Na Damas Makangale, Dar es Salaam, Tanzania
Zaidi ya wanafunzi
1,000 kutoka Kusini mwa jangwa la Sahara wamepata udhamini wa kwenda
kusoma shahada zao za kwanza katika nchini za China, Marekani, Canada,
Uingereza, India, Australia, Afrika ya Kusini, Sweden, Denmark na Norway.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo jijini
Dar es Salaam, Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Universities Abroad Link (UAL),
ambacho ni shirika la kuratibu wanafunzi wa kiafrika wanaotaka kwenda kusoma
nje ya nchi, Bw Tony Rodgers Kabetha amesema kwamba shirika hilo linaratibu
wanafunzi kutoka nchi za Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Msumbiji, Botswana na
Afrika ya kusini ambao wana nia ya kwenda kusoma nje ya nchi.
Mkurugenzi na Mwanzilishiwa Universities Abroad Link (UAL) Bw.Tony
Rodgers Kabetha (kulia) akiwaaga baadhi ya wanafunzi waliopata udhamini wa kwenda kusoma nje ya nchi.
|
"Kwa dhati
kabisa tuliamua kuanza kusaidia wanafunzi kutoka kusini mwa jangwa la sahara na
Afrika kwa ujumla kuhusu taarifa za sahihi za vyuo bora kabisa duniani na kozi
wanazotoa ambazo zitakuwa na manufaa kwa wanafunzi hao baada ya kuhitimu masomo
yao,” alibainisha.
Aliendelea kusema kwamba wanafunzi kutoka nchi hizo
za Afrika wanaweza kuomba na kupata udhamini kutoka kwenye vyuo vikuu bora kabisa
kutoka nchi za Marekani, Uingereza, Canada, China, India, Australia, Sweden,
Afrika Kusini, Denmark na Norway na ada ya masomo inaweza kuwa chini zaidi
kulingana na ada za hapa nyumbani.
Kabetha, ambaye kitaaluma ni Injinia wa mawasiliano
ambaye amegeuka na kuwa mdau wa elimu ya juu alisema kwamba wazo la kuja na
shirika lilianza miaka tisa iliyopita baada ya wanafunzi na baadhi ya waaafrika
waliokuwa wakiishi na kufanya kazi marekani kuamua kuanza kuwasaidia watanzania
namna bora ya kupata vyuo vya kusoma nje ya nchini.
"Tumeamua kuja na shirika hili la elimu ya juu ili
kuwapa Watanzania na wa afrika kwa ujumla taarifa sahihi kuhusu vyuo vikuu na
kozi sahihi ambayo inaambatana na mahitaji ya soko la ajira," aliongeza.
Alibainisha kuwa UAL pia hutoa ushauri wa kitaaluma
na wa kazi kwa wanafunzi ili kuhakikisha kwamba hawasomi shahada ambazo
watajikuta mwisho wa siku hawana ajira ndani ya Tanzania na hata kama wakienda
nje ya Tanzania pia watakosa ajira.
"Unataka kujifunza nini? Wapi unataka kwenda kujifunza?
Na Kwa nini ni uchukue kozi hii ni maswala ambayo tunapenda kuuliza wanafunzi
katika juhudi za kuwasaidia lakini pia tunawapa taarifa za hali ya hewa za nchi
husika wanapokwenda,” alisisitiza.
Kabla ya kuanzishwa kwa shirika hilo wanafunzi na
wazazi walikuwa wakipewa taarifa za uongo kuhusu vyuo vingi katika nchi
ziilizoendelea na kutoa fedha nyingi ambazo zilikuwa hazina manufaa yoyote
kwao.
Kabetha ilisisitiza kwamba changamoto kubwa kwa
Watanzania walio wengi ni kuchagua kusoma fani ambazo hazina soko na uwezekano
wa kupata kazi ni mdogo na kutokana ukweli huu tunawaelimisha wanafunzi umuhimu
wa kuchagua kozi zenye manufaa kwenye maisha yao.
Alisema kuwa soko la ajira kwa sasa limepanuka zaidi
kwenye fani ambazo ni chache sana watu kwenda kuomba kusoma kama vile mambo ya
mafuta, gesi, teknolojia, uchumi wa biashara.
Post a Comment