Sudan
Kusini: Maelfu wafurika kando ya vijito kusubiri chakula cha msaada
Na
Mwandishi Wetu
Maelfu
ya raia ambao wamekumbwa na baa la njaa lililosababishwa na shughuli za
binadamu nchini Sudan Kusini, wamekimbilia kwenye maeneo ya mabwawa na mito
mwishoni mwa juma wakitumaini kupokea chakula cha msaada.
Kwa
miezi sasa Bol Mol mwenye umri wa miaka 45 ambaye alikuwa mlinzi wa zamani
kwenye kituo cha mafuta, amekuwa akipambana kwaajili ya familia yake kuishi,
akifanya shughuli za uvuvi kwenye mito ya jirani huku wake zake watatu
wakitafuta maji kwaajili ya chakula.
Wanakula
mlo mmoja tu ikiwa watapata bahati, lakini wanasema ni bora wakaishi kando na
mito hiyo kwa usalama wao dhidi ya wanajeshi wenye silaha wanaofanya vitendo
vya kihalifu.
"Maisha
hapa hayana umuhimu" amesema Mol ambaye alikuwa anaonekana mchovu huku
akiendelea kuwasubiri mamia ya raia wengine wanaowasili kwenye eneo hilo kwa
msaada.
Mashirika
ya misaada yameshauriana na Serikali ya Sudan Kusini na waasi kuanzisha vituo
maalumu vya kufanya usajili tayari kwaajili ya kuanza kupokea chakula cha
msaada ambacho kitaanza kupelekwa hivi karibuni.
Umoja
wa Mataifa ulitangaza baa la njaa nchini Sudan Kusini wiki moja iliyopita,
lakini njaa imesababisha madhara kwa zaidi ya watu wanaokadiriwa kufikia laki
1, ambapo wataalamu wanasema hali hiyo haikutokana na sababu za mabadiliko ya
tabia nchi.
Kwa
zaidi ya miaka mitatu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, vimesabisha raia
kushindwa kufanya kilimo, vimeharibu hazina za vyakula na kuwalazimisha raia
kuyakimbia makazi yao.
Misafara
ya misaada ya chakula na kimatibabu pia imekuwa ikishambuliwa kwa makusudi na
wafanyakazi wa mashirika hayo kushambuliwa pia.
Mwisho
Post a Comment