Katika mwendelezo wa dhamira yake ya kuendeleza vipaji na kukuza utafiti nchini, kampuni ya Barrick nchini imekuwa mmoja wa wadhamini wa maadhimisho ya kumi ya wiki ya Utafiti na Uvumbuzi uliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo imetunukiwa cheti cha tuzo kutokana na udhamini huo.
Katika maadhimisho ya mwaka huu Barrick imetoa shilingi milioni 10 kwa mmoja wa washindi katika utafiti Dkt. Juma Mmongoyo, kutoka Mkwawa University College of Education (MUCE) kwa mradi wake wa utafiti kuhusu “Mbinu za kudhibiti mdudu mharibifu wa nyanya kwa ajili ya ukuaji wa zao la nyanya mkoani Iringa.
Barrick mbali na udhamini huo imekuwa imekuwa ikidhamini programu mbalimbali za utafiti ,uvumbuzi,na inazo programu za mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu na vya kati kwenye migodi yake nchini ya North Mara na Bulyanhulu ambayo inaiendesha kwa ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals pia imekuwa kila mwaka ikifadhili semina za kuwajengea wanafunzi wa vyuo vikuu uwezo kupitia taasisi ya AIESEC Tanzania.
Meneja wa Barrick nchini, Dkt Melkiory Ngido akiuliza swali kutoka kwa vijana wa Chuo Kikuu kuhusu uvumbuzi na utafiti kwenye moja ya mabanda kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwenye maadhimisho ya kumi ya wiki ya utafiti na uvumbuzi ulimalizika jana , kushoto ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia , Profesa peter Msoffe.



Post a Comment