Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam,
WITO
umetolewa kwa taasisi za serikali, mamlaka, wafanyabiashara na wadau wengine wa
maendeleo kuwashirikisha watanzania kwenye miradi mikubwa kama moja ya hatua ya
kuwakuza ili kuchochea mapato ya nchini kwa ujumla.
Akizungumza
wakati akifunga kongamano la nne la Ushiriki wa watanzania kwenye uchumi na
uwekezaji (Local Content) ambapo lilihudhuriwa na washirikia takribani 300 hivi
karibuni jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati , Dkt
Dotto Biteko alisema kwamba ushirikishaji wananchi kuingia kwenye miradi
mikubwa kutafungua milango ya ukuaji wao.
“Ushirikishaji
wanachi kuingia katika miradi mikubwa ya kimkakati ya kitaifa ni moja ya hatua
ya kuwakuza watanzania kushiriki katika uchumi wao na taifa kujiepusha na fedha
zake kwenda nje nchi kwa vile kwa muda mrefu miradi mikubwa ilikuwa inatekelezwa
na wageni ambao faida walikuwa wanazipeleka nchini kwao na kukuza uchumi wa
mataifa yao,” alisisitiza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
Aliongeza
pia hii ni hatua muhimu kwa vile taifa letu katika kipindi hiki lipo katika
hatua ya kujenga miradi mbalimbali ya kimkakati ambayo kimsingi lengo lake ni
kuchochea uchumi na kukuza ustawi wa wananchi hivyo kupitia mkakati huo
wananchi hawataachwa nyuma na uchumi utaimarika Zaidi.
Dkt
Biteko alisema kwamba serikali ipo tayari kutoa fursa kwa watanzania kuweza
kushiriki kwenye miradi hiyo na watanzania wajitokeze kuchangamkia fursa hizo
na kwa sasa kuna mradi kama ya Bomba la mafuta kutoka Uganda kupitia Tanga,
mradi mwingine wa bomba la mafuta Uganda kuja hapa nchini na muhimu watanzania
wakapambana kupata kazi hizo.
“Mheshimiwa
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pia alisema kuna upanuzi wa bomba la mafuta la
Tazama , kuna mafuta mengi yanakwenda Zambia tunataka kufanya upanuzi mkubwa na
kupunguza msongamano wa malori yanayoingia Dar es Salaam kuja kuchukua mafuta
na hii miradi yote inataka ushiriki wa watanzania,” alisema Dkt Biteko.
Dkt
Biteko pamoja na mambo mengine katika kuchangamkia hizi fursa aliwaasa taasisi
za serikali na watanzania kuacha kuendekeza vitendo vya rushwa wakati wa kutoa
au utafutaji na mchakato wa kupata tenda hizo za kazi hasa miradi hii ya
kimkakati.
“Tuache
vitendo vya kutoa rushwa ili kupata tenda za kiserikali hii muhimu katika
kudumisha umuhimu wa kuzingatia ushiriki wa watanzania kwenye shughuli za
uwekezaji na biashara, alisisitiza Dkt Biteko kwenye kongamano hilo ambapo
lilihudhuriwa pia na wawekezaji kutoka nje,”
“Madhara
ya kutoa fedha huku na kule ile kupata kazi matokeo yake ukipata kazi husika
unashidwa kuikamilisha kwa sababu ya kutumia fedha nyingi na kukosa faida ,
matokeo namba zinagoma jamani tuache vitendo hivi vya rushwa,” alifafanua Dkt
Biteko
Aliendelea
tuache tabia pia za kusema bado hatujawa tayari kuendelea kujitafuta na hili
jambo ndio linawarudisha nyuma watanzania kama kuamini kazi kubwa za miradi ya
kimkakati hapa nchini.
Kwa
upande wake, Waziri wa Nchini, Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera , Bunge na Uratibu,
Bi Jenista Mhagama alisema kwamba serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu
itaendelea kuhakikisha watanzania wanpata fursa ya kushiriki kwenye uwekezaji
na uchumi wa nchini yao.
“Mheshimiwa
mgeni rasmi kwa upande serikali tutahakikisha kwamba tunakuwa na sera ya
kitaifa ya ushirikia wa watanzania kwenye miradi hii na uchumi kwa ujumla kwa
kutunga sheria na kanuni mbalimbali ili kupanua wigo wa watanzania kwenye
biashara na uwekezaji,” aliongeza Bi Mhagama.
Akizungumza
kwenye kongamano hilo la nne Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi (NEEC), Bi Beng’I Issa alisema kwamba kongamano hilo hufanyika kila
baada ya miaka miwili na hutoa fursa kwa wadau, serikali na wafanyabiashara
kufanya tathimini ya ushiriki wa watanzania kwenye uchumi wao.
“tangu tumeanza na sera na kanuni hizi za
kuwataka wawekezaji kutoka nje wanaoshika miradi mikubwa kutoa fursa kwa
watanzania kushiriki kwenye shughuli zao za kiuchumi na tumepata mafanikio
makubwa sana idadi ya watanzania inaongezeka kila siku,” alisema Bi Issa
Aliongeza
kwamba baraza hilo litaendelea kujenga uwezo wa watanzania kushirki kwenye
miradi hiyo ya kimkakati ili waendelee kupata ajira, kutengeneza bidhaa ambazo
zitapata masoko ya uhakika na kuweza kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja.
Bi
Issa alifafanua kwamba kongamano hilo lilianza rasmi 2017 na lengo la kuwa nayo
kila baada ya miaka miwili ni kuongeza uelewa wa watanzania umuhimu wa
kushiriki kwenye uwekezaji unaofanyika hapa nchini na kuweza kuzitambua fursa
huku serikali ikiendelea kutengeneza mazingira mazuri kw awatu wake kushiriki
kimamilifu.
Naibu
Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Dotto Biteko (Katikati) akimpa tuzo, Bw
Waisile Bairi , Meneja Mahusiano wa AKO Group kwa kutambua mchango wao katika
kutekeleza dhana ya ushiriki wa watanzania kwenye uchumi na uwekezaji (Local
Content) , Kulia kwa Naibu Waziri Mkuu , Mwenyekiti wa Bodi wa (NEEC) Profesa
Aulelia Kamuzora na mwanzo kulia ni Katibu Mtendaji wa (NEEC) Bi Beng’I Issa
Alisema
kwamba baraza limefanikiwa kuunda mwongozo wa (Local content) na kutengeneza
kamati za Taifa katika sekta zote
Aliongeza
kwamba tangu kuanza kwa mfumo wa (Local content ) ajira 162,968 za moja kwa
moja zimepatikana lenye ongezeko la 37.8% na vijana wenye umri kati ya miaka 18
hadi 35 walipata ajira 112,572 ambayo ni sawa na 69.1% ya ajira zote.
Alisema
kwamba ajira za vijana 70% zilikuwa za ujuzi wa chini na 19% zilikuwa na ujuzi
wa kati na 11% zilikuwa za ujuzi wa juu huku kampuni takaribani 3,360 za
kitanzania zimepata fursa katika sekta za uziduaji (madini, mafuta na gesi)
fedha, bima, uwekezaji, nishati, ujenzi, uchukuzi na ununuzi zimepiga hatua
kubwa kwenye local content.
“Juhudi
moja wapo za serikali ni kutungwa kwa sheria na kanuni zinazozingatia masuala
ya ushirki wa watanzania , kwa mfano wakandarasi waliongia ubia ni 64 , haya ni
mafanikio makubwa, “alisema Bi Issa
Alisema
kwamba idadi ya miradi ya ujenzi iliyotekelezwa ni 4,539 yenye thamani ya Tsh
8.5 Trilioni na miradi iliyotekelezwa na wakandarasi wa ndani ilikuwa 4,404
yenye thamani ya Tsh 3.6 Trillioni.
“Kwa
uhakika tumepiga hatua kubwa sana na miradi iliyotekelezwa na wakandarasi wa
kigeni ilikuwa ni 135 yenye thamani ya Tsh 4.9 Trillioni na ushiriki wa
wakandarasi wa ndani ulikuwa ni 97% na thamani ya mradi ni 42.4% na ushiriki wa
wakandarasi wan je ulikuwa ni 3% na thamani ya miradi ilikuwa 57.6%,”
alifafanua Katibu Mtendaji huyo
idadi
ya watanzania kwenye ushiriki wa uwekezaji na biashara hapa nchini umeongezeka
na upatikanaji wa ajira unaleta matumaini na
uwekezaji , masoko na kutengeneza bidhaa
Aliongeza
kwamba kongamano hilo lilihudhuriwa na washiriki takribani 300 kutoka sekta
mbalimbali binafsi , taasisi za umma na wawekezaji wa ndani na nje ya nchini
chini wa uratibu wa Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
Na
katika kongamano hilo baadhi ya makampuni ya ndani na nje yalipata tuzo ya
kutambua mchango wao na kufanikiwa kwa kutekeleza kwa vitendo dhana ya ushiriki
wa watanzania kwenye uwekezaji na uchumi (Local Content)
Post a Comment