2026

Arsenal 1-0 Chelsea (jumla 4-2): Gunners wafuzu kwenda fainali ya Kombe la Carabao baada ya Kai Havertz kufunga bao la ushindi dakika za mwisho katika mkondo wa pili wa nusu fainali.

Arsenal wameingia fainali ya Kombe la Carabao kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-2 dhidi ya Chelsea; bao la Kai Havertz aliyetokea benchi liliihakikishia Arsenal ushindi wa 1-0 katika mkondo wa pili uliokuwa na ushindani mkali; Arsenal watakutana na ama Manchester City au Newcastle kwenye fainali.


Habari kwa msaada wa Skysports.

Arusha, Januari 29, 2026

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Dkt. Bill Kiwia, leo (Januari 29, 2026) amefanya ziara katika Ofisi za Makao Makuu ya Compassion International Tanzania (CIT) zilizopo jijini Arusha. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Dkt. Bill Kiwia na Bi. Mary Lema Mkurugenzi wa Compassion Internation Tanzania (CIT) wakibadilishana hati za makubalino.

Ziara hii ni moja ya mikakati ya HESLB ya kutafuta wadau wa kimkakati ili kuongeza vyanzo mbadala vya ufadhili (alternative financing) kwa wanafunzi katika elimu ngazi ya kati na elimu ya juu nchini.


Dhana hii inaendana na maono ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha vijana wa kitanzania wanafikia ndoto na malengo yao  kielimu.

Aidha, katika ziara hiyo Dkt. Kiwia na Bi. Mary Lema Mkurugenzi wa Compassion Internation Tanzania (CIT)  wamesaini tamko la nia ya kushirikiana (Statement of Intention to Collaborate) ili kuweka utaratibu madhubuti wa kuwatambua wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu ili wapewe kipaumbele katika utoaji wa Mikopo. 

Aidha mashirikiano haya yatalenga  kutafuta vyanzo mbadala vya rasilimali fedha kwa ajili ya kuongeza wigo wa wanufaika wa mikopo na ruzuku kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, Yatima na wanaotoka katika Kaya masikini. ‎



Na Mwandishi wetu

Bank of Africa Tanzania (BoA) imeshiriki katika maadhimisho ya wiki ya Huduma ya Kifedha yaliyoandaliwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango  yaliyofanyika  katika viwanja vya Usagara vilivyopo jijini Tanga.



Yakiwa na kauli mbiu isemayo “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi,” malengo makuu ya maadhimisho hayo yalikuwa ni kuongeza uelewa, kuboresha ufahamu na hatimaye kuhamasisha mabadiliko ya tabia za wananchi katika usimamizi wa fedha na matumizi ya huduma rasmi za kifedha.



Aidha, tukio hilo lililenga kuwahamasisha Watanzania kutumia huduma rasmi za kifedha kama sehemu ya jitihada za kupunguza kiwango cha umaskini katika jamii, ili kufikia maendeleo ya kiuchumi jumuishi na endelevu.



Mpaka sasa Tsh 8 billioni zimetolewa kwa malipo ya mrahaba  

‎Na Mwandishi Wetu, Tarime 

‎Miradi mipya ya kijamii imeanza kutekelezwa kwa kasi katika vijiji vitano kutokana na fedha za gawio wa mrabaha wa asilimia moja zilizotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara katika miaka ya hivi karibuni  ambazo zimekuwa zinawekwa kwenye akaunti za benki kwa muda mrefu bila matumizi ya yoyote ili kuleta matokeo Chanya kwa wananchi.


‎Kila robo ya mwaka  vijiji vya Genkuru, Nyangoto, Kerende, Nyamwaga na Kewanja ambavyo vipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Mkoani Mara vimekuwa vikipokea gawio la mrabaha kutokana na  haki ya kuchimba dhahabu katika shimo la Nyabigena (ambalo ni sehemu ya Mgodi wa Barrick North Mara) kabla ya kampuni ya Barrick kukabidhiwa kuendesha mgodi huo kwa ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals kuanzia mwaka 2019.

‎‎Wakizungumza na waandishi wa habari jana, viongozi wa vijiji hivyo walisema fedha hizo za mrabaha zimeelekezwa kwenye miradi ya kijamii inayogusa mahitaji ya wananchi wengi.

‎‎Katika kijiji cha Genkuru pekee, zaidi ya Tsh 2 bilioni zilizotokana na mrabaha zimeelekezwa kwenye ujenzi na ukarabati wa miradi mbalimbali ya elimu, afya, barabara na ununuzi wa eneo la kujenga soko. “Tulianza na ukarabati wa barabara yenye urefu wa kilomita 7.8  na nyingine yenye urefu wa kilomita zaidi ya tatu inayounganisha kijiji chetu cha Genkuru na kijiji jirani cha Msege, na utekelezaji wa miradi hii umefikia asilimia 90.

‎“Kwa upande mwingine, tumetumia sehemu ya fedha yetu ya mrabaha kununua mashine ya usingizi ya Kituo cha Afya Genkuru,” alisema Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Genkuru, Juma Elias Kegoye. ‎Kegoye anaongeza kuwa wametumia sehemu ya fedha hiyo pia kununua (microscope) ya kupima wagonjwa na kwenye ujenzi wa nyumba pacha ya watumishi katika kituo hicho cha afya.

‎‎Lakini pia, alisema wanakarabati nyumba ya mwalimu katika Shule ya Sekondari Bwirege, nyumba saba za walimu katika Shule ya Msingi Genkuru na ujenzi wa jengo la utawala wa shule ya msingi mpya ya Kerondo. “Miradi mingine inayotekelezwa ni ujenzi wa jengo la utawala katika shule ya msingi mpya ya Kuruya na ununuzi wa viti 350 na meza zake kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Bwirege,” aliongeza Kegoye


Alitaja mradi mwingine uliyo kwenye mpango wa kutekelezwa kutokana na fedha za mrabaha kuwa ni ujenzi wa nyumba ya walimu katika Shule ya Msingi Rewandwi. “Tunajenga pia vyumba vinne vya madarasa na kuchimba matundu sita ya vyoo katika shule hiyo ya Rewandwi,” aliongeza Mwenyekiti Kegoye.

‎Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kewanja, Joshua Chacha - maarufu kwa jina la Chia, alisema: “Sisi tumeelekeza fedha za mrabaha kwenye ujenzi wa nyumba pacha (two in one) ya walimu katika Shule ya Msingi Kewanja.”

‎“Vilevile, tunajenga nyumba pacha ya watumishi katika zahanati ya kijiji chetu,” aliongeza Chia na kubainisha kuwa miradi yote hiyo ilitengewa  Tsh  milioni 280 zilizotokana na gawio la mrabaha.

‎Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nyamwaga, Emmanuel Wankaba, alitaja miradi inayotekelezwa katika kijiji hicho kutokana na fedha za mrabaha kuwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba saba vya madarasa ya shule ya msingi mpya ya Maika. “Sambamba na vyumba hivyo vya madarasa, tunajenga jengo la utawala na nyumba ya kuishi familia mbili za  walimu na tunakarabati nyumba ya mwalimu katika Shule ya Msingi Nyamwaga,” aliongeza Wankaba.

‎Alitaja miradi mingine iliyo kwenye mpango wa kutekelezwa kijijini hapo kuwa ni ukarabati na uzibuaji wa barabara mbili zenye urefu wa kilomita zaidi ya 10 na uwanja wa michezo wa Shule ya Msingi Nyamwaga. Viongozi hao wa vijiji walisema utekelezaji wa miradi mingi uko katika hatua za mwisho kukamilika na kwamba wananchi wameipokea kwa furaha - wakitarajia kuona maboresho ya huduma za kijamii na kuchochea maendeleo katika maeneo yao.

Dar es Salaam, Tanzania- Bank of Africa Tanzania yawapa mbinu mpya wafanyabishara wa kati na waodogo jinsi ya kupanua wigo wa biashara , matumizi , elimu ya fedha , uwekezaji wa kimkakati ili kusaidia ukuaji wa biashara zao nchini.

‎Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika mafunzo hayo, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo , Bw Hamza Cherkaoui alisema kwamba sekta ya SME ina mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa Tanzania , utoaji wa ajira na kuboresha maisha ya watu wenye kipato cha kati na kidogo.

Bank of Africa Tanzania , Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Biashara) , Bw Hamza Cherkaoui akizungumza kwenye mafunzo ya siku moja ya masuala ya usimamizi wa fedha na biashara katika muendelezo wa utaoaji wa mafunzo kwa wafanyabiashara nchini ‘SME Clinics’ yaliyowakutanisha wafanyabiashara zaidi 100 jijini Dar es Salaam 

‎“Takribani wafanyabiashara na wajasiriamali 100 wamehudhuria mafunzo haya ya elimu ya fedha na kupata mbinu za kuweza kuvuka changamoto na vikwazo vyao vya kibiashara kwa kupata mafunzo kutoka kwa wataalamu wa fedha waliobobea,” 

‎Aliongeza kwenye mafunzo hayo wanapata fursa na nafasi ya kukutana na kupanua wigo wa mtandao wa ushirikiano wa kibiashara na kutafuta masoko mapya ya bidhaa zao kwa kupata fursa za majukwaa mapya ya biashara.

‎“tuna matawi sehemu mbalimbali za Africa , kuanzia Kigali, kampala , Lubumbashi na sehemu zingine na ni muhimu ukienda kufanya biashara huko mnaweza kutembelea matawi yetu na kuongeza wigo wa ushirikiano wafanyabiashara wa nchini hizo na kufungua fursa zingine za biashara Afrika Mashariki,” alisema Bw Cherkaoui 

‎Alisema kwamba Bank of Africa itaendelea kutoa mafunzo na ushirikiano na wafanyabiashara na wajasiriamali hapa nchini ili kuhakikisha kwamba wanakua pamoja katika kuboresha na kukuza uchumi wa nchini na mtu mmoja mmoja kwa kufanya biashara kwa ufanisi.

‎Kwa upande wake , Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa kati na Wadogo (SME) , Bi Beatrice Richard alisema kwamba wafanyabiashara waliopata mafunzo hayo wanatoka kwenye sekta tofauti kama vile usafirishaji , kilimo, vyakula , vifaa vya umeme, ujenzi na sekta ya fedha katika Mkoa wa Dar es Salaam,

Bank of Africa Tanzania,  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa kati na Wadogo (SME) , Bi Beatrice Richard akizungumza na wafanyabiashara wa kati na wadogo kutoka sekta mbalimbali (hawapo pichani) kwenye mafunzo ya siku moja ya mafunzo ya elimu ya fedha , biashara na masoko yaliyofanyika jijini Dar es Salaam

‎“Umuhimu wa kuendesha mafunzo haya ya fedha na biashara kwa wafanyabiashara wa kati na wadogo ni kuwasaidia kupanua uelewa wao uhusu maswala ya fedha , kodi na na jisni ya kupata masoko mapya ili kukuza mapato yao,” alisema Bi Beatrice 


‎Alifafanua kwamba katika kauli mbiu ya “kukua Pamoja” ni juhudi za benki katika kuhakikisha kwamba uelewa biashara kwa wafanyabiashara unaongezeka , jinsi ya kuweka akiba na mbinu za kuja na bidhaa mpya sokoni.

‎Naye mfanyabiashara ambaye alihudhuria mafunzo hayo , Ndugu Kahlan Mazrui alisema kwamba mafunzo ni muhimu wa wafanyabiashara kwa sababu inaongeza uelewa wa matumizi ya fedha na maswala ya kodi na jinsi ya kuzungumza na wateja ili kukuza biashara zao.

‎“Mimi ni Mkurugenzi wa Sokoni Microfinanc kupitia benki hii nimeweza kuwa na matawi 28 ya biashara ya ukopeshaji fedha kwa wajasiriamali wadogo wadogo na wajane hapa nchini ni hatua kubwa sana nimeipiga,” alisema 

‎Pamoja na mambo mengine mafunzo haya yalikuwa ni fursa adhimu kwa wafanyabiashara kupata nafasi ya kujifunza namna bora ya kuzungumza na wateja na uanzishwaji wa bidhaa na uelewa mahitaji ya soko husika, Aliongeza Mazrui 

‎Meneja wa Tawi Jipya la Lumumba la Bank of Africa Tanzania, Bi Gloria Victor alisema kwamba ni muhimu kwa wafanyabiashara kupata mafunzo ya fedha , mikopo na aina ya uwekezaji ambao unafaa.

‎Alisema kwamba Bank of Africa Tanzania wamefungua tawi jipya la Lumumba ili wajasiriamali na wafanyabiashara kupata huduma za kifedha na mikopo kwa karibu zaidi.

‎Bank of Africa Tanzania wamejikita katika kuhakikisha wanawapatia wajasiriamali wadogo na wa kati maarifa, nyenzo na masuluhisho ya kifedha wanayohitaji ili kustawi. 

 Baadhi ya wafanyabiahsara waliohudhuria mafunzo hayo ya “SME Clinics’ wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalamu wa fedha kutoka Bank of Africa Tanzania , jijini Dar es Salaam.

‎Kupitia programu kama SME Clinic, wanajenga ushirikiano endelevu na wa kudumu na wateja wao Kwa kauli mbiu ya , “Kuwezesha Ukuaji Pamoja” , wanadhihirisha dira yao ya kuwa mshirika wa kifedha anayeaminika anayekua sambamba na wateja wake  na sekta ya biashara  za Tanzania.

‎Warsha n mafunzo kama hayo hufanyika kila mwaka na  ikisisitiza dhamira yake ya utoaji wa elimu ya masuala ya kifedha inayo lenga kuwawezesha wajasiriamali na kusaidia ukuaji wa biashara zao nchini kote.

‎SME Clinic ni sehemu ya Programu ya Elimu ya Fedha ya Bank of Africa Tanzania , iliyoanzishwa mwaka 2021 kufuatia Kanuni za Ulinzi wa Watumiaji wa Huduma za Fedha za mwaka 2019. Kifungu cha 19 cha kanuni hizo kinahitaji kila mtoa huduma za kifedha kuandaa programu za elimu ya fedha kwa wateja wake. 

‎Tangu ilipoanzanishwa programy hii, Bank of Africa Tanzania  imefanikiwa kuendesha warsha hizi (SME Clinics) mikoa ya  Dar es Salaam , Mwanza na Kahama na tayari imeweza kuwafikia zaidi ya wateja 800. 

‎Kwa kauli mbiu ya mwaka huu  “ukuaji wa Pamoja”  SME Clinic inaendelea kutimiza malengo makuu ya benki yakiwemo, Kuunga mkono agenda ya Bank of Africa Tanzania  ya maendeleo endelevu hasa ahadi  yake namba 5, Kuhamasisha maendeleo ya watu kila maeneno na katika kutimiza Kanuni za Ulinzi wa Watumiaji wa Huduma za Fedha ya mwaka 2019.

‎Mafunzo hayo yanalenga kuboresha ujuzi katika usimamizi wa biashara kwa wateja, Kuimarisha uhusiano kati ya Bank of Africa Tanzania  na wateja wake, na Kuhimiza matumizi ya mifumo na teknolojia za kidijitali ili kuongeza ufanisi wa biashara.

‎Kuhusu Bank of Africa (T) Limited

‎BANK OF AFRICA – TANZANIA ni benki ya kibiashara binafsi inayofanya shughuli zake nchini Tanzania kwa kuhudumia wateja wakubwa, wateja wadogo na wa kati pamoja na wateja wa rejareja. Ilianza rasmi nchini Tanzania mwezi Juni 2007 baada ya kununua Eurafrican Bank ambayo ilikuwa inafanya kazi tangu Septemba 1995. BANK OF AFRICA – TANZANIA ni sehemu ya BANK OF AFRICA GROUP ambayo ilianzishwa mwaka 1982 nchini Mali.

‎BANK OF AFRICA GROUP ni kundi la kibenki la kimataifa barani Afrika, likifanya kazi katika nchi 18 za Afrika ikiwemo Afrika Magharibi, Afrika Mashariki, Afrika ya Kati, na pia ina ofisi Paris, Uhispania, London (Uingereza) na China. Tangu mwaka 2010, BANK OF AFRICA imekuwa kampuni tanzu inayomilikiwa kwa kiwango kikubwa na BMCE Bank, benki ya tatu kwa ukubwa nchini Morocco, yenye uwepo katika nchi 31 na mabara manne.

‎Kwa sasa, BANK OF AFRICA – TANZANIA ina matawi 17 ikiwemo 8 jijini Dar es Salaam na 9 katika mikoa mingine kama Arusha, Mwanza, Zanzibar na miji mingine mikuu.

Bank of Africa Tanzania , Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Biashara), Bw Hamza Cherkaoui akimkabidhi cheti mmoja ya wafanyabiashara aliyeshiriki mafunzo hayo ya masuala ya fedha yaliyoandaliwa na benki hiyo.

Bank of Africa Tanzania , Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Biashara0 Bw Hamza Cherkaoui akibadilishana mawazo na wafanyabiashara waliohudhuria mafunzo hayo ya masuala ya fedha , uelewa kodi na jinsi ya kupanua masoko ya bidhaa zao ,yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

‎Mwisho

Quality Assurance in Higher Education Conference: Integrating Artificial Intelligence for Institutional Excellence

26th –27th  March 2026 @ The Capital Empire, Sandton, Johannesburg.

 

Dear Colleague,

We are pleased to invite you to the Quality Assurance in Higher Education Conference: Integrating Artificial Intelligence for Institutional Excellence, a high-impact international forum designed to address one of the most critical transformations facing higher education today.

Under the theme "Harnessing AI to Transform Quality Assurance and Drive Global Competitiveness in Higher Education," this conference responds to the growing need for smarter, data-driven, and future-ready quality assurance (QA) systems. As higher education institutions navigate globalisation, digitalisation, and increasing accountability demands, traditional QA approaches are no longer sufficient on their own. Artificial Intelligence (AI) now offers powerful tools to enhance transparency, efficiency, and institutional performance.

This conference brings together senior university leaders, QA professionals, policymakers, ICT specialists, and EdTech innovators to explore how AI can be practically and ethically integrated into QA frameworks. Through keynote addresses, hands-on workshops, panel discussions, and a dedicated technology exhibition, participants will gain real-world insights into AI-driven performance monitoring, accreditation support, curriculum enhancement, and strategic decision-making.

Key highlights of the conference include:

·       Practical demonstrations of AI tools for QA and institutional performance monitoring

·       Regional and global case studies on successful AI integration

·       Expert discussions on policy, ethics, governance, and data protection

·       Strategic guidance on funding and investment models for AI-driven QA systems

·       Opportunities to build regional and international collaboration networks

Participants will leave with actionable strategies, an AI-integrated QA roadmap, and access to a post-conference implementation guide to support institutional transformation.

We believe your participation will add significant value to the dialogue while equipping you with the knowledge and networks needed to lead quality assurance innovation in your institution and beyond.

We would be honoured to have you join us and contribute to shaping the future of higher education. For registration or inquiries, please contact us at+27 (0)11 568 8240 / Email: admin@cskba.co.za.

Regards,

 

Asanda

CSK Business Architects

447 vale avenue

Randburg, Ferndale

South Africa

Call: +27 (0) 11 568 8240

Email:admin@cskba.co.za

Website. www.cskba.co.za

 Mgodi wa North Mara viongozi wake kwa asilimia 100 ni Watanzania

Dodoma:Waziri wa madini,Mh.Antony Mavunde amesema mgodi wa North Mara uliopo wilayani Tarime mkoani Mara ambao unaendeshwa na kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals umekuwa kinara katika kwa utekelezaji wa sheria na kanuni ya Maudhui ya Ndani (Local Content) ikiwemo upande wa ajira ambapo asilimia 100 ya viongozi wanaoendesha mgodi ni Watanzania.Mbali na viongozi wa mgodi huo pia Meneja wa Barrick nchini (Country Manager)  ni Mtanzania.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu mkakati wa Serikali wa kuhakikisha watanzania wanashiriki kikamilifu kwenye mnyororo mzima wa sekta ya madini alisema  kwenye miradi ya madini, amesema kumeshuhudiwa ongezeko la ajira kwa watanzania kutoka ajira 6,668 kati ya ajira 7,003 sawa na asilimia 95 kwa mwaka 2018 hadi kufikia ajira 18,853 kati ya ajira 19,356 sawa na asilimia 97 kufikia Desemba 2024.

Alisema katika nafasi zinazohitaji kupata uzoefu kutokana na kukua kwa teknolojia duniani, kumekuwa na utaratibu wa kisheria wa urithishwaji wa Watanzania kwa nafasi zinazoshikiliwa na Wataalamu wa Kigeni na kutoa mfano wa kampuni ya Barrick kupitia mgodi wake wa North Mara ambapo nafasi zote za juu za uongozi wanaoendesha shughuli kwa weredi mkubwa zinashikiliwa na Watanzania kwa asilimia 100.

Kupitia mkutano huo Waziri Mavunde pia alitangaza rasmi orodha ya Huduma na Bidhaa 20 zinazopaswa kutolewa Migodini kupitia kampuni zinazomilikiwa na watanzania kwa asilimia 100 ikilenga kuongeza wigo wa ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Madini ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kuhakikisha watanzania wanashiriki kikamilifu kwenye mnyororo mzimawa sekta ya madini baada ya kufanywa marekebisho ya Kanuni za Ushirikishwaji wa Watanzania kwenye Sekta ya Madini za Mwaka 2018.

‘’Kwa awamu ya kwanza tarehe 14 Novemba, 2025 Tume ya Madini ilitangaza orodha ya bidhaa na huduma zinazotakiwa kutolewa na kampuni zinazomilikiwa na kampuni za kitanzania kwa asilimia 100, ambapo kwa mara ya kwanza Tume ya Madini itatatangaza kupitia Kanuni 13A,’’ amesema Waziri Mavunde.

Akizungumzia manunuzi ya huduma na bidhaa kwa kampuni za kitanzania amesema yameongezeka kutoka kiasi cha Shilingi trilioni 1.85 kati ya manunuzi ya huduma na bidhaa za jumla ya kiasi cha Shilingi trilioni 3.01 sawa na asilimia 62 kwa mwaka 2018 hadi kufikia Shilingi trilioni 4.41 ambayo ni sawa na asilimia 88 ya kiasi cha Shilingi trilioni 5.00 ya manunuzi yote yaliyofanyika mwaka 2024.

Pia alisema Serikali inaendelea kufungua wigo kwa ushiriki wa watanzania katika sekta ya madini na kuongeza manufaa ya rasilimali madini kwa kutenga eneo maalum la uwekezaji la ulipokuwa Mgodi wa uchimbaji mkubwa wa madini ya dhahabu la Barrick Buzwagi lenye ukubwa wa ekari 1331, kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya kuzalisha bidhaa za migodini na kusema tayari viwanda sita vimekwisha jengwa huku wamiliki wa viwanda 15 wakionesha nia ya kujenga viwanda katika eneo hilo.

Waziri Mavunde ameitaka sekta binafsi nchini Tanzania kuchangamkia fursa ya usambazaji wa bidhaa na utoaji wa huduma migodini ili kuhakikisha fedha kiasi kikubwa inabaki nchini Tanzania na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

Amewasisitiza wawekezaji wote kuzingatia Sheria za madini na utekelezaji wa Kanuni za Ushirikishwaji Watanzania kwenye sekta ya madini sambambamba na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa zilizopo katika miradi ya madini ili kukabiliana na changamoto za ajira kwa manufaa ya mtu mmoja mmoja na manufaa ya taifa.

Waziri wa Madini , Anthony Mavunde akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) juu ya ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini nchini.

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.