Wafanyabiashara
wa mboga mboga, samaki wa kuzindika na bidhaa zingine za kilimo wameombwa
kutumia fursa ya kuuza bidhaa zao nje ya nchi kufuatia kuzinduliwa kwa Bohari
ya kwanza ya kisasa katika bara la Africa iliyogharimu shilingi bilioni 26 za
kitanzania.
“Matarajio
ya ukuaji wa huduma za usafirishaji wa bidhaa za kilimo, chakula na mifugo
kupitia bohari hii ya kisasa Zaidi nchini na ni dhamira ya serikali kuhakikisha
wafanyabishara katika sekta ya kilimo wananufaika kupitia mradi huu kabambe,”
amesema Waziri wa Kilimo, uvuvi na Ushirika, Dkt Charles Tizeba wakati wa
uzinduzi wa bohari hiyo ya jana kwenye Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
Sekta
ya usafiri wa anga ni nyeti, ambayo uwepo na ukuaji wake unategemea huduma
zinazoaminika—kama vile pamoja na mambo mengine utunzaji na usimamizi wa
mizigo, bohari, utunzaji na usimamizi wa barua, utunzaji wa nyaraka zinazohusu
mizigo iliyopakiwa au kupakuliwa.
Dkt
Tizeba aliongeza pia kwamba wizara yake itaanza kuhamamisha wakulima na
wafugaji kuanza kutengeneza na kuandaa nyama kuweka katika ubora wa uhakika ili
kuweza kuuza nje ya nchi na kuuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa
ujumla.
“Kwa
sasa machinjio yetu ya Ruvu wanaweza kuchinjwa takribani ng’ombe 4,000 kwa siku
ila tupo katika mpango kabambe kuhakikisha idadi inaongezeka ili waweze kutumia
fursa ya bohari hii ya kisasa kutafuta masoko nje ya nchi,” amesema Dkt Tizeba
Amesema
kwamba serikali itaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara wa ndani ili waweze
kutumia uwanja huu wa ndege wa Mwl nyerere ili kuuuza mtandao wa kuuza bidhaa
zao za kilimo, mboga mboga na maua nje ya nchi.
Alisisitiza
kwamba ni muhimu wa Serikali kuendelea kushirikiana na taasisi, sekta binafsi
katika sekta ya anga ili kuleta tija na kutumia sekta hii kama kichocheo cha
ukuaji wa uchumi wan chi nzima.
“wafanyabiashara
wa maua na bidhaa zingine za kilimo wanapaswa kuendelea kutumia fursa hii
adhimu katika kupambana na umaskini na kupunguza tatizo la ajira nchini.
Bw
Temu alisema kwamba uzinduzi rasmi wa jengo hilo jipya la kuhudumia mizigo
inayoingia na kutoka nchini ni la kisasa barani Afrika na litaongeza ufanisi wa
huduma katika sekta ya usafirishaji nchini.
Alisema
kwamba kampuni hiyo Swissport ni ya kimataifa ambayo inatoa huduma zake kwa
takribani nchini 58 duniani kwa kiwango cha ubora wa kimataifa ya kusafirisha,
kuhifadhi na kupokea mizigo ya aina zote na bidhaa mbalimbali.
Bw
Temu aliongeza kwamba kitengo cha bohari ya kupakia mizigo kimetengenezwa kwa
teknolojia ya juu kabisa katika kuhakikisha ufanisi na uharakishaji wa upakiaji
mizigo ambapo kinaweza kupakia tani 30 kwa siku.
Kwa
kutambua umuhimu wa huduma Kampuni ya Swissport inayotoa, Bw Temu alisema:
“Tumeamua kuboresha huduma zetu za kupakia na kupakua mizigo…kwa kweli, hizi ni
nguzo muhimu kwa ukuaji endelevu wa hii sekta nchini Tanzania.”
Akielezea
uboreshaji ambao umefanyika, Bw Temu alisema kwa sasa chumba maalum cha baridi
cha Swissport kimepanuliwa kwa kuongeza huduma mpya kama vile mfumo wa ukaguzi
wa mizigo ndani ya chumba chenye mitambo maalum.
Alisema “chumba hiki maalum
kimegawanywa katika maeneo mawili: eneo moja lina ukubwa wa mita 200 za mraba
na lingine ni mita 100 za mraba.”
Akifafanua zaidi, ofisa mkuu huyo wa Swissport
alisema kampuni yao imefunga mizani ya futi 20 katika eneo lao kwa kutoa huduma
kulingana na mahitaji ya shirika la ndege husika.
Kwa
upande wa kuhifadhi mizigo, kampuni ya Swissport imejenga bohari ya kisasa na
salama na inayoweza kufiwa kwa urahisi. Imefungwa mitambo maalum ya CCTV na ya
ukaguzi wa magari. Pamoja na mambo mengine, bohari hii ina vifaa maalum kwa
ajili ya ukaguzi, uangalizi na utunzaji salama wa mizigo.
Uboreshaji
uliofanywa hivi karibuni umefanywa kwa lengo la kuisaidia serikali katika
jitihada zake za kuboresha huduma za usafiri wa ndege, ambao ni muhimu sana
katika kukuza uchumi wa nchi na kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi za
ustawi wa mamilioni ya Watanzania, kwa mujibu wa Meneja Mikataba na
Masoko-Swissport, Bw James Mhagama.
Post a Comment