SPIKA
Mstaafu, Anna Makinda ameiomba serikali na mamlaka husika kuanza mchakato wa
kusukuma mabadiliko ya sheria ya ndoa ili kupanua wigo wa haki za wanawake na
watoto nchini.
Akizungumza
katika kongamano la wanawake lilioandaliwa na Mfuko wa msaada wa kisheria
nchini (LSF) jana jijini Dar es Salaam, Makinda alisema kwamba sheria ya ndoa
ya mwaka 1971 imepitwa na wakati na inahitaji marekebisho makubwa ili kutoa
haki kwa wanawake nchini.
“Hii
sheria ya ndoa inawatenga sana wanawake nchini katika swala la mirathi na
kuacha watoto wengi wakiteseka ni wakati muafaka sasa kwa wanaharakati kusaidia
na wabunge ili kuleta marekebisho hayo kwa manufaa ya nchini nzima,” alisema
Makinda ambaye ni spika mstaafu.
Alisema
kwamba marekebisho hayo makubwa au kuandikwa upya kwa sheria ya ndoa itakuwa
hatua moja kubwa katika kulinda haki za wanawake za kumiliki mali, kama vile
mashamba na kadhalika.
Alisisitiza
kwamba swala la mirathi ni tatizo kubwa sana nchini ambapo wanawake wengi
wamepoteza mali zao walizochuma na wenzi wao wakati wa ndoa.
“Nikiwa
mbunge, waziri na baadaye spika tulipambana vikali katika kubadilisha sheria ya
ardhi ili kuwapa watu wa hali ya chini kupata nafasi ya kumiliki ardhi, sasa na
hii sheria ya ndoa inapaswa kushughulikiwa kwa haraka ili kuweza kutoa matokeo
chanya kwa jamii,” aliongeza.
Alifafanua
kwamba marekebisho hayo ya sheria ya ndoa yatasaidia kunusuru maelfu ya
wanawake ambao wanateseka kutokana na kila aina ya unyanyasaji wa kijinsia na
vipigo ambavyo vinaongezeka kila kona ya nchini.
Aliomba
mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kushirikiana na serikali katika majadiliano
hasa katika mambo ya mirathi na ndoa ili kuhakikisha upatikanaji wa marekebisho
hayo yanapatikana haraka.
“ni
muhimu pia maswala haya ya haki za wanawake na watoto kufundishwa katika shule
za msingi na sekondari ili kupeleka elimu hiyo ya uraia kwa wanafunzi nchini
nzima, ila ni muhimu kushirikiana na serikali ili kufanikisha hayo,” aliongeza
Kwa
upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu, Mfuko wa Msaada wa Kisheria (LSF), Bw, Kees
Groenendijk alisema kwamba mfuko lengo lake kuu ni kuongeza haki na usawa kwa
wanawake nchini kupitia uwezeshaji wa fedha na mafunzo.
“Kutokana
na mustadha huo, mfuko uliamua kwamba mfuko kusaidia mashirika yasiyo kuwa ya
kiserikali yanayotoa msaada wa kisheria kwa jamii hasa wanawake ambao wapo
katika wilay zote za Tanzania Bara,” alisisitiza.
Alisema
tangu mfuko huo uanze zaidi ya wanawake 2,000 walifikiwa kwa msaada wa kisheria
ambao ni asilimia 60% ya wanawake nchini nzima.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania
(TAWLA) Bi, Tike Mwambipile alisema kwamba serikali ni lazima kuanzisha kitengo
maalum cha kushughulikia matatizo ya ndoa na mirathi katika mifumo ya utoaji
haki nchini.
Post a Comment