Na Damas Makangale, Dar es Salaam, Tanzania
Zaidi ya wanafunzi  1,000 kutoka Kusini mwa jangwa la Sahara wamepata udhamini wa kwenda kusoma shahada zao za kwanza katika nchini za China, Marekani, Canada, Uingereza, India, Australia, Afrika ya Kusini, Sweden, Denmark na Norway.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Universities Abroad Link (UAL), ambacho ni shirika la kuratibu wanafunzi wa kiafrika wanaotaka kwenda kusoma nje ya nchi, Bw Tony Rodgers Kabetha amesema kwamba shirika hilo linaratibu wanafunzi kutoka nchi za Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Msumbiji, Botswana na Afrika ya kusini ambao wana nia ya kwenda kusoma nje ya nchi.
 

Mkurugenzi na Mwanzilishiwa Universities Abroad Link (UAL) Bw.Tony Rodgers Kabetha (kulia) akiwaaga baadhi ya wanafunzi waliopata udhamini wa kwenda kusoma nje ya nchi.
 "Kwa dhati kabisa tuliamua kuanza kusaidia wanafunzi kutoka kusini mwa jangwa la sahara na Afrika kwa ujumla kuhusu taarifa za sahihi za vyuo bora kabisa duniani na kozi wanazotoa ambazo zitakuwa na manufaa kwa wanafunzi hao baada ya kuhitimu masomo yao,” alibainisha.
Aliendelea kusema kwamba wanafunzi kutoka nchi hizo za Afrika wanaweza kuomba na kupata udhamini kutoka kwenye vyuo vikuu bora kabisa kutoka nchi za Marekani, Uingereza, Canada, China, India, Australia, Sweden, Afrika Kusini, Denmark na Norway na ada ya masomo inaweza kuwa chini zaidi kulingana na ada za hapa nyumbani.
Kabetha, ambaye kitaaluma ni Injinia wa mawasiliano ambaye amegeuka na kuwa mdau wa elimu ya juu alisema kwamba wazo la kuja na shirika lilianza miaka tisa iliyopita baada ya wanafunzi na baadhi ya waaafrika waliokuwa wakiishi na kufanya kazi marekani kuamua kuanza kuwasaidia watanzania namna bora ya kupata vyuo vya kusoma nje ya nchini.
"Tumeamua kuja na shirika hili la elimu ya juu ili kuwapa Watanzania na wa afrika kwa ujumla taarifa sahihi kuhusu vyuo vikuu na kozi sahihi ambayo inaambatana na mahitaji ya soko la ajira," aliongeza.

Alibainisha kuwa UAL pia hutoa ushauri wa kitaaluma na wa kazi kwa wanafunzi ili kuhakikisha kwamba hawasomi shahada ambazo watajikuta mwisho wa siku hawana ajira ndani ya Tanzania na hata kama wakienda nje ya Tanzania pia watakosa ajira.
"Unataka  kujifunza nini? Wapi unataka kwenda kujifunza? Na Kwa nini ni uchukue kozi hii ni maswala ambayo tunapenda kuuliza wanafunzi katika juhudi za kuwasaidia lakini pia tunawapa taarifa za hali ya hewa za nchi husika wanapokwenda,” alisisitiza.
Kabla ya kuanzishwa kwa shirika hilo wanafunzi na wazazi walikuwa wakipewa taarifa za uongo kuhusu vyuo vingi katika nchi ziilizoendelea na kutoa fedha nyingi ambazo zilikuwa hazina manufaa yoyote kwao.
Kabetha ilisisitiza kwamba changamoto kubwa kwa Watanzania walio wengi ni kuchagua kusoma fani ambazo hazina soko na uwezekano wa kupata kazi ni mdogo na kutokana ukweli huu tunawaelimisha wanafunzi umuhimu wa kuchagua kozi zenye manufaa kwenye maisha yao.
Alisema kuwa soko la ajira kwa sasa limepanuka zaidi kwenye fani ambazo ni chache sana watu kwenda kuomba kusoma kama vile mambo ya mafuta, gesi, teknolojia, uchumi wa biashara.
"Changamoto nyingine kubwa kwa shirika na tofauti ya mihura kwa nchi za ulaya, asia na Amerika na hapa nyumbani nchini Tanzania ambao wakati wa kupokea maombi ya kujiunga na vyuo huku nyumbani wanakuwa wamefunga au wamemaliza lakini hawana vyeti lakini bado tunazungumza na serikali jinsi ya kurekebisha haya,”  alifafanua.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.