Shirika la kisheria lisilo la kiserikali la Legal Services Facility (LSF) wiki
hii litatoa msaada wa komputa 176 zenye thamani ya shilingi million 146
kwa ajili ya vituo 160 vya wasaidizi wa kisheria vilivyoko mikoani—kama
sehemu ya mkakati wake wa kuongeza ufanisi na kuboresha utoaji wa
huduma za kisheria nchini.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari hivi karibuni,
komputa hizo zitatolewa wakati wa warsha (itakayofanyika Ijumaa hii Dar
es Salaam) kwa viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotoa
msaada wa sheria na yanayofadhiliwa na LSF—kutekeleza miradi ya
wasaidizi wa kisheria nchini.
Bw Kees Groenendijk,
Meneja wa LSF, alisema komputa ni zana muhimu kwa vituo vya wasaidizi
wa kisheria na wasaidizi wa kisheria wenyewe wanaotoa msaada wa kisheria
nchini. Tangu kuanzishwa kwake miaka mitano iliyopita, LSF imekwishatoa
ufadhili wa mabilioni ya fedha, ambazo, pamoja na mambo mengine,
zimerahisisha kuanzishwa kwa vituo vya wasaidizi wa kisheria sehemu
mbalimbali nchini.
Mkurugenzi wa Shirika la Legal Services Facility (LSF), Bwana. Kees Groenendijk akizungumza leo Jijini Dar es Salaam |
“Ni
ukweli usiopingika kwamba wasaidizi wa kisheria wamekuwa wakifanya
vizuri sana linapokuja suala la kuwasaidia wanaohitaji msaada wa
kisheria hasa vijijini. Ndiyo maana tumeamua kutoa hizi zana, ambazo
naamini vitaongeza ufanisi wa huduma za kisheria. Naamini zitaongeza
ufanisi na utendaji wa wasaidizi wa kisheria na vituo vya wasaidizi wa
kisheria,” alisema Bw Groenendijk.
Komputa
zitatolewa kwa mashirika yasiyo ya kiserikali 27 yanayotoa msaada wa
sheria, ambayo ndiyo yatakayotoa hizo komputa kwa vituo vya wasaidizi wa
kisheria katika maeneo yao ya kazi. Mashirika yasiyo ya kiserikali
yanayotoa msaada wa sheria yametoa mchango mkubwa sana katika
uanzishwaji wa vituo vya wasaidizi wa kisheria kupitia ufadhili wa LSF.
Kwa
mujibu wa taarifa ya LSF, warsha inayofanyika wiki hii itatoa nafasi
kwa washiriki kujadili mambo mbalimbali na changamoto zake katika
kutekeleza miradi inayofadhiliwa na LSF na kupata suluhisho.
Pamoja
na hayo, warsha hiyo itawezesha LSF kuelezea njia mkakati yake ya
2016-2021, nini LSF inataka kupata na matokeo yake kwa mashirika yasiyo
ya kisherikali yanayotoa ushauri wa kitaalam (RMOs). Masuala mengine
yanahudu namna ya kutatua migongano kati ya malengo ya kitaasisi ya RMOs
na malengo mkakati ya LSF na namna ya kuongeza matokeo.
Kutakuwa
na majadiliano pia juu ya kuyajengea uwezo mashirika yanayofadhiliwa na
LSF/yanayotoa ushauri wa kitaalam, namna ya kujenga uwezo kwa wasaidizi
wa kisheria na LSF, umuhimu wa kupima kazi na matokeo yake na kuripoti
kwa njia ya mtandao.
Post a Comment