Umoja wa watanzania Ujerumani UTU e.V watingisha jiji la Essen nchini
Ujerumani baada ya kufanya mkutano mkuu kwa mujibu wa katiba
ulioandamana na sherehe za ushindi wa viongozi wapya. Hapo jijini Essen
katika ukumbi wa Bob's Cafe, watanzania zaidi ya 75 ambao wanaishi
nchini humo walihudhuria mkutano huo ili kutimiza haki yao ya msingi ya
kuchagua viongozi wao, katika safu ya uongozi mpya Mhe Mfundo Peter
Mfundo alichaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa umoja huo baada ya kukosa
mpinzani. Makamo mwenyekiti mpya ni Mhe Salim Malumbo Jr. Katibu mkuu ni
Julieth Myn, muweka Hazina ni Bi Nashe Mvungi, Mkaguzi wa mahesabu
namba 1 ni Mhe Bi Jovither Mushashu, Mkaguzi wa mahesabu namba 2 ni mhe
Bi. Lilian Sorogo.
Mjumbe namba Moja ni Mhe Ebrahim Makunja aka Kamanda
Ras Makunja na Mjumbe namba 2 ni Mhe Vanessa Lymo. pamoja na mengi
yalioongelewa kwenye mkutano huo azma ya umoja wa watanzania Ujerumani
UTU e.V ni kuwaendeleza watanzaniawanaoishi hapa ujerumani na hata
kuwaletea maendeleo watanzania wanaoisho Tanzania, umoja ni Nguvu na
utengano ni Udhaifu.
|
Bwana Mfundo Peter |
|
Bwana Mfundo Peter, Mwenyekiti wa umoja wa Watanzania waishio Ujerumani |
|
Watanzania waishio Ujerumani wakifurahia keki |
|
Add caption |
Post a Comment