Makampuni ya ulinzi yanayofanya shughuli zake Jijini Dar es Salaam yametakiwa kutoa mafunzo ya kila mara kwa askari wake kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kukabiliana na changamoto za usalama zinazolikumba Jiji hilo kwa sasa. Rai hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi katika Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni SACP Suzan Kaganda wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa askari 70 wa kampuni ya ulinzi ya SGA Security yaliyofayika katika makao makuu ya kampuni hiyo, Mbezi Beach. Mafunzo haya yaliandaliwa na Polisi Tanzania katika kuimarisha ufanisi wa askari katika makampuni binafsi. “Natoa rai kwa makampuni mengine ya ulinzi yaliyopo Mkoa wa Kinondoni yaige mfano mzuri kutoka SGA Security kwa kutoa mafunzo kwa watumishi wao ili kuwaongezea maarifa yatakayowawezesha kufanya kazi kwa kujiamini na kwa uhakika,” alisema. Alisema jeshi la polisi liko tayari kutoa ushirikiano, msaada wa kitaalamu na ushauri pale itakapohitajika huku akiongeza kuwa jeshi hilo pekee haliwezi kumaliza kabisa uhalifu bila kushirikiana na wadau mablimbali yakiwemo makampuni kama SGA Security.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni SACP Suzan Kaganda akikagua gwaride rasmi lililoandaliwa na askari wa SGA Security wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku tano kwa askari 70 wa kampuni hiyo.

  “Aidha nawaasa kuzingatia taratibu na sheria za nchi tunapokuwa tukitimiza majukumu yetu ili kazi yetu iwe na tija kwa jamii tunayoihudumia na taifa kwa ujumla,” alisema na kuwaasa askari waliopata mafunzo kuyatumia vizuri kwa manufaa yao na kampuni kwa ujumla. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Security -Tanzania, Eric Sambu, alisema mafunzo hayo ya mara kwa mara yamekuwa na manufaa makubwa kwa kampuni kwani wameweza kuwajengea askari wao uwezo mkubwa hivi kuwafanya wananchi waongeze imani kwao. Zaidi, Mkurungenzi Mtendaji alishukuru Polisi kuanzisha mchakato huu wa kutoa mafunzo wao wenyewe moja kwa moja hii ni ishara kuwa kazi zetu katika makampuni binafsi zinatambuliwa na Polisi wanatuchukulia kama wadau wao katika kuimarisha ulinzi na usalama nchini. “Tumekuwa tukiendesha mafunzo haya kwa kushirikiana na jeshi la polisi kwani kazi zetu zinafanana kwa kuwa tupo ili kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao,” alisema. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni SACP, Suzan Kaganda akikabidhi cheti kwa mmoja wa maaskari wa SGA Security wakati akifunga mafunzo kwa askari 70 wa kampuni hiyo.
Alisema katika siku tano za mafunzo askari hao waliweza kujifunza mada tofauti kama vile matumizi ya nguvu na silaha za moto, haki za binadamu, polisi jamii, uvunjifu wa haki za binadamu, huduma kwa wateja na uhusiano wa jamii, doria, eneo la tukio, usuluhishi wa migogoro na nguvu ya kukamata. “Tutaendelea kutoa mafunzo ya aina hii mara kwa mara kwa kuwa tayari tumeona matunda yake ili askari wetu kote nchini katika sehemu ambazo tunafanya kazi waendelee kuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa weledi,” alisema. Kampuni ya SGA ni moja ya makampuni makubwa ya ulinzi Afrika Mashariki huku ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 40 katika ukanda huu na imeajiri zaidi ya wafanyakazi 17000 huku ikiwa imewekeza vikamilifu katika rasilimali tofauti za shughuli za ulinzi na usalama.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni SACP Suzan Kaganda akipewa maelezo kuhusu chumba cha mawasiliano cha SGA Security kilichopo Mbezi Beach, Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo kwa askari 70 wa kampuni hiyo. Kulia ni Mkuu wa Ufundi wa SGA-Tanzania Prochest Peter.

SGA Security ni kampuni ya kwanza binafsi kusajiliwa nchini Tanzania mwaka 1984, kama Group Four Security baadae ikajulikana kama Security Group, baada ya zaidi ya miaka 32 ya shughuli na mafanikio Tanzania na 48 Afrika Mashariki, kampuni imeweza mpaka sasa kuajiri wafanyakazi takriban 5,000 nchini Tanzania na zaidi ya 18,500 katika kanda ya Afrika Mashariki, SGA Security ni moja ya waajiri kubwa katika eneo hilo. SGA Security ina uwakilishi wa kiasi kikubwa sana katika kila eneo la huduma ya usimamizi na usafirishaji wa pesa na vitu vyenye thamani na inatoa huduma hizi kwa zaidi ya Mabenki na Taasisi za Fedha 55 katika eneo la Afrika Mashariki, pia kwenye kutoa huduma za ulinzi kwa takribani mashirika 65 binafsi, kidiplomasia na NGO sekta katika eneo hilo. SGA Security imejikita zaidi pia katika ulinzi shirikishi kupitia teknolojia zaidi za kisasa kama Closed Circuit TV na Access Control, huduma za radio, Tracking ya magari na ufuatiliaji wa mizigo iwapo safarini (RFID).


Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.