Na Damas Makangale , Kakola , Bulyanhulu
Mbunge wa Kahama Mjini , Mheshimiwa
Jumanne Kishimba amewaasa wananchi wa jimbo lake kuwekeza nguvu zao kwenye
kilimo na ufugaji zaidi ili kujihakikisha uhakika kwa chakula na mapato kwa
ustawi wa maisha na nchini kwa ujumla.
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizi leo asubuhi kwa njia ya simu, Mbunge huyo wa Kahama mjini, amesema kwamba
wananchi wa Jimbo langu lazima waanze kubadiisha mtazamo (mindset) na kuanza
kuwekeza kwa nguvu zao zote kwenye maeneo ya kilimo na ufugaji ambao ni
endelevu kwa ustawi wa maisha yao.
“Ukitizama kwenye jimbo la kahama na
vitongoji vyake watu wake wamewekeza kwenye nyumba za kulala na za wageni
lakini nyumba ni kwa ajili ya kulala tu , sio kwa ajili ya maendeleo endelevu
ni lazima waanze kuwa na mtizamo tofauti na kuwekeza kwenye kilimo na ufugaji,”
“Kilimo cha matunda, mazao ya
biashara , michikichi kwa kutumia kilimo
cha asili bila kununua mbolea na mbegu za viwandani , wananchi wa jimbo langu
wanaweza kuanza kuona kwa kuweka nguvu zaidi kwenye kilimo na ufugaji,”
aliongeza
Mheshimiwa Kishimba alifafanua kwamba
kilimo cha asili au hai kinaweza kukuza mnyororo wa thamani na kukuza
uzalishaji, vifungashio vitokanavyo na kilimo hao na uanzishwaji wa viwanda
zitokanazo na kilimo na kupunguza tatizo la ajira.
“kilimo hai pamoja na ufugaji wa ng’ombe na mbuzi kunaweza
kuleta matokeo Chanya kwa wananchi na wanaweza kujitengenezea ajira na kupata
masoko ya kikanda na kimataifa.
Mbunge huyo alipinga vikali dhana ya
ng’ombe kuwekewa hereni ili kudhibiti wizi a ng’ombe kwenye jimbo lake na
kusisitiza kwamba mpango wowote utaoletwa na serikali ni lazima wananchi
washirikishe ili uwe tija kwa watu wote.
“Moja ya manufaa ya kilimo hai ni
njia sahihi ya kuboresha afya za watanzania na kilimo hiki kinalinda mazingira
yetu mashambani na kinatosha lishe iliyo bora kabisa kwa manufaa ya
watanzania,” Alisisitiza Mheshimiwa Kishimba
Mwisho
Post a Comment