Na Happy Shirima - Habari Maelezo.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake
na Maendeleo [WAMA] anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya
siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika Machi 8 mwaka huu katika
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam .
Akizungumzia
maadhimisho hayo leo jijini Dar es salaam , Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar
se salaam Mhe. Raymond Mushi amesema kuwa maadhimisho hayo mwaka huu
yataongozwa na kauli mbiu isemayo “Uwezeshaji Wanawake Tekeleza, Wakati
ni Sasa “.
Amesema
ujumbe huo unaikumbusha jamii kujenga mazingira wezeshi kwa kutambua
mchango wa wanawake katika kuleta maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla .
Ameeleza
kuwa wadau kote nchini wanatakiwa kuelimishwa ili kuangali upya wajibu
wao kwa kuwashirikisha, kuwaamini na kuwapa wanawake haki sawa katika
nafasi za elimu , uchumi na uongozi ili waweze kuwa chachu ya maendeleo
yao binafsi, familia na taifa zima.
“Lengo
la maadhimisho haya ni kukumbuka wajibu wa kila mmoja kushiriki katika
mikakati ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za wanawake kuanzia
ngazi ya kaya hadi Taifa” Amesema.
Akitoa
ufafanuzi kuhusu maadhimisho hayo amesema kuwa yanaambatana na
maonyesho ya kazi na bidhaa mbalimbali za vikundi vya ujasiriamali na
kuzishirikisha Asasi za Kiraia zinazojishughulisha na masuala ya utoaji
wa Elimu ya Uraia na sheria ya utunzaji fedha.
Ameongeza
kuwa siku ya kilele kutakuwa na maandamano yatakayoanzia Barabara ya
Lumumba na kuishiaviwanja vya mnazi mmoja ambayo yatapokewa na mgeni
rasmi na wananchi wa mkoa wa Dare s salaam.
Post a Comment