Wanafunzi 6000 wa Shule za Msingi Dar wanufaika na elimu ya usalama barabarani

.Mradi ulioanzishwa na Total Energies Marketing Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MRADI wa “VIA Creative” unaolenga kuwapatia elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa Shule za Msingi umewafikia takribani wanafunzi 6000 kwenye Shule za Makuburi, Ubungo, NHC, Buza, Jangwani, Ugindoni na Uzuri katika jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Total Energies, Bw Mamadou Ngom akizungumza na wageni waalikwa , wanafunzi kwenye hafla ya kukabidhi tuzo na vyeti kwa wanafunzi na shule iliyofanya vizuri kwenye shindano wa mradi wa “VIA Creative” wa kutoa elimua ya usalama barabarani hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni .

Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo ya kukabidhi tuzo wa wanafunzi waliofanya vizuri na shule  iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni,  Mkuu wa Idara ya Mafunzo ya Trafiki Kinondoni, A.S.P Rose Bernard Maira aliwapongeza Total Energies Marketing Tanzania Limited, TotalEnergies Foundation Pamoja na Nafasi Art Space kwa juhudi zao za kutoa elimu ya usalama barabarani zinastahili kupongezwa na kuigwa na makampuni mengine ili kuchochea usalama wa watoto waendapo na watokapo mashuleni.

“Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani tupo Pamoja nanyi kwenye jambo hili na katika kutoa elimu ya usalama barabarani pamoja na kuzijua sheria, kanuni na taratibu za barabarani kwa wanafunzi na watumia Barabara wote.

“Aidha, tumefurahia kujua kwamba mradi huu pia unalengo la kutimiza mapendekezo ya kuboresha hali ya usalama kwa wanafunzi wa shule iliyoshinda kama trulivyopata kuona kwenye filamu ya wanafunzi hao. Pia niwatakie kila la heri washindi hawa kwenye hatua nyingine ya shindano ambalo wanatarajia kuingia, nawasihi muiwakilishe Tanzania vizuri na mungae Pamoja na kushinda ngazi za shindano la VIA Creative zijazo.” Aliongeza.

Mmoja ya wanafunzi wa Makuburi akipokea tuzo yake kutoka kwa Mgeni rasmi , ASP , Rose Bernard Maira 

Alisema kwamba usalama barabarani ni suala muhimu katika jamii yetu,kila mwaka tunashuhudia ajali nyingi za barabarani ambazo zinaweza kuzuiliwa kwa njia rahisi ya kueneza elimu sahihi ya sheria, alama na utumiaji salama wa barabara.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Total Energies, Bw Mamadou Ngom alisema kwamba shindano hilo ambao lilikuwa kwa njia ya sanaa ya michoro, muziki, maigizo na mashairi kuna ongeza uelewa wa wanafunzi kwenye mambo ya usalama barabarani na kupunguza ajali.

“Tunayo furaha kubwa kuwa hapa leo tukisherehekea mafanikio ya mabalozi wetu wa usalama barabarani kupitia mradi wa VIA Creative amabo tumeshirikiana na Nafasi Art Space ambao wamekuwa wakiwapatia wanafunzi hawa elimu ya usalama barabarani kwa kupitia sanaa,”

“Kupitia mradi huu tumeweza kuunda klabu za mabalozi barabarani 120, 20 kutoka kwenye kila shule. Pia wanafunzi hawa wameweza kutoa mapendekezo yao ya jinsi ambavyo usalama wao wa barabara unaweza kuboreshwa nasi tutatekeleza mapendekezo hayo kwa shule ya msingi ya Makuburi ambao ndio washindi wa kitaifa wa shindano hili kwa mwaka 2024.” Alisema Bw Ngom

Aliongeza kwamba usalama barabarani ni suala muhimu katika jamii yetu,kila mwaka tunashuhudia ajali nyingi za barabarani ambazo zinaweza kuzuiliwa kwa njia rahisi ya kueneza elimu sahihi ya sheria, alama na utumiaji salama wa barabara.

Alisema kwamba  ni jukumu letu sote kuhakikisha tunafuata sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepuka ajali ambazo athari zake kiuchumi na kijamii ni kubwa sana.

“Ningependa kuchukua fursa hii kuwapongeze  wanafunzi wote 120 walioshiriki kwenye mradi huu na kushindanishwa kwenye shindano la VIA Creative, nyinyi nyote ni washindi na mabalozi bora wa usalama barabarani. Tunawaomba muendele kuwafundisha wenzenu, wadogo zenu, na hata wazazi wenu juu ya utumiaji salama wa Barabara Pamoja na sheria na kanuni zake,” alisisitiza.

Bw Ngom aliongea kwamba Total Energies wapo pamoja na Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani  kwenye jambo hilo na katika kutoa elimu ya usalama barabarani pamoja na kuzijua sheria, kanuni na taratibu za barabarani kwa wanafunzi na watumia Barabara wote.

Mkuu wa Idara ya Mafunzo ya Trafiki Kinondoni, A.S.P Rose Bernard Maira akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya kugawa tuzo kwa wanafunzi na shule za jijini Dar es Salaam kwenye mradi wa “VIA Creative” unaolenga kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi jijini Dar es Salaam. 

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Nafasi Art Space ambaye ni mdau wa mradi huo, Felix Muchira alisema kwamba waliona ni muhimu kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi kwa njia rahisi ya maigizo na uchoraji ili waweze kufikisha ujumbe kwa haraka zaidi.

“ajali hapa nchini limeanza kuwa jambo la kawaida na ni jukumu letu sote kuendelea kutoa elimu kwa kushirikiana na serikali na hasa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani kutoa elimu ya michoro, alama na sheria za usalama barabarani kwa Watoto wetu,” alisema Bw Muchira.

Mgeni rasmi wa shughuli hiyo, ASP Rose Bernard Maira akigawa cheti/ tuzo kwa mwalimu wa Shule ya msingi Makuburi iliyoibuka kidedea kwenye shindano la mradi huo 

Shindano hilo la kimataifa la "VIA CREATIVE" ni shindano linalolenga wanafunzi wa shule za msingi wa miaka 4 -19 kwa lengo la kuwapatia elimu ya usalama barabarani kwa njia ya sanaa ya michoro, muziki, maigizo na mashairi na kisha kuwapa fursa wanafunzi hao kuelezea uleewa wao na mapendekezo yao ya usalama barabarani kwa njia ya michoro na maigizo.

Mwaka huo  wa VIA Creative umewafikia wanafunzi 6000 kutoka shule za msingi Makuburi, Ubungo NHC, Buza, Jangwani, Ugindoni na Uzuri zilizopo jijini Dar es salaam na kuendeleza uundaji wa klabu za mabalozi wa usalama barabarani. 


Mwanafunzi kutoka  Shule ya Msingi Makuburi akipita baada ya kupokea cheti chake mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Total Energies, Bw Mamadou Ngom

VIA Creative ni mradi ulioanza mwaka 2022 ambao tangu mwaka huo zaidi ya wanafunzi 22,000 wamefikiwa na mradi huu na kuweza kujenga klabu za mabalozi wa usalama barabarani kwenye shule 100 jijini Dar es Salaam na Bagamoyo.

Hafla ya kukabidhi tunzo kwa wanafunzi walioshinda kwenye msimu huu wa tatu wa VIA Creative zilifanyika kwenye ofisi za TotalEnegies Marketing Tanzania Limited jijini Dar es Salaam ambapo shule ya msingi ya Makuburi Primary school iliibuka mshindi wa kitaifa wa shindano lwa shindano hili na muwakilishi wa Tanzania kwenye ngazi ya kimataifa munamo mwezi Novemba 2024.


Mwanafunzi kutoka  Shule ya Msingi Makuburi akipita baada ya kupokea cheti chake mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Total Energies, Bw Mamadou Ngom.



Baadhi ya wafanyakazi wa Total energies wakifuatilia tukio hilo kwenye hafla hiyo 

Mwisho

 


Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.