Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuutangazia Umma na wadau wote wa Elimu nchini, kuwa mfumo wa Udahili wa pamoja yani Online Central Admission System (CAS), umefunguliwa rasmi tarehe 4 Machi, 2016, saa 6 mchana, kwa kupokea maombi ya mwombaji katika kozi mbalimbali, ikiwemo ngazi ya, Astashahada, Stashahada na Shahada kwa mwaka wa masomo 2016/17. Mfumo utajumuisha kozi zifuatazo;

1. Astashahada na Stashahada
2. Shahada za Elimu ya Juu
Mwombaji wa Astashahada na Stashahada anaweza kuomba kwa ajili ya eneo moja au zaidi katika maeneo ya taaluma yafuatayo;
1. Biashara na Utalii, mfano; Uhasibu, Meneja rasilimali watu, Wanyama pori, Mipango.
2. Sayansi shirikishi, mfano; Kilimo, Uhandisi, Mifumo ya mawasiliano, Usanifu majengo, Mifugo.
3. Afya, mfano; Uganga, Maabara, Ufamasia, Uuguzi
Ada ya maombi ni kama ifuatavyo;
1. Kwa eneo la Afya ada ya maombi ni Tshs 30,000/=.
2. Kwa eneo moja kati ya maeneo mengine yaliyobaki, ada ni Tshs 20,000/=
3. Kwa zaidi ya eneo moja la taaluma, mfano; Afya pamoja na Ualimu, ada ni Tshs 30,000/=, muombaji anaruhusiwa kuchagua maeneo yote.
4. Kwa waombaji wa Shahada za Elimu ya juu, ada ya maombi ni Tshs 50,000/=
Mwisho wa kutuma maombi haya ni tarehe 31/05/2016.
Bonyeza hapa kufanya maombi

Imetolewa na:
Baraza la Taifa la Elimu yaUfundi, 4 Machi, 2016

Source: http://nacte.go.tz/

oopfjopasjop-155636-2563685
Martin Reiter walked into work yesterday one of the poorest men in the building; four hours and a half shift later, he walked out one of the richest.

Never one for stability or long-term employment, Martin Reiter has been shuffling jobs for the past 9 months, working anywhere from his local Walmart chain to his neighborhood McDonald’s in Nevada. Whatever the case, work for him has been strictly a “get in and get out” affair. It wasn’t until his night shift 2 weeks ago that it appeared Martin would be “getting out” forever.

While browsing Facebook on his lunch break, Martin came across an online bingo site giving away $25 in free spins. With nothing to lose and 30 minutes of free time, Martin decided to try his luck. What happened 12 spins and 20 minutes later would change his fate forever.

In one single spin, Martin won the progressive jackpot, cashing out on $362,259 in the matter of 5 seconds. Having won over 20 times his annual salary in a single spin, Martin’s McDonald’s career had come to an abrupt end.

“I just didn’t believe it at first,” Martin said. “I thought it was some sick April Fool’s day joke my coworkers had played on me. It was until I hit the cash out button and saw the the dollar signs next to my name that I knew it was real.”
After some choice words for his boss upon exiting, Martin hasn’t been seen at McDonald’s since.

Dear Alumni/Friends of the University of Dar es Salaam,

On behalf of the University of Dar es Salaam Convocation, I am honoured to invite you to the 7th Convocation Symposium that will take place on 22nd January 2016 in Nkrumah Hall at the University of Dar es Salaam, from 01.30 pm to 06.00 pm. The theme for the symposium is “Reflections on Post-2015 Tanzania Elections: Pitfalls, Lessons and the Way Forward” with three sub-themes namely: “Leadership Challenge and the Constitution”; “Funding, Political Corruption, Sectarianism and Ethnicity in Politics”; and “The Role of the Civil Society and the Media”.
 
The Symposium will bring together over 700 participants including University alumni, academicians, public officials, researchers, politicians, private sector, diplomats, civil society, media, observers of the 2015 Tanzania General Elections and the general public. We will reflect on the post-2015 elections for the best interests of our nation and its future elections.
 
It is my belief that you would wish to use this platform to share views, concerns and vision with the Tanzanian people on this most important subject.  
It is my earnest hope that you will accept this invitation.
 
Please accept the assurances of my highest consideration.
 
Yours sincerely,
 
 
Prof. Rwekaza S. Mukandala
VICE CHANCELLOR


ALIYEKUWA Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova amestaafu rasmi na kuagwa jana huku akikiri kuwa hatasahau joto la uchaguzi mkuu 2015 lililosababishwa zaidi na mchuano wa wafuasi wa wagombea urais John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Edward Lowassa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Akizungumza wakati wa kuagwa kwake na kisha kukabidhi majukumu kwa kamanda mpya wa kanda hiyo, Naibu Kamishna wa Polisi, Simon Sirro, Kova alisema uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 25, 2015 ni miongoni mwa vipindi vitatu asivyotarajia kuvisahau katika maisha yake yote ya kulitumikia jeshi la polisi.

Alivitaja vipindi vingine asivyovisahau wakati akilitumikia jeshi la polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwa ni tukio la kuvamiwa kwa kituo cha polisi Stakishari lililoacha vifo kwa baadhi ya askari wake na pia ajali ya helikopta.

Akieleza zaidi kuhusiana na uchaguzi mkuu, Kova alisema uchaguzi huo ulimpa changamoto kubwa kutokana na wagombea hao kuungwa mkono na watu wengi kiasi cha kuhofia kutokea machafuko, hasa kutokana na kuwapo kwa mwamko mkubwa wa kisiasa miongoni mwa wafuasi wa wagombea.
Hata hivyo, Kova alisema anashukuru kuwa serikali iliwaunga mkono vya kutosha katika kulinda usalama na hivyo kufanikisha uchaguzi huo kwa ufanisi.

“Napenda kuishukuru serikali kwa ushirikiano mkubwa waliotupatia jeshi la polisi wakati wa uchaguzi kwa kutuongezea vifaa vya kazi kama magari ya kufanyia doria, silaha pamoja, kwani vilituwezesha kufanikiwa kulinda amani na utulivu wa hali ya juu,” alisema Kova.

Akisimulia safari yake ndani ya jeshi la polisi kwa ufupi, Kamanda Kova alisema kabla ya kuteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi wa Kandaa Maalumu ya Dar es Salaam, aliwahi kuwa katika idara ya upelelezi kwenye mikoa ya Arusha, Kigoma, Mwanza, Kinondoni (Magomeni) na baadaye kuwa Kamanda wa Polisi katika Mkoa wa Mbeya. 

“Nina utumishi wa miaka 40 ndani ya jeshi la polisi na nilikuja kuwa Mkuu wa Polisi wa Jiji la Dar es Salaam (RPC) nikitokea Mbeya mwaka 2008,” alisema.

MATUKIO 

Akielezea matukio ya ajali ya helikopta na uvamizi Stakishari, Kova alisema hayo hatayasahau kama ilivyokuwa kwa mikikimikiki ya uchaguzi mkuu 2015.

Alisema tukio la Stakishariu lililowapoteza askari wanne hatalisahahu kwani hapo kabla alizoea kukabiliana na vitendo vya ujambazi vinavyohusisha uporaji wa fedha na mali na siyo ugaidi wa kuiba silaha kwenye vituo vya polisi.

Hata hivyo, alisema anafarijika kuona kuwa kwa kushirikiana vya kutosha ndani ya jeshi lao Kanda maaalum ya Dar es Salaam aliyokuwa akiiongoza, walifanikiwa kuwakamata wahusika wote waliofanya tukio hilo. 

Alisema tukio jingine ni kuanguka kwa helikopta wakati wa kutembelea wananchi waliokumbwa na mafuriko mwaka 2014 jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal, aliyekuwa Waziri wa Ujenzi ambaye sasa ni Rais wa Tanzania, John Magufuli na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik.
Simon Sirro
Simon Sirro
AMTAMBULISHA KAMANDA SIRRO 

Kamanda Kova alimtambulisha rasmi Naibu Kamishna wa Polisi Sirro, kuwa mrithi wa wadhifa wake.

Akiongea na waandishi wa habari juu ya hatua hiyo, Kova alisema kwake yeye, kukabidhi madaraka kwa Kamanda Sirro ni kitendo cha kihistoria kwani ilikuwa ni ishara ya kuhitimisha salama utumishi wake ndani ya jeshi hilo. 

“Ni siku ya kihistoria katika maisha yangu kutokana na tendo hili. Lakini naahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa kila namna kwa Kamishna Sirro,” alisema

AKABIDHI VYETI

Katika hatua nyingine, Kova alikabidhi vyeti kwa maofisa 110 wa jeshi la polisi kutokana na utendaji wao katika hafla ya kumuaga.

Alitumia fursa hiyo kufanya ukaguzi wa baadhi ya vitu vilivyokamatwa na jeshi la polisi yakiwamo meno ya tembo, gari mbili, moja likiwa aina ya Toyota Ford liliibwa nchini Afrika Kusini na Toyota Toyota GX210 ambayo yote yalikamatwa eneo la Buguruni Jijini Dar es Salaam.

Kova alimtaka mrithi wake, Kamanda Sirro kufuata nyayo za uongozi wake kwa kuendeleza amani na utulivu katika jiji la dare s Salaam kwa kuhakikisha idadi ya matukio inaendelea kuwa ndogo zaidi.

Kwa upande wake Kamanda Sirro alimsifu Kamanda Kova kwa kazi yake nzuri aliyofanya kwa muda wote alipokuwa wakifanya kazi pamoja na kusema kuwa alikuwa kama mwalimu kwa kila afisa wa jeshi hilo kwa muda mrefu wa utumishi wake.

Alisema kuwa amefanya kazi kama kaimu wake wa kanda hiyo kwa miaka miwili, na kwa muda wote huo kanda hiyo ilikuwa shwari bila kuwepo na wimbi la machafuko.

“Nimefanya naye kazi vizuri kwa miaka isiyozidi miwili na amekuwa mwalimu kwangu na siyo kiongozi tu… ninachoweza kumuahidi ni kuwa nitaendeleza jitihada za kulinda usalama wa raia na mali zao,” alisema.

People watch the New Year firework display on the London skyline in Westminster, London, United Kingdom on January 1, 2015
London is on alert amid fears of an attack between Christmas and New Year

LONDON is on a high terror alert following fears of a jihadi terror attack on New Year’s Eve.
A “friendly” intelligence service warned of a gun or bomb attack being carried out in a crowded area of a major European city between Christmas and New Year.
The news comes as Russian authorities told citizens the “safest” way of seeing in the New Year was to stay at home.

new-years-eve-london-3
'Friendly' intelligence has warned of a gun or bomb attack in a major European city


But Labour MP Keith Vaz has urged Britons not to let the terrorists win this New Year saying: “We should never allow the threat of terrorism to frighten us into changing our normal lives.
“We need to continue with our celebrations.
“Given the current climate, of course we should be extra vigilant and continue to be well protected but if we give into fear then they would have won.”
Source by www.thesun.co.uk



















































IMG_9410
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifurahi jambo na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Dkt. Evaristo Kasanga (kulia) wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya mwishoni mwa juma mkoa wa Lindi.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Na Mwandishi wetu, Mtwara

NAIBU Waziri katika Wizari wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla ameagiza kubadilishwa kwa mifumo ya utawala, malipo  na uendeshaji katika katika hospitali nchini ili kuleta ufanisi na tija.
Akizungumza katika ziara yake ya kujifunza kuona katika hali ya kawaida huwa zinatolewaje katika hospitali za wilaya na mikoa alisema kukosekana kwa mifumo bora ya malipo na motisha kumedumaza utumishi.

Ziara yake hiyo ambayo aliifanya katika hospitali ya mkoa wa Lindi ya Sokoine na Ile ya Mtwara ya Ligula ililenga kuona masuala mbalimbali yanayohusiana na utoaji huduma ili kuwa na nafasi ya kutengeneza hali bora zaidi kimkakati.
Alisema tatizo la upungufu wa dawa na hata raslimali watu linasababishwa na kukosekana kwa mfumo waukusanyaji mapato ulio sahihi na wenye salama ambao utawezesha pia kutoa motisha mbalimbali kwa watumishi ili kuwavutia kufanyakazi katika mikoa ya pembezoni.

Aidha alisema malipo yanayofanyika katika hospitali hizo yanatakiwa kuwa ya kielektroniki kwa kuwa imethibitishwa kila kunapokuwapo na mfumo wa malipo kielektroniki unaboresha mapato na hatimaye kuboresha ufanisi katika uendeshaji wa hospitali pamoja na kuwapo kwa huduma bora za dawa.
Pia ameagiza kuharakishwa kwa mfumo wa malipo kielektroniki kwa wateja wa Bima ili mchango wao usaidie kwa haraka utoaji wa huduma  ndani ya hospitali.

Hata hivyo Naibu Waziri huyo alisema aliridhishwa na utendaji katika hospitali ya Sokoine na Ligula na kusema ufanisi wao unatokana na kuwapo kwa mipango inayowezesha kazi kufanywa.
Alisema hospitali ya Sokoine imeanzisha utaratibu wa mawasiliano ambao unawezesha daktari mahali popote pale kuitwa huku kila mmoja akijua kwamba daktari ameitwa eneo Fulani.

Alitaka hospitali nyingine nchini hasa za rufaa kuangalia mfumo wa mawasiliano ya ndani wa Hospitali ya Sokoine ili kuleta ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Pia alipongeza utendaji wa hospitali ya Ligula na kusema kwamba kutokana na ufanisi wao na huduma nzuri ndio maana hata wananchi wa nchi jirani wanafika katika hospitali hiyo kupata huduma.

Alisema kama kusingelikuwa na huduma bora wananchi hao wasingelivuka kuja kutafuta huduma Ligula.
Hata hivyo Naibu Waziri huyo alitaka kuwapo na utaratibu wa kudhibiti hali hiyo na kusema kwamba ni matumaini yake kuwa wataalamu wataketi pamoja na kutafuta namna ya kufanya katika mazingira hayo ya pia kuhudumia raia wa nchi jirani.
Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa, alisema kwamba pamoja na huduma wanazotoa wanakabiliwa na changamoto kadha hasa wodi ya wanawake na wajawazito.
Alisema kutokana na ongezeko la watu katika mji wa Mtwara kutokana na kuwapo kwa fursa kubwa za uchumi wa gesi na kiwanda cha saruji cha Dangote, wafanyakazi wamekuwa wakifika na familia zao na hivyo kwa sasa wodi hiyo haitoshi.

Hata hivyo alisema hali ingekuwa mbaya zaidi kama kituo cha afya cha Lipombe  kisingesaidiana na hospitali hiyo.
Alisema wodi ya watoto kwa sasa inafanyiwa ukarabati na benki ya Eco na wana mkakati mwingine wa kuomba msaada wa kuondoa ufinyu wa wodi ya wanawake.
Alisema anashukuru Katibu Tawala wa mkoa wa Mtwara, Alfred Luwanda na Mkuu wa mkoa wameshafika katika hospitali hiyo na wameahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba matatizo yake yanatatuliwa na kukidhi hospitali ya rufaa.

Kuhusu upatikanaji wa dawa alisema kwamba hospitali hiyo wa sasa ina akiba ya kutosha baada ya serikali kuipelekea sh milioni 80 na tayari wameshazilipa kwa Bohari ya Dawa (MSD).
Aidha alisema dawa za bima afya zipo na kwamba hawatarajii tatizo kwa kuwa wamekubaliana na mamlaka husika kukitokea upungufu watatumia hata fedha za bima kwa ajili ya kupunguza upungufu wa dawa.
Hata hivyo alisema kwamba wanakabiliwa na uhaba wa madaktari bingwa kwani kwa sasa wana dakatri bingwa wa mifupa na wanawake.

IMG_9338
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipewa maelezo na Kaimu Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Damasiana Msalla alipotembelea wodi ya wazazi na kuridhishwa na huduma za hospitalini hiyo wakati wa ziara ya kushtukiza aliyoifanya mwishoni mwa juma mkoani Lindi.

IMG_9435
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Dkt. Evaristo Kasanga akizungumza jambo na Eleuteri Mangi, Afisa kutoka Idara ya Habari -MAELEZO jijini Dar es Salaam.
IMG_9423
Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi imetwaa kombe la mshindi wa pili kwa utoaji wa huduma bora Tanzania kwa mwaka 2015.

18
Jedwali linaloonesha baadhi ya gharama za matibabu katika huduma zinazotolewa hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi.
IMG_9349
Ujumbe wa watoa huduma kwa wateja wanaofika kupata huduma hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi.
IMG_9572
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiongozana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa (kushoto) pamoja na Daktari wa zamu kitengo cha dharura hospitalini hapo, Dkt. Ester Tumwanga kuelekea wodi za wagonjwa wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya mwishoni mwa juma mkoani humo.

IMG_9525
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye chumba cha dharura katika Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara. Kushoto ni Daktari wa zamu kitengo cha dharura hospitalini hapo, Dkt. Ester Tumwanga.

IMG_9606
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoka kwenye wodi ya wazazi Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya mwishoni mwa juma mkoani humo. Aliefuatana nae ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa.

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.