Articles by "Local News"

Showing posts with label Local News. Show all posts



Wakulima wadogo nchini Tanzania hivi karibuni wataweza kupata taarifa mbalimbali za kijiditali kuhusu masuala ya pembejeo, ukiwemo ushauri utakaosaidia kutatua matatizo yanayowakabili kama vile upatikanaji wa fedha, pembejeo na mafunzo. Mradi huo umezinduliwa na taasisi tatu za Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA), Positive International Limited (PIL), na Grameen Foundation katika sherehe zilizohudhuriwa na maofisa wa serikali, wawakilishi wa vyama vya wakulima, taasisi za fedha, kampuni za mbegu, wafanyabiashara wa nyenzo za kilimo na wale wanaojishughulisha na biashara za mazao ya sekta ya kilimo. 

Kifaa hicho cha dijitali kitawawezesha wakulima kulipia mapema pembejeo wanazohitaji kupitia simu za mkononi kwa bei nafuu. Pia kifaa hicho kitawapa wakulima pembejeo kulingana na mazao na malengo yao ya uzalishaji na pia kupata taarifa za ushauri kuhusu matumizi bora ya pembejeo hizo. “Moja ya changamoto kubwa zinazowakabili wakulima ni kwamba hukosa fedha mwanzoni mwa msimu wa upandaji mazao, jambo ambalo huwalazimisha kutafuta fedha hizo kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo na hivyo kuwaongezea mzigo,” alisema Hedwig Siewertsen, kiongozi anayeshughulikia masuala ya fedha wa shirika la Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA). “Kifaa hicho cha dijitali kwa ajili kusaidia upatikanaji pembejeo za kilimo ni ufumbuzi wa kipekee. Kitawaimarisha na kuwasaidia wakulima kutenga fedha kwenye akaunti zao za simu ili waweze kununua pembejeo bora kwa muda muafaka na kwa bei nafuu ya asilimia 30.” Wakulima wadogo nchini Tanzania huzalisha asimia 70 ya chakula ingawa karibu nusu yao hawazalishi chakula cha kutosha kwa ajili ya mauzo. Wanakabiliwa na ukosefu wa teknolojia ya kilimo cha kisasa, hawana uwezo wa kujipatia pembejeo bora na wanakosa huduma za kiufundi za ughani zinazoweza kuwasidia kukuza kilimo pamoja na ukosefu wa mafunzo. 





Mwakilishi wa AGRA nchini, Bw. Vianey Rweyendela akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo. Badala yake wakulima hawa wanategemea zaidi kilimo cha mvua, zana duni za kilimo na mbegu hafifu ambazo ubora wake hupungua kila msimu wa kilimo. Isitoshe, wakulima wanaotaka kuwekeza katika kilimo cha kisasa wanashindwa kupata mikopo kwenye taasisi za fedha kwa vile ni asilimia 6 tu ya mikopo ya benki ndio imetengwa kusaidia sekta ya kilimo. Wakulima wanatumia fedha zao chache kununua pembejeo za kilimo kutoka kwa walanguzi; pembejeo ambazo mara nyingi hazina uthibitisho wa ubora. Wakati huo huo, wafanyabiashara wa pembejeo za kilimo wa sekta binafsi wamegundua kwamba usambazaji wa huduma bora maeneo ya vijijini una faida ndogo kutokana na gharama kubwa za kufanya biashara hiyo, uwezo mdogo wa kifedha kwa upande wa wakulima na umaskini uliokithiri miongoni mwa wananchi wengi vijijini. 

 Matokeo yake ni kwamba wastani wa uzalishaji wa mazao mengi kwa hekta unakadiriwa kuwa ni tani 1.7 na kwamba mavuno ya mazao muhimu ya chakula kama vile mahindi yamekuwa yakipungua kwa sababu ya uharibifu wa ardhi na hali mbaya ya hewa. Jinsi ya kupeleka kifaa cha dijitali kwa wakulima Kifaa cha dijitali kitakuwa na mpango mahsusi wa mazao utakaowawezesha wakulima kupata pembejeo kwa kuzingatia malengo yao ya uzalishaji. 

Pia, kupitia simu za mkononi, kitawezesha upatikanaji wa huduma za ughani kwa njia ya ujumbe (SMS) kuwaelimisha wakulima matumizi ya pembejeo. AGRA, shirika linaloongozwa na Waafrika wenye weledi wa kuwasaidia wakulima wadogo barani Afrika, ndilo linalogharimia ukuzaji wa kifaa hicho cha dijitali kupitia ufadhili wa MasterCard Foundation. Taasisi ya Grameen Foundation, ambayo ni taasisi inayojitegemea inayotumia teknolojia ya dijitali kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya umaskini, ndio inasisimia ukuzaji wa chombo hicho cha dijitali. Kifaa hicho pamoja na huduma zake kitatolewa na kampuni ya pembejeo za kilimo ya Positive International Limited, ambayo nembo yake ya kibiashara ya Snow Brand imesaidia sana kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili wakulima nchini Tanzania. Mfumo huo wa ununuzi wa pembejeo utazingatia uwepo wa huduma za fedha za simu za mkononi zinazokua kwa kasi nchini Tanzania. 





Uzinduzi ukifanywa na Mkuu wa AGRA nchini Bw. Vianey Rweyendela (wa pili kulia) kwa kushirikiana na wawakilishi wa Positive International Limited (PIL), na Grameen Foundation. Mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi kumi na nane, ikiwemo awamu ya miezi sita ya utafiti na maendeleo, na miezi kumi na mbili ya awamu ya majaribio ya kifaa hicho cha dijitali. Majaribio yataanza na wateja 15 wa kampuni ya Positive International na wakulima wadogo 15,000 wa mikoa ya Arusha na Mbeya. Mazao yatakayohusika katika mradi huo ni mahindi na maharage, ambayo ni muhimu sana katika maeneo hayo. Kwa mfano, mkoani Arusha – moja ya maeneo yanayohusika katika mradi – mazao hayo mawili hulimwa katika eneo la hekta 150,000 ingawa kuna pengo la mavuno la asimilia 213 kwa upande wa mahindi na asilimia 152 kwa upande wa maharage. Matumizi ya pembejeo bora ndio njia pekee itakayosaidia kuongeza mavuno kwa asilimia 150 ili kutosheleza mahitaji ya chakula katika ngazi ya kaya na pia kukuza mapato. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Positive International, Karan Kapoor, anasema soko la matumizi ya kifaa cha dijitali kwa mauzo ya pembejeo za kilimo nchini Tanzania ni kubwa. “Mamilioni ya wakulima wadogo Tanzania wanahitaji upatikanaji wa pembejeo bora za kilimo kwa bei nafuu. Tutaanza matumizi ya kifaa hiki cha dijitali kwa kuwahusisha wafanyabiashara 15 kwa kipindi cha miezi 18 ijayo. Lengo litakuwa kuwafikia wakulima 15,000 ili kuthibitisha matumizi endelevu ya kifaa hicho.” “Baada ya hapo, tumepanga kupanua matumizi yake ili kuwafikia wafanyabiashara 500 nchini bila ya kuwepo miundombinu mpya.” “Watanzania milioni 19 wanaishi kwa kutegemea mashamba madogo ingawa mtu mmoja kati ya watu 25 hupata huduma ya umeme na watu wengi hawana maji safi na salama majumbani mwao,” anasema Raphael Wolf, Meneja Mradi wa Grameen Foundation

“Kifaa hiki kitaleta mapinduzi makubwa ya dijitali mashambani. Kwa mara ya kwanza, wakulima wengi wataweza kupata raslimali wanazohitaji kuongeza uzalishaji na mapato yao.” Jinsi wakulima wanavyopata pembejeo muhimu za kilimo kama vile mbolea na kuongeza mavuno yao, shirika la AGRA litapata fursa ya kutumia uwepo wa ubia wake na vitega uchumi vilivyopo Tanzania kuwaunganisha wakulima na masoko kupitia ushirikiano na wanunuzi wa kimataifa, wawezeshaji wa biashara na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayoshughulika na upatikanaji wa masoko. Mradi huu ukifanikiwa Tanzania, washirika wake wanakusudia kutumia uwezo wao wa pamoja kuanzisha dhana hii na kifaa hicho cha dijitali katika nchi nyingine za Afrika, ukiwemo mtandao wa wafanyabiashara za kilimo katika nchi za Malawi, Msumbiji, Zambia na nchi nyingine katika bara hili.

Tanzanian Prime Minister, Hon, Kassim Majaliwa is expected to grace the second national economic empowerment symposium to citizens on June 10, 2017 in Dodoma which will attract together the public and private sector to discuss issues on empowerment to fuel the country’s economic drive on industrialization to champion by the President Dr John Magufuli.
Image result for majaliwa kassim majaliwa
Tanzania Prime Minister, Mr. Kassim Majaliwa Kassim
National Economic Empowerment Council (NEEC), Executive Director, Ms Beng’I Issa said that during the press conference in Dar es Salaam, that symposium will pave the way for the important stakeholders private and public sector to discuss on the better way to foster the industrialization drive that will uplift ordinary people from poverty.
  
“The national symposium is focusing on how to get opinions from stakeholders from that sectors so that it will helpful for them during the implementation process that seek to rescue and empowering people from extreme poverty by assisting financial  and economical,” the one day  symposium with the motto “empowering Tanzanians to participate in the industrial economy,” she added Ms Issa

She said the second symposium have various goals including receiving reports on the implementations and coordination on the empowerment process and policy to ordinary people in the national level while the Premier is expected also to attend the discussion.

Other goals are to recognize other ministries, department, institute, local government and districts across the country that have achieved their targets in the areas of empowering people in their respective areas, while the workshop will fuel the implementation and strategic planning will be deploy in order to expand their service to ordinary people across the country.

The symposium will be use also as platform for other people to learn from one another on the basis of empowerment mode as a path way for others to follow the foot step and among other thing the Premier will also launch the annual empowerment report which comes from the assessment of empowerment implementation report.

Ms Beng’I explained further that the report is implementing by various stakeholders and they will hand over awards for those who did better as a stepping stone to foster the government agenda on the empowerment policy to ordinary people.

She added that the council has invited more than 300 stakeholders from private and public sector and other development partners, NGOs, Research Institutes and Universities to attend the workshop.
Ms Issa noted that they signed an agreement with Tanzania Standard Newspaper (TSN) in the process of promoting and educating process to the public about the pros and cons on the empowerment policy and implementation plans to the public.

On his part, the Managing Editor of TSN, Dr Jim Yonazi said that the government newspapers is ready to work shoulder to shoulder with council to achieve the government targets and goals in ensuring ordinary people are economic empowered while the fifth phase government reached its target on green industrial revolution.

“We have re-organized to ensure that will walk on the government/Presidents talks to meet the industrial economy country’s by informing and educating people about the existing opportunities that the government is providing,” Dr Yonazi added.

The symposium is taking place every year under the council and it comes from the coordination of the empowering ordinary people from the Ministry, department, local government authorities, districts and the private sector, while it was officially launched February 9, last year by the Premier.

The directives has always fueling the coordination and implementation of the national policy on the empowering ordinary people economical in the private sector by creating a council of empowering people and coordinators in the ministries,  26 regions and all 185  municipalities across the country.  


Tanzania has made significant progress in delivering education and health services, particularly in the areas of rural health infrastructure and teacher attendance, according to the latest Service Delivery Indicators.
 
However, the new data also highlight weaknesses that are contributing to low levels of learning in primary schools and tragic mortality levels among mothers and newborns. Tanzania’s maternal mortality rate is very high at 432 deaths per 100,000 live births.
 
“While Tanzania has reduced child mortality, mothers and newborns are still at high risk of untimely death; and while the country has achieved near-universal primary school enrollment, one in four children cannot read a paragraph in Kiswahili in Standard Four,” said Keith Hansen, World Bank Group Vice President for Human Development. 
 
“Service Delivery Indicators are public data that citizens can use to hold the government accountable for education and health services, and that the government can use to inform reform efforts in these sectors. As Tanzania aspires to achieve middle-income status by 2025, SDI is an example of the kind of data transparency and accountability that could be transformational.”
 
Health infrastructure is improving rapidly, especially in rural Tanzania, going from 5 percent of health facilities with clean water, power, and improved sanitation in 2010 to 36 percent in 2014. Serious challenges remain, including getting more health workers out to rural areas—which have only 9 percent of the country’s doctors and 28 percent of its health workforce—and boosting their diagnostic capacity. The data show that three out of five health workers cannot identify severe dehydration, a fatal condition for children.
 
According to the latest information available to the press says in education, teacher absenteeism from schools has fallen sharply by 40 percent, leading to 24 more teaching days a year. 
 
However, 37 percent of the teachers who were in school were still not in the classroom and teaching. Therefore, classroom absence remains a challenge and points to school leadership and management issues. 
 
Teacher-pupil ratios have become more manageable, dropping by 20 percent across the country, but remain very high in urban schools. Importantly, teacher knowledge continues to be a serious issue, with only one in five mastering the curriculum they teach.
 
The World Bank, REPOA and the African Economic Research Consortium (AERC) have partnered to produce this round of data for Tanzania. SDI surveys have so far been done in eight African countries—Kenya, Mozambique, Niger, Nigeria, Senegal, Tanzania, Togo, and Uganda, capturing the service delivery experience of 370 million people. Tanzania and Senegal pioneered these surveys in 2010.
 
Ends.

Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Mkoka wakitazama Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake ukikatiza kwenye moja ya daraja wakati wakielekea katika kijiji hicho cha Mkoka,Wilayani Kongwa mkoani Dodoma,Ndugu kinana aliweka jiwe la msingi la kitega uchumi cha tawi la CCM pamoja na kufungua Ofisi ya CCM Tawi la Mkoka.Ndugu Kinana akiwa amembatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye anaendelea na ziara yake ya siku tisa mkoani humo,akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwemo sambamba na kuimarisha uhai wa chama,kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
Mamia ya wakazi wa kijiji cha Mkoka wakishangilia jambo wakati
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo katika mkutano wa hadhara Wilayani Kongwa mkoani Dododoma.Ndugu Kinana akiwa amembatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye anaendelea na ziara yake ya siku tisa mkoani humo,akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwemo sambamba na kuimarisha uhai wa chama,kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mkoka,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.



 sehemu ya umati wa watu wakimsikiliza katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mkoka,Wilayani Kongwa.

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwa wamefuatana na wananchi walipokuwa wakiwasili katika uwanja wa Mkoka kwa ajili ya kufanya mkutano wa hadhara,mbali ya Uongozi huo wa juu wa CCM,pia waliambatana Mbunge wa jimbo la Kongwa Mh.Job Ndugai,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh.Chiku Galawa,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma,Mh.Addam Kimbisa pamoja na viongozi wengine wa wilaya.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani juu ya jengo akiwa sambamba na Mbunge wa jimbo la Kongwa Mh.Job Ndugai wakishiriki ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Njoge,Kata ya Njoge pamoja na kusalimia Wananchi wa eneo hilo.
Mbunge wa jimbo la Kongwa Mh.Job Ndugai akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mara baada ya kushiriki ujenzi wa darasa la shule ya msingi Mlali,katika kijiji cha Mlali Wilayani Kongwa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizindua mradi wa maji katika kijiji cha Mlali Wilayani Kongwa,mradi huo uliogharimu zaidi ya shilingi milioni mia sita ulianza kujengwa mnamo mwaka 2013 na kutarajiwa kumalizika mei 2014,lakini kwa bahati mbaya mradi huo haukukamilika kwa wakati kutokana na ukosefu wa fedha.Mbunge wa jimbo hilo la Kongwa,Mh.Ndugai alieleza kuwa mradi huo kwa sasa umekwishakamilika kwa asilimia tisini na kwamba mradi huo wa maji safi na salama utawanufaisha wanakijiji wapatao mia saba na zaidi.

Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame amesema kuwa hatua ya Mwenyekiti wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuhudhuria Mkutano wa Tisa wa Nchi Zilizoungana Kutekeleza Miradi ya Miundombinu Ukanda wa Kaskazini za Northern Corridor Projects ni hatua muhimu katika kufungua utekelezaji wa miradi ya miundomninu katika kanda nyingine za EAC. 
Aidha, Rais Kagame amemshukuru Rais Kikwete kwa uamuzi wake kuhudhuria Mkutano huo uliofanyika leo, Jumamosi, Machi 7, 2015, katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena mjini Kigali, Rwanda. 
Rais Kikwete amefanya ziara hiyo ya siku moja kuhudhuria Mkutano huo kwa mwaliko wa Rais Kagame. 
Naye Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema kuwa ni jambo la kufurahisha kwamba Rais Kikwete ameweza kuhudhuria Mkutano wa leo, kwa sababu sasa njia imefunguka kuanza kazi ya utekelezaji wa miradi kwenye Ukanda wa Kati wa Central Corridor unaokatisha katikati ya Tanzania. 
Marais Kagame na Kenyatta walikuwa wanazungumza wakati wa hotuba za ufunguzi za Mkutano huo uliofanyika kwa kiasi cha saa mbili unusu mara baada ya Rais Kikwete kuwasili Kigali akitokea Dar es Salaam kiasi cha saa sita mchana. 
Akifungua Mkutano huo, Rais Kagame alisema: “Nawashukuru waheshimiwa marais wote kwa kuja. Lakini hasa hasa, namshukuru sana mwenyekiti wetu wa EAC Rais Kikwete kwa kupata muda wa kuja kujiunga nasi katika mkutano huu.” Aliongeza Rais Kagame huku makofi yakiendelea kumkaribisha na kumshangilia Rais Kikwete: 
“Kuwepo kwake hapa leo, kunaongeza matumaini kuwa miradi mbali mbali na mingi zaidi katika kanda mbali mbali za nchi zetu wanachama wa EAC, sasa inaweza kutekelezwa kwa haraka zaidi. Nakushukuru sana Mheshimiwa Rais.” Mbali na Marais Kikwete, Kagame na Kenyatta, Mkutano wa leo pia umehudhuriwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini, Makamu wa Rais wa Pili wa Burundi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia. 
Nchi za Kenya, Uganda,Rwanda na Sudan Kusini ndizo wanachama wa Northern Corridor na kwenye mkutano wa leo, Burundi pia imetangaza kuwa imeamua kuwa mshiriki kamili wa mikutano ya Ukanda huo badala ya kuwa msikilizaji kwa muda mrefu. 
Akizungumza katika Mkutano huo, Rais Kenyatta amesema: “Tunafurahi sana kwamba Mwenyekiti wetu wa EAC yuko nasi leo kwa sababu uwepo wake utaongeza msukumo wa kutuwezesha kuanza utekelezaji wa miradi mingine hasa katika Ukanda wa Kati. Tanzania ina mengi kuchangia katika jambo hilo. Kwa mfano, umeme mwingi ambao utaanza kuzalishwa na Tanzania mwaka huu, unahitajika kwa nchi zote za EAC na Northern Corridor.” 
Rais Kikwete ambaye alikuwa msikilizaji tu kwa sababu Tanzania inaendelea kuwa mwanachama wa EAC bila kuwa mshirika wa Northern Corridor amezugumza kwa ufupi tu akisema kuwa kwa sababu yeye ni mwalikwa na msikilizaji asingeweza kusema mengi. 
Amewaambia viongozi wenzake: “Nakushukuru Rais Kagame kwa kunialika. Kama unavyojua, mimi ni msikilizaji tu na hivyo siwezi kusema sana. Lakini napenda kuwapongezeni nyote kwa kazi mnayoifanya. Sote tunajua kuwa hakuna utengamano bila kuendeleza miundombinu.” Ameongeza Rais Kikwete: “Kinachoendelea kule Northern Corridor kitasaidia sana katika mawazo na utekelezaji wa kazi ambayo tunajiandaa kuianza kwenye Ukanda wa Kati. Nawatakieni mafanikio zaidi na kasi ya Mwenyeji Mungu katika utekelezaji wa miradi yenu.” 
Chini ya Northern Corridor nchi hizo zimebuni miradi 14, ambayo baadhi yao imeanza kutekelezwa ikiwa ni pamoja na kuanzisha visa moja ya kusafiria ya watalii. 
Nchi hizo ziliunda kundi hilo mwaka mmoja na miezi tisa iliyopita na wakuu wa nchi wanachama hukutana kila baada ya miezi miwili kwa mashauriano na maamuzi. Rais kikwete amerejea nyumbani usiku wa leo baada ya kumalizika kwa Mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kwa furaha  sahada la maua baada ya kuwasili Kigali, Rwanda, tayari kwa mkutano  na viongozi wenzake wa Jumiya hiyo katika mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi hizo kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini (Northern Corridor Integration Projects)  katika Hoteli ya Serena mjini Kigali. 
Mkutano wa leo pia umehudhuriwa na wakuu wa nchi za Kenya, Uganda na wenyeji Rwanda. Mbali na nchi hizo na mbali na Tanzania, nchi za Burundi na Sudan Kusini pia zilialikwa kuhudhuria mkutano huo. Mkutano huo ni ulijadili hatua za utekelezaji wa miradi mbali mbali iliyokubaliwa kulingana na maelekezo yaliyotolewa katika mkutano wa nane wa namna hiyo uliofanyika Nairobi, Kenya, Desemba 11, mwaka jana, 2014.
 Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mwenyeji wake Rais Paul Kagame wa Rwanda kabla ya kuanza kwa mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi hizo kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini (Northern Corridor Integration Projects)  katika Hoteli ya Serena mjini Kigali. 
 Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wenzake wa Jumiya hiyo katika mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi hizo kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini (Northern Corridor Integration Projects)  katika Hoteli ya Serena mjini Kigali. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Paul Makonda baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni leo Machi 7, 2015 akitokea Kigali Rwanda, alikohudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kati ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Sophia Mjema. PICHA NA IKULU


The United Republic of Tanzania plans to review its procurement legislation to close loopholes that make it possible for corrupt officials to profit from the public purse. 


Addressing parliament last year in the December session, minister of state Stephen Wassira, pledged to take action to ensure items could not be purchased at inflated prices under the law, which results in unreasonably high profit margins for suppliers. As well as helping to reduce corruption, he said the more robust rules would boost competitiveness among businesses looking to supply to government.


Announcing his intention, Wassira, said: “The time has come to review the law. You can hide under the law and steal according to the law. If we do not act now and [instead] let corruption thrive, everything we buy or make will be substandard. And if we continue like this we will erode development.”


Around 70 per cent of the country’s development budget will be channelled through public sector procurement. The minister used this to strengthen the case for ensuring regulations are tight and robust.

Ends,



Chuo cha BBC cha Uandishi wa Habari, (BBC Academy, College of Journalism) chafungua upya tovuti ya Kiswahili kwa ajili ya waandishi wa habari duniani kote.

Chuo cha BBC cha Uandishi wa Habari kimeanzisha upya tovuti ya Kiswahili katika mfumo (mtindo) mpya na maswala mapya.
Tovuti yenyewe inaweza kupatikana kwenye simu ya mkononi, tabiti (tablet) na komputa kubwa.

Lengo la tovuti ya Kiswahili ni kuonesha mtindo wa uandishi katika idhaa za lugha mbali-mbali zinazotangaza katika Idhaa Kuu ya Dunia ya BBC, na ni sehemu ya jukumu la BBC la kuhudumia jamii na kusambaza ujuzi wake ili kunufaisha waandishi wa habari wa Kiswahili dunia nzima.

Ali Saleh, Mhariri wa Idhaa ya Kiswahili:

"Baada ya serikali za Afrika Mashariki kuruhusu vyombo vingi vya habari binafsi kuanzishwa, vinatoa ushindani mkubwa kwa vyombo vya habari vya kimataifa. Ingawa vyombo hivyo vimestawi na kuzidi kukua, vyombo vinavyojitegemea vinakabiliwa na tishio katika nchi kadha, ambako waandishi wa habari wamekimbia kwa sababu ya kulengwa kwa mashambulio na mashtaka. Serikali katika nchi ambako BBC inasikika zinatayarisha sheria kali kupunguza uhuru wa kujieleza, haki ya kutofichua chanzo cha taarifa, na kuwafunga waandishi wa habari kwa yale waliyotangaza."
Tovuti ina maeneo matatu muhimu, ufundi wa uandishi, lugha ya Kiswahili, na maadili ya BBC.

Kupitia sehemu hii ufundiutapata ushauri kuhusu televisheni, redio na mtandao, utangazaji, uandishi, mitandao ya jamii na mengi mengineyo.

Katika sehemu hii wahariri na waandishi wa BBC wanaeleza namna ya kutangaza na kuandika taarifa za televisheni na jinsi ya kuandika ripoti kuhusu michezo. Tovuti inatoa mwongozo jinsi ya kuthibitisha habari zilizoko kwenye mitandao ya jamii.

Katika sehemu yavigezo, kuna ushauri kuhusu msimamo wa kutopendelea upande wowote, ukweli, uhuru, maslahi ya jamii, uwajibikaji na sheria.

Lakini msingi wa kila tovuti ni lugha. Sehemu yalugha inatoa ushauri kuhusu lugha isiyopendelea upande wowote, lugha sahihi, tahajia, ufupisho, majina ya kigeni na ufundi wa kutafsiri na mengineyo.

Sehemu ya lugha ya tovuti ina vielelezo vilivyotengenezwa maalumu kulingana na utamaduni wa Kiswahili. Juhudi zimefanywa kuelezea sehemu hii kwa picha zinazoonesha Idhaa iliyohusika ya BBC pamoja na wasikilizaji na watazamaji.
Pamoja na tovuti ya Kiswahili, Chuo cha Uandishi wa Habari cha BBC, (College of Journalism) piya kinaanzisha lugha tatu nyengine,Burmese,Pashto naVietnamese. Tovuti hizo nne zinafanya jumla ya tovuti za chuo cha BBC zilizoanzishwa upya kufikia 11.

Katika miaka mitano iliyopita BBC College of Journalism, imeanzisha jumla ya tovuti 27 katika lugha tofauti.
Unaweza kusoma tovuti za BBC College of Journalism bila ya kutozwa pesa kokote uliko duniani.

KATIKA miaka mitano iliyopita BBC College of Journalism, imeanzisha jumla ya tovuti 27 katika l
ugha tofauti. Unaweza kusoma tovuti za BBC College of Journalism bila ya kutozwa pesa kokote uliko duniani.

Chanzo:BBC Swahili


1. Aboud Jumbe ......................(M.B.L.M-Zanzibar) makamu wa Rais
2. Edward M. Sokoine (MONDULI)...........Waziri mkuu
3. Rashid M. Kawawa( LIWALE)..............Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa
4. Alhaj Hasnu Makame(aliteuliwa-zanzibar)........Waziri wa nchi ofisi ya Rais ustawishajiwa makao makuu.
5. Amir H. Jamal (MOROGOR).....................Waziri wa mawasiliano na uchukuzi
6. Cleopa D. Msuya(aliteuliwa)....................Waziri wa viwanda.
7. John S. Malecela(DODOMA VIJIJINI)...........Waziri wa kilimo
8. Alfed C. Tandau(MBINGA).....................Waziri asiye na wizara maalum
9. Hassan Nasoro Moyo( M.B.M-Zanzibar).. Waziri wa mambo ya ndani ya nchi
10.Julie C. Manninga(aliteuliwa)..................Waziri wa sheria
11.Alphonce Rulegura(sengerema)............waziri wa biashara
12.Nicholus kuhanga(mbunge wa taifa).....Waziri wa elimu ya taifa
13.Dkt leader strling(mbunge wa taifa).....Waziri wa afya
14.S.A.Ole saibul(arusha)................Waziri wa maliasili na utalii
15.Tabitha siwale(aliteuliwa)..........Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo mijini
16.Crispin Tungaraza..................(Mbunge wa Taifa)waziri wa kazi na ustawi wa jamii
17.Anour Kassum(aliteuliwa).........Waziri wa Maji, umeme na madini.
18. IsacK A. Sepetu................(Aliteuliwa) waziri wa habari na utangazaji
19.Edwin Mtei (Aliteuliwa)............waziri wa fedha na mipango
20.Benjamin Mkapa(Aliteuliwa)......waziri wa mambo ya nchi za nje.
21. Abel k. Mwanga(msoma mjini).. waziri wa maendeleo ya watumishi
22.Abdalla S. Natepe(M.B.M-Zanzibar)….Waziri wa nchi ofisi ya Rais
23.Ali Mzee Ali (M.B.M-Zanzibar)...waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais
24.Jackson Makweta (NJOMBE)........waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu.
25. Chediel Y. Mgonja(PARE)......waziri wa utamaduni wa taifa navijana
26.Samwel J. Sitta(URAMBO).....Waziri wa Ujenzi.
27. Daniel M. Machemba(MWANZA)…. ..Waziri asiye na Wizara Maalum


Tanga Cement Company Limited (TCCL) has handover a well constructed health centre worth Tsh 98m to Kichangani residents in Tanga region as part of the company’s efforts to support the central government on health, education and water sanitation issues in Tanga region. 

Speaking to invited guests during the official handover ceremony, the Deputy Minister for Health and Social welfare Dr Seif Rashidi said that the government is welcomed the support from the private sector in a move to construct health facilities to the people especially in remote areas.

He said that the government will continue to allocate funds for the construction of health centre and recruit more medical practitioners, doctors, specialists and reliable stock of drugs to regional, districts and villagers health centre across the country.

“On behalf of the ministry and the government I would like to thanks the management of Tanga cement and staff for the strongly support of the health centre that worth Tsh 98m which will serve majority of kichangani residents and other neighboring villagers,” he said. 

On his part, Tanga Cement Managing Director Reinhardt Swart said that the company takes its Corporate Social Responsibility program into the higher level that deserves to serve the public and the country at large.

“We have a policy that allows us to set a side up to 1 percent of our profit for the Tanzanian community, Kichangani village is within that Tanzanian community,” he added.

He further said that the firm conducted a campaign on sensitization and HIV testing and counseling for TCCL surrounding communities of Pongwe and Kichangani.

“During that campaign, we realised that this area had no health center. People, who needed health services, were forced to go the either health centres at Maweni Prisons, Pongwe or Kange.”  He underscored. 

Swart noted that the company is now undertaking another health project in Handeni district which is within Tanga region, his optimistic that it will be completed early 2014.
Ends.


WATU watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia kituo cha mafuta cha EAFCO kilichopo eneo la Mwenge mjini Singida, na kupora shilingi laki tano baada ya kufyetua risasi moja hewani kwa lengo la kuwaogofya wafanyakazi.


 Watu hao wanadaiwa walikuwa wamebeba bunduki moja ya kienyeji inayodhaniwa kuwa ni aina ya gobore na bastola moja.


 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida,Geofrey Kamwela,alisema tukio hilo limetokea Septemba tisa mwaka huu saa 11.00 jioni eneo la Mwenge mjini Singida.


 Alisema awali watu hao waliteka taksi yenye usajili T.637 AGL aina ya Toyota mark 11 iliyokuwa ikiendeshwa na Ernest Joseph (32) mkazi wa Misuna mjini Singida,na kisha kuitumia katika kutekeleza azma yao.


 “Huyu dereva wa taksi baada ya kutekwa,alifungwa kamba ya katani na kuweka kwenye buti ya nyuma na kwenda naye kwenye eneo la tukio na wakati uporaji huo unafanyika,dereva huyo alikuwa ndani ya buti la gari lake”,alisema Kamwela.


 Kamanda huyo alisema majambazi hayo yalipofika kwenye kituo hicho cha mafuta,walifyetua risasi moja hewani kwa kutumia bunduki aina ya gobore kwa lengo la kuogofya watumishi na wateja waliokuwa kwenye kituo hicho.Baada ya hapo,ndipo yalipofanikiwa kupora shilingi 500,000.


 Alisema polisi walipopata taarifa ya tukio hilo,walifika mara moja kwenye kituo hicho na kukuta majambazi hayo kwa kutumia taski waliyoiteka,waliishatoroka lakini hawakufika mbali walipata ajali na kuitekeleza taksi hiyo na wao kukimbilia kusikojulikana.


 “Wakati majambazi hayo yanatoroka,moja lilidondosha bunduki aina ya gobore ambalo limeokotwa na polisi.Kwa sasa tunaendelea na msako wa kuyasaka majambazi hayo ili sheria iweze kuchukua mkondo wake”alisema Kamwela.


 Wakati huo huo,Kamanda Kamwela alisema dereva Ernest alifikiwa katika hospitali ya mkoa na kupata matibabu na kisha kuruhusiwa.


MWISHO.

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.