Baadhi
ya Wananchi wa kijiji cha Mkoka wakitazama Msafara wa Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake ukikatiza kwenye moja ya
daraja wakati wakielekea katika kijiji hicho cha Mkoka,Wilayani Kongwa
mkoani Dodoma,Ndugu kinana aliweka jiwe la msingi la kitega uchumi cha
tawi la CCM pamoja na kufungua Ofisi ya CCM Tawi la Mkoka.Ndugu Kinana
akiwa amembatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye
anaendelea na ziara yake ya siku tisa mkoani humo,akikagua na kuhimiza
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwemo sambamba
na kuimarisha uhai wa chama,kusikiliza matatizo ya Wananchi na
kuyatafutia ufumbuzi.
Mamia ya wakazi wa kijiji cha Mkoka wakishangilia jambo wakati
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia jioni ya
leo katika mkutano wa hadhara Wilayani Kongwa mkoani Dododoma.Ndugu Kinana akiwa amembatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye
anaendelea na ziara yake ya siku tisa mkoani humo,akikagua na kuhimiza
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwemo sambamba
na kuimarisha uhai wa chama,kusikiliza matatizo ya Wananchi na
kuyatafutia ufumbuzi.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha
Mkoka,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo wilayani Kongwa
mkoani Dodoma.
sehemu ya umati wa watu wakimsikiliza katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mkoka,Wilayani Kongwa.
sehemu ya umati wa watu wakimsikiliza katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mkoka,Wilayani Kongwa.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye wakiwa wamefuatana na wananchi walipokuwa wakiwasili katika
uwanja wa Mkoka kwa ajili ya kufanya mkutano wa hadhara,mbali ya Uongozi
huo wa juu wa CCM,pia waliambatana Mbunge wa jimbo la Kongwa Mh.Job
Ndugai,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh.Chiku Galawa,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Dodoma,Mh.Addam Kimbisa pamoja na viongozi wengine wa wilaya.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani juu ya jengo akiwa sambamba na Mbunge
wa jimbo la Kongwa Mh.Job Ndugai wakishiriki ujenzi wa zahanati ya
kijiji cha Njoge,Kata ya Njoge pamoja na kusalimia Wananchi wa eneo
hilo.
Mbunge
wa jimbo la Kongwa Mh.Job Ndugai akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Kinana mara baada ya kushiriki ujenzi wa darasa la shule ya
msingi Mlali,katika kijiji cha Mlali Wilayani Kongwa.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizindua mradi wa maji katika kijiji cha
Mlali Wilayani Kongwa,mradi huo uliogharimu zaidi ya shilingi milioni
mia sita ulianza kujengwa mnamo mwaka 2013 na kutarajiwa kumalizika mei
2014,lakini kwa bahati mbaya mradi huo haukukamilika kwa wakati kutokana
na ukosefu wa fedha.Mbunge wa jimbo hilo la Kongwa,Mh.Ndugai alieleza
kuwa mradi huo kwa sasa umekwishakamilika kwa asilimia tisini na kwamba
mradi huo wa maji safi na salama utawanufaisha wanakijiji wapatao mia
saba na zaidi.
Post a Comment