Kauli aliyoitoa Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholaus Musonye, dhidi ya kocha wa Yanga, Marcio Maximo, inanadimiza soka katika ukanda huo kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Shrikisho la mpira Afrka Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholaus Musonye

Musonye akizungumza na Mwananchi (Gazeti dada la Mwanaspoti), alisema Maximo aache woga wa kuhofia kufungwa kwa kupeleka kikosi cha pili kwenye mashindano ya kombe la kagame linaloanza leo jijini Kigali, Rwanda.

Musonye amemhukumu Maximo kwa kumwita mwoga bila ya kuzingatia programu ambayo kocha huyo amejipangia katika timu yake ya Yanga. Kauli aliyoitoa Musonye, pia imekuwa ikitolewa na baadhi ya wadau wa soka hapa nchini ambao nao mara kwa mara wanasema kocha huyo ni mwoga wa kufungwa.

Sitaki kuamini kama Maximo anaogopa kufungwa kwa kuwa atashiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara na atakutakana na upinzani, hivyo kama kufungwa atafungwa tu.
Naamini kocha huyo anajipanga na kuamini kile anachokifanya kwa ajili ya timu yake na kazi aliyopewa.

Watanzania wanaosema Maximo ni muoga watakuwa bado hawajaelewa falsafa ya kocha huyo kwani hata alipokuwa akiifundisha Taifa Starz, aliamnini katika kujenga timu kwa kuwatumia wachezaji vijana.

Maximo anajua anachokifanya katika kuandaa timu yenye ushindani tofauti na kauli ya Musonye.

Tatizo la watu wa Afrika Mashariki na Musonye akiwamo, tumekariri majina ya wachezaji wa soka tofauti na mipango ya kocha kama Maximo.

Tunapenda njia za mkato, ndiyo maana Tanzania na Kenya zimetolewa na  Msumbiji na Lesotho katika harakati za kuwania kufuzu makundi kuelekea fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Morocco mwakani.

Musonye alitaka Yanga ishiriki Kagame kama Tanzania na Kenya zilivyoshiriki mbio za kwenda Morocco dhidi ya Msumbiji na Lesotho, kwa kuwa hazikuwa na maandalizi ya kutosha,

Maximo hajakaa na kikosi chake chote na kuna wachezaji mpaka leo hii anaziona picha zao magazetini tu. Wachezaji aliokaa nao ni hao aliowachagua kwenda Rwanda.

Lakini mtu kama Musonye ambaye naamini hajui lolote kuhusu ukocha pamoja na kuwepo kwenye soka kwa muda mrefu, anaendelea na kukariri majina ya akina Mrisho Ngasa!

Katimu Mkuu huyo wa Cecafa hajiulizi kwa nini nchi za Malawi, Zambia, Lesotho na Zimbabwe zinapiga hatua katika soka?

Kwa nini Musonye anaendeleza siasa zilizozifanya nchi hizo kuanzisha shirikisho lao la Cosafa ambalo linaonekana kuwa na nguvu kuliko Cecafa?

Ikumbukwe kwamba wakati tukiwa pamoja, nchi zetu za Afrika Mashariki zilikuwa zikipata upinzani wa kweli kutoka kwao, Tanzania haikuwa na uwezo wa kuifunga Zambia!
Baada ya nchi hizo kujitoa na kuunda Cosafa, bado kina Musonye wanaendelea kupiga siasa zilizotufikisha hapa.

Musonye hawataki wachezaji vijana, eti hawawezi kufanya biashara anadhani kina Ngasa watacheza soka mpaka lini?

Naamini biashara ingeweza kuanguka kama timu mwenyeji angeingiza kikosi cha pili lakini kwa Yanga siioni madhara zaidi faida ya kuzalisha vipaji vinavyopotea.

Katika hili siiuoni uoga wa Maximo, kocha hawezi kuwabeba wachezaji kama mizigo kwenye mashindano.

Tanzania tunahitaji vipaji vipya, Maximo alikuwa na mkakati wa kuvizalisha kwa ajili ya Yanga, Taifa Stars na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Binafsi nitamhukumu Maximo kwa uwezo wake wa kufundisha uwanjani siyo wa kwa tuhuma za woga.

Makala hii imeandikwa na Mohamed Kuyunga kupitia Meseji Senti ya gazeti la Mwanaspoti kuyungajunior@gmail.com

Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wamewajia juu waliokuwa Wajumbe wa Kamati ya Kukusanya Maoni ya Katiba wakidai kuwa kazi yao ilishaisha, hivyo kuendelea kujadili masuala kuhusu Rasimu ya Katiba si sahihi.


Baadhi ya wajumbe hao walitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti jana, wakati wakichangia Azimio la Kufanyia Marekebisho ya Kanuni za Bunge Maalumu iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalumu, Pandu Ameir Kificho.

Mjumbe Dk Hamisi Kigwangwala, ambaye ni Mbunge wa Nzega, alisema ni vyema Mwenyekiti wa
Bunge, Samuel Sitta akashauri wajumbe wa Tume hiyo ambao ni wazee wenzake kwamba jukumu lao limeisha na kwa uungwana waachie Bunge Maalumu lifanye kazi yake:

“Wajumbe wale kazi yao ilishaisha, lakini kila siku wanakosoa, mara midahalo, makongamano. Wazuiwe kufanya hivyo, hata waambiwe tu kibinadamu maana hata sisi hatukuwaingilia wakati wanaendesha mchakato wao.

“Wanatuponda sana kana kwamba hakuna cha kujadili, kama ni hivyo zile siku 70 zilikuwa za nini?” 

Naye Dk Zainab Gama, alisema kazi ya Tume ya Katiba ilishaisha na kwamba kwa wanaopiga kelele
nje ya Bunge Maalumu la Katiba watakuwa na lao jambo nyuma ya pazia.

Mjumbe Hamad Rashid Mohammed, ambaye pia ni Mbunge wa Wawi (CUF), alisema kwa taratibu za mabunge jambo lolote likishawasilishwa bungeni linakuwa chini ya mamlaka ya Bunge, ambalo nalo linafanya kazi kwa niaba ya wananchi.

Dk Pindi Chana akichangia, alisema ambao hawajarudi bungeni hawawatendei haki Watanzania.
Kwa upande wake John Cheyo alisema hakuna haraka ya kupata Katiba na kwamba ni vyema umakini mkubwa ukawepo katika kuhakikisha inapatikana Katiba bora.
“Tusiharakishe suala la Katiba, kama tunaona gharama basi tujaribu fujo, ghasia na kutoelewana, hiyo ndiyo gharama zaidi,” 
alisema. (via HabariLeo)

Mjumbe wa Bunge Maalumu, Kundi la Vyama Vya Siasa, Peter Kuga Mziray, ambaye pia ni Rais Mtendaji wa APPT-Maendeleo, amesema katiba nzuri zote zimetungwa na watu wachache zaidi.
Alisema wanaoandika Katiba ni wazalendo na kwamba hata yeye asipokuwepo katiba lazima itatungwa kwa kuwa katiba si ya mtu mmoja au kundi fulani.

Alisema hayo akijibu hoja za waandishi wa habari kuhusu bunge la Katiba ambalo linaanza ngwe yake ya pili.

Alisema hata yeye akiwepo hapo asiwepo katiba lazima itatungwa na anaamini kwamba Watanzania watapata katiba mpya na bora zaidi.

Bunge la Katiba linaanza leo na kama kusipokuwapo na mabadiliko, japo wabunge wengi wa ukawa wanaonekana mjini hapa, bunge hilo litaendelea kujadili hoja muhimu zilizopo mezani ambaozo zinagusa rasimu takribani 15 zilizobaki.

Alisema Bunge hilo haliwezi kukwamishwa na kutokuwapo kwa ukawa, na wakati mazungumzo yanaendelea ya kuwarejesha ukawa bungeni, bunge litaendelea kwa kuwa ana matumaini koramu itapatikana.

“Mimi nawasihi tu wenzangu warejee, bungeni kila mtu anawaisihi wao wanakataa,” alisema Mzirai na kufafanua kwamba wasiporudi wana lao jambo kwani hiyo katiba wanayosema ni ya wananchi, wananchi wenyewe ukiacghia wanasiasa wachachre wanawasilishwa na taasisi ambazo zimesema warejee bungeni.

“Ukiachia Kakobe, makanisa yote yametaka ukawa warejee Bungeni, taasisi ya umoja wa mataifa imesema, waislamu wamesema,” alizungumza Mzirai na kusema kama wote wamesema wakiendelea kukataa lazima tujihoji nyuma yao kuna nani.

Pamoja na kusisitiza kwamba katiba itapatikana pamoja na matatizo ya kisera ambayo ndiyo yanaozinga muundo wa serikali amesisitiza haja ya vyombo vya habari kuacha kushabikia mambo ambayo yanawatenga zaidi watanzania badala ya kuwarejesha pamoja.

Alisema vyombo vya habari vimekuwa na tabia ya kukatisha tamaa (negativity) ambayo haifai katika suala zima la kujenga uwezo wa kufikia muafaka wa katiba kwa manufaa ya taifa.

Alisema uandishi wenye mwelekeo wa kukwamisha kinachoendelea katika bunge si tu hauwapatii watanzania nafasi ya kufanya maamuzi lakini pia inaonesha waandishi nao wamekuwa chama kingine cha siasa kikifurahia mambo yanayokwamisha mchakato mzima wa kupatikana kwa katiba.


Pamoja na kusema kwamba kazi ipo Mziray alisema anaamini kwamba watanzania watapata katiba wanayoihitaji na matatizo ya sasa yamejikita zaidi katika uroho mwa madaraka na matatizo ya kisera.

“Watu wajifunze kupokea na kutoa… hili suala la kisera si rahisi hivyo… ni lazima kujifunza kutoa na kupokea,” alisema Mzirai akifafanua kwanini anaona ni vyema UKAWA wakarejea bungeni na yafanyia kazi yale yanayowezekana.

Alisema serikali mbili au tatu ni misimamo ya kisera ambayo haiwezi kubadilishwa kwa mtu mmoja lakini yapo mambommengi ya muhimu kwa upande wa upinzani na wananchi ambayo yakifanyiwa kazi inaonesha neema za baadaye.

Alitaja mambo hayo kama Tume Huru ya uchaguzi, mgombea binafsi na raslimaliza taifa.

Alisema anaamini UKAWA wakirejea ukumbini CCM italegeza mambo mengi kwa manufaa ya watu wa taifa hili.

Alisema kwa sasa upinzani ni kundi la minority (wachache) hivyo hawana sababu ya kutaka kila kitu kwani vyote vinawezekana poklepole na kwa elimu.

Alisema ni dhahiri kwa sasa CCM ambayo inasema wazi kwamba imeingia madarakani kwa kunadi sera yake ya serikali mbili haiwezi kuachia hivyo kirahisi kama sera za Chadema na CUF zinavyotaka serikali tatu.

“Kubadili ni lazima kurejea kwa wanachama wao, …lakini yapo ya msingi ya kushughulikia ambayo yanawezekana,” alisema Mzirai.

Alisema Rais amekuwa Mwungwana kuacha watu wazungumze lakini kiukweli ni kuwa wanaokwenda kwa wananchi sasa wanafanya kosa la kisheria kwani rasimu ya kwenda kunadiwa kwa wananchi haijapatikana.

Alisema vitendo vya kuzungumza kwamba kuna rasimu kwa wananchi na kuwataka wafanya si sawasawa klwani rasmu ndio ninatengenezwa sasa.

Aklisema kongamano la tarehe 9 na 10 limelenga kuwaleta pamoja wahusika wote na kuundwa kwa kamati mpya.

Mzirai anasema kama wanasiasa wakiondolewa mzizi utakuwa umeondolewa na waliobaki watatunga katiba.

Naye Diana Chilolo, mjumbe na mbunge wa viti maalumu kutoka Singida amesema ana uhakika kwamba koramu itatimia na mkutano kuendelea kwa kuwa wao wanatekeleza kazi za wananchi na wananchi wanataka vitendo.

Chilolo alisema haelewi Ukawa wanataka kuwafanyia nini watanzania kupitia rasimu hiyo.
Alisema kazi ipo Bungeni na kukaa nje kwao kuna shida kubwa ya kutotekeleza kazi walizoagizwa na wananchi za kuwapatia katiba bora.

“Sisi tumekuja kufanyakazi na kuwajibu katiba ipo na itapatikana” alisema katika viwanja vya bunge jana.

Naye aliyewahi kuwa waziri nchini hapa William Ngeleja alisema kwamba ana matumaini makubwa ya kuendelea kwa kikao kwa kuw amakundi ya uwakilishi yapo bungeni na yamefika kukamilisha kazi.

Mjumbe mwingine Magdalena Likwina amesema kwamba wao wamefika ili kuhakikisha kwamba mahitaji ya wananchi kuhusu ardhi, elimu na afya yanaelezwa kinagaubaga katika katiba.

Alisema suala la serikali kwake halina uzito mkubwa kwani kama serikali mbili haijaweza kutatua matatizo yaliyiopo serikali tatu itatatuaje?

Alisema yeye anaamini katika serikali mbili iliyoboreshwa na anafikiri wanaotaka serikali tatu hawajafanya kazi ya kutosha kuwaeilimisha kwa kuzingatia mahitaji halisi ya watanzania katika nyanja za elimu, afya na ardhi.

Alisema wanaotaka serikali 3 wanatakiwa kueleza kilichondikana ambacho kinahitaji serikali tatu na namna ambavyo kinaweza kutatuliwa kama ndio tatizo la msingi la watanzania. (via Lukwangule)
 
Source: www.wavuti.com


Benki ya Barclays Tanzania imezindua mpango wa kuboresha huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa kuweka dhamana katika huduma zake kwa wateja. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Bidhaa na Kaimu Mkurugenzi wa wateja binafsi, Musa Kitoi alisema kuwa katika mpango huo wa dhamana katika huduma, benki inaahidi kutoa huduma zake kwa muda na kipimo kinachokubalika. 

“Siku zote tunahakikisha mteja anapoingia katika benki yetu anapata huduma bora kama anavyotegemea na kwa kupitia dhamana hii ya huduma tunatoa ahadi kuwa huduma zetu zitakuwa bora maradufu.

“Kwa kuanzia, mteja yeyote atakayeomba kadi ya ATM, atapatiwa katika muda usiozidi dakika ishirini na vile vile kwa wanaohitaji vitabu vya hundi watapatiwa ndani ya siku tano, viwango hivi ni vya juu sana katika soko letu. 

“Lakini pia, pale tutakapogundua kuwa mteja hakupata huduma kama tulivyomuahidi tutahakikisha tunamlipa fidia ndani ya masaa 24,” alielezea Bw Kitoi.

Alisema kwamba Barclays inajizatiti kutoa huduma tofauti za kibenki kwa wateja wake ambazo zinatumia teknolojia ya hali ya juu na pia huduma za viwango vya juu kupitia wafanyakazi wake.
Kitoi alifafanua kwamba benki hiyo imepiga hatua kubwa kuboresha njia mbali mbali za utoaji wa huduma kwa kuzindua mipango ya kupunguza foleni katika matawi yake na kuondoa utumiaji wa fomu za kibenki ambazo zinachelewesha utolewaji huduma haraka.

 “Nia yetu ni kuwa benki inayotoa huduma haraka zinazostahili kwa wateja wetu na tutaendelea kuleta mabadiliko mbalimbali yenye nia ya kuboresha huduma, ziwe za kisasa ili kutimiza azma yetu ya kufanya huduma za benki kuwa rahisi kupatikana na kwa haraka na hivyo kuwapa wateja wetu muda zaidi wa kushughulikia biashara zao,”  alielezea zaidi Bw Kitoi.

Kwa upande wake, Meneja wa Miradi na Mikakati ya Kibenki wa Benki hiyo, Jane Mbwilo alisema kwamba hivi karibuni Barclays ilizindua huduma ya benki bila kutumia makaratasi ambayo inaruhusu wateja kuweza kutoa na kuweka fedha kwa kutumia tu kadi zao na hivyo kupunguza muda mwingi unaotumika kujaza fomu mbali mbali za kuombea huduma. 

Aliongeza kwamba benki hiyo imewekeza katika technolojia mbali mbali ili kutoa huduma za kisasa na kwa bei nafuu.

BARCLAYS Bank Tanzania has official launched service guarantee product an initiative geared to improvcustomers experience at the bank in the country.

Speaking at the launch which took place at the bank’s Head Office, Barclays Head of Products, Segments and Retail Strategy & Acting Retail Director, Musa Kitoi said that with the service guarantee initiative, the bank commits to provide the customer delivery of service at a defined standard and defined time.

He said that the initiative aims to give its customers much easier in financial transactions across the country.

“Barclays strive to deliver on expectations every time a customer walks into the bank with our service guarantee initiative we make a promise to our customers to deliver a more efficient and effective service,”

“To begin with, we guarantee that a customer can apply and receive his ATM card within 20 minutes and we also guarantee cheque book deliver y within 5 days; these turn around times are the fastest you can get in the market. Furthermore, we also commit to compensate customers within 24 hours of discovering that there has been a service breach,” said Kitoi

He said that they are proud to be the first bank to introduce such as unique initiative in the Tanzanian market and East African region at large.

Kitoi added that Barclays bank endeavors to lead the industry by offering a new way to bank that combines great technologies and the best people to people service.

He further noted that the bank has made tremendous strides to enhance the overall customer experience through launching of various initiatives which are geared to reduce queues, ling turn around times, and manual processes that are paper intensive to a bank.

“Our aim is to be the bank where service is guaranteed to customers and where processes are automated to make banking easier and more convenient and therefore we will continue offering a range of new services designed to do exactly that, giving our customers time to focus on running their business,” Kitoi Further explained.

On her part, Barclays Bank Strategic Project Manager, Jane Mbwilo said that recently the bank launched Paperless banking where customers deposits or withdrawals. In addition, the bank has invested in new technology and ways to make banking simpler and easier for all their customers to use these alternate channels.

She said that Barclays strategy highlights implementation of technology that makes customers lives much easier while introducing efficiencies that drive costs lower for the bank and therefore for the customers.


Metl yajipanga kupanua soko lake la mafuta Afrika mashariki na kusini

Na Damas Makangale wa Makangale Sattellite

KAMPUNI ya Mohammed Enterpries (Metl) kupitia kampuni yake dada ya kuingiza, kuhifadhi na kusambaza mafuta nchini ya Star Oils Ltd imepata mkopo wa bilioni 100 kutoka kwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).
 

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mohammed Enterpries (Metl) na Mbunge wa Singida Mjini, Mhe, Mohammed Dewji akibadilshana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Bi Mizinga Melu muda mfupi kabla ya kuanza shughuli za utiliaji saini wa mkopo wa aina yake wa Bilioni 100
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya hafla ya utiliaji saini wa mkopo huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu na Mbunge wa Singida Mjini, Mhe, Mohammed Dewji (MO) amesema mkopo utafungua mianya zaidi kwa kampuni ya Star Oils kusambaza mafuta nje na ndani ya nchi.
 

Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi Mizinga Melu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Metl, Nhe Mohammed Dewji wakitiliana saini ya mkopo huo wa bilioni 100
Amesema kwamba baada ya majadiliano ya muda mrefu kati ya timu ya wataalamu kutoka Metl makao makuu na maafisa wa NBC kutoka nchini na Afrika Kusini wamefikia makubaliano ya kupata mkopo huo mkubwa na wa aina yake katika sekta ya mafuta hapa Tanzania.
Amesema kwamba kampuni ya Star Oils ina mipango ya kusambaza mafuta katika nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa jangwa la Sahara ikiwa ni sehemu ya mikakati yake ya kujipanua kibiashara ndani na nje ya Afrika.

"Mpango huu utaiwezesha Star oils kupanua malengo yake katika soko la kimataifa ikiwa ni pamoja na kukuza uzalishaji na usambazaji wake katika ngazi ya Afrika Mashariki na Kusini mwa jangwa la sahara," amesema MO

MO aliongeza kuwa hatua ambayo kampuni hiyo imefikia ni kubwa kwa kuonyesha dhamira ya kuwekeza na kufanya biashara ya mafuta Afrika mashariki na kusini mwa jangwa la sahara.

"Mkopo huu utasaidia kampuni ya star oil kuongeza uzalishaji na usambazaji wa mafuta ya kwenye soko la Afrika mashariki na kusini mwa Afrika,” 

"Sisi tuna mipango ya kuanza kusambaza mafuta na bidhaa za petroli katika nchini za  Kusini mwa Afrika kama sehemu ya jitihada za kampuni za kupanua biashara zake katika soko la Afrika," amesema.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Star Oils Ltd, Nazir Haji amesema kwamba mkopo huo utachochea chachu ya uzalishaji, uhifadhi na usambazaji wa mafuta na kusukuma maendeleo ya sekta mafuta nchini.

Amesema kwamba kampuni ya Star Oils inajipanga kufanya biashara ya mafuta kuwa endelevu hapa nchini na Afrika mashariki ili uchumi wa nchi za Afrika mashariki ziweze kukua kwa kutegemea tija ya uzalishaji wa mafuta. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi Mizinga Melu amesema kuwa benki hiyo inahitimisha safari ya majadiliano na kampuni mama ya Star Oils, Mohammed Entrepries Tanzania Limited (Metl) ya mkopo wa bilioni 100.

"Star oils ni kampuni dada ya METL ni moja ya makampuni yanayokwenda kasi katika biashara ya ushindani katika Afrika Mashariki na Kusini mwa jangwa la sahara na rekodi yao ya mauzo na biashara ni ya kuridhisha," amesema.

 Aliongeza kwamba METL ni moja ya makampuni yalionyesha rekodi nzuri katika biashara ya viwanda, nguo, vinywaji, bima na mafuta na wanastahili kuwezesha kwa kupata mikopo mikubwa na ya muda mrefu kupitia taasisi za kifedha nchini na nje ya nchi,” 

"Sisi kwenye benki ya NBC tunayofuraha kubwa kwa kupata nafasi ya kufanya biashara na moja ya makampuni yanayokuja kwa kasi katika bara la Afrika na vile vile NBC ni benki ambayo ipo tayari kusaidia wateja wake,” aliongeza
Bi Melu alisisitiza kuwa baada ya NBC kuridhisha na shughuli za kibiashara na mzunguko wa fedha wa Metl wameamua kutoa mkopo huo ili waweze kupanua biashara yao katika masoko ya kimataifa.

Star Oils kwa sasa  inatekeleza awamu ya pili ya mradi mkubwa wa kuhifadhi mafuta ya petroli na baadaye kujenga usambazaji wa mafuta nchi nzima kwa njia ya mlolongo wa vituo vya karibu 200 ya petroli nchini.
 
Uwezo wa jumla ya uhifadhi wa kituo hiki juu ya kukamilisha mradi itakuwa lita 68 milioni, kuundwa tu kwa ajili ya kuhifadhi ya petroli, gesi mafuta na mafuta ya taa. Wingi wa bidhaa hizi kwa sasa ni kuuzwa kwa misingi ya jumla na mipango ya baadaye soko yao kupitia vituo vya METL Group vya rejareja vya petroli.

NBC imetiliana saini ya mkopo wa shilingi za kitanzania bilioni 100 na kampuni ya kusambaza mafuta ya jijini Dar es Salaam, Star Oils Ltd katika mpango mkakati wa kuendeleza sekta ya mafuta nchini.



Mkuu wa Idara- Huduma za Kibenki kwa Wateja wakubwa na Uwekezaji, Andre Potgieter akizungumza na wageni waalikwa kwa kuonyesha shughuli mbalimbali na bidhaa huduma za benki hiyo



Mkuu wa Idara wa NBC, Huduma Kibenki akipeana mkono wa pongezi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Metl, Mhe, Mohammmed Dewji.


Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi Mizinga Melu akizungumza kwenye hafla hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam


 Baadhi ya wageni waalikwa













































































































Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.