi vya majeshi yake, Rais wa Zanzibar alipewa mamlaka ya kuigawa Zanzibar katika sehemu ndogondogo kama mikoa, Wilaya;  Pia imekuwa ikiaminika kuwa Rais aliyoko madarakani alidhamiria kuwaachia zawadi Watanzania ya katiba mpya ambayo itawafanya wakumbuke utawala wake (Legacy). 


Kwa hali ya mchakato ilivyo sasa, hili bado tunasubiri kuliona iwapo kweli litatimia. Hizi ni baadhi tu ya sababu zilizosababisha chama tawala na serikali kusalimu amri na kukubali shinikizo la kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya. Ifahamike kwamba, mchakato huu ulianza si kwa mapenzi au hiari ya chama tawala bali kwa shinikizo.

Kutokana na kukosekana kwa dhamira ya kweli ya kuwapatia Watanzania katiba mpya, ndio maana, serikali mwaka 2011, ilitaka kuwasilisha Bungeni muswada wa Mabadiliko ya Katiba ambao ulikuwa na mapungufu mengi. Moja ya mapungufu hayo: ulitayarishwa kwa lugha ya Kiingereza ambayo Watanzania wengi hawaijui; muswada huu ulitaka kuwasilishwa chini ya hati ya dharura (under certificate of emergency); Zanzibar ilisahaulika kabisa; ulimpa madaraka makubwa Rais na ulizuia baadhi ya masuala yasijadiliwe (limit constitutional debate to certain issues).
 Muswda huu ulipingwa kila kona na huko Zanzibar ulichwanwa hadharani.

 April 2011, Serikali iliamua kuondoa muswada huu kwa ajili ya kuandikwa upya. Muswada uliondolewa na kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili, lakini wadau wengi walistaajabu muswada huu kwenda kusomwa kwa mara ya pili badala ya kusomwa kwa mara ya kwanza ili kutoa nafasi kwa watanzania kujadili kwani sasa wanaelewa maudhui. Suala hili lilipitishwa kibabe bila maridhiano. 


Novemba 2011, Bunge lilipitisha muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba licha ya chama kikuu cha upinzani kupinga na kutoka nje ya Bunge. Tarehe 27 November 2011, Rais alianza kukutana na vyama vya siasa na wadau mbalimbali ili kusikiliza malalamiko yao na mnamo February 2012, Bunge lilifanya marekebisho katika sheria ya mabadiliko ya Katiba. Ukiangalia kwa makini, utaona mchakato huu unasonga mbele kwa shinikizo na si utashi wa kisiasa, na sababu kuu ni kuwa suala la kuandika katiba mpya, halijawahi kuwa agenda ya chama tawala.

Yapo mapungufu mengi katika sheria hii ya mabadiliko ya katiba, lakini yalio wazi kabisa na ambayo yalipigiwa kelele na wadau wengi ni kosa la kugeuza Bunge la Jamhuri na Baraza la Wawakilishi kuwa ni Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba. Hili lilikuwa ni kosa kubwa na sasa tunalipa gharama za makosa hayo, hasa tukikumbuka lugha za matusi, kejeli, dhihaka na kibaguzi zinatumika katika Bunge maalumu la katiba. Ndio maana, Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka chama tawala wanapinga rasimu ya pili na hasa katika maeneo yote yanayogusa maslahi yao. 

Mathalani, wanapinga kuwapo ukomo wa vipindi vya ubunge, yaani vipindi vitatu (Limited tenure for MPs), wanapinga pendekezo la wabunge kutokuwa mawaziri, wanapinga pendekezo la Spika asiwe miongoni mwa Wabunge, wanapinga mamlaka waliyopewa wananchi ya kumkataa Mbunge ambaye amedhihirika ameshindwa kutekeleza majukumu yake ya ubunge (power of recall). Wabunge ambao wamekuwa wakitumia rushwa, hila, vitisho, ujinga na umaskini wa wapiga kura kuhakikisha kuwa wanabaki kuwa Wabunge daima, wataweza vipi kuafiki pendekezo la kuwa na ukomo wa vipindi vitatu tu? Ni wazi kuwa hili watalipinga kwani linagusa maslahi yao. 

Ni ujinga kutarajia wajumbe wa aina hii wataunga mkono mapendekezo ambayo yanagusa maslahi yao na kuwaondolea ulaji.
Tatizo hapa ni sheria ya mabadiliko ya katiba, tatizo hapa ni muundo wa Bunge maalum la katiba. Ndio tatizo. Tunayoshuhudia sasa ni matokea ya ubovu wa sheria hiyo iliyozaa muundo mbaya wa bunge maalaum la katiba. 

Wajumbe wameacha kujadili Rasimu iliwasilishwa na wamejikita katika ubabe wa kutukanana na kupigana vijembe. Kwa kuwa hakuna dhamira ya kweli, hawajali hata pale Wajumbe kutoka vyama vya upinzani walipoamua kutoka nje, hawajali hata kama  Bunge litavunjika. Kwani kwa mujibu wa sheria, tukishindwa kupata katiba mpya, tutarudi katika katiba ya zamani, na hili hasa ndio wanalolitaka na wamekwishaanza kulisema mara kadhaa. Hatuna budi kujiuliza, ni athari zipi tutazipata iwapo tutarudi katika katiba ya zamani? Je hatuna jambo lolote la kujifunza kutoka kwa majirani zetu wa Kenya?

Tujiulize, tunaweza vipi kupata katiba mpya kwa aina ya wajumbe wa Bunge maalum la katiba ambao wana tofauti za kiitikadi na kivyama? Ambao wanaligeuza suala la muundo wa muungano kuwa ni suala la imani? Kama dini! Eti kuna waumini wa serikali mbili! Tunaweza vipi kupata katiba mpya wakati tuna tofauti na misimamo mikali juu ya muundo wa Muungano? Hapa muafaka utapatikana vipi? Ingekuwa busara sana suala la muungano kushughulikiwa lenyewe peke yake na kwa uwazi na uhuru kabla ya kuanza zoezi la kuandika katiba. 

Lakini, kwa bahati mbaya watawala wetu waliona wanaweza kulipiga danadana na kupuuza kero na malalamiko ya muungano kwa miaka 50!! Wanahitaji miaka mingine mingapi kumaliza kero za muungano kwa muundo huu wa serikali mbili?
Bunge maalum la katiba lilitakiwa liwe ni chombo huru na lichaguliwe moja kwa moja na wananchi wenyewe kwa ajili ya kazi hiyo badala ya kuligeuza baraza la wawakilishi na bunge la sasa ambalo limehodhiwa na chama tawala. Kosa hili ndio limeufanya mchakato huu kufikia hapa ulipo.

 Hata idadi ya wajumbe ni wengi mno na hivyo kushindwa kuwa na mijadala ya afya.
Ushahidi mwingine unaodhihirisha mapungufu ya sheria hii ni mvutano na tafsiri tofauti juu ya mamlaka ya Bunge maalum la katiba ambapo wanasheria wamebaki wakibishana iwapo Bunge Maalumu lina mamlaka ya kufanya mabadiliko makubwa.

 Mabishano haya ni ushahidi tosha kuwa sheria hii si nzuri sana kiasi cha kutoa tafsiri tofauti.Tume ya Mabadiliko ya Katiba Iliundwa na kuanza kazi ya kukusanya maoni ya wananchi. June 3 2013, Tume ilitoa Rasimu ya Kwanza ya Katiba. Rasimu hii ilijadiliwa na Mabaraza ya Katiba ya Wilaya na Taasisi zenye malego sawa. Hapa pia tuliona kukosekana kwa dhamira ya dhati katika kuwapatia wananchi katiba mpya na wanayoitaka. Uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya katiba uligubikwa na rushwa na wajumbe wengi walilishwa maoni ya chama tawala. Kitendo hicho nacho kinanipa wasiwasi kama kweli kuna nia thabiti ya kuwapa Watanzania katiba wanayoitaka.
 
Pigo lingine katika mchakato huu, ni pale Bunge kwa mabavu lilipoamua kubadili sheria na kufupisha ukomo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuamua kuwa ukomo wa Tume uishe mara tu baada ya kuwasilisha rasimu ya pili katika Bunge maalumu katiba. Hali hii imefanya kuwe na ombwe kwani Tume ingefanya kazi nzuri ya kutoa ufafanuzi na hata ushauri ambao ungesaidia mchakato kusonga mbele. Lakini, kutokana na kukosekana dhamira ya kweli serikali ya chama tawala ilifupisha ukomo wa Tume hii licha ya suala hili kupingwa kila kona. Ilikuwa ni vyema kwa Tume hii kuendelea kuwapo na kuwa na nguvu ya kisheria.


Dhamira ya kweli pia haikuonekana katika uundwaji wa Bunge maalum la katiba ambapo tulishuhudia wajumbe wengi wanaonekana kutoka chama tawala ikiwa ni pamoja na mwakilishi wa waganga wa kienyeji. Baada ya hapo tukashuhudia sarakasi ndani ya Bunge maalum. Bila aibu wala soni, utaratibu ukabidilishwa, Rais akapangiwa kuongea baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Sote tukashuhudia, hotuba yake ikijikita katika kujibu hotuba ya Mwenyekiti wa Tume, si hivyo tu, akatumia nafasi hiyo kueleza msimamo wa chama chake, kupinga serikali tatu na kutoa vitisho kuwa eti jeshi litapindua serikali kwa kuwa serikali ya muungano haitakuwa na mapato ya kutosha kwalipa wanajeshi!!
Kwa kiasi kikubwa mchakato wa kuandika katiba mpya ulianza kuvurugika kuanzia hapo.

 Baadae yakafuata maneno ya kejeli, matusi, dhihaka na vitisho kutoka kwa wajumbe wa Bunge maalum wa kutoka chama tawala. Wengine wakadiriki kufanya kampeni na vitisho katika nyumba za ibada, eti Jeshi linaweza kupindua nchi endapo mfumo wa serikali tatu utapitishwa!! na wengine wakauwambia umma wa Watanzania kuwa eti zikipita serikali tatu, wataingia msituni! Kiburi na jeuri iliyopilitiza kiasi. 

Na wapo wanaosema serikali mbili ni lazima! Kama hiyo haitoshi, wenyeviti na manaibu wa kamati mbalimbali za Bunge takribani wote, wakatoka chama tawala. Huu nao ni ushahidi tosha kuwa hakuna dhamira ya dhati ya kufikia maridhiano bali ni mbinu na hila za chama tawala kutaka kuhodhi mchakato huu ili kupitisha matakwa yake.

Kumekuwa pia na kauli mbalimbali zinazodhihirisha kuwa hakuna dhamira ya dhati ya kuandika katiba mpya. Wapo viongozi wamesikika wakisema, “hivi katiba mpya ndio inapiga kura”? Wengine wakisema, “kipaumbele cha Watanzania sio katiba bali ni maji, barabara, elimu bora na afya.”

 Na wapo waliosema kirahisi tu, bila kujali gharama kubwa tulizokwishaingia katika mchakato huu kuwa, “tukishindwa kupata katiba mpya, tutarudi katika katiba ya zamani” bila kujali athari za hilo na bila kujiuliza mafundisho yapi tunaweza kuyapata kutoka kwa majirani zetu wa Kenya.  

Ninapoangalia mchakato huu, historia yake, tulipotoka, tulipo na tunapokwenda, ni wazi kuwa suala la kupata katiba mpya ni ndoto. Wapo ambao walitabiri hili. Lakini walipuuzwa. Itawezekana tu kupata katiba mpya kwa kuelendelea kushinikiza serikali na chama tawala, isihodhi mchakato, tukikumbushe kuwa hatuandiki katiba ya chama tawala, hawana hati miliki ya Tanzania na mawazo yao wao si mawazo ya Watanzania wote. 

Tuna haki ya kutoa mawazo yetu na ni lazima yasikilizwe na kuheshimiwa.Tunaweza kupata katiba mpya kwa kuwa na ubia mtakatifu kati ya vyama vya ushindani, asasi za kiraia, taasisi za elimu ya juu, vyombo vya habari, sekta binafsi na wananchi, kuendelea kushinikiza na kulitaka Bunge lijadili Rasimu ya Warioba na si vinginevyo. Tukubali kuwa jambo hili si rahisi na halipendwi na chama tawala ambccho malengo yake ni kulinda na kutetea hadhi yake (Status quo).

 Hatuna budi kujiuliza, chama ambacho kimekuwa madarakani kwa miongo mingi, kikishinda chaguzi mbalimbali, kikihodhi Bunge na Taasisi mbalimbali, kikinufaika na katiba iliyopo ambayo inakifanya kiwe chama dola, kina sababu gani za kuandika katiba mpya? Msukumo wa kuandika katiba mpya kwa chama tawala ni upi? Ili iweje? 



Na Selemani Rehani
0654 00 20 82

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.