Nafasi Za Mafunzo Ya Ujasiriamali
RafikiElimu Foundation

Date Listed: Oct 7, 2012
Email Address: Click to Email
Phone: +255 763 976 548
Area: Dar Es Salaam
Application Deadline: Oct 25, 2012
Start Date: Nov 01, 2012


Position Description:
RafikiElimu    FOUNDATION  ni  Taasisi  Isiyokuwa  ya  Kiserikali  ( NGO  )   inayo  jihusisha  na  maendeleo  ya  jamiitAASISI  kupitia  mradi  wake  " Elimu  Ya  Ujasiriamali  Mijini  &  Vijijini "  ( EUMIVI- Project )  inapenda  kuwatangazia  wakaazi  wote  wa    jijini  Dar  Es  salaam,  nafasi   za    mafunzo  ya  ujasiriamaliMafunzo  yatakayo  tolewa   ni  pamoja  na  :

1. Utengenezaji  na  uzalishaji  wa  bidhaa  mbalimbali  kama  vile    Sabuni  Za  Aina  ZoteBatiki, Chaki, Mishumaa, Batiki  na  Usindikaji,
2.  Elimu  ya  ujasiriamali
3.  Sheria  za  biashara,
4.  Usimamizi  na  uongozi  wa  biashara
5.  Usimamizi  wa  miradi,,
 6.  uwekaji  na  ukopaji     nakadhalika.

Washiriki  wa  mafunzo  watawekwa  katika  vikundi  vya   maendeleo   ya  jamii  vya  watu  20  kila  kikundi   na  wataunganishwa  katika  Mtandao  Wa  Vikundi  Vya  Maendeleo  Ya  Jamii  Tanzania, ambao  upo  chini  ya  asasi  ya  RafikiElimu  Foundation.

Mafunzo  yataanza  kutolewa  tarehe  01  Novemba  2012.

Tarehe  Ya  Kuanza  Kujiandikisha  ni  tarehe   08  OKTOBA  2012.

Mwisho  wa  kujiandikisha  katika  mafunzo  haya  ni  tarehe   25  OKTOBA  2012.

ADA  YA  KUJIANDIKISHA  :  Ada  ya  Kujiandikisha  katika  mradi  huu  ni  Shilingi   ELFU  TANO  tu ( Tshs. 5,000/=za  Tanzania.

Ili  Kujiandikishafika  katika  ofisi  zetu  zilizopo katika  eneo  la  CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU.

MAHALI  ZILIPO  OFISI  ZETU  :

Kufika  katika  ofisi  zetu,  panda   gari  za   UBUNGO- CHANGANYIKENI,  kisha   Shuka  kituo  kinaitwa   TAKWIMU.  Ukifika  kituo  cha  TAKWIMU  tembea   hatua  Ishirini   kufuata  barabara  ya  lami  halafu  upande  wako  wa  kulia  utaona  bango  limeandikwa  RafikiElimu  FOUNDATION.

Kwa  maelezo  zaidi,  wasiliana  nasi  kwa  SIMU  : 0763976548     AU     0782405936.


EWE  KIJANA  WA  KITANZANIA,  TUMIA  FURSA  HII  KUPATA  UJUZI, UWEZO  NA  MAARIFA  YATAKAYO  KUWEZESHA  KUTENGENEZA  FURSA  ZA  KUJIAJIRI  MWENYEWE.


Application Instructions:
Kwa  maelezo  zaidi, tembelea website yetu

Website: Go to Website
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.