Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa siku
ya jumapili kati ya Simba SC na Young African utakaofanyika kwenye
dimba la Uwanja wa Taifa kuanzia majira ya saa 10 kamili za jioni.
Mchezo
huo utachezeshwa na mwamuzi Martin Saanya kutoka Morogoro, akisaidiwa
na Soud Lila (DSM) mshika kibendera wa kwanza, Florentina Zabron
(Dodoma) mshika kibendera wa pili, Mwamuzi wa akiba Israel Mjuni (DSM),
na kamisaa wa mchezo ni Ame Santimeya (DSM).
Viingilio
vya mchezo huo, VIP A sh. 40,000, VIP B sh. 30,000, VIP C sh. 20,000,
Rangi ya Machungwa (Orange) sh. 10,000, huku Rangi ya Bluu na Kijani
ikiwa ni sh. 7,000.
Tiketi
zitaanza kuuzwa keso (jumamosi) saa 2 kamili asubuhi katika vituo vya,
Karume (Ofisi za TFF), Mgahawa wa Steers (Posta Mpya), Oilcom
(Buguruni), BigBon (Kariakoo), Olicom (Ubungo), Dar Live (Mbagala),
Uwanja wa Uhuru, Kivukoni (Ferry) na Makumbusho (kituo cha mabasi).
Magari
yenye vibali maalum ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia ndani ya uwanja siku
ya jumapili kwa kupitia barabara ya Mandela na Uwanja wa Uhuru,
barabara ya Chang'ombe itafungwa kuanzia saa 12 kamili asubuhi.
TFF
inawaomba, wapenzi, washabiki na wadau wa mchezo kununua tiketi katika
vituo vilivyotajwa ili kuepuka kuuziwa tiketi bandia, ili kuimarisha
ulinzi na usalama wa mchezo, mashabiki wenye mabegi, silaha, vilevi na
chupa za maji hawataruhusiwa kuingia navyo uwanjani.
Aidha
katika mchezo huo TFF itatoa ujumbe maalum kupitia kwa wachezaji
kuhamasisha juhudi za Taifa za kuzuia mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu
wa ngozi (Albino).
Post a Comment