Latest Post

Na Mwandishi wetu-Arusha,

Kampuni ya Barrick yenye ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga imetunukiwa  cheti cha tuzo  kwa kudhamini kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichomalizika  leo jijini Arusha.

Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati , Dkt Dotto Biteko  ambaye alikuwa mgeni rasmi wa kufunga kikao hicho cha siku nne ambapo pia alitoa tuzo kwa taasisi nyingine zilizodhamini mkutano huo.


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh. Dotto Biteko akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Bodi ya Twiga, bw.casmir Kyuki (kulia) baada ya kumkabidhi cheti cha udhamini (kushoto) ni Meneja wa Barrick nchini, Dkt.Melkiory Ngido.

Akiongea kuhusu udhamini huo kabla ya kukabidhiwa cheti cha tuzo,Meneja wa Barrick nchini Dkt.Melkiory Ngido alisema kampuni imedhamini kikao hicho kama mdau mkubwa wa maendeleo inayoamini kuwa sekta binafsi na Serikali zikishirikiana zinaweza kuleta  matokeo Chanya kwenye uchumi wa nchi kama inavyoonyesha kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025-2050.

Meneja wa Barrick nchini Dkt.Melkiory Ngido akiongea katika CEOs Forum kuhusu mafanikio yaliyopatikana kutokana na ubia wa Barrick na Serikali


Dkt.Ngido pia alisema kuwa Barrick imekuwa ikitekeleza falsafa ya 4R ya Rais Samia kwa vitendo ambayo imeleta ufanisi katika uendeshaji wa shughuli zake nchini kwa kushirikiana na Serikali ambapo imekuwa kioo cha uwekezaji wenye mafanikio nchini.

“Kupitia uwekezaji wetu na  uendeshaji wa shughuli zetu kwa ubia na Serikali tumepata mafanikio makubwa baadhi yake yakiwa ni kuwa kinara wa kulipa kodi na tozo mbalimbali ,kutoa gawio nono kwa Serikali,kunufaisha wazabuni wa ndani na kupanua wigo wa ajira kwa watanzania, matumizi ya teknolojia za kisasa  na kufanikisha miradi mikubwa ya kijamii hususani katika sekta za elimu,afya,miundombinu kupitia fedha za CSR zinazotolewa na migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara”.

Dkt.Ngido pia alisema kuwa kampuni inaendelea kufanya tafiti mbalimbali za kijiolojia kwa lengo la utambuzi wa maeneo mapya ya uchimbaji na imeweza kurefusha maisha ya migodi yake kwa muda mrefu zaidi na kuendelea kunufaisha taifa.

Mwisho

Dar es Salaam, Tanzania -

Bank of Africa Tanzania joins diplomatic figures, business people, invited dignitaries and other cultural representatives to celebrate 26th anniversary of His Majesty King Mohammed VI’s accession to the throne of the Kingdom of Morocco as of its efforts to foster bilateral ties between Tanzania and Morocco.

Bank of Africa Tanzania proudly took part in the 26th anniversary celebration, the commemorative event, held in Dar es Salaam recently which among other things brought together distinguished delegates, diplomacy and other representatives to mark this important occasion.

Bank of Africa Tanzania is a subsidiary of the BANK OF AFRICA Group, a pan-African banking network headquartered in Morocco, with operations in 17 African countries and a strategic presence in France.

The Group is majority-owned by BANK OF AFRICA - BMCE, Morocco’s second-largest private bank. The bank reaffirmed its commitment to strengthening bilateral ties between Tanzania and Morocco through financial cooperation and cultural engagement.

The celebration underscored the growing relationship between the two nations, with Bank of Africa Tanzania standing as a bridge between East Africa and North Africa, fostering economic integration and shared prosperity.

Bank of Africa Tanzania remains committed to promoting regional development through strategic partnerships and impactful community engagement, in line with the group’s broader mission across Africa and beyond.

 The guest of honour was Hon. Ambassador Mahmoud Thabit Kombo (MP), Minister for Foreign Affairs and East African Cooperation.

Staa wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, Thierry Henry, ametangazwa rasmi kuwa balozi mpya wa kimataifa wa kampuni ya michezo ya kubashiri mtandaoni, Betway, wakati huu ambapo ligi kuu za barani Ulaya zinarudi dimbani kwa msimu mpya.

Thierry Henry 

Katika nafasi yake hiyo mpya, Henry anatarajiwa kuwa kiungo muhimu kati ya mashabiki wa soka na mchezo wenyewe, kupitia maudhui maalum na mitazamo ya kitaalamu atakayoshiriki kwa ushirikiano na kampuni hiyo.

Henry alianza soka lake la kulipwa nchini Ufaransa akiwa na AS Monaco, kabla ya kujiunga na Juventus kwa kipindi kifupi na kisha kutua Arsenal mwaka 1999, ambako alijizolea umaarufu mkubwa kwa kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo. Aliisaidia Arsenal kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu England (EPL), ikiwemo msimu wa ‘Invincibles’ mwaka 2003/04, na mataji matatu ya FA Cup.

Baadaye alijiunga na Barcelona, alikoshinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) mwaka 2009 kama sehemu ya kikosi kilichotwaa mataji sita ndani ya msimu mmoja — rekodi ya aina yake barani Ulaya.

Katika ngazi ya kimataifa, Henry alikuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa kilichoshinda Kombe la Dunia mwaka 1998, na pia alitwaa taji la Euro 2000. Tangu astaafu soka, amekuwa kocha na mchambuzi maarufu wa soka katika vituo vya runinga mbalimbali.

“Soka siku zote limekuwa mchezo wa kasi na msisimko, na hayo ndiyo mambo ambayo Betway huwapatia mashabiki kwa namna ya kipekee,” alisema Henry. “Ninatarajia kushiriki kwenye kitu kikubwa kinachowaunganisha watu na mchezo wanaoupenda.”

Tangazo hilo limetolewa wakati ambapo Ligi Kuu England (EPL), La Liga na ligi nyingine kubwa barani Ulaya zinarejea, kipindi ambacho huwa na ushawishi mkubwa kwa mashabiki na wadau wa soka duniani kote.

Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo, uteuzi wa Henry unaonesha dhamira ya kuendelea kuwekeza kwenye soka la kimataifa. Betway tayari ni mshirika wa klabu kadhaa maarufu ikiwemo Arsenal, na inaendesha shughuli zake katika masoko mbalimbali ya Afrika, Ulaya na Amerika.

Mwisho

Utagharimu takribani  shilingi Bilioni 4.8 za kitanzania

Na Mwandishi Wetu, Kahama Shinyanga

Mgodi wa  Barrick Buzwagi ambao uko katika mchakato wa kufungwa  umefadhili mradi wa ujenzi wa chujio la maji ya mvua eneo la mwendakulima  wilayani Kahama mkoani Shinyanga unaoghalimu takribani shilingi Bilioni 4.8  kwa ajili ya kuwapatia wananchi wa mji wa kahama maji safi na salama.

Akiongea wakati wa hafla ya kupokea mwenge ulioambatana na kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo wa mradi wa maji, Meneja wa Ufungaji wa Mgodi wa Buzwagi ,Zonnastraal Mumbi alisema  mgodi katika hatua zake za mwisho za ufungaji umeamua kufadhili mradi huo ili kuondoa tatizo la upatikanaji wa maji kwenye Wilaya ya Kahama.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa , Ismail Ali Ussi (Mbele mwanzo kushoto) akikata utepe na uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa chujio wa maji ya mvua , mradi unaofadhiliwa na Barrick Buzwagi na serikali ya Tanzania eneo la mwendakulima Wilaya ya Kahama katika upokeaji wa mbio za mwenge leo mchana mjini Kahama , mwanzo kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda.

“haya ni matokeo ya ufungaji wa mgodi wa Buzwagi kwa kuamua kufadhili mradi mkubwa kabisa wa maji ya mvua kwa kutengeneza miundombinu ya uvunaji , ukusanyaji na usambazaji wa maji ya mvua kwa ajili ya matumizi wa wananchi wa mji ya Kahama,” alisema Mumbi.

Kiongozi wa Mbio wa Mwenge , Ismail Ali Ussi akihutubia hadhara na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa maji ya mvua eneo la mwendakulima.

Aliongeza kwamba moja ya dhamira ya kampuni ya Barrick inayoendeha shughuli zake nchini kwa ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals ni kuunga mkono jitihada za Serikali kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.

Sehemu ya jiwe la msingi wa mradi wa ujenzi wa chujio wa maji ya mvua mjini kahama , shinyanga.

“Mgodi wa Buzwagi umefadhili mradi huu wa maji ya mvua kwa 62% kwa ajili ya kuhakikisha kwamba miundombinu ya kisasa na bora inajengwa kwenye mradi huu kama sehemu za kuleta matokeo Chanya kwa wananchi wa mji wa kahama,” alisisitiza

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na  Usimamizi wa Mazingira, , Mamlaka ya Maji Safi  wa Mazingira Kahama (KUWASA)Mhandisi , Magige Marwa , alitoa pongezi kwa kampuni ya Barrick nchini  kwa kufadhili mradi huo mkubwa ambao ukikamilika utaondoa changamoto ya upatikanaji maji safi na salama wilayani Kahama,


Aliongeza kwamba mradi wa ujenzi wa chujio la maji mwendakulima unatazamiwa kuhudumia zaidi ya 66% ya wakazi waishio manispaa ya Kahama na una uwezo wa kuzalisha lita milioni 10 kwa siku.

“Mradi huu unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu na mpaka sasa 78% ya mradi mzima umeshakamilika kutokana na kasi ya ujenzi wa mradi huu mkubwa kwenye mji huu wa kahama,” alisisitiza

Mhandisi Marwa alifafanua kwamba mradi huo wa chujio la maji ya mvua 62% imefadhiliwa na mgodi wa Barrick- Buzwagi na 38% ni KUWASA kupitia Wizara ya Maji na Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Meneja wa Ufungaji wa Mgodi wa Buzwagi , Zonnastraal Mumbi wa pili kulia kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

Kwa upande wake , kiongozi wa mbio za mwenge , Ismail Ali Ussi alisema wizara ya maji inaendelea kufanya vizuri na kutekeleza kwa vitendo maono ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kupeleka huduma ya maji mijini na vijijini.

 

Kiongozi wa mbio za mwenge, Ismail Ali Ussi (Katikati) akisikiliza maelezo ya mradi kutoka kwa msimamizi wa mradi huo ,  Mhandisi , Magige Marwa (wa kwanza kulia) ambaye ni Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na  Usimamizi wa Mazingira, , Mamlaka ya Maji Safi  wa Mazingira Kahama (KUWASA) wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama , Frank Nkinda. 

“Nachukua fursa hii kuwapongeza wataalamu wote wa wizara na mamlaka za maji hapa kahama kwa kufanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha watanzania wanapata maji safi na salama,” amesema.

Sehemu ya ujenzi wa mradi wa maji ya mvua mwendakulima , Kahama shinyanga ndani ya mgodi wa Buzwagi Barrick.

Kwa upande wake , Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda alisisitiza kwamba umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii na kuendelea na ari hiyo ya kutekeleza miradi ya huduma za wananchi kwa viwango vya juu ili kukidhi mahitaji ya wananchi.

Mwisho

 Washindi 20 wa kwanza katika kampeni ya ‘Miamala ni Fursa’ wazawadiwa

Bank of Africa -Tanzania imetoa zawadi kwa washindi wake 20 wa kwanza wa wiki kupitia kampeni ya huduma za kibenki kwa njia ya kidigitali iitwayo “MIAMALA NI FURSA”, ambapo kila mmoja amepokea zawadi ya Sh50,000 kwa kutumia huduma za kibenki kwa njia ya simu za mkononi kupata huduma za huduma za kifedha.

Akizungumza kuhusu maendeleo ya kampeni hiyo iliyozinduliwa Juni 4, 2025, Afisa Mkuu wa Huduma za Kidigitali wa Bank of Africa-Tanzania, Bw Lameck Mushi, alisema kuwa mwezi mmoja tangu kuanza kwa kampeni hiyo ya miezi mitatu, imepokelewa vyema na umma wa Watanzania.

Bw Mushi alieleza kuwa kampeni hiyo inalenga kuhamasisha matumizi ya jukwaa la benki kupitia simu kwa kuwazawadia wateja wanaofanya miamala ya kila siku. Juhudi hizi ni sehemu ya dhamira ya benki yao kuendeleza matumizi ya huduma za benki kidigitali na kuendeleza ujumuishwaji wa kifedha nchini Tanzania.

Afisa Mkuu wa Huduma za Kidigitali wa Bank of Africa-Tanzania, Bw Lameck Mushi, akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu kampeni ya “Miamala ni Fursa” kwa wateja wao kwa kutumia huduma za kibenki kwa kupitia simu zao za kiganjani , kushoto ni Afisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa RejaReja Asupya Nalingigwa na kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano Nandi Mwiyombella.

“Tunafurahia mwitikio mkubwa tulioupokea hadi sasa. MIAMALA NI FURSA tayari imefanya huduma za kibenki kupitia simu kuwa za kuvutia na muhimu katika maisha ya kila siku ya wateja wetu,” alisema Bw Mushi.


Akiendelea, alisema ukweli kwamba “Wateja wanashinda zawadi za fedha kwa kufanya miamala ya kulipa bili au kutuma fedha unaonyesha kuwa vitendo vidogo, lakini vya mara kwa mara vina mchango mkubwa. Zaidi ya hapo, tumeongeza unafuu kwa wateja wetu kwa kupunguza ada za miamala ya Bank-to-Wallet kwa zaidi ya asilimia 50."


Kila wiki, wateja watano watakaokamilisha miamala mitatu ya Bank-to-Wallet (B2W) na muamala mmoja wa ziada (malipo ya bili, ununuzi wa muda wa maongezi au umeme) kupitia B-Mobile watakuwa na nafasi ya kushinda.

Mwisho wa kampeni hii, ambayo itaendelea hadi Septemba 2025, mshindi mkuu atajinyakulia zawadi ya pesa taslimu Sh5 milioni.

Afisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa RejaReja Asupya Nalingigwa, alisisitiza: “Lengo letu ni kufanya huduma za kibenki ziweze kufikiwa kwa urahisi, ziwe na manufaa na ziwaguse wateja wetu kwa ukaribu zaidi. Iwe uko mjini au kijijini, mradi una B-Mobile, unaweza kushiriki na kushinda.”

Ili kuhakikisha ushirikishwaji wa wote, Bank of Africa-Tanzania imehamasisha timu zake za matawi kote nchini kusaidia kuwaunganisha wateja wapya na kutoa mafunzo ya kutumia huduma hizo za kidigitali. Timu maalumu ya msaada wa kiufundi pia ipo tayari kusaidia kutatua changamoto zozote za upatikanaji na kuhakikisha uzoefu mzuri kwa watumiaji wote.

Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano Nandi Mwiyombella, aliongeza: “Kampeni hii si kuhusu zawadi pekee, bali ni kuhusu kuwapa nguvu wananchi. Kwa kuhamasisha matumizi ya huduma za kidigitali kwa njia shirikishi na rahisi, tunawasaidia Watanzania wengi zaidi kushiriki katika mfumo rasmi wa kifedha.”

Kwa zawadi zaidi za fedha na washindi wapya kutangazwa kila wiki, Bank of Africa -Tanzania inawaalika wateja wake wote kufanya miamala, kushinda, na kufurahia huduma za kibenki kwa urahisi kupitia simu zao.

 

 Kuhusu BOA Bank (T) Limited

BOA-Tanzania ni benki ya biashara binafsi inayotoa huduma kwa wateja wa kampuni kubwa, wateja wa kati (SME) na wateja wa rejareja nchini Tanzania. Ilianza shughuli zake Juni 2007 baada ya kununua Eurafrican Bank iliyokuwa ikifanya kazi nchini tangu Septemba 1995.

Benki hii ni sehemu ya kundi la Benki ya Afrika, ambalo lilianza shughuli zake mwaka 1982 nchini Mali.

Kundi hili linafanya kazi katika nchi 19 za Afrika, ikiwa ni pamoja na Afrika Magharibi, Afrika Mashariki, Afrika ya Kati, pamoja na ofisi za uwakilishi Paris (Ufaransa), Hispania, London (Uingereza) na China. Tangu mwaka 2010, Benki ya Afrika imekuwa chini ya umiliki mkubwa wa BMCE Bank, benki ya tatu kwa ukubwa nchini Morocco, inayotoa huduma katika nchi 31 na mabara 4.

Kwa sasa, BOA-Tanzania ina matawi 17 ya rejareja, yakiwemo 8 Dar es Salaam na 9 katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Zanzibar na miji mingine mikubwa.


Mawasiliano ya Vyombo vya Habari:

Tovuti: www.boatanzania.com

Beatrice E. Mirigo – Maendeleo ya Bidhaa & Mawasiliano

Barua Pepe: beatrice.mirigo@boatanzania.co.tz

 

Simu: +255 699 000 260

 

 Mwisho………..

Na Mwandishi Wetu

Ikiwa imebaki miezi michache tu kufanya uchaguzi mkuu, serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetekeleza miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali za uchumi na kuboresha huduma za kijamii nchini. Katika yote haya, imekuwa nyota inayong’aa si tu kwa Afrika Mashariki, bali pia kwa Bara la Afrika kwa jumla.

Utekelezaji wa miradi ya maendeleo na uboreshaji wa huduma za kijamii umefanyika kwa kuongozwa na sera, sheria, kanuni, taratibu na utekelezaji wa mikakati mbalimbali kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo endelevu.

 Dkt Samia Suluhu Hassan alianzisha ajenda ya ‘4R’ kama nguzo muhimu ya maendeleo inayolenga maridhiano, ustahimilivu, mabadiliko na kujenga upya mustakabali wa kitaifa kisiasa. Lengo ni kuboresha mahusiano kitaifa, kikanda na kimataifa, na kuhakikisha tunajenga taswira mpya ya Tanzania, huku tukiendelea kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika sekta mbalimbali za uchumi.

 Alipolihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 22, 2021, Dkt Samia Suluhu Hassan aliahidi kuimarisha demokrasia, haki za binadamu, kuboresha huduma za kijamii na miundombinu ya maji, kuboresha usafiri wa umma na usafirishaji wa mizigo, kuimarisha mazingira ya uwekezaji na mahusiano ya kitaifa, kikanda na kimataifa, na kuendeleza mazuri ya awamu zilizopita, ikiwa ni pamoja na kuleta mambo mapya, yanayoendana na wakati tuliomo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madaktari na wauuguzi nchini.

Ukuaji wa Uchumi:

Serikali yoyote duniani katika ukusaji wa mapato ili kuimarisha uchumi wa ndani inategemea usimamiaji madhubuti wa sera, programu na mikakati mbalimbali kwa kuhakikisha mapato yanazidi kukua siku hadi siku. Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21, serikali ilikusanya kiasi cha Shilingi trilioni 20.59 na katika mwaka wa fedha 2023/24, ilikusanya kiasi cha Shilingi trillioni 28.83, ambazo ni mapato ya ndani. Pamoja na mambo mengine, katika ukusanyaji wa mapato, Shilingi trilioni 120.16 zilikusanywa kutoka vyanzo vya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wizara, wakala wa serikali na serikali za mitaa.

 Elimu:

Katika kuhakikisha Ilani ya CCM inatekelezwa kikamilifu, serikali ya awamu ya sita iliamua kuondoa ada, na ilianza kusambaza vitabu, na kujenga madarasa, na pamoja na mambo mengine kufanya mapitio ya Sera ya Elimu, mafunzo ya ufundi na mitaala ili kuhakikisha wahitimu wanapata maarifa na ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipata maelezo jinsi miundombinu ya maji safi na salama inavyojengwa ili kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa Watanzania wote. Pamoja naye ni Waziri wa Maji Juma Aweso.

Katika sekta ya elimu, ambapo mapitio ya Sera ya Elimu ya mwaka 2014 (Toleo la 2023) yanalenga kuhakikisha wahitimu wanakuwa na maarifa, ujuzi, na maadili ili waweze kupenya katika soko la ajira.

Serikali iliamua kujenga shule 26 za wasichana za masomo ya sayansi kila mkoa, na shule 7 za wavulana kila kata nchi nzima, shule za msingi na sekondari 191,708 zilijengwa hadi mwaka 2020, na shule 254, 393 zimejengwa nchi nzima hadi mwaka 2025.

Pamoja na mambo mengine, shule za msingi mpya zilizojengwa mwaka 2025 ni 17, 986 na hadi mwaka 2020 zilizokuwepo shule 16,406. Idadi ya shule zote hizi ni matokeo chanya ya Ilani ya CCM.Vile vile serikali iliongeza vyuo vya ufundi stadi kutoka vyuo 662 mwaka 2020 hadi vyuo 860 mwaka 2024 kuendeleza ujuzi wa Watanzania katika sekta ya ufundi.

 Afya:

Msingi wa maendeleo ni pamoja na kuboresha afya ya umma. Serikali chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan iliwekeza katika sekta ya afya kwa kuongeza vituo vya afya kutoka 8,783 mwaka 2020 hadi vituo vya afya 12, 846, na kuboresha miundombinu ya majengo, kununua vifaa tiba, kuboresha huduma za kibingwa na kusomesha madaktari na wahudumu wengine katika sekta ya afya.

“Miaka minne iliyopita idadi ya vifo vya akina mama wanaojifungua ilikuwa 556 kati ya 100,000, lakini kutokana na uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya, idadi ya vifo ilipungua hadi kufikia 104. Lengo la dunia ni vifo 70. Nina hakika tutafika huko na kuondoa kabisa vifo vya akina mama wakati wa kujifungua,” alisema Dkt Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa hospitali mpya mojawapo nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, akimjulia hali mgonjwa katika moja ya hospitali za rufaa nchini. Rais Samia Suluhu Hassan ndiye mfariji mkuu wa Watanzania


Maji:

Miaka michache iliyopita akina mama walikuwa wakiamka alfajiri na kutembea umbali mrefu kutafuta maji, ambayo pia walikuwa hawana uhakika kama wangeweza kuyapata. Hadi kufikia mwaka huu, serikali ya awamu ya sita imetekeleza miradi ya usambazaji wa maji 2,331 katika miji na vijiji. Miongoni mwa miradi hiyo, ni ile ya Same, Mwanga na Korogwe ambapo wananchi wapatao 456,930 wamenufaika na miradi ya maji safi na salama.

Kilimo

Kwa miaka mingi kumekuwa na kauli mbiu mbalimbali za uhamasishaji wa kilimo tangu serikali ya awamu ya kwanza kama vile siasa ni kilimo, kilimo cha kufa na kupona, na kilimo kwanza (ambayo ilikuwa kauli mbiu ya serikali ya awamu ya nne). Kilimo ni uti wa mgongo, na kauli mbiu hii inathibitisha utekelezaji wa sera ya kilimo kwa serikali ya awamu ya sita kwa kuongeza bajeti yake kutoka Shilingi bilioni 294 mwaka 2021/22 hadi Shilingi trilioni 1.24 mwaka 2024/25, na kuifanya sekta ya kilimo kuchangia asilimia 26.2 kwa pato la taifa

Miaka ya nyuma Tanzania ilitofautisha mazao ya chakula, na ya biashara, lakini kwa sasa mazao karibu yote ni ya biashara, na mahitaji ni makubwa kwenye soko la nje, hata nyama kutoka Tanzania ambayo ni fursa muhimu kwa wakulima na wafugaji, lakini pamoja na mambo mengine, uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kutoka tani milioni 17.1 mwaka 2021 hadi tani million 22.8 mwaka 2024, huku serikali ikitoa ruzuku ya Shilingi billioni 300 katika kuimarisha sekta ya kilimo, ambayo huajiri takribani asilimia 65 ya nguvu kazi.

 Mifugo na Uvuvi

Serikali ya awamu ya sita imbadilisha mfumo wa kizamani na kuweka mfumo wa kisasa kuhakikisha ajira za Watanzania zinaendelea kuongezeka na usalama wa chakula una kuwa wa uhakika kwa kuongeza uzalishaji wa chakula cha mifugo kutoka tani millioni 1.38 mwaka 2020 hadi tani millioni 2.6 mwaka 2025, na kuongeza maeneo ya malisho ya mifugo kutoka hekta millioni 2.78 hadi hekta millioni 3.48. Ongezeko hili limepunguza migogoro ya wakulima na wafugaji, huku mauzo ya nyama nje ya nchi yakiongezeka pia kutoka tani 1,774 zenye thamani ya Dola za Kimarekani (USD) millioni 4.2 mwaka 2020 hadi tani 9,863.41 zenye thamani ya Dola za Kimarekani (USD) millioni 44 mwaka 2025.

 

Madini:

Sekta ya madini kwa muda mrefu ilionekana kama urithi wenye laana, lakini kwa sasa sekta hii muhimu kwa maendeleo ya taifa imeboreshwa kupitia mabadiliko ya Sheria ya Madini ya mwaka 2019, na mwaka 2022 mchango wake katika pato la taifa umeongezeka kutoka asilimia 6.8 mwaka 2020 hadi asilimia 10.1 mwaka 2025. Masoko ya madini yameongezeka kutoka 41 mwaka 2021 hadi kufikia 43 mwaka 2025 na vituo vya madini vimeongezeka kutoka 61 hadi kufikia vituo 109. Uboreshaji katika sekta ya madini umesogeza huduma kwa wananchi, na kuongeza uwazi katika sekta hii muhimu kwa maendeleo ya taifa.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, akizindua Mradi wa maji Butimba Mwanza.

Katika kuhakikisha mchango wa sekta hii unaendelea kukua kwa kasi, serikali ya awamu ya sita iliamua kununua mitambo 15 ya uchongoraji kwa wachimbaji wadogo wadogo na kuisambaza sehemu mbalimbali ili kuongeza upatikanaji wa taarifa za kijiolojia na kupanua uwazi wa sekta ya madini.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Amali-Mwamapalala katika kukamilisha ujenzi wa shule kama moja ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika sekta ya elimu nchini.

Pamoja na mambo mengine, baada ya kilio hicho cha muda mrefu na baadaye kwa kuwa na Sera ya Madini ya mwaka 2009 ya kuwawezesha Watanzania wazawa kushiriki katika sekta ya uchimbaji wa madini, kupata kazi za ukandarasi, zabuni na kutoa huduma mbalimbali kupitia Kanuni ya Maudhui ya Ndani (Local Content) Watanzania wamekuwa wakipata ajira ndani ya migodi na nafasi za menejimenti kushikwa na wazawa.

 Kwa sasa serikali iko mbioni kujenga kituo cha kisasa cha maabara kwa ajili ya upimaji wa madini katika ukanda wa Afrika Mashariki kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ambayo ipo jijini Dodoma. Katika kipindi cha miaka minne ya awamu ya sita, chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan, serikali imefanya marekebisho ya Sheria ya Maudhui ya Ndani (Local Content) kwa kutoa fursa kwa wazawa katika sekta ya madini kwa upatikanaji wa kazi migodini na marekebisho ya Uwajibikaji wa Jamii (CSR).

 Viwanda

Katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na uchumi wa kijani kupitia viwanda, na kupunguza tatizo la ajira nchini kuanzia mwaka 2020 hadi 2025 jumla ya viwanda 47,063 vilianzishwa. Kati ya hivyo, viwanda vikubwa ni 428, vya kati ni 1,393, vidogo ni 11,847 na vidogo sana ni 33,395, na pamoja na mambo mengine, kuendeleza kiwanda cha ngozi (Kilimanjaro Leather International Company Limited) kinachomilikiwa na Mfuko wa Hifadhi kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa asilimia 86, na Jeshi la Magereza kwa asilimia 14 kwa uwekezaji wa Shilingi billioni 152.96. Kwa hakika sekta ya viwanda ni injini kwa maendeleo ya taifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, akitizama ng’ombe kwenye moja ya programu za BBT za kunenepesha mifugo hapa nchini ili kukuza mahitaji ya mauzo ya nyama nje ya nchi na kuongeza kipato kwa wakulima na serikali kwa ujumla.

Makala haya hayawezi kutosha kueleza utekelezaji wa Ilani ya CCM, ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ameisimamia kikamilifu ili kulinda na kuendeleza maliasili na utalii, uchukuzi, miundombinu, ardhi, nishati, mawasiliano na sekta zingine mtambuka kwa masilahi mapana ya nchini yetu.

Mwisho….


MJI WA SERIKALI, DODOMA –

Serikali ya Tanzania imepongezwa kwa mafanikio yake katika kuimarisha mifumo ya tahadhari na ufuatiliaji wa majanga kupitia Kituo cha Dharura cha Taifa (Situation Room) kilichopo Mtumba, Dodoma.

Pongezi hizo zimetolewa na wataalamu kutoka Ghana, Togo na Burkina Faso waliopo nchini kwa mafunzo ya siku tatu ya kubadilishana uzoefu, yaliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maafa, Brigedia Jenerali Hosea Ndagala amesema kituo hicho kimeongeza uwezo wa taifa kutoa tahadhari mapema kwa wananchi na kuratibu mashirika mbalimbali kukabili majanga.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Kituo hicho, Bi. Jane Kikunya, amesema wageni hao wameonesha nia ya kuiga mfumo huo katika nchi zao kutokana na mafanikio waliyojionea.

Aidha, wageni hao wameeleza kufurahishwa na jinsi taarifa zinavyokusanywa, kuchakatwa na kuwasilishwa kwa wananchi kwa haraka na kwa usahihi.










 NAMWANDISHI MAALUM

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. James Kilabuko amehimiza ushirikiano wa kikanda katika kukabiliana na majanga ya kibinadamu yanayochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa, kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kitaalamu na kuimarisha vituo vya ufuatiliaji wa majanga na tahadhari ya mapema (Situation Room).

Akizungumza leo wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya kubadilishana uzoefu, yaliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na UNDRR na Kituo cha Sayansi cha Afrika Magharibi kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (WASCAL), Dkt. Kilabuko alisema mafunzo hayo ni sehemu ya kuimarisha uwezo wa kanda katika kukabili matukio ya majanga. Mafunzo hayo yalihusisha ujumbe kutoka Ghana, Togo na Burkina Faso.

Dkt. Kilabuko alieleza kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa majanga, kupitia vituo vyenye uwezo wa kukusanya taarifa mbalimbali, zikiwemo za hali ya hewa, maji, kijamii na kiuchumi, jambo linalosaidia kukabili majanga kama vile ukame na mafuriko.

 “Tunauzoefu mkubwa wa kiutendaji ambao unasaidia kuhakikisha vituo vyetu vinafanya kazi kwa ufanisi kwa kuratibu taasisi mbalimbali kukabiliana na majanga,” alisema Dkt. Kilabuko.






Serikali yazindua mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini Nyamongo kwa udhamini wa Barrick

 Na Mwandishi Wetu, Nyamongo,

Serikali imezindua mafunzo ya siku 14 ya kuvijengea uwezo vikundi 48 vya vijana wachimbaji wadogo wa madini kutoka ukanda wa Nyamongo wilayani Tarime, mkoani Mara.

Mafunzo hayo yataanza kesho Juni 21, 2025, chini ya udhamini wa Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara kwa kushirikiana na North Mara Trust Fund.

Vikundi hivyo vyenye wanachama 2,736 vilikabidhiwa leseni 96 za uchimbaji madini bure na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, mwanzoni mwa Mei 2025.

Hafla ya uzinduzi wa mafunzo hayo imefanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Ingwe - Nyamongo leo, mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Chikoka, ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Chikoka (kulia), Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, Francis Uhadi na viongozi wengine wakifurahia uzinduzi wa mafunzo kwa wachimbaji wadago wa madini uliofanyika Nyamongo wilayani Tarime, Mara leo Juni 20, 2025.

Katika hotuba yake, Chikoka amewahimiza vijana hao kuhudhuria mafunzo hayo kikamilifu na kuyazingatia ili yawe muongozo na dira ya shughuli zao cha uchimbaji madini.Sambamba na hayo, amewataka kuepuka migogoro katika vikundi vyao na kutokubali kukatishwa tamaa katika hatua hiyo ambayo aliita safari ya mafanikio.“Kupitia kwenu tunatarajia kuona mabilionea wapya ndani ya Nyamongo. Serikali itakuwa nanyi bega kwa bega, mkiwa na shida pigeni hodi mtafunguliwa na kusikilizwa,” Chikoka amewambia wachimbaji hao.Aidha, ameishukuru Barrick kwa kuridhia kutoa baadhi ya maeneo yake kwa ajili ya wachimbaji hao, akisema hatua hiyo itasaidia kukomesha tatizo la vijana kuvamia mgodi wa North Mara kwa kisingizio cha kukosa maeneo ya kuchimba madini.

 

Sehemu ya wachimbaji wadogo wa madini waliohudhuria uzinduzi wa mafunzo yao.

Kwa upande wake, Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, Francis Uhadi, amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa anazofanya kuboresha sekta ya madini nchini.Uhadi ambaye amemwakilisha Meneja Mkuu wa Mgodi huo, Apolinary Lyambiko, amesema wataendelea kuunga mkono jitihada hizo, na kwamba mafanikio katika mradi huo wa wachimbaji wadogo wa madini yanahitaji ushirikiano kati ya serikali na wadau.

 

Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo, Dkt. Elisante Mshiu, amesema Serikali ya Tanzania inastahili pongezi kubwa kwa kuwa ya kwanza duniani kuanzisha hatua ya kurasimisha wachimbaji wadogo wa madini.Dkt. Mshiu amesema mafunzo hayo yatahusu elimu ya uchimbaji na uchenjuaji madini, biashara, tabia ya fedha, afya na utunzaji wa mazingira, ushirikiano katika vikundi, sheria na miongozo mbalimbali ya uchimbaji madini.

 

Nao baadhi ya wachimbaji wadogo wanaokwenda kunufaika na mafunzo hayo, wakiwemo Dominic Daniel, Bedi Elias, Careen John na Ester Max, wameeleza kupokea hatua hiyo kwa furaha, huku wakiomba hatua zilizobaki ziharakishwe ili waanze uchimbaji. “Tunaishukuru serikali kwa kutuletea mafunzo haya lakini tunaiomba isitucheleweshee hatua zinazofuata ikiwa ni pamoja na kutuonesha maeneo ya kuchimba na kusaidia vitendea kazi vya kisasa,” amesema Ester.

 

Sehemu ya wachimbaji wadogo wa madini waliohudhuria uzinduzi wa mafunzo yao.

Mafunzo hayo yatafanyika kwa makundi na siku tofauti kwenye kumbi za shule za sekondari Bwirege, Ingwe, Nyamongo, Nkenge, Kemambo na Julius Kambarage Nyerere zilizopo tarafa ya Ingwe.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Chikoka (aliyesimama) akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mafunzo hayo.

Picha ya pamoja ya viongozi walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa mafunzo hayo.


Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini (mbele) wakiwakilisha wenzao katika picha ya pamoja na viongozi.


Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.