VYOMBO VYA HABARI
Kuendesha gari katika msimu huu wa sikukuu
Uber
huendesha modeli fanisi inayoitwa bei hai, ambayo huwawezesha watumiaji
kupata gari wakati wanaihitaji sana - hasa wakati wa siku za mwaka
zenye shughuli nyingi, kama vile Siku ya Kuamkia Mwaka Mpya au baada ya
hafla kubwa ya michezo
DAR ES SALAAM, Tanzania, Desemba 13, 2016/ -- Msimu
wa sikukuu ukianza nchini Tanzania, tunakabiliana na changamoto ya
mwaka: tutawezaje kufika nyumbani sikukuu zikiisha? Ijapokuwa ni rahisi
sana kuwajibika, watu wengi bado huendesha magari wakiwa wamelewa.
Tumeshughulikia mambo msingi ya kusafiri katika msimu huu wa sikukuu,
ili daima uweze kufanya maamuzi salama.
Panga mapema
Je, unafikiria kinywaji chako cha baada ya kazini kinaweza kujumuisha glasi nyingine zaidi kuliko ulivyotarajia? Panga mapema na utumie Uber (www.Uber.com)
kwenda kazini. Unaweza hata kupanga safari yako mapema ili usiwe na
wasiwasi kuhusu kutatiza sikukuu zako hadi dereva wako awasili. Au, kama
sherehe itakupata kwa ghafla, tumia Uber kwenda nyumbani, acha gari
lako ofisini na ulichukue wikendi.
Wakati hatua hii inaweza kuonekana kama kazi ya ziada mara ya kwanza,
ni bei nafuu ikilinganishwa na kuhatarisha usalama wako na usalama wa
wengine kwa kunywa na kuendesha gari.
Jua kuwa utapata dereva, hata wakati kuna shughuli nyingi
Katika
misimu ya likizo, mara kwa mara kuna wasiwasi kuwa hakutakuwa na
madereva wa kutosha. Hiyo si uongo lakini kwa kuwa jukwaa la Uber
linaendelea kukua na kubadilika, Uber huendesha modeli fanisi inayoitwa
bei hai, ambayo huwawezesha watumiaji kupata gari wakati wanaihitaji
sana - hasa wakati wa siku za mwaka zenye shughuli nyingi, kama vile
Siku ya Kuamkia Mwaka Mpya au baada ya hafla kubwa ya michezo.
Wakati
kuna mahitaji mengi, ni muhimu kuwa kuna madereva wa kutosha kwenye
jukwaa hili ili kuwahudumia wale wanaotafuta gari. Kwa sababu hii, Uber
huongeza nauli ili kuwahimiza madereva zaidi kuja kwenye jukwaa hili.
Hesabu
ya bei hai huongeza bei kiotomatiki ili kuwahimiza madereva zaidi kuja
kwenye jukwaa hili na kushughulikia mahitaji haya. Wakati mahitaji na
ugavi umesawazishwa, bei hurejea kawaida kwa haraka. Utajua wakati bei
hai inatumika, kwa sababu utaarifiwa kuanzia wakati unapofungua app, na
kukumbushwa unapokuwa ukiomba safari yako. Bei hai uhakikisha kuna
magari yanayopatikana wakati wowote unapofungua app hiyo.
Vipengele vya usalama
Tumejitolea kwa usalama na tunataka kila mmoja kuwa na imani kuwa Uber ni chaguo thabiti msimu huu wa sikukuu.
Teknolojia
yetu huifanya iwe rahisi kufanya maboresho ya usalama ambayo hayakuwa
hapo awali kabla ya Uber. Wakati dereva anapokubali ombi lako, unaweza
kuona jina lake la kwanza, picha, na nambari ya leseni ya gari. Magari
yote hufuatiliwa kwa kutumia GPS na unaweza kushiriki Muda Unaokadiria
Kuwasili hivyo kuwawezesha wapendwa wako kuona safari yako kwa wakati
halisi (hata kama hawana app ya Uber).
Pesa ziko salama
Je,
huna kadi? Hakuna shida! Unaweza bado kusafiri na sisi na ulipe kwa
pesa taslimu. Chagua tu chaguo la PESA TASLIMU, safiri na ulipe nauli
moja kwa moja kwa dereva wako mwisho wa safari. Safari zote za Uber
zinafuatiliwa kwa kutumia GPS na tunajua eneo lako katika kila safari
ili kuhakikisha usalama wa wahusika wote. Tumewahimiza
pia kuweka pesa kwenye benki mara kwa mara na kubakia na hela kidogo
kama iwezekanavyo (pesa za kulipia mafuta na kununua bidhaa). Hadi sasa
hatujaona ongezeko lolote la uhalifu katika nchi zinazoendesha chaguo za
malipo ya pesa taslimu.
Je, unahitaji msaada? Tuko hapa kila wakati kwa ajili yako
Tunajua
kwamba kuna wakati unahitaji kuwasiliana: pochi ilisalia ndani ya gari,
au pengine nauli si sahihi. Sasa, kuwasiliana ni rahisi kama kutumia
jukwaa letu. Tumeunda mtandao mkubwa wa vituo vya usaidizi ili kutoa
usaidizi 24/7. Kitendaji chetu cha Msaada ambacho ni rahisi kutumia ndani ya app hujibu maswali yako yote. Bofya tu "Msaada" na maelezo yote unayohitaji yako hapo.
Furahia, bila kuwa na wasiwasi kuhusu safari yako
Licha
ya haya yote, msimu wa likizo ni wakati wa kuwa bila mawazo. Unahusu
kushughulikia mambo machache ili uweze kufurahia. Kwa kunufaika na
chaguo za kushiriki gari, hustahili kuwa na wasiwasi kuhusu kuegesha
gari, kumpa dereva bakshishi (madereva wetu hubaki na kiasi kikubwa cha
nauli), 'kuzidisha kikomo' au jinsi utakavyofika nyumbani. Wakati huduma
hii inafurahisha, rahisi, na inapatikana hivi, hakuna sababu ya
kutochagua kuwajibika.
Kusambazwa na APO kwa niaba ya Uber.
Kwa maelezo zaidi:
Samantha Allenberg
Uber Communications Africa
Tel: +27 82 453 7495
Email: Samantha.Allenberg@Uber.com
Jessica Gois - Jenni Newman
Public Relations (Uber South Africa - PR Agency)
Tel: + 27 (0) 82 777 5427
Email: Jessica@JNPR.co.za
Samantha Allenberg
Uber Communications Africa
Tel: +27 82 453 7495
Email: Samantha.Allenberg@Uber.com
Jessica Gois - Jenni Newman
Public Relations (Uber South Africa - PR Agency)
Tel: + 27 (0) 82 777 5427
Email: Jessica@JNPR.co.za
Mitandao ya Kijamii:
Twitter: @UberNigeria | Facebook: /UberNigeria | Instagram: @UberNigeria
Kuhusu Uber:
Twitter: @UberNigeria | Facebook: /UberNigeria | Instagram: @UberNigeria
Kuhusu Uber:
Lengo
mahususi la Uber ni kusaidia watu kupata usafiri kwa kubonyeza kitufe
tu – mahali popote na kwa kila mtu. Tulianza mwaka 2009 kwa kutatua
tatizo dogo – ni kwa jinsi gani unaweza kupata usafiri kwa kubonyeza
kitufe? Baada ya miaka sita na zaidi ya bilioni ya safari fupi, tumeanza
kutatua hata matatizo makubwa: kupunguza mrundikano na uchafuzi wa
mazingira katika miji yetu kwa kubeba watu wengi kwa kutumia magari
machache.
Mtandao wa Uber
kwa sasa unapatika kwenye nchi zaidi ya 75 ndani ya mabara 6 na zaidi ya
miji 475. Kuomba usafiri, watumiaji wanapaswa kupakua app (ni bure) kwa
ajili ya Android, iPhone, Blackberry 7, au kujiunga kupitia tovuti ya www.Uber.com/go. Kwa taarifa zaidi na maswali tembelea tovuti yetu: www.Uber.com.CHANZO
Uber
Maudhui multimedia
- Download logo
- Link: Uber
- Link: Uber Registration
Post a Comment