Serikali imewataka viongozi wa kisiasa pamoja na watendaji wa serikali kutotumia madaraka yao vibaya kuwanyanyasa na kuwasumbua wawekezaji wazawa waliowekeza ndani ya nchi.
Aidha viongozi hao wametakiwa kuwaheshimu na kuwajengea mazingira rafiki yatakayowawezesha kufanya biashara zao kwa amani ili kuweza kukuza uchumi wa taifa na kuongeza ajira kwa vijana.
Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda mkoani Simiyu, wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa huo pamoja na tovuti ya Mkoa.
Prof. Mkenda amewasihi viongozi wote wa serikali ngazi za mikoa na wilaya nchini kujivunia uwepo wa wajasiriamali na wafanyabiashara wakubwa ambao ni wazawa kwani wao ni chachu ya kuongeza kwa ajira za vijana.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (anayetazama kamera) akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu nje ya ukumbi wa Kanisa Katoliki Bariadi wakati wakimsubiri mgeni rasmi kuwasili kwenye sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji na tovuti ya mkoa wa Simiyu.(Picha zote na Thebeauty.co.tz).
Amesema kuwa si vyema wafanyabishara kutukanwa, kutolewa lugha zisizokuwa sahihi na kuonekana kama wana uadui na serikali, na badala yake watukuzwe ili kuweza kulipa kodi pamoja na kufuata sheria na taratibu za nchi.
“hawa wafanyabishara hasa wazawa na wajasiriamali tuwaone kama wenzetu, ndugu zetu na watu muhimu, kwani wameajiri vijana wetu, wanalipa kodi ili nchi ipate maendeleo, lakini wanatekeleza kauli mbiu ya Rais, Tanzania kuwa nchi ya viwanda, tuwathamni” alisema Prof.Mkenda.
Katibu Mkuu huyo amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatenga maeneo kwa ajili ya wawekezaji wakubwa na wadogo kwa ajili ya kujenga viwanda.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo S. Kiswaga mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki Bariadi, mkoani Simiyu kushiriki uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani humo pamoja na kuzindua tovuti ya mkoa huo.
Akizungumza katika sherehe hizo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka amesema kuwa ili Tanzania iweze kufanikiwa katika azma yake ya kuwa na viwanda lazima serikali iwekeze kwanza katika utafiti wa fursa zilizopo.
Amesema kuwekeza katika utafiti utasaidia kutoa uthubutu wa kufanya na kutenda mambo mbalimbali yatakayoifanya nchi kuwa na uchumi wa kati na kuwaletea wananchi maendeleo.
“nchi hii tusingelihitaji kuona wakuu wa mikoa kuwa wabobezi katika kila sekta na badala yake wawaache wataalam na watafiti wafanye kazi zao kitaalamu ili kuepuka mvurugano wa shughuli za kimaendeleo ndani ya nchi” amesema Mtaka.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne A. Sagini akitoa utambulisho wa meza kuu na maelezo ya lengo la mwongozo wa uwekezaji katika sherehe hizo zilizofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Bariadi, Mkoani Simiyu.
Kwa upande wake Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF) Dk. Gratian Bamwenda, amesema kukamilika kwa utafiti huo mkoani Simiyu utatoa fursa kwa wananchi na wafanyabishara kutambua wapi kuna fursa sahihi na haraka kuwekeza.
Utafiti huo ulifanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF) kati ya mwezi Januari na Februari mwaka huu mkoani humo kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ambapo zaidi ya shilingi Milioni 60 zilitumika katika utafiti huo na kubaini uwepo wa fursa 26.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani humo ulioratibiwa na ESRF chini ya ufadhili wa UNDP.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda akitoa hotuba ya ufunguzi kwenye sherehe ya uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu ulioenda sambamba na uzinduzi wa tovuti ya mkoa wa Simiyu.
Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF) Dk. Gratian Bamwenda akitoa wasilisho la fursa za uwekezaji mkoani Simiyu wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani humo.
Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF) Dk. Gratian Bamwenda akiitambulisha timu iliyoshiriki kwenye utafiti huo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF), Dkt. Tausi Kida, Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Bi. Margareth Nzuki, Afisa wa Habari Mwandamizi wa ESRF, Abdallah Hassan pamoja na UNDP Programme Specialist, Amon Manyama.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini ambao ndio wafadhili wa utafiti huo, Awa Dabo akitoa salamu za UNDP wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa salamu za ESRF wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Bariadi.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani humo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara akitoa salamu za NSSF wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu uliofanyika katika Kanisa Katoliki Bariadi.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda akisaidiana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki Bariadi, Mkoani Simiyu.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka wakionyesha mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu baada ya kuzindua.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu kwa ajili ya utekelezaji wakati wa hafla ya uzinduzi wa mwongozo huo ulioratibiwa na ESRF chini ya ufadhili wa UNDP.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (katikati) akimkabidhi nakala Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini Awa Dabo ambao ndio wafadhili wa utafiti wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoani Simiyu.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (wa pili kushoto) akikabidhi nakala ya mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF), Dkt. Tausi Kida.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (wapili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara nakala ya mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo huo zilizofanyika kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki Bariadi, Mkoani Simiyu. Mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda akiabidhi nakala hizo kwa watendaji wa mkoa wa Simiyu.
Kikundi cha Kwaya ya Simiyu kikiimba wimbo maalum wa kuhamasisha uwekezaji mkoani Simiyu wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini ambao ndio wafadhili wa utafiti huo, Awa Dabo, Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne A. Sagini, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF), Dkt. Tausi Kida, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka pamoja na mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda wakitazama burudani ya kwaya kutoka mkoani Simiyu kwenye sherehe za uzinduzi huo.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu katika sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani humo.
Pichani juu na chini ni sehemu ya viongozi wa mkoa wa Simiyu, Wafanyabiashara, Wanahabari, Viongozi wa madhehebu ya dini pamoja wawekezaji waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa Simiyu.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini,, Awa Dabo akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kijamii na Uchumi (ESRF), Dkt. Tausi Kida mara baada ya kumalizika sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu.
Post a Comment