Mtindo
wa karate mkongwe duniani, Okinawa Goju Ryu wa chama cha Jundokan
Tanzania chini ya mwakilishi wake Sensei Rumadha Fundi mwenye Dan 4,“Yondan” pia mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 38 ya mafunzo ya sanaa ya Karate mtindo wa Goju Ryu chini ya walimu wakuu wengi maarufu toka Okinawa, Japan kama vile Master Mario Higaonna(IOGKF), Master Masataka Muramatsu( Goju Ryu Kyokai), Teruo Chinen( Jundokan International), na hatimae Kancho Yoshihiro Miyazato, mwenyekiti wa (Jundokan So Honbu, Naha, Okinawa)Master Tetsunosuke Yasuda, Master Tsuneo Kinjo na Master Tetsu Gima.
Tunatarajia kufanya mitihani ya mikanda mieusi miezi ijayo madaraja tofauti kupitia dojo za “ Kaizen dojo”
Jamhuri na dojo dada ya Hekalu la Kujilinda Zanaki dojo. Hii ni moja ya
jitihada za kusambaza mwenendo huu kwa kina na pia ufundishaji wa mbinu
za utumiaji wa tafsiri za “Kata” uijulikanao kama “Bunkai”, au uchambuzi wa matumizi ya mbinu za kujilinda. Mitihani yote itafanywa na sensei Rumadha Fundi chini ya utaratibu wa “Syllabus” ya Jundokan, Okinawa.
Lengo
pia ni kuzungumzia yale yote yaliojiri katika semina kuu ya Jundokan
bara la Ulaya chini ya master wake toka jijini Naha, Okinawa mwezi wa
Julai 2017. Ufundishaji sahihi wa mfumo huu ni moja ya malengo
kuhakikisha tu kwamba wana Jundokan duniani mkote wapo kwenye msimamo
mmoja katika uchambuzi na ufanyaji wao wa Kata na matumizi yake.
Pia
wakati huohuo, kutakuwa na semina ya wanafunzi wa ngazi za mikanda
mieusi wa Jundokan Tanzania ikiwemo na dojo ya Zanaki katika kuwawezesha
wanafunzi wake kuuliza na kupata majibu ya matumizi yao ya ufanyaji
Kata kama jinsi ipasavyo chini ya chama hicho chenye ufahasa wa mtindo
huo unaofuata nyanyo za mafunzo ya Master Chojun Miyagi, mwanzilishi wa
mtindo wa Okinawa Goju Ryu.
Hivyo,
hii ni moja ya fursa kubwa kwa wana Jundokan kuweza kushiriki semina
hii chini ya mwakilishi wa Jundokan Tanzania, ama kamaijulikanavyo “Tanzania Shibu-Cho”,
sensei Rumadha Fundi. Sensei Rumadha, amesisitiza kwa niaba ya chama
hicho kwamba Kila mwanafunzi wa mkanda mweusi, hana budi kuhudhuria
semina za walimu angalau mara moja kila miaka miwili na kupata
usahihisho muhimu kimafunzo. Hilo ndio lengo kuu hata kipindi kile kwa
mwanzilishi wa Okinawa Goju Ryu Tanzania, marehemu Sensei NC Bomani
kufanya ziara za mara kwa mara kwenda huko Naha, Okinawa kupata
marekebisho toka kwa magwiji wa Karate duniani na chimbuko lake.
Pia
vilevile, Tanzania imepatiwa mwaliko wa kuhudhuria maadhimisho ya miaka
65 tokea kuanzishwa kwa chama cha Jundokan itayofanyika November 2018
mjini Naha, Okinawa, Japan. Chama hicho kilianzishwa na mwanafunzi mkuu
wa Master Miyagi aitwae Master Eiichi Miyazato sensei 1957 ambae pia
alikuwa ndio mwalimu wa sensei Nantambu C Bomani. “ Chuo kinacho fundisha nyayo au mwenendo wa Master Chojun Miyagi”. Ikimaanisha,
hamna mabadiliko yeyote kimafunzo na Kata zake kama jinsi alivyokuwa
akifundisha mwanzilishi wake Chojun Miyagi sensei.
Post a Comment