Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali kwenye red carpet wakati wa sherehe ya siku ya wanawake duniani iliyowakutanisha wanawake kutoka kila kona ya visiwani Zanzibar ambayo iliandaliwa na Kikundi cha Wanawake cha Zanzibalicious na kufanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya hoteli ya Bwawani.

DSC_0148
DSC_0099
DSC_0095
Mbunifu wa mavazi kutoka bara Mama wa mitindo Asia Idarous (kushoto) akipozi na mbunifu wa mavazi kutoka visiwani Zanzibar Matilda Ishungisa wa Malty design.

DSC_0092
DSC_0106
Makamu mwenyekiti wa kikundi cha Wanawake wa Zanzibalicious, Zaning'ha Otembo.

DSC_0109
DSC_0111
DSC_0055
Mwenyekiti wa kikundi cha Wanawake wa Zanzibalicious Bi. Evelyne Wilson.

DSC_0057
DSC_0034
DSC_0035
DSC_0041
DSC_0043
DSC_0045
DSC_0052
Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe Thuwaiba Kisasi.

DSC_0066
Wanaume nao hawakubaki nyuma kutoa sapoti kwa wanawake.

DSC_0113
Mama wa mitindo Asia Idarous aking'ara kwenye red carpet.
DSC_0119
DSC_0125
DSC_0128
Kutoka kushoto ni Make up artist Sada, Mama wa mitindo Asia Idarous na MC wa sherehe ya siku ya wanawake duniani visiwani Zanzibar, Mishi Bomba ambaye pia ni mtangazaji wa Magic FM.

DSC_0131
DSC_0134
DSC_0139
DSC_0141
DSC_0143
DSC_0155
DSC_0162
Mke wa Naibu Waziri wa Afya serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Zakhia Kombo (kulia) akiwa na Mama wa mitindo Asia Idarous. Kwa picha zaidi bofya link hii

Picha na taarifa hii tumeshirikishwa na Zainul Mzige

CORPORATE SOCIAL RESPONSIBILITY PROGRAMME MANAGER
Forestry, Iringa, Tanzania
Ref
13979
Mar
16
A fabulous opportunity for CSR programme Manager in a forestry company. The ideal candidate should be self-driven and capable to implement, improve and develop strategies that can provide effective growth of the company.

Reporting Structure

Reporting To
Country CEO
Supervision Of
Community Development Officers
Interacts With
staff


Job Description
  1. Oversight and management of all community development projects in the communities surrounding the plantations
  2. Implement a comprehensive monitoring and evaluation system which measures the effectiveness of community development projects
  3. Lead the annual budgeting process for the corporate responsibility programme
  4. Drive fund raising strategy and implementation in Tanzania
  5. Support forestry operations in ensuring highest international labor health and safety practices
  6. Provide proactive, cooperative support in dealing with operational issues
  7. Provide support to the forestry management team in the Forest Stewardship Council certification and auditing processes, particularly in the social area.
  8. Manage the recruitment and performance of staff.
  9. Advise the CEO and Chief Impact Officer regularly to identify, assess, measure and monitor major business risks .


Candidate Specification

Experience
7 years
Education Level
Degree
Qualifications
Bachelor
Software
Ms Office application
Equipment
Industry related


Knowledge Of
management, fund raising for sizeable program budgets
Skills To
communication skills, budgeting, financial management and programme
Ability To
solve problems, mentor
Personality
Hard working
Other



Organisation

Industry
Forestry
Culture
Multicultural
Gender Profile
Mixed
Age Profile
Between 26 and 55 years of age


Terms And Conditions

Employment
Permanent
Location
Iringa, Tanzania
Remuneration
Negotiable

Application: You must be registered with CVPEOPLEAFRICA.com to apply for this position.

photo 4
Pichani juu na chini ni baadhi ya majengo yaliyokamilika ya Shule ya msingi Kakuni yaliyojengwa na Waziri Mkuu Pinda kupitia michango ya wadau wa maendeleo.


Kila mmoja wetu anatambua mchango mkubwa wa elimu hasa ile inayotolewa ikiwemo ngazi ya Awali, Msingi, Sekondari na elimu ya juu ikiwemo chuo. Pia katika hilo ni jamb la msingi sana na la maana hasa unapokumbuka mahala ulipopatia elimu husika.
Mtandao huu wa Mo dewjii blog tunapenda kuungana na kumpongeza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa juhudi zake za dhati kabisa katika kuhakikisha shule yake aliyowahi kusoma hapo inasaidiwa na kufikia malengo yake.
Waziri Mkuu alipaata elimu yake katika Shule ya msingi Kakuni. Kwa kusoma hapo darasa la kwanza hadi la nne. Lakini kwa mapenzi mema na juhudi za kutaka kuona watoto wa hali ya chini hasa wa wakulima wanapata elimu bora, kwa juhudi zake binafsi, ameweza kusaidia shule hiyo ikiwemo kutafuta wafadhili mbalimbali wa kuipiga tafu, akiwa kama Mizengo Pinda. Ambapo unaweza kusoma kiunganishi hichi hapa cha mtandao ili kusoma habari hiyo zaidi ya wadau kumuunga Waziri Mkuu Pinda katika kuisaidia shule ya Kakuni: http://dewjiblog.com/2015/03/11/japan-yachangia-sh-milioni-160-shule-ya-msingi-kakuni/
photo 1
Mtandao huu unapongeza juhudi hizo za Waziri Mkuu Mizengo Pinda hivyo pia nawe ukiwa ni miongoni mwa unayeguswa na maendeleo ya elimu hapa nchini, ni wakati wa kutembelea shule yako uliosoma awali iwe elimu ya ‘vidudu’ yaani Chekechea/Awali, Shule ya Msingi ama Sekondari basi ni wakati wa kurejea na kusaidia chochote kile ili kuendeleza Elimu hapa Nchini.

Bila shaka kama Watanzania tutaiga juhudi hizi za Waziri Mkuu Mizengo Pinda, bila shaka elimu ya Tanzania itapanda maradufu kwani tumeweza kushuhudia kwa upande wa juhudi hizo za Mizengo Pinda ikiwemo kushawishi wadau ikiwemo Serikali ya Japan, kutoa msaada wa dola za Marekani, 90,286, ambazo ni sawa na Sh. Milioni 160.

Fedha hizo ni kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Shule ya Awali kwenye Shule ya Msingi, Kakuni iliyopo kijiji cha Kibaoni, Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi.

PM-PINDA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mizengo Pinda.

Juhudi za Mizengo Pinda za kuanzisha wazo hilo la kusaidia kuijenga shule yake ni kama njia ya kumshukuru Mungu na kuwashukuru wananchi waliosaidia kumfikisha hapo alipo. 

Kwani alipata kusoma darasa la kwanza hadi la nne katika shule ya msingi Kakuni mwaka 1957 hadi 1960.
Hivyo, tunatambua wapo wasomi wengi, wapo wabunge, wapo Mawaziri, wapo Wakurugenzi na wengine wenye vyeo vikubwa Serikali, sekta binafsi na waliopo ndani nje ya nchi, shime tujitokeze kwa wingi kwa kila mmoja kwenda kwenye shule aliyosoma na kuchangia chochote.

Tunatambua sisi tumepata elimu wakati gani na kiwango cha elimu wakati huo kilikuwaje, hivyo tutakapojitokeza kama alivyofanya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, hii itasaidia kukuza elimu yetu hapa Nchini.

photo 3
Muonekano wa majengo yaliyokamili ya shule ya msingi Kakuni alipopata elimu ya msingi Waziri Mkuu Pinda na kuamua kuijenga upya kwa gharama ya zaidi ya Shilingi bilioni 1.3/- kutokana na michango ya wadau mbalimbali wa maendeleo.
photo 5

Mwanamapinduzi na Rais wa zamani wa Burkina Faso Thomas Sankara alisema kuwa ili kuleta mabadiliko ya kimapinduzi ni lazima kuwa na hali fulani ya uendawazimu. Ila tusiufikirie uendawazimu huu wa kuokota makopo bali ule ukichaa mzuri wa kuamini katika mambo au misingi fulani na kuisimamia kwa dhati pamoja na changamoto nyingi.
Zitto akiwashukuru wananchi wa Kigoma
Kwa kuamini kwa dhati katika mabadiliko haya na kutaka kuboresha maisha ya wanakigoma, mwaka 2005 nilikuja kwenu kuwaomba ridhaa ya kuwatumikia kama mwakilishi wenu Dodoma. Nikiwa na umri wa miaka 29 tu. Labda ulikuwa ni msukumo wa matumaini yangu makubwa yanayoambatana na ujana yaliyowashawishi, kwani mliniamini na kunipa kazi hiyo ya heshima kubwa ya kuwawakilisha.

Mwaka 2010 mliniamini tena, naamini kutokana na utekelezaji wangu mzuri wa kazi na mafanikio tuliyoyaweza kuyapata katika jimbo letu. Hivyo kwa miaka kumi tumekuwa bega kwa bega katika safari hii ya pamoja ya kujenga na kuiendeleza jimbo letu, na leo nimekuja kuwashukuru kwa fursa mliyonipa kwani safari yetu inafikia mwisho. Fursa mliyonipa ni ya kipekee kwani ilikuwa fursa si tu ya kuwatumikia ninyi bali kulitumikia Taifa langu.

Katika miaka kumi hii kuna mambo makubwa tumeyafanya pamoja na kufanikiwa; na kuna mambo ambayo hatukuweza kuyafanya. Kwa yale ambayo hatukuweza kuyafanya naomba radhi. Kwa yale ambayo tumeweza kuyafanya naomba kuwapongeza sana kwa kufanikisha. Kwani kama Mwalimu Nyerere alivyotuambia kuhusu Uhuru na Maendeleo: “Uongozi ni kuongea na kujadili na wananchi, kuwaelewesha na kuwashawishi. Uongozi ni kufanya kazi pamoja na wananchi na kuonyesha kwa vitendo mnachotaka kufikia. Uongozi ni kuwa mmoja wa wananchi na kutambua kuwa mko sawa…. Wananchi hawawezi kuendelezwa bali wanajiendeleza.” Na ndivyo tulivyofanya kwa miaka kumi, na kwa ushirikiano wenu tumeweza kufanikisha miradi mikubwa katika Jimbo letu.

Mwaka 2005 tulikuwa hatuna barabara ya lami hata moja. Leo hii, ninapoongea nanyi tuna barabara za lami zenye zaidi ya kilomita 100 kuunganisha Jimbo letu na majimbo mengine kwa pande zote za nchi kavu. Vilevile tuna mradi mkubwa wa kuunganisha vijiji vya ufukweni mwa Ziwa Tanganyika kwa barabara. Kiujumla kwa mkoa wa Kigoma tumefanikiwa kumaliza daraja la Malagarasi na hivyo kuunganisha mkoa wetu na mkoa wa Tabora kwa lami jambo ambalo lilikuwa kilio chetu cha muda mrefu sana tokea enzi na enzi. Muhimu zaidi ni kuwa barabara hizi zinatumika na wananchi, wafanyabiashara na wakulima ili kuwasiliana, kufanya biashara na kupanua masoko.

Tumefanikiwa kuongeza huduma ya Nishati ya Umeme kwa kuunganisha vijiji zaidi ya 16 hivi sasa. Changamoto kubwa iliyobakia mkoani kwetu ni uzalishaji mdogo wa umeme na wenye gharama kubwa sana. Suluhisho la kudumu ni kufanikisha mradi wa Malagarasi wenye uwezo wa kuzalisha 44MW ambao utakuwa nafuu na kuwezesha pia kusambaza umeme mikoa jirani ya Katavi na Tabora, na hata kuuza nchi jirani ya Burundi. Viongozi wa kisiasa wa mkoa wa Kigoma watakaoingia kwenye uongozi baada ya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka 2015 hawana budi kuweka kipaumbele kikubwa kwa mradi huu. Bila ya umeme wa uhakika na nafuu hatuwezi kupiga hatua ya kuongeza thamani ya mazao yetu kwa kujenga viwanda vya usindikaji na kuongeza ajira ya vijana wetu.

Tumefanikiwa kuanza miradi ya Bandari na Soko kubwa kijiji cha Kagunga. Lengo likiwa ni kukuza biashara ya bidhaa kati yetu na nchi ya Burundi. Kigoma ni mji wa biashara kiasili na biashara ilichukua nafasi kubwa ya uchumi wa mkoa huu kwa miaka mingi sana. Kuimarishwa kwa miundombinu ya Biashara ni sehemu ya miradi ya kimkakati katika kuuweka mkoa kuchukua nafasi yake ya kiuchumi katika nchi yetu. Katika muktadha huo ndio maana tunaendelea na miradi ya Bandari Kibirizi na Bandari ya Nchi Kavu Katosho. Ndio maana tunaendelea na mradi wa Kituo cha Usafirishaji Mwandiga ( Mwandiga International Transportation Terminal ) na eneo maalumu la kiuchumi Ujiji. Haya yote tuliyaanzisha kwa pamoja nanyi ili kuhakikisha kuwa uchumi wetu unazalisha ajira kwa watu.

Tumefanikiwa kuongeza udahili wa wanafunzi wa sekondari kwa kuwa na shule katika kata na baadhi ya kata tumejenga shule kila kijiji. Hata hivyo, tuna changamoto kubwa sana ya ubora wa elimu katika mkoa wetu. Katika jimbo la Kigoma Kaskazini zaidi ya 90% ya watahiniwa wa Kidato cha Nne wanapata madaraja ya mawili ya chini, wakati ule daraja la nne na daraja la sifuri. Tumeanzisha mradi wa majaribio ya kutoa motisha kwa Walimu ili kuona namna bora zaidi ya kuhakikisha elimu inaboreshwa. Shirika la Twaweza linaendesha mradi mkubwa wa motisha kwa walimu na baada ya mwaka huu tutakuwa tumejifunza njia bora za kuongeza ubora wa elimu kwa watoto wetu. Bila Elimu bora miradi yote niliyoeleza hapo awali haina maana yeyote. Serikali imetoa Sera mpya ya Elimu, ni wajibu wetu kuona namna ya kuitekeleza katika ngazi yetu ili kupata mafanikio. Hata hivyo, uongozi wa kisiasa utakaoingia baada ya uchaguzi mkuu mwaka huu hauna budi kujielekeza vya kutosha katika elimu ya ufundi ili kujenga stadi za kazi kwa vijana waweze kujiajiri na kuajiriwa.

Tumefanikiwa kupanua huduma ya Afya kwa kuboresha Zahanati zetu chache zilizokuwepo na kujenga zahanati kadhaa mpya na miradi ya vituo vya afya vya Mahembe na Nyarubanda. Hata hivyo nasisitiza sana umuhimu wa kinga kuliko tiba kwani gharama za afya zimekuwa kubwa sana. Ndiyo maana tulipojadili hili suala, ilionekana kuwa suluhisho linatakiwa lipatikane kwa kufanya kile ambacho hatujawahi kufanya ili kuleta maendeleo ya kweli. Na mniruhusu hapa kunukuu wosia wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, alipotuasi kuwa “Maendeleo ni maendeleo ya watu. Barabara, Majengo, kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao na masuala mengi kama haya si maendeleo, bali ni vitendea kazi tu vya maendeleo” Ndiyo maana kulikuwa na umuhimu wa kutafuta njia mpya na mbadala kuboresha maisha ya mwananchi, hususan kwa upande wa afya. Uthibitisho wa ubunifu wetu ni kuwa katika kipindi hiki cha miaka 10 tumefanikiwa kuanzisha hifadhi ya jamii kwa wakulima.

Tulianza na Ushirika wa Wakulima wa Kahawa wa RUMAKU ambapo wananchi walijiunga na NSSF na hivyo kupata mikopo ya muda mfupi, huduma za afya bure na kujiwekea akiba kwa ajili ya mafao ya muda mrefu. Mafanikio makubwa yaliyopatikana yamewezesha wazo hili kusambaa nchi nzima na hivi sasa wakulima wa Korosho, Chai, Pamba, Tumbaku wanafuata nyayo za Wakulima wa Ushirika wa RUMAKU. Hapa Kigoma wazo hili sasa linatekelezwa kwa wavuvi wa mwambao mwa Ziwa Tanganyika. Ndoto yetu ni wananchi zaidi ya theluthi moja kwenye nguvu kazi wawe na Hifadhi ya Jamii. Natoa wito kwa wananchi wengine wenye uwezo wa kuchangia hifadhi ya jamii wajiunge na vikundi vya ushirika na kuchangia ili kufaidika na mafao ya muda mrefu kama pensheni lakini pia yale ya muda mfupi kama bima ya afya, mikopo kupitia SACCOS na mengine yatakayoanzishwa kama bima ya mazao.

Tumefanikiwa kujenga heshima ya watu wa Kigoma hapa nchini. Hivi sasa watu wa Kigoma tunatembea kifua mbele bila woga kuliko hapo awali. Kujiamini na kushiriki kikamilifu katika Ujenzi wa Jamhuri ya Muungano ni wajibu wetu kama raia. Changamoto za kujiona raia wa daraja la pili zimeondoka na zinaendelea kutokomezwa. Juhudi zetu ni silaha kubwa katika kuhakikisha tunakuwa sehemu ya Jamhuri yetu katika kila Nyanja za maisha yetu. Nafurahi kupata fursa ya kushiriki nanyi katika kujenga heshima hiyo ya Mkoa wetu. Nitaendelea kushiriki katika kudumisha heshima hiyo.

Nimejifunza mengi sana katika safari hii ya utumishi kwenu. Kama nilivyosema hapo awali, mliamua kufanya kile kisichozoeleka katika siasa ya nchi yetu kwa kunipa jukumu hili nikiwa kijana mdogo. Naamini kuwa ule ukichaa wangu mzuri wa kusimamia misingi ya kuleta maendeleo kwa wananchi wangu na kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia nimezipigania. Na katika safari hii nimejenga marafiki wengi sana na pengine hata maadui ingawa hao ni wachache. Lakini haijalishi kwani mi binafsi sina uhasama na binadamu mwenzangu.

Katika utumishi wangu kwenu, bungeni nimejifunza namna nchi yetu inaendeshwa. Katika kujifunza huko kuna mambo kadhaa nimefanya ya kujivunia na mengine ni makosa. Mliniruhusu kufanya makosa na kuyarekebisha makosa hayo kwa hiyo kukomaa zaidi. Shukrani za dhati ziwaendee wazee wangu ambao mliniongoza mpaka hapa tulipofika na kunishauri hata kunionya pale palipohitajika. Kwa ujumla nimejifunza kuwa mzalendo zaidi kwa nchi yangu na kuwatumikia watu wa nchi hii. Ndio maana hamkunisikia tu kutetea watu wa Kigoma pekee, bali watu maeneo mengine ya nchi yetu na makundi mbalimbali ya kijamii kama Wakulima, Wafanyakazi, Wasanii, Wavuvi, Wana michezo na wana habari.

Katika safari hii ya miaka 10 kuna watu nimewafurahisha na kuna watu nimewaudhi. Kwa wale niliowaudhi ninaomba radhi. Kwa wale niliowafurahisha ninaomba wasiache kuniongoza na kunishauri kila wakati. Haikuwa safari rahisi na sikutegemea iwe rahisi. Kiuhalisia ilikuwa safari ngumu yenye mafunzo makubwa kwangu. Ilikuwa ni safari yangu kama kiongozi na pia safari yangu binafsi ya kupevuka kifikra na kupata mafunzo kuhusu maisha. Ukifika ulikokuwa unakwenda katika safari, unaweza kutathmini mengi kuhusu safari hiyo, lakini mwisho wa siku unatakiwa ujue kama safari hii ilikuwa njema ama la. Ninajivunia safari hii na ninasema kwa dhati kabisa ilikuwa ni safari njema.

Ni wakati sasa wa kutoa nafasi kwa nguvu mpya kuongoza Jimbo letu. Kushika kijiti pale ninapoishia. Kurekebisha pale nilipokosea. Kuimarisha pale nilipofikia.

Sitakuwa mbunge wenu baada ya Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba lakini nitaendelea kutetea maslahi ya Mkoa wa Kigoma na Taifa letu kwa njia nyingine.

Sitaacha ule uendawazimu mzuri aliyoizungumzia Thomas Sankara unaoleta maendeleo ya kimapinduzi. Na misingi ni ileile na maadui ni walewale ambao mwasisi wetu Mwalimu Nyerere aliyokuwa anasema tupambane nao, yaani umaskini, ujinga, maradhi na sasa tumeongeza ufisadi. Kizazi chetu kina jukumu la kipekee kuendeleza mapambano haya na nitaendelea kuhakikisha tunafanya mapinduzi na kuwa na Taifa lenye misingi madhubuti ya uwajibikaji ili kuondoa kila aina ya ufisadi na kutumia rasilimali za nchi kuondoa umasikini, ujinga na maradhi.

Asanteni sana Kigoma Kaskazini!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgBM8KxdswAubyKIGHF7hbJWNdRplHyfs7viyxvvvf8HU7ZxpE4f-IIA6G612gQZzqNv4Tg9oY-E2ySYgrLEbXXC1m2YI3bZlCHUehvtu-Wua31TfocvkK9OvpZdGba9t0srqKGrKqDdMQE/s1600/Slaa+kuongea+na+waandishi.JPG
Dr. Willibroad Slaa akiwa anaongea na waandishi wa Habari jana jijini Dar Es Salaam mara baada ya kohojiwa na polisi kuhusu madai ya kutaka kuuawa na mlinzi wake binafsi
KIONGOZI mkuu wa upinzani nchini, Dk. Willibroad Slaa, amekoleza moto kuhusu madai ya kutokomeza maisha yake.

Dk. Slaa amelieleza jeshi la polisi jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi) kuwapo mpango wa kumuua uliokuwa unasukwa na baadhi ya viongozi wakuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).

Katibu mkuu huyo wa Chadema, ameiambia MwanaHALISI Online, muda mfupi baada ya kusajili maelezo yake kituo cha Polisi cha Kati, “Mungu bado ananipenda na anakipenda Chadema.”

Alisema, “Tumepata ushahidi usio na shaka kuhusu mpango wa kutaka kuniua. Kumekuwa na mawasiliano mazito sana kati ya maafisa usalama, viongozi wakuu wa CCM na mlinzi wangu. Mawasiliano haya yalilenga kudhuru maisha yangu.”

Amesema, “Tumebaini kwamba Idara ya Usalama wa Taifa walikuwa wanafanya ujasusi dhidi ya Chadema. Walikuwa wanatoa fedha kwa mlinzi wangu binafsi ili kumshawishi kuvujisha siri za chama. Jambo hili ni kinyume cha sheria ya kuanzishwa idara ya usalama wa taifa.

Amesema, kutaka kufanya au kutishia kuua, ni kosa la jinai, hivyo analitaka jeshi la polisi kuhakikisha mhalifu huyo, anakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Taarifa zinasema, aliyekuwa anashirikiana na TISS na viongozi wa CCM kutokomeza maisha ya Dk. Slaa, ametajwa kuwa ni Khalid Kagenzi.

Kwa mujibu wa mawasiliano katika simu ya Kagenzi, aliyekiri kushiriki njama za kumuua Dk. Slaa, waliokuwa wanawasiliana na Kagenzi, ni pamoja na Philiph Mangula, makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara; Gwamaka Mwang’onda na wengine kadhaa, ambao watachapishwa katika mtandao huu katika toleo lake la Jumamosi.

Akizungumza kwa uchungu na mwandishi wa gazeti hili, Dk. Slaa amesema, “Idara ya usalama wa taifa imepoteza heshima katika jamii na kuwataka viongozi wake wajiuzulu.”

Ametoa mfano wa nchini Marekani, kwamba “…ilipothibitika Rais Nixon na chama chake cha Republican walikuwa wamefanya ujasusi dhidi ya chama cha democrats, Rais Nixon alilazimika kujiuzulu. Hata CCM na idara yao ya usalama wa taifa wanafanya kosa kama hilo.”

Mwenyekiti wa CCM na ambaye ni Rais wa Jamhuri, ni Jakaya Kikwete.

Dk. Slaa amesema yeye alifika polisi kama mlalamikaji. Alitoa maelezo yake ili kuwawezesha kufanya kazi yao ya uchunguzi.

Amesema, “Sikuhojiwa kama baadhi ya watu wanavyofikiri. Mimi sio mtuhumiwa. Mimi ni mlalamikaji.”

Amesema haki zake zote zimezingatiwa alipokuwa polisi. Aliongozana na wanasheria watatu wa Chadema, Prof. Abdallah Safari, Nyaronyo Kicheere na John Mallya.

Prof. Safari, pia ni makamu mwenyekiti wa chama hicho, Tanzania Bara.

Zoezi la kuandika maelezo yake, lilitanguliwa na majadiliano kati yake na polisi ili kujenga picha ya pamoja kuhusu jambo litakalo andikwa.

Anasema, polisi waliuliza kama nataka waandike maelezo yangu wao au nataka kuyaandika mwenyewe. Nilichagua kuyaandika mwenyewe. Sheria inaruhusu hili pia.

Malalamiko yake yana kurasa tisa.

Akizungumzia wanachama watatu wa Chadema wanaoshikiliwa na polisi, Ahmed Sabula, Benson Mramba na Jacob Boniface (Diwani wa Ubungo), Dk. Slaa amesema, “Ni jambo la kusikitisha, muuaji yuko nje na waliozuia mauaji ndiyo wanaoshikiliwa.”

Habari ambazo zimepatikana baadaye zinasema, jeshi la polisi limeahidi kuwapa dhamana “makachero” hao wa Chadema kesho.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh0f309AsmPlk9hOaHD81YBHX11pMbXxraT_JJjskbI9zTLgY3Fp-U4MMMhd88I3P8-xemvKeiUwJ8yE5imZUtiaJmCVFfkFE7xw44pT8pq6cP9b1SDh2zXDx9V2iQqZQMG9Prz_QI2Xz67/s1600/Slaa+akitoka+Pols.JPG
Mawakili waliomsindikiza Dr. Slaa katika utoaji wake wa maeleo wakiwa na mteja wao mara baada ya kumaliza kutoa maelezo hayo.(Kushoto ni Mwanasheria John Mallya akifuatiwa na Nyaronyo Kicheere).



Mkurugenzi wa Kampuni ya Serengeti Brewers Ltd, Steve Gannon (kushoto) akimpa mkono wa pongezi Linah (katikati) baada ya kukubali kusaini mkataba wa kuwa Balozi wa Jebel.  Kulia ni meneja wa Linah, Tonny Akwesa, akishuhudia makabidhiano hayo

Akizungumza wakati wa makubaliano ya mkataba huo, mkurugenzi wa kampuni hiyo, Steve Gannon, alisema  wameamua kumpatia ubalozi wa kinywaji hicho Linah kufuatia uwezo wake mkubwa katika kuwashawishi wateja wao, na pia hiyo ni njia mojawapo ya kusapoti kipaji chake na itakuwa pia njia ya kushirikiana na wasanii wa Tanzania kwa kila kitu.

“Kampuni yetu imeingia mkataba wa mwaka mmoja na Linah ikiwa njia  ya kutambua sanaa ya muziki Tanzania.   Serengeti Brewers Ltd kupitia kinywaji chetu cha Jebel, tumefurahishwa na uwezo wa Linah hivyo tunaamini kupitia kwake tutaweza kupata manufaa makubwa ya kutangaza kinywaji chetu cha Jebel,” alisema na kuongeza:

“Tunatarajia kuanza naye kazi rasmi kwa kutengeneza video ya wimbo wake mpya ambayo ataifanyia katika nchi ya Kenya na Afrika Kusini.  Video hiyo itakuwa chini yetu, ila mkataba huu utambulike kwamba tunaanza na mwaka mmoja ingawa utakuwa endelevu zaidi.


Linah (kulia) akisaini mkataba  huo na Mkurugenzi wa Serengeti, Steve Gannon, ndani ya ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi kuu za kampuni hiyo Temeke, Chang’ombe, jijini Dar es Salaam.

Linah na Mkurugenzi wa Serengeti Gannon wakionyesha kinywaji cha Jebel.(P.T)

Steve Gannon akiangalia T-shirt yenye nembo ya kinywaji hicho mara baada ya kusainiwa na Lina

Akionyesha T-shirt hiyo baada ya kusainiwa na Linah

Linah akiongea jambo kwa waandishi wa habari baada ya kusaini mkataba



Mkurugenzi Masoko wa Serengeti, Cescar Mloka (wa pili kulia), akifurahia jambo akiwa ameshikilia kinywaji hicho na Linah.  Wengine ni Tonny Akwesa na Steve Gannon


Linah akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Serengeti.


 

Linah akiwa na wafanyakazi wa Serengeti.MSANII kutoka nyumba ya kukuza vipaji Tanzania  (THT) Estelinah Sanga ‘Linah’, leo ameingia mkataba  na Kampuni ya Serengeti Breweries Ltd, kupitia kinywaji chake cha Jebel.
 
”(Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)


Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.