Nchi za Afrika zinaweka mikakati inayolenga
kukomesha uzalishaji na matumizi ya dawa bandia na sizizo na viwango, tatizo
kubwa linalorudisha nyuma maendeleo ya nchi za Africa.
“Lengo letu kuu ni kuhakikisha ubora wa dawa
zinazotumiwa na waafrika,” amesema Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Faustine Ndungulile, wakati wa ufunguzi wa Mkutano
wa Jukwaa la Kudhibiti Ubora wa Madawa Afrika (African Medicines Quality Forum—AMQF). Kongamano hili limeandaliwa na Shirika la
Maendeleo Afrika (NEPAD), The United States Pharmacopeia convention (USP), Mamlaka
ya Chakula na Dawa (TFDA),
Kwa mujibu wa Waziri Ndungulile, dawa bandia na
sizizo na viwango ni tatizo kubwa barani Afrika, linalohitaji mikakati
madhubuti, na kusisitiza kuwa Afrika mikakati haiwezi kufanikiwa bila
ushiriakiano wa wadau wote.
“Dawa bandia na sizizo na viwango zinagharimu pesa
nyingi nchi za Afrika. Kuna watu wanakufa kwa ajili ya dawa hizi, pia kuna watu
walazimika kutumia dawa nyingine za ziada. Zote hizi ni gharama kwa mwananchi
mmoja mmoja na Serikali zetu kwa ujumla,” amesema Waziri Ndungulile.
Kama njia ya kudhibiti
ongezeko la madawa bandia na sisizo na viwango, nchi za Afrika sasa hivi
zinaweka mpango mkakati wa pamoja unaolenga kudhibiti usambaji na matumizi wa
dawa bandia. Ameutaka Mkakati
huo kama AMQF—jukwaa jipya la Africa lengo lake kuu ni kuweka mikakati mipana itakayotatua
matatizo na changamoto zinazotokanazo na madawa yenye ubora hafifu
yanayosambazwa kwa matumizi barani Afrika.
Kuanza kwa Jukwaa la AMQF kunakuja wakati kukiwa na ongezeko kubwa la
matumizi ya madawa bandia na yasiyo na kiwango, yaliyokwisha muda wake katika
sehemu mbalimbali barani Afrika, ikiwemo Tanzania.
Kwa mujibu wa
shirika la afya duniani yaani ‘WHO’ asilimia 42 ya taarifa zinahusu madawa
bandia na madawa yaliyokwisha muda wake, huripotiwa katika nchi za Afrika.
“Kupitia jukwaa
hili matatizo ya ubora ya madawa yatashughulikiwa kikamilifu na hatimae
kukomesha kabisa uzalishaji na usambazaji wa madawa bandia na zisizo na viwango
katika masoko ya Afrika,” amesema Waziri.
Kwa mujibu wa Waziri Tanzania Tanzania ni moja ya
nchini iliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa katika udhibiti wa dawa bandia, jambo
lilosababisha “Mkutano huu ufanyike hapa kwetu ili nchi zingine za Afrika
zipate nafasi ya kujifunza kutoka kwetu.”
Aliongeza kwamba Tanzania imeweza kujitosheleza kwa
dawa za kutosha na zenye viwango vya kimataifa na changamoto kubwa ilikuwa na
kudhibiti dawa zinazoingia kwa njia ya panya ambapo tayari mamlaka husika
(TFDA) imeanza kushughulikia, kwa
kufungua ofisi za kanda zinazolenga kupunguza mianya ya dawa zinazoingia kwa
njia ya panya.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA), Bi Agnes Kijo alisema “Tanzania ina mahabara ya kisasa,
zilizosambaa sehemu mbalimbali nchini…yote haya ni kuhakikisha ubora na viwango
vya dawa zinazosambazwa katika masoko yetu na kutumiwa na watu.”
“Katika mkutano huu jambo kuu litakuwa na kwa namna
ngani tunaweza kudhibiti dawa bandia kwenye masoko na kuhakikisha kwamba
wazalishaji pia wanatoa dawa zenye ubora unaokubalika katika soko,” alisisitiza
Bi Kijo.
Mkuu wa Mipango wa NEPAD, Margareth Ndomondo,
amesema “Mamlaka za uthibiti lazima zitengeneze mifumo ya pamoja ikayosaidia
kudhibiti usambazaji na matumizi katika nchi za Afrika kwa urahisi.”
Mkutano huo imekutanisha
washiriki kutoka nchi 18 za Afrika –ikiwa ni pamoja na Nigeria, Ghana, Ethiopia, Uganda,
Malawi, Zambia, Zimbabwe, Cameron, Ivory Coast, Mali, Burkina Faso, Mauritania,
Senegal, Sierra Leone, Sudan, Guinea, and South Africa pamoja na mawakala
barani Afrika kama vile Wakala wa Afya Afrika Magharibi (WAHO) na wafadhili wa
maendeleo kama vile Shirika la Afya duniani yaani WHO, Shikla la misaada la
Marekani yaani USAID pamoja na Benki ya Dunia.
Post a Comment