Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimetakiwa kuhakikisha kwamba wanatumia vyema kijiji cha kidigitali cha Ololosokwan katika kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na uwezo mkubwa katika tiba mtandao. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya wakati akifunga warsha ya siku 2 ya tiba mtandao iliyofanyika chuoni hapo. Warsha hiyo ilikuwa inakokotoa tiba mtandao ili kuwezesha mradi wa majaribio wa Tiba mtandao unaohusisha wadau mbalimbali kutekelezwa. Kitovu cha mradi huo ni kijiji cha Ololosokwan kilichopo Waso wilayani Ngorongoro.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya akizungumza na wataalamu kutoka KCMC, MUHAS wadau kutoka The Africa Foundation, Aga Khan Foundation, Ubalozi wa Uswisi, Bill & Melinda Gates Foundation, XPRIZE pamoja na Maafisa wa afya wa mikoa na wilaya za Arusha na Ngorongoro walioshiriki kwenye warsha ya siku mbili ya tiba mtandao iliyofanyika MUHAS jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Thebeauty.co.tz)

Katibu huyo alisema kutumia kikamilifu kwa kijiji hicho hakumaanishi kuwa na majengo bali kutumia kufunza wataalamu mbalimbali kutokana na ukweli kuwa kijiji hicho sasa kitakuwa mfano wa utendaji katika kusaidia wananchi wa Tanzania. “Uwapo wa kijiji hiki ni tukio kubwa kwetu kwani ni kijiji cha kujifunzia, namna ya kutibu, namna ya kukusanya takwimu namna ya kubaini mahitaji na … ni mfano wa namna gani teknolojia inaweza kufanya mambo makubwa” alisema Ulisubisya . Alisema yeye anaamini kwamba si lazima wataalamu watiba wafundishwe eneo moja, kama ilivyo sasa, lakini wanaweza kufundishwa katika eneo kama Ololosokwan na hivyo kuwajenga pia kisaikolojia kwamba wanaweza kufanyakazi pembezoni bila ya tatizo.


Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kushoto) akichangia jambo wakati wa kuhitimisha warsha ya siku 2 ya tiba mtandao iliyofanyika chuoni hapo. Wa pili kushoto ni mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof Ephata Kaaya (wa pili kulia) na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya (kulia).

Alisema mafanikio ya dhana ya tiba mtandao yatasaidia sana kuboresha hali ya watanzania kwa kuwa mahitaji yao yatajulikana mapema na kutokana na ukweli kuwa mradi wenyewe unahusisha pia ukusanyaji wa data wa uhakika kwa kuzingatia mahudhurio ya watu na magonjwa yao. Pia alisema kwa utekelezaji thabiti utaonesha namna ambavyo Watanzania tuko mbele na kusema kwamba mradi huo wa tiba mtandao anauelewa na ameupigania sana nje ya nchi ambako amekwenda kuzungumza. “Mwaka jana mwezi Desemba nilienda kwenye mkutano Washington unaohusu Tiba mtandao na tumeuza sana hili wazo la tiba mtandao kwa wenzetu, kwa hiyo watakuja kujifunza tunafanyaje” alisema Dk. Ulisubisya na kuongeza kwamba Wizara yake itatoa ushirikiano wa kutosha kuona dhana hiyo inatekelezeka tena kwa ufanisi.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi - Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya (kulia) akitoa maoni wakati wa kufunga warsha ya siku 2 ya tiba mtandao iliyofanyika chuoni hapo.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Zulmira Rodrigues utoaji huo wa tiba mtandao kwa majaribio utaanza mapema zaidi kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu na kutanuka kwa jinsi inavyowezekana kwa kuangalia ufanisi wa kijiji. “Dhana hii itawezesha kuendelea na utoaji wa huduma bora za afya, zenye ufanisi wa kitaalamu zaidi katika maeneo ya vijijini, ambayo mara nyingi huachwa nyuma katika utoaji wa huduma hizo,” alisema Zulmira Tiba mtandao katika kijiji hicho itahusisha upasuaji mdogo ambao utafanywa na watendaji waliopo katika kliniki za kijiji hicho wakielekezwa na mtaalamu bingwa.

Mhadhiri na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Tehama wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi - Muhimbili (MUHAS), Felix Sukums akiwasilisha mapendekezo ya mpango wa utekelezaji wa mradi wa tiba mtandao kwa mgeni rasmi (hayupo pichani), Kushoto ni Meneja Mradi wa Kijiji cha Kidigitali kutoka UNESCO, Tiina Neuvonen.

Aidha akizungumza katika ufungaji wa warsha hiyo Zulmira alitaka kuwapo kwa matumizi ya maabara ya kisasa iliyopo hapo ili iweze kusaidia taifa. Hata hivyo mwakilishi huyo wa UNESCO alisema kwamba Daktari wa wilaya ambako kijiji cha Ololosokwan kipo anahitaji kiasi cha dola elfu 70 kukamilisha baadhi ya mambo ili kuwa na uhakika pamoja na kuleta madaktari wa Afrika mabingwa kuja kufanya kazi kwa muda. Akizungumzia suala hilo, Dk Ulisubisya alisema kwamba anajua shida iliyopo, lakini akamwagiza DMO kukaa na DAS (Katibu Tawala Ngorongoro) kuona namna ya kufanikisha haja ya sasa ya nyumba za makazi kwa gharama nafuu na kusema anaamini wanaofaidika wako tayari kusaidia kidogo. Alisema bajeti hiyo naamini inaweza kupungua kwa kutumia mali ghafi rahisi yenye kudumu zaidi.


Majadiliano yakiendelea katika kuboresha mpango wa utekelezaji wa mradi wa tiba mtandao wa kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati wa kuhitimisha warsha hiyo ya siku 2 iliyofanyika MUHAS.


Pia aliwashukuru UNESCO kwa kuwezesha Ololosokwan kuwa sehemu ya kujifunza na kutanua mradi wa tiba mtandao ambao amesema kwa kuzingatia teknolojia iliyopo sasa Watanzania na dunia kwa ujumla wanapata nafasi ya tiba bila kuwa karibu na bingwa. Katika utekelezaji wa mradi huo hatua ya pili mifumo yote (maunganisho ya kisetelaiti) inatarajiwa kuwa tayari ifikapo Julai na hivyo kuwa na nafasi ya kuanza matibabu ifikapo Oktoba mwaka huu au mapema zaidi. Mradi huo unoanza kwa majaribio unahusisha zaidi wagonjwa wanaoweza kufika kupata matibabu katika kijiji cha kidigitali cha Ololosokwani na kwa kuanzia huduma hiyo itatolewa kwa mama na mtoto na afya ya kinywa, masikio, pua na koo (ENT), ambapo mabingwa kutoka KCMC na MUHAS wanaweza kufanya tiba kwa kutumia mtandao.

Mratibu wa E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia akifafanua jambo kwa mgeni rasmi wakati wa kuhitimisha warsha hiyo.

 Kliniki ya Digitali ilizinduliwa katika kijiji cha Ololosokwan Ngorororo, Arusha mwezi Novemba mwaka 2016. Kijiji hicho tayari kina uwezo wa kupata huduma hizo. Warsha hiyo iliyokutanisha wataalamu mbalimbali wa tehama na madaktari kutoka Arusha , Manyara , Kilimanjaro na Dar es salaam ilichambua dhana ya tiba mtandao na kuidadavua dhana ya utekelezaji kamilifu wa jaribio la utoaji wa huduma za afya kwa kutumia teknolojia ya kisasa, na na namna ya kuirasimisha kama mfumo wa kuboresha afya maeneo yaliyo pembezoni ya miji na vijijini.

Mmoja wa washiriki akiwalisha maoni kwenye warsha ya siku 1 ya kujadili mapendekezo ya mpango wa utekelezaji wa mradi wa tiba mtandao iliyomalizika MUHAS jijini Dar es Salaam.

Picha juu na chini wataalamu kutoka KCMC, MUHAS, UNESCO, wadau kutoka The Africa Foundation, Aga Khan Foundation, Ubalozi wa Uswisi, Bill & Melinda Gates Foundation, XPRIZE pamoja na Maafisa wa afya wa mikoa na wilaya za Arusha na Ngorongoro walioshiriki kwenye warsha ya siku mbili ya kuandaa mpango wa utekelezaji wa mradi wa tiba mtandao iliyofanyika MUHAS jijini Dar es Salaam.




Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akimshukuru mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya mara baada ya kufunga warsha hiyo ya siku 2 iliyofanyika katika kumbi za MUHAS, jijini Dar es Salaam.  

Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller (kushoto) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (katikati) pamoja na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya (kulia) baada ya kuhitimisha warsha ya siku 2 ya mradi wa tiba mtandao iliyofanyika jijini Dar es Salaa., MUHAS.


  Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo.

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya akimpongeza Meneja Mradi wa Kijiji cha Kidigitali kutoka UNESCO, Tiina Neuvonen mara baada ya kufunga warsha ya siku 2 iliyofanyika katika kumbi za MUHAS, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Injinia Enocent Msasi akizungumza katika semina ya wanavyuo iliyoandaliwa na taasisi ya Trust Care Tanzania Foundation.

Msanii Nick Wa Pili akiwasilisha mada leo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE).  

MKURUGENZI Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu alisema semina hiyo ni maalum kwa wanafunzi waliopo vyuoni kwa ajili ya kuwajengea uwezo. Alisema mada zilizotolewa ni pamoja na Umuhimu wa Kujiamini na Kujijengea Uwezo, Uwezo wa Uthubutu, Vipaji na Jinsi ya Kuviendeleza, Maadili na Nidhamu katika Kazi na Ubunifu katika Kufikia Malengo. Kwa upande wa wadhamini wakuu wa semina hiyo Kampuni ya TTCL, Injinia Enocent Msasi Mkurugenzi wa Biashara TTCL alisema kampuni hiyo imeunga mkono kampuni ya Trust Care Tanzania kwa dhumuni lake la kuisaidia jamii katika maeneo mbalimbali, ikiwemo sekta za kiafya, kielimu na kijamii. Aliongeza kuwa lengo hilo linashabihiana na lengo la TTCL kuhakikisha inakuwa na jamii bora zaidi kiteknolojia, kielimu, kiafya na kimaendeleo kwa ujumla. “TTCL imedhamini semina hii kwasababu inatoa mchango mkubwa katika kujenga taifa lenye vijana wachapakazi, vijana wenye mtizamo chanya, vijana wenye uwezo wa uthubutu, na kupambana na changamoto mbalimbali za kimaisha, ” alisema Msasi na kuongeza kuwa TTCL kupitia huduma zake bora za intaneti, sauti na SMS inawaunga mkono vijana mara zote na itakuwa mstari wa mbele kufanikisha juhudi zao za kuleta mabadiliko chanya katika jamii.  

Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu akizungumza kwenye semina ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Injinia Enocent Msasi akizungumza katika semina ya wanavyuo iliyoandaliwa na taasisi ya Trust Care Tanzania Foundation.

Sehemu ya wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam wakishiriki semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE).

Sehemu ya wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam wakishiriki semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE).

Mmoja wa wawasilishaji mada kwa wanafunzi (hawapo pichani) wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE).

Mkurugenzi Mtendaji wa Trust Care Tanzania Foundation, Zambert Mbwafu, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) nje ya ukumbi wa semina hiyo leo.

Sehemu ya wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya jijini Dar es Salaam wakishiriki semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na Trust Care Tanzania Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE).

Umoja wa watanzania Ujerumani UTU e.V watingisha jiji la Essen nchini Ujerumani baada ya kufanya mkutano mkuu kwa mujibu wa katiba  ulioandamana na sherehe za ushindi wa viongozi wapya. Hapo jijini Essen katika ukumbi wa Bob's Cafe, watanzania zaidi ya 75 ambao wanaishi nchini humo walihudhuria mkutano huo ili kutimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wao, katika safu ya uongozi mpya Mhe Mfundo Peter Mfundo alichaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa umoja huo baada ya kukosa mpinzani. Makamo mwenyekiti mpya ni Mhe Salim Malumbo Jr. Katibu mkuu ni Julieth Myn, muweka Hazina ni Bi Nashe Mvungi, Mkaguzi wa mahesabu  namba 1 ni Mhe Bi Jovither Mushashu, Mkaguzi wa mahesabu namba 2 ni mhe Bi. Lilian Sorogo.

Mjumbe namba Moja ni  Mhe Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja na Mjumbe namba 2 ni Mhe Vanessa Lymo. pamoja na mengi yalioongelewa kwenye mkutano huo azma ya  umoja wa watanzania Ujerumani UTU e.V ni kuwaendeleza watanzaniawanaoishi hapa ujerumani na hata kuwaletea maendeleo watanzania wanaoisho Tanzania, umoja ni Nguvu na utengano ni Udhaifu.

 
Bwana Mfundo Peter


Bwana Mfundo Peter, Mwenyekiti wa umoja wa Watanzania waishio Ujerumani


Watanzania waishio Ujerumani wakifurahia keki

Add caption




























Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ameikabidhi bendera timu ya Azania ambayo inaelekea nchini Uingereza kushiriki mashindano ya Standard Chartered Safari kwenda Anfield. Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi bendera pamoja na hati za kusafiria, Waziri Mwakyembe alisema ni fursa ya kipekee ambayo Tanzania imeipata kushiriki mashindano kama hayo na ni muda sasa dunia kujua kuwa Tanzania kuna vipaji vya soka hivyo wahakikishe wanarudi nchini na kikombe. “Mtuwakilishe vyema huko muendako ni muda sasa wa dunia kuwa Tanzania tuna uwezo wa kisoka, kila mmoja acheze vizuri na kuonyesha uwezo wake, tunaamini mtarudi na kikombe na nawatakia kila la kheri,” alisema Waziri Mwakyembe.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi bendera pamoja na hati za kusafiria kwa timu ya Azania ambayo inaelekea nchini Uingereza kushiriki mashindano ya Standard Chartered Safari kwenda Anfield iliyofanyika katika hoteli ya Southern Sun jijini Dar Es Salaam.

Nae Mjumbe wa Bodi ya Standard Chartered Tanzania, Ami Mpungwe amesema benki yao inajivunia kupata wawaklishi kutoka Tanzania na wamesimamia gharama zote za safari kwa muda wote ambao timu itakuwa Uingereza na ni matumaini yao kuwa timu hiyo ya Azania itarejea nchini na kikombe. “Tupo hapa kuiaga timu ya Azania ambao ni mabingwa wa Tanzania na Afrika Mashariki wa kombe la Standard Chartered Safari kwenda Anfield, tunajivunia timu hii sababu imetuletea heshima kubwa, tunawaombe ushindi mkubwa na tunategemea watakuja na ubingwa,” alisema Mpungwe.


Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke akitoa pongezi kwa timu ya Azania kupata nafasi ya kwenda Uingereza wakati wa hafla ya kukabidhi bendera kwa timu hiyo inayokwea pipa kesho 18 Mei. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.

Kwa upande wa Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke aliipongeza timu ya Azania kwa kupata nafasi ya kwenda Uingereza kucheza kwenye moja ya kiwanja maarufu cha Anfield lakini pia kuipongeza benki ya Standard Chartered kwa kufikisha miaka 100 tangu kuanza kutoa huduma nchini. “Hii ndiyo nguvu ya michezo inauwezo wa kuwaunganisha watu pamoja, mnakwenda Uingereza tunaijua ni timu kubwa nawapongeza Azania kwa kupata nafasi, hongereni sana nawatakia kila la kheri najua mtafurahi kwa kipindi ambacho mtakuwa kule, “Mnakwenda kwenye moja ya uwanja maarufu nchini Uingereza, Liverpool ni timu yenye historia na wachezaji wakubwa kama Steven Gerarld, Kenny Dalglish na wengine wengi, pia niwapongeze Standard Chartered kwa kufikisha miaka 100 tangu kuanza kufanya kazi Tanzania,” alisema Cooke.


Mkuu wa idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahman Said akizungumzia safari ya timu ya Azania katika hafla ya kukabidhi bendera kwa timu hiyo inayokwea pipa kesho 18 Mei kuelekea nchini Uingereza.

Nae nahodha wa timu hiyo, Khalid Sultan Said aliahidi kuwa timu hiyo inajiamini kuwa inauwepo wa kupambana na timu zingine na kuahidi kuwa itahakikisha kikombe kinakuja nchini. Timu hiyo itaondoka nchini Mei, 18 watafika Mei, 19 wakiwa huko watakutana na timu zingine, Mei, 20 watatembelea uwanja wa Anfield, Mei, 21 watashuhudia mchezo wa Liverpool na Middlesbrough na baada ya hapo wataingia uwanjani kwa ajili ya mashindano na watarejea nchini Mei, 22.

Mjumbe wa Bodi ya Standard Chartered Tanzania, Ami Mpungwe (kushoto) akizungumzia wakati wa halfa ya kukabidhi bendera timu ya Azania inayotarajia kukwea pipa kesho Mei 18 kuelekea nchini Uingereza. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.

Nahodha wa timu ya Azania, Khalid Sultan Said akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhiwa bendera kuelekea nchini Uingereza kesho Mei 18.


Kikosi cha Timu ya Azania katika hafla ya kukabidhiwa bendera kuelekea nchini Uingereza kesho Mei 18.


Picha juu na chini ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akiabidhi hati za kusafiria kwa wachezaji wa timu ya Azania wanaotarajia kukwea pipa kesho Mei 18 kuelekea nchini Uingereza.Katikati ni Mkuu wa Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba.
 

Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke akikabidhi hati ya kusafiria kwa mwandishi wa TV1 atakayeambatana na msafara wa timu hiyo kuelekea nchini Uingereza.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akikabidhi rasmi bendera kwa Nahodha wa timu ya Azania, Khalid Sultan Said. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mjumbe wa Bodi ya Standard Chartered Tanzania, Ami Mpungwe (suti nyeusi) na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke (kulia). Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi jezi Nahodha wa timu ya Azania, Khalid Sultan Said wakati wa hafla ya kukabidhi bendera timu hiyo. Katikati ni Mjumbe wa Bodi ya Standard Chartered Tanzania, Ami Mpungwe.

Eligibility criteria

Please read all the requirements carefully:
  • These scholarships are to aid students in financial hardship due to the fact that they are from a country that is in crisis as a result of the political situation, war, natural disaster etc.
  • The scholarship is available for students on full time Master's programmes (not MBA) based at the University of Bradford. Students must be self funded.
  • You no longer need to have secured an offer to study at Bradford before you apply for this scholarship. However you must already have completed your undergraduate degree and know your results to be able to apply.
  • You must send proof of your results with your application form. Any evidence sent after your application will not be accepted.
  • Please apply for the scholarship before applying for a place on a course if you will be reliant upon the scholarship to cover your fees and living expenses.
  • You must now already have the required English qualifications to be able to study your chosen course, we will not be able to consider your application unless you meet these requirements. Details of the qualifications we accept can be found on our website.  Please note that we also accept the WAEC qualification at a grade C6 or higher for students from certain African countries.
For further information please see http://www.bradford.ac.uk/fees-and-financial-support/university-scholarships-and-support/info/global-development-scholarship-2017-18

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker akizungumza.


Ni ongezeko la asilimia 2.4 la faida • 

Kwa miaka 10 mfululizo, NMB imeendelea kuongoza kwa faida nchini.

BENKI ya NMB imepata ongezeko la faida la asilimia 2.4 baada ya kodi kwa mwaka 2016. Mkurugenzi Mkuu wa benki ya NMB - Ineke Bussemaker amesema kwamba licha ya changamoto zilizoikabili sekta ya fedha na uchumi kwa ujumla kwa mwaka 2016, benki ya NMB iliweza kufanya vizuri. “Faida ya benki kwa ujumla iliongezeka kutoka shilling billioni 150.3 kwa mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 153.7 kwa mwaka 2016. Ongezeko hili limetokana na kuongezeka kwa pato linalotokana na Biashara ya benki lililokuwa kwa asilimia 16,” alisema Bussemaker. Riba katika mikopo ilikua kutoka shilingi bilioni 438.7 kwa mwaka 2015 hadi billioni 551.0 mwaka 2016 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 25.6. 

Pia Rasilimali za benki ziliongezeka kwa asilimia 8 kutoka shilingi bilioni 4,580 kwa mwaka 2015 hadi shilingi Bilioni 4,951 mwaka 2016. Mikopo kwa wateja iliongezeka hadi shilingi 2,794 billioni, ikiwa ni ongezeko la asilimia 13% kutoka shilingi bilioni 2,482 kwa mwaka uliotangulia. 

Ongezeko hili la mikopo ilitokana kwa kiasi kikubwa na ongezeko la mikopo kwa wafanyakazi kwa asilimia 16 kwa mwaka 2015 hadi kufikia shillingi bilioni 1,698 kwa mwaka 2016. Pamoja na ukata wa fedha uliozikumba benki nyingi mwaka 2016, ongezeko la amana za benki lilichangiwa kwa kiasi kikubwa na ongezeko la amana za wateja kwa shilingi bilioni 172 billioni, fedha ambayo benki ilikopa kiasi cha shilingi bilioni 312 pamoja na hati fungani ambayo ilipatikana kiasi cha shilingi bilioni 41. 

Gharama za riba ziliongezeka kwa asilimia 49 kutoka shilingi bilioni 68.5 kwa mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 102.2 kwa mwaka 2016. “Amana za wateja ambazo kwa kiasi kikubwa ziliwekwa katika akaunti zisizokuwa na riba ziliongezeka kwa asilimia 4.8% kutoka shilingi bilioni 3, 568 kwa mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 3,737 kwa mwaka 2016,” alisema. 

Aliongeza, “Idadi ya wateja wetu iliathiriwa sana na hali ya kibiashara kwa mwaka 2016, hali ambayo iliathiri ubora wa mikopo na kuchangia ongezeko la mikopo mibovu (NPL) hadi asilimia 4.8 kwa mwaka 2016 kutoka asilimia 2.4 mwaka 2015,” Ikishikilia asilimia 20% ya soko kwa mikopo na amana za wateja, benki ya NMB ni ambayo ni ya pili kwa ukubwa wa mizania ya Rasilimali za kibenki nchini, kwa miaka 10 mfulululizo benki imekuwa ikiongoza kwa kupata faida kubwa kuliko benki zote nchini. 


Projects from 17 countries – including Poland, Croatia, Azerbaijan, Canada, the US, Italy, Germany, the UAE, Iran, Australia, China, Spain, Poland and Turkey – were celebrated and rewarded at the fortieth Lighting Design Awards in London last night. The winners were announced at a glamorous black-tie event at the London Hilton Park Lane attended by over 700 designers, architects and suppliers and hosted by Tom Allen.

The lighting designer of the year for 2016 was named as Gerd Pfarré, whom the judging panel described as ‘a designer of stellar talent and boundless creativity’.
The lighting design practice of the year is Arup, who has had ‘an astonishing run of fantastic projects’. The architect of the year is Diller Scofidio + Renfro. The judges said: ‘Few firms handle daylight as sensitively and as passionately as this one’.

Other winners included the US light artist Christine Sciulli for the Roil artwork in New York, David Atkinson for the UAE Pavilion at the Expo 2015 and the Society of Light & Lighting for the Night of Heritage Light.
The full list of winners are: follow the link below


Winners announced at the 40th Lighting Design Awards 2016

Mrembo wa Tanzania mwenye tamaa ya kuwa na himaya ya samani za kimataifa kupitia kampuni yake, kama alivyowahi kuelezwa na jarida la Forbes hivi karibuni, Jacqueline Ntuyabaliwe ametwaa tuzo mbili za ubunifu kupitia kampuni ya Molocaho by Amorette. Ushindi wake huo unamuingiza katika kundi la watu wenye ubunifu mkubwa wa bidhaa za majumbani na katika maofisi, muda mfupi tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo. Molocaho by Amorette kampuni ya kubuni na kutengeneza samani ilizinduliwa Septemba 2016. Miezi michache tu tangu kuundwa kwake inaonesha kukimbia na kufanikisha tuzo tatu za kimataifa. Katika tuzo zenye ushindani mkali na heshima kubwa kwenye ubunifu za kimataifa zijulikanzo kama A-Prime Design (A'Design) zilizofanyika mjini Roma mwishoni mwa wiki Jacqueline amepata tuzo katika kategori mbalimbali na kuwa wa pili kategori nyingine. 

Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi.

Bidhaa zilizompatia tuzo ni samani na pia za mwanga. Ngorongoro Settee ilimpatia medali ya shaba kwa upande wa samani na katika bidhaa za mwanga Sayari Lamp pia ilimpatia tuzo ya shaba. Nafasi ya pili ilipatikana katika kiti cha Flamingo. Taarifa zilizofikia thebeauty zinasema kategori ya Furniture, Decorative Items and Homeware Design Category ya mwaka 2016 na kiti cha Ngorongoro na kategori ya Lighting Products and Lighting Projects Design Category ya mwaka 2016 ilikuwa na Sayari lamp. Na Kiti cha Flamingo kilimpatia nafasi ya pili katika kategori ya Furniture, Decorative Items and Homeware Design Category ya mwaka 2016.


Muonekano wa kiti cha Ngorongoro Settee uliompatia tuzo Jacqueline Mengi kupitia kampuni yake ya Molocaho by Amorette.[/caption] A-Prime Design Shindano aliloshiriki Jacqueline Mengi akiwa na kampuni yake ya Molocaho by Amorette la A’Design hushirikisha wabunifu, wagunduzi na makampuni yanayotengeneza bidhaa mbalimbali za ubunifu wa ndani. Shindano la A' Design limeanzishwa kwa lengo la kuhakikisha kwamba wabunifu wanakuja na bidhaa bora kabisa zenye ushindani mkali katika soko la kimataifa. Kwa kawaida tuzo zake hutolewa katika kusanyiko kubwa la wabunifu linalofanyika Roma, Italia kwa kuratibiwa na OMC Design Studios SRL . Jacqueline, Miss Tanzania (2000) hivi karibuni alishiriki tuzo za rais za CTI na ana mafunzo ya Interior Design kutoka Rhodec International. Kampuni ya Molocaho by Amorette, kampuni ya Tanzania inajishughulisha na utengenezaji wa samani bora kwa namna mteja anavyohitaji, nyuzi, taa, urembaji, samani za nje na kwenye bustani.


Sayari Lamp iliyompatia tuzo katika kategori ya Lighting Products and Lighting Projects Design Category ya mwaka 2016.


Molocaho inatengeneza samani zenye mahadhi ya kiafrika ikichanganya utamaduni wa Tanzania katika mazingira ya kisasa na kumalizia na ubunifu wa kimataifa. Molocaho, moja ya makampuni ya Afrika Mashariki ya samani yanayokua kwa kasi, imejipatia nafasi kubwa ya heshima kwa kuhakikisha kwamba inatumia mali ghafi na mbao njema pekee za Tanzania kutengeneza samani zenye kwenda kimataifa. Katika mahojiano na jarida maarufu la Forbes alishawahi kusema kwamba anawania soko la kimataifa kutokana na ukweli kuwa bidhaa anazotengeneza zimejipambanua kwa wateja.


Muonekano wa kiti cha Flamingo kilimpatia nafasi ya pili katika kategori ya Furniture, Decorative Items and Homeware Design Category ya mwaka 2016.[/caption] Jacqueline Ntuyabaliwe, pamoja na kuwa na ratiba yenye changamoto sana (Yeye ni balozi wa WildAid na yumo ndani ya bodi kadhaa; mama wa watoto pacha wavulana; mke kwa mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa na akiendesha taasisi ya hisani ya elimu), huhakikisha anakagua kila samani inayozalishwa kiwandani kwake kabla ya kuuzwa au kusafirishwa. Mume wake, Reginald Mengi, ni tajiri mwenye mafanikio makubwa nchini Tanzania ambaye ameujenga utajiri wake kwa kufanya karibu kila kitu kuanzia uzalishaji wa kinywaji cha Coca-Cola hadi uchimbaji wa madini na kumiliki vituo vya televisheni na magazeti. Kwa tuzo hizo Amorette, inajidhihirisha kuwa chata yenye mafanikio makubwa nchini Tanzania na huku ikipanda kwa kasi kimataifa.


WATANZANIA wametakiwa kuingia katika ubia kama wajasiriamali badala ya kufikiria kwamba wao ni maskini na hawana fedha za kuingia ubia na makampuni ya nje. kauli hiyo imetolewa katika wiki ya Ufaransa ambapo makampuni 50 yanashiriki kuonesha uwezo wa utayari wa ushiriki wao katika ujenzi wa uchumi wa kati wa Tanzania unaotegemea viwanda. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi ambaye aliwasilisha haja na matamanio ya Watanzania kwenye sekta binafsi katika kushirikiana na wawekezaji kutoka Ufaransa, alisema watanzania wamekuwa waoga kuomba ubia wakidhani kwamba hawana kitu cha kutoa wakati wao wana akili na rasilimali.
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi akizungumza katika kilele cha wiki ya Ufaransa ambapo wawekezaji kutoka makampuni 50 ya Ufaransa walishiriki katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliombatana na maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wafaransa. (Picha zote Thebeauty.co.tz)

Kauli hiyo ambayo aliisema kwenye mazungumzo na wawekezaji hao wa Ufaransa wakati akielezea utayari wa sekta binafsi kushirikiana na Wafaransa alisema kwamba watanzania wengi hawajiamini na kwamba wakati umefika kwa Watanzania kujitambua kwa kuwa wao (wafaransa) walijaribu wakaweza kwani kama sisi walikuwa na vitu vya ziada katika uthubutu wao. Katika mazungumzo yake Dk. Mengi akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye alisema kwamba sekta binafsi ambayo ina mchango mkubwa katika uchumi wa nchi inawezekana kwa watanzania kuthubutu. Aidha alisema uwapo wa Wafaransa utaweza kusaidia kupandisha uwezo, teknolojia na utaalamu hali ambayo inawezekana kupitia uwapo wa shughuli za ubia kati ya wawekezaji wa Kitanzania na Wafaransa. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye (kulia) akizungumza wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika mkutano huo wa kilele cha wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.


Alisema baada ya sekta ya umma kuweka miundombinu mahala pake, ni kazi ya sekta binafsi kutumia miundombinu hiyo kubuni na kuwekeza katika viwanda na kuzalisha bidhaa mbalimbali. Dk.Mengi alisema kwamba TPSF inaamini kwamba sekta binafsi ni ufunguo katika kuongoza na kuimarisha uchumi wa Tanzania ambao unatakiwa kuwa endelevu kama awamu ya tano inavyotaka. Aliwaambia wafanyabiashara wa Ufaransa kwamba Tanzania ina kila kitu wanachohitaji na kwamba makampuni makubwa ya Ufaransa kama Airbus, Renault, Alstrom, Systra wana mtandao mpana duniani wa kufanyabiashara na wawawekezaji wadogo duniani hivyo wanaweza kufanya hivyo hapa nchini.
  Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira akiuliza swali kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa kilele cha wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.

Alisema changamoto za utaalamu zitaondoka kwa ushirikiano na uwezeshaji. Aliwataka wawekezaji hao wa Kifaransa kwamba Tanzania kwa sasa ndio nchi ya uwekezaji na kusema changamoto zilizopo ni fursa za uwekezaji nchini Tanzania hasa katika nishati ambapo taifa hili litahitaji megawati 10,000 ifikapo mwaka 2040. Aidha alisema anaamini kwamba wengi wa watanzania wapo tayari kushirikiana na Ufaransa katika kuhakikisha kwamba wanaingia ubia katika biashara halali na yenye kusaidia pande zote. Naye Simbeye alisema anatamani kuona kwamba wafaransa wanawekeza kiwanda cha magari nchini kwani inawezekana kutokana na mabadiliko makubwa ya mfumo wa uwekezaji kwa sasa

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo katika mkutano huo kwenye kilele cha wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.

  Mmoja kati ya wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa akiuliza swali kwa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) katika kilele cha mkutano wa wiki ya Ufaransa unaolenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.

  Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi, Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira katika mkutano wa kilele cha wiki ya Ufaransa uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya Taifa.

  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, anayeshughulikia Biashara na uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (wa pili kulia) pamoja na baadhi ya viongozi wa wizara walioshiriki mkutano huo wa kilele cha wiki ya Ufaransa iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
  Ofisa wa ubalozi anayeshughulikia masuala ya biashara katika Ubalozi wa Ufaransa nchini, Blevin Claude (wa pili kushoto) akiwa na Ofisa anayeshughulikia masuala ya Uchumi katika Ubalozi wa Ufaransa nchini, Beatrice ALPERTE (kushoto) katika mkutano huo.

  Pichani juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaochukua masomo ya biashara walioshiriki mkutano wa kilele cha wiki ya Ufaransa uliofanyika katika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya wadau na wafanyabiashara kutoka makampuni 50 ya nchini Ufaransa walioshiriki mkutano huo.
  Mkutano ukiendelea.
  Sales Executive wa kampuni ya CMC Formula wauzaji wa magari ya Renault, Erica George akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi wakati akitembelea mabanda katika maadhimisho ya wiki ya Ufaransa iliyofanyika kwa mara ya kwanza nchini katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi akipata maelezo katika banda la kampuni ya TOTAL.
  Meneja Mauzo wa Kampuni ya AIRBUS HELICOPTERS, Jean-Marc Royer (kulia), akitoa maelezo ya shughulli wanazofanya kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi (wa pili kushoto) alipotembelea mabanda ya kampuni mbalimbali kutoka nchini Ufarasan zilizoshiriki kwenye maadhimisho ya wiki ya Ufaransa yaliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam Kushoto ni Ofisa wa ubalozi anayeshughulikia masuala ya biashara Ubalozi wa Ufaransa, Blevin Claude.
  Ofisa wa ubalozi anayeshughulikia masuala ya biashara Ubalozi wa Ufaransa, Blevin Claude akitoa neno la shukrani kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TSPF) Dk. Reginald Mengi wakati Dk. Mengi akijiandaa kuondoka katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa yalipofanyika maadhimisho ya wiki ya Ufaransa jijini Dar es Salaam.

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.