Umoja wa Mataifa nchini umeendelea na hekaheka za ufundishaji wa machampioni wa kusaidia kueneza malengo 17 ya dunia yanayohusu maendeleo endelevu.
Miongoni mwa mambo yaliyofanywa siku ya pili ya ziara ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kwa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha ni kuendelea kwa mkutano wa vijana unaoakisi Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini Arusha , na kuoongoza kampeni ya elimu ya maendeleo endelevu katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU).
Akiwa MoCU Rodriguez aliwataka vijana kujikita katika kuyaelewa malengo ya dunia na kuyafanyia kazi.
Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa akiitambulisha meza kuu kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) wakati wa kutoa uelewa juu ya malengo ya dunia chuoni hapo.
Akifafanua mchango wa vijana katika kufanikisha malengo hayo, Matibu huyo alisema: “Mchango wa vijana ni muhimu katika kufanikisha malengo endelevu kufika mwaka 2030; hivyo ni vyema kila kijana akafahamu na kuwafundisha vijana wenzie malengo hayo muhimu.”
Septemba 2015, wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa walikubaliana juu ya malengo mapya ya dunia, malengo ya maendeleo endelevu.
Malengo hayo yanatarajiwa kufanyiwa kazi katika kipindi cha miaka 15 ijayo na kuleta mabadiliko makubwa katika jamii, uchumi na mazingira kwa namna ya kuwa endelevu.
Wakati Umoja wa Mataifa (UN) mwaka jana ukiadhimisha miaka 71 tangu kuanzishwa kwake, Mratibu huyo wa mashirika ya Umoja wa Mataifa aliahidi kuwatumia vijana katika utekelezaji wa malengo yake 17 ya maendeleo kutokana na idadi yao kubwa kubwa zaidi ya asilimia 67 na pia kwa kuwa wao ndio wanaobeba hali ya baadaye ya nchi hii.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza juu ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) walioshiriki semina ya uelewa wa malengo hayo 17 ya dunia iliyofanyika chuoni hapo.
Aidha alisema ili kufanikisha hilo, UN pamoja na mashirika mengine itatoa mafunzo ya vitendo kwa vijana zaidi ya 50,000 ifikapo mwaka 2017 ambao wataingizwa katika mpango wa utekelezaji wa malengo hayo.
"UN itaendelea kushirikiana na vijana pia itatoa elimu ya vitendo.Hadi sasa vijana zaidi ya elfu 20,000 wamepewa mafunzo na wanatambua malengo hayo, na kwamba
UN na wadau wengine wanatarajia kufundisha vijana zaidi ya 50, 000 ifikapo mwaka 2017, ili ifikapo 2030 vijana wengi wawe wanajua malengo hayo na namna ya kuyatekeleza," alisema.
Ofisa wa dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ngusekela Karen Nyerere akitoa neno kwa wanafunzi wa MoCU wakati wa semina ya uelewa wa Malengo ya Dunia iliyofanyika chuoni hapo.
Amesema miongoni mwa mafunzo yatakayotolewa kwa vijana hao ni pamoja na jinsi ya kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu na jinsi ya vijana watakavyoweza kujiajiri.
Akiwa Moshi jana, alizungumza na wanachuo na wahadhiri ambapo katika chuo hicho cha MoCU 460 walipatiwa mafunzo na pia walimhoji mambo mbalimbali yanayohusu Umoja wa Mataifa na malengo ya dunia ya maendeleo endelevu.
Kwa mafunzo yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha Umoja wa Mataifa ulifua vijana 50 ambao ni machampioni.
Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akisisitiza jambo kwa wanafunzi wa MoCU wakati wa semina ya uelewa wa malengo ya dunia iliyofanyika chuoni hapo.
Aidha idadi ya vijana waliofikiwa na mafunzo hayo kwa kuambukizana wameongezeka na kufikia zaidi ya elfu 20.
Tangu kuzinduliwa kwa kampeni hiyo na mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez, mwaka jana vijana zaidi wamepata elimu katika maeneo yao kwa kupitia machampioni wa malengo.
Kwa sasa Tanzania imehusisha malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) kwenye mpango wa maendeleo wa miaka mitano.
Picha juu na chini ni wanafunzi na walimu MoCU walioshiriki semina ya uelewa wa malengo ya dunia iliyoendeshwa na Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini chuoni hapo.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akibadilishana mawazo na Eng. Salvatory Matemu kutoka Ofisi ya RC Kilimanjaro huku Ofisa wa dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ngusekela Karen Nyerere (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Rasilimali watu MoCU, Daud Massambu wakielekea kwenye zoezi la picha ya pamoja.
Picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa MoCU.
Picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa MoCU.
Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa UN Chapter MoCU, Isaac Evarist (kushoto) pamoja na wanafunzi chuoni hicho.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwapiga msasa machapioni wa malengo ya dunia katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha.
Mmoja wa machampioni akipitia kipeperushi kinachoelezea kwa kina malengo 17 ya dunia wakati wa mafunzo yaliyoendeshwa na Mratibu Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (hayupo pichani).
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akisikiliza swali kwa umakini kutoka kwa Waziri wa Habari wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha, John Semindu wakati wa mafunzo kwa machampioni wa SDGs chuoni hapo.
Mmoja wa machampioni wa Makumira akiuliza swali kwa Mratibu wa Mashirika ya UN nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).
Picha juu na chini ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akikabidhi vyeti kwa machampioni wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha na Taasisi ya Uhasibu ya Arusha (Institute of Accountancy Arusha -IAA) walioshiriki mafunzo hayo.
Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa akimuelekeza jambo mmoja wa machampioni wa malengo ya dunia wakati wa mafunzo yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na baadhi ya machampioni wa malengo ya dunia chuoni hapo.
Post a Comment