Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuutangazia Umma na wadau wote wa Elimu nchini, kuwa mfumo wa Udahili wa pamoja yani Online Central Admission System (CAS), umefunguliwa rasmi tarehe 4 Machi, 2016, saa 6 mchana, kwa kupokea maombi ya mwombaji katika kozi mbalimbali, ikiwemo ngazi ya, Astashahada, Stashahada na Shahada kwa mwaka wa masomo 2016/17. Mfumo utajumuisha kozi zifuatazo;

1. Astashahada na Stashahada
2. Shahada za Elimu ya Juu
Mwombaji wa Astashahada na Stashahada anaweza kuomba kwa ajili ya eneo moja au zaidi katika maeneo ya taaluma yafuatayo;
1. Biashara na Utalii, mfano; Uhasibu, Meneja rasilimali watu, Wanyama pori, Mipango.
2. Sayansi shirikishi, mfano; Kilimo, Uhandisi, Mifumo ya mawasiliano, Usanifu majengo, Mifugo.
3. Afya, mfano; Uganga, Maabara, Ufamasia, Uuguzi
Ada ya maombi ni kama ifuatavyo;
1. Kwa eneo la Afya ada ya maombi ni Tshs 30,000/=.
2. Kwa eneo moja kati ya maeneo mengine yaliyobaki, ada ni Tshs 20,000/=
3. Kwa zaidi ya eneo moja la taaluma, mfano; Afya pamoja na Ualimu, ada ni Tshs 30,000/=, muombaji anaruhusiwa kuchagua maeneo yote.
4. Kwa waombaji wa Shahada za Elimu ya juu, ada ya maombi ni Tshs 50,000/=
Mwisho wa kutuma maombi haya ni tarehe 31/05/2016.
Bonyeza hapa kufanya maombi

Imetolewa na:
Baraza la Taifa la Elimu yaUfundi, 4 Machi, 2016

Source: http://nacte.go.tz/
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.