Na Hudugu Ng'amilo.

Bunge Maalumu la Katiba linaahirishwa leo baada ya kukutana kwa siku 67 bila kupitisha hata ibara moja kati ya 240 zilizomo katika Rasimu ya Katiba.
 bunge 4c2f3
Badala yake Bunge hilo likiongozwa na Samuel Sitta "Mzee wa Kasi na Viwango" linaahirishwa hadi Agosti, mwaka huu likiendelea kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita zenye jumla ya Ibara 19, zinazohusu masuala yanayojenga msingi wa aina ya Muungano unaopendekezwa.

Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika rasimu iliyowasilishwa bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba ilipendekeza muundo wa shirikisho lenye serikali tatu, pendekezo ambalo limeligawa Bunge hilo vipande viwili.

Kutokana na mgawanyiko huo, kauli zenye utata, kejeli, matusi, dhihaka na ubaguzi ni mambo yaliyoshika hatamu katika mjadala wa sura hizo mbili, huku viongozi wa Bunge; Sitta na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan wakilaumiwa kwa kushindwa kudhibiti hali hiyo.

Mwanzoni mwa wiki hii, Mjumbe wa Bunge hilo, Ezekiah Oluoch alimshutumu Sitta kwamba ameshindwa kudhibiti nidhamu katika Bunge na kwamba ndiye chanzo cha kuondoka kwa wajumbe wapatao 200 ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

"Mwenendo wa Bunge Maalumu ulikuwa na dalili zote za kuonyesha kungetokea matatizo ndani yake kutokana na mipasho ambayo ilikuwa ikitokea kwa wajumbe pamoja na lugha ambazo siyo za staha wakati wa kutengeneza kanuni," alisema Oluoch na kuongeza:

"Kwanza matumizi ya lugha zisizo na staha, mwenyekiti anaruhusu wajumbe kuchangia hoja kwa kupeana mipasho bila kujali hoja iliyopo mezani kinyume na kanuni," alisema Olouch.

Hata hivyo, Suluhu alisema amekuwa akiendesha Bunge hilo kwa umakini mkubwa na kwamba kila anaposikia lugha chafu amekuwa akiwabana wajumbe kwa kuwaamuru kufuta kauli au kuomba radhi kwa matamshi. "Sipendezwi na lugha chafu, kwa hiyo mojawapo ya mambo ambayo huwa najitahidi kusikiliza kwa makini kila michango inapotolewa na wajumbe bungeni ni kubaini kama wametumia lugha zisizostahili, kisha kuchukua hatua kwa mujibu wa kanuni zetu," alisema Suluhu.

Alikiri kwamba wapo baadhi ya wajumbe ambao wamekuwa wakigoma au kukataa kuomba radhi na kwamba masuala yao hupelekwa kwenye Kamati ya Maadili ambayo ina mamlaka ya kuchukua hatua zaidi kwa mujibu wa kanuni za Bunge hilo.

Matakwa ya Kanuni
Sehemu ya Tano ya Kanuni za Bunge Maalumu inatoa mwongozo wa mambo yanayokatazwa na yale yanayopaswa kufuatwa wakati wa mjadala.

Kanuni ya 46 imeorodhesha mambo yasiyoruhusiwa ambayo ni pamoja na kusema uongo, kutoa taarifa zisizokuwa za kweli, kuzungumza jambo lolote ambalo halipo kwenye mjadala na kutumia majina ya marais na waasisi wa Taifa kwa dhihaka.Pia inazuia matumizi ya lugha ya kuudhi, kubagua, kunyanyapaa au inayodhalilisha watu wengine, kuzomea, kupiga kelele za aina yoyote zinazoweza kuvuruga mjadala au mwenendo bora wa shughuli za Bunge hilo.

Licha ya makatazo hayo, wajumbe wamekuwa wakikiuka kanuni bila kuchukuliwa hatua na hali hiyo imekuwa chanzo cha mivutano, zomeazomea, kelele na mambo mengine hadi kundi la Ukawa kususia kikao wakieleza kutokuridhishwa na mwenendo wa Bunge.
Kuufyata na kuufyatua
Baadhi ya kauli tata zilizojitokeza ni pamoja na ile iliyotolewa na Asha Bakari Makame kwa mjumbe mwenzake, Ismail Jussa kuwa anafanana na watu wenye mabusha nyuma ambao ndiyo huufyata.

Makame ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), alikwenda mbali zaidi na kumwambia Jussa kuwa ana matatizo ya kiafya na si mwanamume kamili, kwani ameshindwa kuoa na hana watoto wakati ana umri mkubwa.
"Huyu Jussa anasema kwamba tumeufyata, hapa tuwekane sawa, maana ya kuufyata ni mtu kuwa na mabusha pale yanapokuwa nyuma ndiyo kuufyata kwa hiyo yeye ndiyo ameufyata, ana busha huyu," alisema Bakari.

Naye Profesa Ibrahim Lipumba alichafua hali ya hewa pale alipowafananisha wajumbe wa Bunge Maalumu na kundi la mauaji nchini Rwanda, Intarahamwe.

"Tumechoka kusikiliza matusi. "Tumechoka kudharau mawazo ya wananchi, tumechoka ubaguzi hatuwezi kuwa sehemu ya kundi la Intarahamwe linalohamasisha ubaguzi ndani ya Tanzania hili hatulikubali. Tunawaachia, watu wote tunaotaka Katiba ya wananchi tunawaachia Intarahamwe mwendelee na Bunge lenu."

Mjumbe mwingine ni Mwanakhamis Kassim Said aliyesema: "Mimi nilikuwa namwomba baba yangu mdogo Seif (Maalim Seif Sharif Hamad) awarejeshe watu wake humu (bungeni) kwa sababu mpira unachezwa huku ndani. Hatutakii mema humu, tena ana choyo na husuda. Namwomba baba mdogo atuache, alichokitaka amekipata, king'ora anazunguka saa 24 Dar es Salaam, Unguja. Mheshimiwa Mwenyekiti Baba mdogo kila mara yuko kwenye pipa (ndege) mara Uingereza, mara Canada mara wapi? Hicho ndicho anachokitaka amekipata."

Mjumbe mwingine, Mohamed Seif Khatibu alisema: "Nimejifunza kuwa baadhi ya wanasiasa wa upinzani ni vinyonga. Lakini Maalim Seif ni kinyonga, wakipita kwenye mvua wanakuwa na rangi ya mvua, kwenye jua wanakuwa na rangi ya jua, baharini wanakuwa na rangi ya bahari."

Tuhuma za rushwa
Mjumbe Ezekiah Wenje alisema baadhi ya mawaziri wamewahonga wajumbe wa kundi la 201 ili waunge mkono msimamo wao, lakini alipotakiwa kufuta kauli hiyo alikataa na suala lake kufikishwa kwenye kamati ya kanuni.Kuna wajumbe wengine walikwenda hadi kwa waziri mkuu ambako walikula, walikunywa hadi saa 7:00 usiku, wengine walikwenda kwa Gaudensia Kabaka (Waziri wa Kazi na Ajira) na walikula na kunywa na kupewa bahasha."

Kuingia msituni
Kapteni John Komba alitangaza kuingia msituni iwapo Bunge Maalumu la Katiba litapitisha muundo wa serikali tatu, huku akimshutumu Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Jaji Joseph Warioba na timu yake ni waasi kama Adamu na Eva waliomuasi Mungu kutokana na kile walichokifanya cha kupendekeza serikali tatu. Mwingine katika orodha ni Bernard Membe aliyesema, Tume ya Mzee Warioba itakuja kukumbukwa kwa kuratibu mauaji ya Muungano na Bunge nalo litakuja kulaaniwa kwa kubariki mauaji hayo.

Watoto wa shetani
Mjumbe Paul Makonda alisema: "Shetani alikuja duniani kuiharibu dunia, kuiangamiza na kuteketeza kila kilichostahili kuungana... watoto wake ni Mheshimiwa Jussa, watoto wake ni Mheshimiwa Mbowe, watoto wake ni Mheshimiwa Lipumba... Hawa ni watoto wa shetani".

Mwingine: Waride Bakari Jabu alisema: "Chiku Abwao mimi namshangaa sana anayesema bora Muungano uvunjike lakini Tanganyika iwepo. Tunafahamu asili yake mwenyewe ni Mkongo mumewe ndiye Mtanganyika, namwambia Muungano huu utakuwepo na utaendelea kuwapo."

Mjumbe Tundu Lissu alisema: "Tanganyika haikuuawa na makubaliano ya Muungano, bali iliuawa kwa amri za Nyerere.... Mwalimu Nyerere hakuwa na mamlaka yoyote ya kikatiba ya kutunga amri na kuua Tanganyika."

Imeandikwa na Neville Meena, Daniel Mjema, Sharon Sauwa na Beatrice Moses
CHANZO MWANANCHI

chanzo cha habari hii na mtandao wa www.mjengwablog.com


The program for the coming months contains intersting courses in the field of agriculture. The knowledge we are going to offer you is unique, it is not only our expertise; more than 6 external facilitators are going to show you how to become a successful organic farmer and what it takes to train farmers in the field and become a good facilitator.
 K1024_IMG_0293
Trainings this year are:
Organic Agriculture Basic
Organic Agriculture Intermediate
Natural Medicine
Zero Tillage Farming
Animal Production Basic
Process Food and add Value
Attract Youth in Agriculture Camp
Sustainable Integrated Waste Management
Permaculture Design Course
Training of Trainers


Organic Agriculture Basic
With more than 5 years experience in the field of organic agriculture we have a lot to share. In these five days you will learn how to fertilize your soil and manage its fertility. Pests and diseases won’t be bothering you so much afterwards, since you`ll gain knowledge about botanical extracts for all sorts of pests and diseases management. In addition you will experience the power of “Sustainable Intensification”. We’ll facilitate you on how to manage your plot most efficient by using an integrated approach that includes crop production with livestock-keeping and forestry. For more information use this link


Organic Agriculture Intermediate
For farmers who have already visited the Organic Agriculture Basic this course gives further insights into sustainable farming practices. The first part of this course is a deeper introduction into soil health and technologies which can be used to increase soil fertility. Furthermore organic pest, disease and water management are pracitcally and theoretically taught. The course closes with different crop propagation techniques which are suitable biotechnologies for organic farmers. For more information use this link


Natural Medicine
Do you know the power of herbs? Do you know that plants are not only for food but also for medicine? Tanzania is rich in plants that can be used as natural medicine and Dr. Feleshi from ANAMED Tanzania will show you how to use them. The course gives you a basic introduction of cultivation, and preparation and usage of medicinal plants. Moreover you will afterwards know how to extract natural oils and to prepare high quality soap. So let’s stay healthy and be prepared to start your cosmetic business. For more Information use this link


Zero Tillage Farming
Zero Tillage, which is also known as conservation agriculture or Farming God’s way  is an agriculture practice that is becoming more and more popular. You will be introduced in this ecologically friendly practice of cultivating your farm by Joshua Moose of Joshua Foundation. Joshua has already several years experience. This approach has shown that you can get a lot out of it, come and see how. For more information use this link


Animal Production Basic
Livestock keeping and crop production can coexist very well since an integrated approach is the key to establish a closed nutrient management cycle. Fresh fish, meat, milk and honey are products which can increase the houshold income for a small scale farmer significantly. To run a livestock enterprise successfully good management practices are needed. The course gives introduction into animal health, feeding, housing and general production. For more information use this link


Process Food and add Value
Processed and value added products fetch a higher price, can be stored for a longer time and need less space. This course will introduce participants to different value addition and food processing techniques. It is made to cater for farmers, small and medium enterprises and those who would like to venture into food processing and value addition. For more information use this link


Attract Youth in Agriculture Camp
This very interesting and fun training is intended to accommodate youth for week long courses where they will learn how to establish vegetable gardens in rural and urban areas, establish tree nurseries, entrepreneurship and life skills as well as management of waste in their homes, schools and institutions. This will be combined with the SAT tournament for the best youth team. For more information use this link


Sustainable Integrated Waste Management
Is waste equal waste? NO! Experts from Kenya (among them the Organic farming legend Molly Njeru and experts from KOATEC institute – Titus Muchangi) will show you how to get the most out of it. In these 5 days you will experience several composting technologies from kitchen and garden waste, using Effective Microorganisms (EM) technology for agriculture, environment and livestock, how to make organic charcoal or char from paper, how to produce valuables from old cloth, plastic bags, old braids and all sorts of waste. Formore information use this link


Permaculture Design Course
Is it right? On one hand you want to reduce your work on the longterm view and on the other you want to get the maximum out of it? The Permaculutre Design Course looks like to be the right thing for you. By observing nature we can use natural patterning to make holistic designs and implement ideas and systems that build on natural processes with energy efficiency, low cost and high yeilding results. We expect that our PDC graduates will leave this course ready to design and implement permaculture into a wide range of scenarios; from urban permaculture systems to small farms and community projects. For more information use this link


Training of Trainers
You want to become a successful facilitator in agriculture? We build up your capacity to work in the field and give your best to your participants. Learn how to prepare sessions, conduct sessions, evaluate sessions make your sessions interesting and participatory, learn how to probe and get more from you participants as you build up their knowledge, skills, understanding and attitudes. Let us help you bring out your full potential for a trainer or facilitator. For more information use this link


Asasi zaidi ya 500 zaunga mkono rasimu ya pili ya Jaji Warioba 

KAULI ya Rais Jakaya Kikwete wakati wa ufunguzi wa Bunge la Katiba na Waziri wa Nchi,  Ofisi  ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu, William Lukuvi kwamba muundo wa serikali tatu utatoa mwanya kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuchukua nchi ni vitisho dhidi ya maoni ya wananchi wanaotaka serikali tatu.

Akizungumza na Makangale Satellite blog Tanzania hivi karibuni jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya mkutano wa waandishi wa habari uliondaliwa na Asasi za Kiraia kuhusu mwenendo wa mchakato wa kutunga katiba Mpya, Mkurugenzi Mtendaji wa Youths Partnership Countywide (YPC), Israel Ilunde amesema kwamba kauli ya Rais Kikwete wakati wa uzinduzi wa Bunge la Katiba ni kutisha wananchi dhidi ya maoni yao kuhusu serikali tatu.

“kimsingi baada ya Rais kutoa maoni yake kwamba serikali tatu itatoa nafasi kwa jeshi kuchukua nchi ni kutisha wananchi wa Tanzania dhidi ya maoni yao ambayo yapo kwenye rasimu ya pili iliyowasilishwa na jaji warioba,” amesema
Ilunde amesema kwamba si kweli kwamba muundo wa serikali tatu italifanya jeshi la wananchi wa Tanzania kuchukua madaraka bali ilikuwa mbinu ya Rais kikwete kutisha na kuwatia hofu wananchi ambao wanataka serikali tatu.

Aliongeza kwamba Waziri Lukuvi aliongeza chumvi kwenye mkutano na baadhi ya viongozi wa dini kwamba serikali tatu itakuwa rahisi kwa JWTZ kuchukua nchi wakati kimsingi ni upotoshaji mkubwa.

“viongozi wakuu wa serikali wamewatisha wajumbe wa bunge maalum la katiba na wananchi kwa ujumla kuhusu swala la serikali tatu ni kinyume kabisa na katiba ya mwaka 1977,” alisisitiza
Kwa upande wake, Mratibu wa Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu, Onesmo Olengurumwa amesema kwamba Bunge la katiba linatumia mamlaka yake vibaya kwa kutaka kuhodhi kila kitu.

“Tume ya Jaji warioba imefanya kazi nzuri ya kuandika rasimu na bunge maalum ya katiba na kuijadili na kuibariki tu rasimu ili iende kwa wananchi na si kubadilisha rasimu yenye maoni ya wananchi,” amesema
Amesema kwamba bunge la katiba halina mamlaka ya kisheria kubadili rasimu ya pili iliyotengenezwa na Tume ya warioba kwa sababu ni kinyume na matakwa ya kisheria.

Awali, Mwenyekiti wa Umoja wa AZAKI wa kutetea Rasimu ya wananchi, Irinei Kiria amesema kwamba asasi za kiraia zaidi ya 500 wanaunga mkono rasimu ya pili ya katiba mpya kwa kuwa imekidhi mahitaji ya watanzania.

“kwamba hatujafurahishwa na mijadala ndani ya bunge maalum la kutunga katiba mijadala ambayo imepoteza utaifa na badala yake imejikita kwenye kutoheshiminiana, ubabe, ubaguzi, vijembe na vitisho,” aliongeza
 Amesema asasi za kiraia wamehuzunishwa na tabia ya kudhihaki na kudharau rasimu ya pili pamoja na Tume ya Mabadiliko ya katiba pamoja na Mwenyekiti wake.

Mwisho


RAIS Jakaya Kikwete ametoa maagizo ya haraka ya utayarishaji mpya wa mfumo (Procurement) wa ulinzi katika viwanja vyote vya ndege nchini katika harakati za kudhibiti usafirishaji na uigizaji wa madawa ya kulevya Tanzania. Makangale Satellite inaripoti.
 

  Rais Jakaya Kikwete akisalimia na maofisa wa uwanja Julius Nyerere International Airport (JNIA) wakati akiingia katika uwanja huo na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria jijini Dar es Salaam.

Rais Kikwete alitoa rai hiyo katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria Julius Nyerere International Airport (JNIA) jijini Dar es Salaam kwa kusema inakera sana kuona wasafirishaji wa dawa za kulevya kukamatwa Afrika ya Kusini.
 
Rais Kikwete akisisitiza jambo baada ya kuona uchoro wa jengo jipya la abiria na mfumo wa ulinzi kutoka, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Injia Suleiman Suleiman mwenye tai nyekundu

“sisi wengine tunaumia sana kusikia msanii fulani au mwanamuziki kukamatwa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini, mtu unajiuliza kapitaje hapa uwanja wa ndege dar au kwa kuwa msanii tu lakini inakera na ninaumia sana,’ amesema Rais Kikwete amesema lazima mamlaka za viwanja vya ndege kwa kushirikiana na wizara na wadau wengine waunganishe nguvu zao katika kupambana tatizo hili la dawa za kulevya kwa kuwa linaichafua nchi nzima kimataifa na kikanda.
 

Rais Kikwete na Waziri Mwakyembe wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo jipya la abiria (Terminl Three)
Rais Kikwete aliongeza kwamba lazima mamlaka zinazohusika zianze mara moja kutengeneza mfumo madhubuti wa ulinzi katika viwanja vya ndege hasa wa Dar es Salaam na KIA kule kilimanjaro ambazo ndio njia kuu za usafirishaji wa madawa hayo.
 

 Rais Kikwete baada ya kuweka jiwe la msingi na kuashiria ujenzi wa jengo jipya umeanza rasmi

Amesema lazima kasi ya kupambana na usafirishaji na uigizaji wa dawa za kulevya kupitia viwanja vya ndege iongeze na siyo kusuasua miaka miwili au mitatu ya kutengeneza mifumo ya ulinzi ya kimataifa.


Rais Kikwete amesema kwamba kama kuna watumishi wa idara ya forodha (TRA), Mambo ya Ndani au Polisi wanaoshirikiana na wauza madawa ya kulevya apewe majina yao na watashughulikiwa mara moja.


“tusimuonee haya mtu yeyote hata kama ni mtumishi wa umma kwa sababu tunaonekana wote tunajishughulisha na biashara hiyo haramu ni lazima tuchukue hatua madhubuti,” aliongeza Rais Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na mwandishi wa habari hizi muda mfupi baada ya Rais kuweka jiwe la msingi amesema kuwa tayari Mamlaka ya viwanja vya ndege (TAA) wameshaweka mifumo hiyo yaani (Procurement) katika kudhibiti dawa za kulevya.
 
Amesema kuwa katika jengo jipya la abiria (Terminal three) kuna hatua tano za kukagua madawa ya kulevya na aina nyingine ya vitu visivyoruhusiwa katika uwanja wa ndege kwa hiyo serikali imejipanga kumaliza kabisa tatizo hili nchini.


“kimsingi mifumo hii ipo tayari katika jengo hili jipya la abiria na kama kuna mtu atapitisha dawa za kulevya basi nitampa zawadi ya fedha,’ amesema Dkt Mwakyembe

Dkt Mwakyembe alisisitiza kwamba katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya lazima wizara na TAA watashirikiana na wadau wengine kama vile Mamlaka ya Mapato (TRA) kupitia idara ya forodha, wizara ya mambo ya ndani yaani Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).


Hayo yanakuja wakati taarifa zilizopo ni kwamba wasafirishaji wa dawa za kulevya kuanza kutumia fukwe ndogondogo za bahari nchini kuziingiza kutoka Mashariki ya mbali.


Mwisho.

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.