Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
ambaye pia mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei, amesema kuwa uamuzi wa
Rais Magufuli wa kufuta sherehe za uhuru utakuwa umeleta tija kubwa kwa
taifa ambapo miaka mingi taifa limekuwa likichezea mabilioni ya shilingi
bila faida kwa taifa.
Mtei alimesema kuwa sherehe hizo
zilizokuwa zikifanyika kwa shamrashara ambazo zilikuwa zinagharimu fedha
za walipa kodi kwa anasa za kula, kunywa na kulewa huku watanzania
wakikosa huduma muhimu.
Aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha
Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ameshauri kuwa sherehe hizo
zifanyeke mara moja kila baada ya miaka mitano ambapo zisihusishe
matumizi mabaya ya fedha za wananchi kama zilivyokuwa za awamu iliyopita
kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.
Naye spika wa kwanza
wa Bunge la Tanzania Pius Msekwa amesema kuwa kitendo hicho kinapaswa
kuungwa mkono kwa kila ambaye anayeitakia mema Tanzania. Sherehe hizo
zimewaunganisha waatanzania wote kwa kufanya jambo moja ambapo sherehe
hizo zilikuwa zikifanyika Dar es Salaam pekee kwa gharama kubwa lakini
sasa zimekuwa za nchi nzima na zenye maslahi na taifa.
Post a Comment