May 2017



Wakulima wadogo nchini Tanzania hivi karibuni wataweza kupata taarifa mbalimbali za kijiditali kuhusu masuala ya pembejeo, ukiwemo ushauri utakaosaidia kutatua matatizo yanayowakabili kama vile upatikanaji wa fedha, pembejeo na mafunzo. Mradi huo umezinduliwa na taasisi tatu za Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA), Positive International Limited (PIL), na Grameen Foundation katika sherehe zilizohudhuriwa na maofisa wa serikali, wawakilishi wa vyama vya wakulima, taasisi za fedha, kampuni za mbegu, wafanyabiashara wa nyenzo za kilimo na wale wanaojishughulisha na biashara za mazao ya sekta ya kilimo. 

Kifaa hicho cha dijitali kitawawezesha wakulima kulipia mapema pembejeo wanazohitaji kupitia simu za mkononi kwa bei nafuu. Pia kifaa hicho kitawapa wakulima pembejeo kulingana na mazao na malengo yao ya uzalishaji na pia kupata taarifa za ushauri kuhusu matumizi bora ya pembejeo hizo. “Moja ya changamoto kubwa zinazowakabili wakulima ni kwamba hukosa fedha mwanzoni mwa msimu wa upandaji mazao, jambo ambalo huwalazimisha kutafuta fedha hizo kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo na hivyo kuwaongezea mzigo,” alisema Hedwig Siewertsen, kiongozi anayeshughulikia masuala ya fedha wa shirika la Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA). “Kifaa hicho cha dijitali kwa ajili kusaidia upatikanaji pembejeo za kilimo ni ufumbuzi wa kipekee. Kitawaimarisha na kuwasaidia wakulima kutenga fedha kwenye akaunti zao za simu ili waweze kununua pembejeo bora kwa muda muafaka na kwa bei nafuu ya asilimia 30.” Wakulima wadogo nchini Tanzania huzalisha asimia 70 ya chakula ingawa karibu nusu yao hawazalishi chakula cha kutosha kwa ajili ya mauzo. Wanakabiliwa na ukosefu wa teknolojia ya kilimo cha kisasa, hawana uwezo wa kujipatia pembejeo bora na wanakosa huduma za kiufundi za ughani zinazoweza kuwasidia kukuza kilimo pamoja na ukosefu wa mafunzo. 





Mwakilishi wa AGRA nchini, Bw. Vianey Rweyendela akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo. Badala yake wakulima hawa wanategemea zaidi kilimo cha mvua, zana duni za kilimo na mbegu hafifu ambazo ubora wake hupungua kila msimu wa kilimo. Isitoshe, wakulima wanaotaka kuwekeza katika kilimo cha kisasa wanashindwa kupata mikopo kwenye taasisi za fedha kwa vile ni asilimia 6 tu ya mikopo ya benki ndio imetengwa kusaidia sekta ya kilimo. Wakulima wanatumia fedha zao chache kununua pembejeo za kilimo kutoka kwa walanguzi; pembejeo ambazo mara nyingi hazina uthibitisho wa ubora. Wakati huo huo, wafanyabiashara wa pembejeo za kilimo wa sekta binafsi wamegundua kwamba usambazaji wa huduma bora maeneo ya vijijini una faida ndogo kutokana na gharama kubwa za kufanya biashara hiyo, uwezo mdogo wa kifedha kwa upande wa wakulima na umaskini uliokithiri miongoni mwa wananchi wengi vijijini. 

 Matokeo yake ni kwamba wastani wa uzalishaji wa mazao mengi kwa hekta unakadiriwa kuwa ni tani 1.7 na kwamba mavuno ya mazao muhimu ya chakula kama vile mahindi yamekuwa yakipungua kwa sababu ya uharibifu wa ardhi na hali mbaya ya hewa. Jinsi ya kupeleka kifaa cha dijitali kwa wakulima Kifaa cha dijitali kitakuwa na mpango mahsusi wa mazao utakaowawezesha wakulima kupata pembejeo kwa kuzingatia malengo yao ya uzalishaji. 

Pia, kupitia simu za mkononi, kitawezesha upatikanaji wa huduma za ughani kwa njia ya ujumbe (SMS) kuwaelimisha wakulima matumizi ya pembejeo. AGRA, shirika linaloongozwa na Waafrika wenye weledi wa kuwasaidia wakulima wadogo barani Afrika, ndilo linalogharimia ukuzaji wa kifaa hicho cha dijitali kupitia ufadhili wa MasterCard Foundation. Taasisi ya Grameen Foundation, ambayo ni taasisi inayojitegemea inayotumia teknolojia ya dijitali kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya umaskini, ndio inasisimia ukuzaji wa chombo hicho cha dijitali. Kifaa hicho pamoja na huduma zake kitatolewa na kampuni ya pembejeo za kilimo ya Positive International Limited, ambayo nembo yake ya kibiashara ya Snow Brand imesaidia sana kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili wakulima nchini Tanzania. Mfumo huo wa ununuzi wa pembejeo utazingatia uwepo wa huduma za fedha za simu za mkononi zinazokua kwa kasi nchini Tanzania. 





Uzinduzi ukifanywa na Mkuu wa AGRA nchini Bw. Vianey Rweyendela (wa pili kulia) kwa kushirikiana na wawakilishi wa Positive International Limited (PIL), na Grameen Foundation. Mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi kumi na nane, ikiwemo awamu ya miezi sita ya utafiti na maendeleo, na miezi kumi na mbili ya awamu ya majaribio ya kifaa hicho cha dijitali. Majaribio yataanza na wateja 15 wa kampuni ya Positive International na wakulima wadogo 15,000 wa mikoa ya Arusha na Mbeya. Mazao yatakayohusika katika mradi huo ni mahindi na maharage, ambayo ni muhimu sana katika maeneo hayo. Kwa mfano, mkoani Arusha – moja ya maeneo yanayohusika katika mradi – mazao hayo mawili hulimwa katika eneo la hekta 150,000 ingawa kuna pengo la mavuno la asimilia 213 kwa upande wa mahindi na asilimia 152 kwa upande wa maharage. Matumizi ya pembejeo bora ndio njia pekee itakayosaidia kuongeza mavuno kwa asilimia 150 ili kutosheleza mahitaji ya chakula katika ngazi ya kaya na pia kukuza mapato. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Positive International, Karan Kapoor, anasema soko la matumizi ya kifaa cha dijitali kwa mauzo ya pembejeo za kilimo nchini Tanzania ni kubwa. “Mamilioni ya wakulima wadogo Tanzania wanahitaji upatikanaji wa pembejeo bora za kilimo kwa bei nafuu. Tutaanza matumizi ya kifaa hiki cha dijitali kwa kuwahusisha wafanyabiashara 15 kwa kipindi cha miezi 18 ijayo. Lengo litakuwa kuwafikia wakulima 15,000 ili kuthibitisha matumizi endelevu ya kifaa hicho.” “Baada ya hapo, tumepanga kupanua matumizi yake ili kuwafikia wafanyabiashara 500 nchini bila ya kuwepo miundombinu mpya.” “Watanzania milioni 19 wanaishi kwa kutegemea mashamba madogo ingawa mtu mmoja kati ya watu 25 hupata huduma ya umeme na watu wengi hawana maji safi na salama majumbani mwao,” anasema Raphael Wolf, Meneja Mradi wa Grameen Foundation

“Kifaa hiki kitaleta mapinduzi makubwa ya dijitali mashambani. Kwa mara ya kwanza, wakulima wengi wataweza kupata raslimali wanazohitaji kuongeza uzalishaji na mapato yao.” Jinsi wakulima wanavyopata pembejeo muhimu za kilimo kama vile mbolea na kuongeza mavuno yao, shirika la AGRA litapata fursa ya kutumia uwepo wa ubia wake na vitega uchumi vilivyopo Tanzania kuwaunganisha wakulima na masoko kupitia ushirikiano na wanunuzi wa kimataifa, wawezeshaji wa biashara na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayoshughulika na upatikanaji wa masoko. Mradi huu ukifanikiwa Tanzania, washirika wake wanakusudia kutumia uwezo wao wa pamoja kuanzisha dhana hii na kifaa hicho cha dijitali katika nchi nyingine za Afrika, ukiwemo mtandao wa wafanyabiashara za kilimo katika nchi za Malawi, Msumbiji, Zambia na nchi nyingine katika bara hili.

Tanzanian Prime Minister, Hon, Kassim Majaliwa is expected to grace the second national economic empowerment symposium to citizens on June 10, 2017 in Dodoma which will attract together the public and private sector to discuss issues on empowerment to fuel the country’s economic drive on industrialization to champion by the President Dr John Magufuli.
Image result for majaliwa kassim majaliwa
Tanzania Prime Minister, Mr. Kassim Majaliwa Kassim
National Economic Empowerment Council (NEEC), Executive Director, Ms Beng’I Issa said that during the press conference in Dar es Salaam, that symposium will pave the way for the important stakeholders private and public sector to discuss on the better way to foster the industrialization drive that will uplift ordinary people from poverty.
  
“The national symposium is focusing on how to get opinions from stakeholders from that sectors so that it will helpful for them during the implementation process that seek to rescue and empowering people from extreme poverty by assisting financial  and economical,” the one day  symposium with the motto “empowering Tanzanians to participate in the industrial economy,” she added Ms Issa

She said the second symposium have various goals including receiving reports on the implementations and coordination on the empowerment process and policy to ordinary people in the national level while the Premier is expected also to attend the discussion.

Other goals are to recognize other ministries, department, institute, local government and districts across the country that have achieved their targets in the areas of empowering people in their respective areas, while the workshop will fuel the implementation and strategic planning will be deploy in order to expand their service to ordinary people across the country.

The symposium will be use also as platform for other people to learn from one another on the basis of empowerment mode as a path way for others to follow the foot step and among other thing the Premier will also launch the annual empowerment report which comes from the assessment of empowerment implementation report.

Ms Beng’I explained further that the report is implementing by various stakeholders and they will hand over awards for those who did better as a stepping stone to foster the government agenda on the empowerment policy to ordinary people.

She added that the council has invited more than 300 stakeholders from private and public sector and other development partners, NGOs, Research Institutes and Universities to attend the workshop.
Ms Issa noted that they signed an agreement with Tanzania Standard Newspaper (TSN) in the process of promoting and educating process to the public about the pros and cons on the empowerment policy and implementation plans to the public.

On his part, the Managing Editor of TSN, Dr Jim Yonazi said that the government newspapers is ready to work shoulder to shoulder with council to achieve the government targets and goals in ensuring ordinary people are economic empowered while the fifth phase government reached its target on green industrial revolution.

“We have re-organized to ensure that will walk on the government/Presidents talks to meet the industrial economy country’s by informing and educating people about the existing opportunities that the government is providing,” Dr Yonazi added.

The symposium is taking place every year under the council and it comes from the coordination of the empowering ordinary people from the Ministry, department, local government authorities, districts and the private sector, while it was officially launched February 9, last year by the Premier.

The directives has always fueling the coordination and implementation of the national policy on the empowering ordinary people economical in the private sector by creating a council of empowering people and coordinators in the ministries,  26 regions and all 185  municipalities across the country.  


Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam 
                
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la pili la Uwezeshaji  wananchi kiuchumi litakalofanyika Juni 10, 2017 mjini Dodoma ambalo litazileta pamoja sekta ya umma na binafsi kujadili suala la uwezeshaji kama njia ya kuongeza chachu ya uwezeshaji na kufikia uchumi wa viwanda.
Image result for majaliwa kassim majaliwa
Mh. Waziri Mkuu Ndugu, Kassim Majaliwa Kassim
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’I Issa alisema hayo wakati akizungumza na wanandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuwa kongamano hilo litawaleta pamoja sekta ya umma na binafsi kujadili masuala ya uwezeshaji kama njia ya kuongeza chachu ya u wezeshaji wananchi kiuchumi na kufikia uchumi wa viwanda.

“Kongamano hili linalenga kupata michango kutoka kwa wadau sekta hizo na hii itasaidia katika kuongeza chachu ya utekelezaji masuala ya uwezeshaji wananchi Kiuchumi,”.Kongamano hilo ni la siku moja lenye kauli mbiu isemayo Wezesha Watanzania Kushiriki Uchumi wa Viwanda, aliongeza kusema ,Bi.Issa.

Alisema kongamano hilo la pili lina malengo mbalimbali yakiwemo ya kukutanisha wadau wa sekta ya umma na binafsi kujadili masuala hayo, kupokea ripoti ya utekelezaji wa uratibu wa masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ngazi ya taifa na pia waziri Mkuu atakuwa Mwenyekiti wa Kongamano hilo.

Malengo mengine ni kutambua wizara, Idara, Taasisi, Serikali za Mikoa na Wilaya nchini zilizofanya vizuri katika kuratibu masuala ya uwezeshaji katika maeneo yao, kuchochea kasi ya utekelezaji wa mikakati ya uwezeshaji wananchi kiuchumi na kujifunza kutoka kwa wadau mbalimbali namna bora zaidi ya kusukuma mbele gurudumu la uwezeshaji. 

Kongamano hilo pia litawezesha wananchi kujifunza na kujitambua kupitia wengine waliofanya vizuri, na pia  Waziri Mkuu atazindua taarifa ya uwezeshaji ya mwaka ambayo inatokana na tathimini ya utekelezaji uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Bi. Beng’I alifafanua kwamba taarifa hiyo inatekelezwa na wadau mbalimbali na atatoa zawadi kwa washindi waliofanya vizuri katika kupeleka mbele ajenda ya uwezeshaji kutoka makundi ya wizara, Idara, na taasisi za umma, mikoa, sekta binafsi na mifuko ya uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

Pia alisema baraza limealika wadau 300 toka sekta ya umma na binafsi, wadau wa maendeleo, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, tasisi za utafiti na elimu ya juu kushiriki kongamano hilo.

Bi. Issa pia alisaini Makubaliano na Kampuni ya Magazeti ya Tanzania Standard Newspaper (TSN) katika kuhamasisha na uelimishaji umma kuhusu uwezeshaji wananchi kiuchumi na katika kongamano hilo watafanya kazi pamoja.

Naye Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya TSN, Dk. Jim Yonazi alisema magazeti ya serikali yatafanya kazi kubwa ya kuelimisha wananchi katika kushiriki  uchumi unaokusudiwa na serikali ya awamu ya tano yenye dhamira uchumi wa viwanda.

”Tumejipanga kuhakikisha shughuli hii inafanikiwa na hii ni fursa nzuri kwetu kuwafikishia wananchi taarifa sahihi na kwa wakati ili wazitumie,” na kwa kufanya hiyo itasaidia kukuza uchumi wao na uchumi wa taifa,aliongeza kusema,Dk. Yonazi.

 Kongamano hilo hufanyika kila mwaka mara moja chini ya baraza hilo na limetokana na mwongozo wa uratibu wa masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi katika Wizara, idara za umma, serikali za mikoa na wilaya na sekta binafsi nchini. Pia ulizinduliwa rasmi Feburuary 9, 2016 na waziri Mkuu Kassim Majawaliwa.

Mwongozo huu umekuwa kichocheo cha uratibu utekelezaji wa sera ya Taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi katika sekta ya umma kwa kuwezesha kuundwa kamati ya uwezeshaji na uteuzi wa waratibu katika wizara mikoa 26 na halmashauri zote 185 nchini.

Ofisa wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah (kushoto) akimkabidhi mpira wa miguu mmoja wa viongozi wa michezo wa Shule ya Msingi Wailes kwa ajili ya shule hiyo. Mpira huo umetolewa na Benki ya NMB kama zawadi kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes mara baada ya elimu ya masuala ya fedha na akiba iliyotolewa na benki hiyo. Wa kwanza kusho to ni Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Msingi Wailes, Zabibu Wasia akishuhudia


Ofisa wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah (kushoto) akitoa elimu ya masuala ya kifedha na akiba kwa wazazi na wanafunzi walioshiriki mafunzo ya programu ya wajibu ya NMB katika Shule ya Msingi Wailes ya jijini Dar es Salaam.



Mmoja wa wachezaji vijana (kulia) wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Azam kupitia kituo chao cha michezo akimkabidhi mpira wa pete mmoja wa viongozi wa michezo wa Shule ya Msingi Wailes kwa ajili ya shule hiyo. Mpira huo umetolewa na Benki ya NMB kama zawadi kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes mara baada ya elimu ya masuala ya fedha na akiba iliyotolewa na benki hiyo.


Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes akijibu swali kwenye mafunzo ya programu ya wajibu iliyotolewa na Benki ya NMB shuleni hapo.



Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes akijibu swali kwenye mafunzo ya programu ya wajibu iliyotolewa na Benki ya NMB shuleni hapo.


BENKI ya NMB imetoa elimu ya masuala ya kibenki na umuhimu wa kujijengea utamaduni wa uwekaji akiba kwa wanafunzi na baadhi ya wazazi wa Shule ya Msingi Wailes iliyopo Temeke jijini Dar es Salaam. Akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes walioshiriki mafunzo hayo ya kifedha, Ofisa wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah alisema NMB inaendelea kutoa elimu ya masuala ya kifedha ikiwa ni pamoja na kujifunza mbinu za kuweka akiba kwa ajili ya maisha ya baadae. Alisema elimu hiyo inatolewa kupitia Programu maalum ya Wajibu ambayo hutoa fursa kwa watoto, vijana na wazazi kujifunza masuala ya kifedha ili kumjengea mtoto utamaduni wa kujiwekea akiba, elimu ambayo watoto wengi hawapati fursa ya kujifunza. 

Akizungumza katika mafunzo hayo, alisema vijana wengi wamekuwa hawana utaratibu wa kujiweka akiba tangu wadogo hivyo NMB kupitia programu ya Wajibu inaendelea kutoa elimu kwa watoto, vijana pamoja na wazazi wao kuelewa umuhimu wa kujiwekea akiba ya fedha kupitia akaunti mbali mbali za benki hiyo, kama vile Mtoto Account, Chipukizi Account na Mwanachuo Account. NMB katika ziara hiyo ambapo ilikuwa imeongozana na wachezaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Azam kupitia kituo chao cha michezo, mbali na anafunzi na wazazi kupata elimu ya masuala ya kifedha na uwekaji akiba kwa manufaa ya baadaye, wachezaji wa Azam walicheza mpira na wanafunzi hao pamoja na kugawa zawadi mbalimbali toka NMB na kampuni ya Azam.  



Picha ya pamoja ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes na wageni wao baada ya mafunzo ya programu ya wajibu iliyotolewa na Benki ya NMB.


Ofisa wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah (kushoto) akimkabidhi zawadi mmoja wa wazazi wa wanafunzi walioshiriki mafunzo ya programu ya wajibu ya NMB.


Ofisa wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah (kulia) akimkabidhi moja ya zawadi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes baada ya kujibu vizuri swali kwenye mafunzo ya programu ya wajibu. Akifafanua zaidi, Bi. Latifa alisema elimu hiyo ni mwendelezo wa programu ya wajibu ambapo NMB imekuwa akizunguka katika shule mbalimbali za msingi na sekondari nchi nzima huku ikitoa elimu ya kifedha na masuala mazima ya uwekaji akiba. Alisema elimu hiyo itawasaidia watoto na vijana kufanya matumizi mazuri ya fedha kwa sasa na baadae, elimu ambayo wengi wameikosa. Alisema elimu hiyo ambayo imepokelewa vizuri kwa wanafunzi na wazazi ambao wameshiriki itaendelea kutolewa na benki hiyo hivyo kuwashauri wazazi na vijana kufungua akaunti mbalimbali ya NMB kulingana na maitaji yao ili waweze kunufaika. 

"...Mwitikio kwa waliopata fursa ya kushiriki katika mafunzo haya ni mzuri kwa kwli hasa katika wilaya yetu ya Temeke, tumekuwa tukipokea watoto mbalimbali wakija kufungua akaunti jambo ambalo linaonesha wamevutiwa na elimu hii," alisema ofisa huyo wa Benki ya NMB Tawi la Temeke. Naye Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Msingi Wailes, Zabibu Wasia aliishukuru Benki ya NMB kwa kutoa mafunzo hayo kwa wanafunzi pamoja na baadhi ya wazazi/walezi wa shule hiyo na kuahidi kuendelea kuwa mabalozi kueneza elimu hiyo kwa wengine kutokana na umuhimu wake.

 "..Tunaishukuru sana NMB kwa kuamua kuleta elimu hiyo kwa wanafunzi na wazazi wa Wailes tunaamini hii ni fursa ya kipekee kwetu maana shule za msingi Dar es Salaam zipo nyingi lakini umeona muanze na sisi...tunashukuru sana kwa kutupendelea," alisema Bi. Wasia. Mbali na elimu hiyo NMB ilitoa mipira miwili kama zawadi kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes, yaani mpira wa miguu kwa wanafunzi wa kiume na mpira wa pete kwa wanafunzi wa kike.  

Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes akijibu swali kwenye mafunzo ya programu ya wajibu iliyotolewa na Benki ya NMB shuleni hapo.



Baadhi ya wachezaji vijana wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Azam kupitia kituo chao cha michezo wakiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes.

Ofisa wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah (kulia) akitoa elimu ya masuala ya kifedha na akiba kwa wazazi na wanafunzi walioshiriki mafunzo ya programu ya wajibu ya NMB katika Shule ya Msingi Wailes ya jijini Dar es Salaam.


Mmoja wa wachezaji vijana (kulia) wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Azam akipiga mpira alipokuwa akicheza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes ya jijini Dar es Salaam.

Umoja wa Mataifa nchini umeendelea na hekaheka za ufundishaji wa machampioni wa kusaidia kueneza malengo 17 ya dunia yanayohusu maendeleo endelevu. Miongoni mwa mambo yaliyofanywa siku ya pili ya ziara ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kwa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha ni kuendelea kwa mkutano wa vijana unaoakisi Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini Arusha , na kuoongoza kampeni ya elimu ya maendeleo endelevu katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU). Akiwa MoCU Rodriguez aliwataka vijana kujikita katika kuyaelewa malengo ya dunia na kuyafanyia kazi.


Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa akiitambulisha meza kuu kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) wakati wa kutoa uelewa juu ya malengo ya dunia chuoni hapo.

Akifafanua mchango wa vijana katika kufanikisha malengo hayo, Matibu huyo alisema: “Mchango wa vijana ni muhimu katika kufanikisha malengo endelevu kufika mwaka 2030; hivyo ni vyema kila kijana akafahamu na kuwafundisha vijana wenzie malengo hayo muhimu.” Septemba 2015, wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa walikubaliana juu ya malengo mapya ya dunia, malengo ya maendeleo endelevu. Malengo hayo yanatarajiwa kufanyiwa kazi katika kipindi cha miaka 15 ijayo na kuleta mabadiliko makubwa katika jamii, uchumi na mazingira kwa namna ya kuwa endelevu. Wakati Umoja wa Mataifa (UN) mwaka jana ukiadhimisha miaka 71 tangu kuanzishwa kwake, Mratibu huyo wa mashirika ya Umoja wa Mataifa aliahidi kuwatumia vijana katika utekelezaji wa malengo yake 17 ya maendeleo kutokana na idadi yao kubwa kubwa zaidi ya asilimia 67 na pia kwa kuwa wao ndio wanaobeba hali ya baadaye ya nchi hii.


Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza juu ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) walioshiriki semina ya uelewa wa malengo hayo 17 ya dunia iliyofanyika chuoni hapo.

Aidha alisema ili kufanikisha hilo, UN pamoja na mashirika mengine itatoa mafunzo ya vitendo kwa vijana zaidi ya 50,000 ifikapo mwaka 2017 ambao wataingizwa katika mpango wa utekelezaji wa malengo hayo. "UN itaendelea kushirikiana na vijana pia itatoa elimu ya vitendo.Hadi sasa vijana zaidi ya elfu 20,000 wamepewa mafunzo na wanatambua malengo hayo, na kwamba UN na wadau wengine wanatarajia kufundisha vijana zaidi ya 50, 000 ifikapo mwaka 2017, ili ifikapo 2030 vijana wengi wawe wanajua malengo hayo na namna ya kuyatekeleza," alisema.

Ofisa wa dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ngusekela Karen Nyerere akitoa neno kwa wanafunzi wa MoCU wakati wa semina ya uelewa wa Malengo ya Dunia iliyofanyika chuoni hapo.

Amesema miongoni mwa mafunzo yatakayotolewa kwa vijana hao ni pamoja na jinsi ya kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu na jinsi ya vijana watakavyoweza kujiajiri. Akiwa Moshi jana, alizungumza na wanachuo na wahadhiri ambapo katika chuo hicho cha MoCU 460 walipatiwa mafunzo na pia walimhoji mambo mbalimbali yanayohusu Umoja wa Mataifa na malengo ya dunia ya maendeleo endelevu. Kwa mafunzo yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha Umoja wa Mataifa ulifua vijana 50 ambao ni machampioni.




Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akisisitiza jambo kwa wanafunzi wa MoCU wakati wa semina ya uelewa wa malengo ya dunia iliyofanyika chuoni hapo.

Aidha idadi ya vijana waliofikiwa na mafunzo hayo kwa kuambukizana wameongezeka na kufikia zaidi ya elfu 20. Tangu kuzinduliwa kwa kampeni hiyo na mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez, mwaka jana vijana zaidi wamepata elimu katika maeneo yao kwa kupitia machampioni wa malengo. Kwa sasa Tanzania imehusisha malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) kwenye mpango wa maendeleo wa miaka mitano.


Picha juu na chini ni wanafunzi na walimu MoCU walioshiriki semina ya uelewa wa malengo ya dunia iliyoendeshwa na Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini chuoni hapo.





Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akibadilishana mawazo na Eng. Salvatory Matemu kutoka Ofisi ya RC Kilimanjaro huku Ofisa wa dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ngusekela Karen Nyerere (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Rasilimali watu MoCU, Daud Massambu wakielekea kwenye zoezi la picha ya pamoja.


Picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa MoCU.



Picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa MoCU.



Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa UN Chapter MoCU, Isaac Evarist (kushoto) pamoja na wanafunzi chuoni hicho.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwapiga msasa machapioni wa malengo ya dunia katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha.

Mmoja wa machampioni akipitia kipeperushi kinachoelezea kwa kina malengo 17 ya dunia wakati wa mafunzo yaliyoendeshwa na Mratibu Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (hayupo pichani).


Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akisikiliza swali kwa umakini kutoka kwa Waziri wa Habari wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha, John Semindu wakati wa mafunzo kwa machampioni wa SDGs chuoni hapo.

Mmoja wa machampioni wa Makumira akiuliza swali kwa Mratibu wa Mashirika ya UN nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).






Picha juu na chini ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akikabidhi vyeti kwa machampioni wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha na Taasisi ya Uhasibu ya Arusha (Institute of Accountancy Arusha -IAA) walioshiriki mafunzo hayo.




Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa akimuelekeza jambo mmoja wa machampioni wa malengo ya dunia wakati wa mafunzo yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha



Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na baadhi ya machampioni wa malengo ya dunia chuoni hapo.

Vyombo vya habari nchini hususani redio za kijamii zimetakiwa kuandika habari ambazo zinaelezea changamoto ambazo zinawakabili wananchi katika maisha yao ya kila siku na jinsi ambavyo wanaweza kuzitatua. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii. Alisema wanahabari na vyombo vya habari ni muhimu nchini kwa maendeleo ya Taifa lakini kama wasipokuwa makini katika utendaji wao wa kazi kunaweza kuwa na madhara makubwa hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanazingatia maadili ya uandishi wa habari.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa kwanza kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia) kabla ya kufungua mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.

Alisema sehemu kubwa ya wananchi ambao wanaishi vijijini hawapati taarifa muhimu zinazohusu maendeleo yao zikiwepo taarifa za kilimo, afya, mazingira na haki za kibadamu hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanaandika habari ambazo wananchi wamekuwa hawazipati kwa muda mrefu. “Ni jukumu lenu sasa kuhakikisha redio hizo zinatimiza malengo yake hususani katika kumuelimisha wanajamii, kuwajengea uwezo wa kutambua na kupambana na mazingira ili kuinua hali zao za kimaisha,” Mhe. alisema Wambura. Alisema mafunzo hiyo ni muhimu kwao kama wawakilishi wa redio za kijamii sababu itawapa mbinu ambazo wanaweza kuzitumia ili waweze kujisimamia wao wenyewe bila kuwa tegemezi kwa kuomba fedha kutoka sehemu zingine.



Picha juu na chini ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura akisoma hotuba ya kufungua mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.

 “Natambua changamoto zilizopo katika uendeshaji wa redio za kijamii ambazo ni kama upatikanji wa habari endelevu na zinazolingana na mahitaji ya jamii husika, uhaba wa rasilimali fedha za kuendeshea redio husika, na udhaifu katika usimamizi stahiki wa taasisi hizo lakini kwa hakika mafunzo haya ni muhimu kwa vile yanalenga kutatua changamoto hizo,” alisema Wambura. Aidha Naibu Waziri Wambura amewashukuru Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kutoa mafunzo hayo ambayo yatasaidia kujenga Taifa lenye waandishi na wasimamizi wa habari wenye weledi na kazi zao pia mafunzo hayo yanakwenda sambamba na dira ya wizara ya kuwa na Taifa lililohabarishwa vizuri ifikapo 2025.
  Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida amesema mafunzo hayo yamekuja baada ya kufanyika utafiti mwaka 2014 kwa ufadhili wa UNDP, utafiti ambao ulifanyika kwenye wilaya tano nchini na kugundua kuwa njia bora ya upashaji habari katika maeneo hayo ni kwa kutumia redio. Amesema baada ya matokeo hayo ya utafiti walipendekeza kuanzishwa kwa redio jamii katika maeneo ambayo utafiti ulifanyika ili kurahisisha taarifa mbalimbali za kuelimisha wananchi ambazo zitakuwa chachu kubwa ya maendeleo kuwafikia wananchi kwa urahisi.



Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho katika mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.[/caption]

“ESRF kwa ufadhili wa UNDP ilisimamia uanzishwaji wa redio jamii nne ambazo ni Redio Unyanja (Nyasa), Redio Bunda (Bunda), Redio Kagera (Bukoba Vijijini) na Redio Ileje (Ileje) na redio zingine mbili Redio Sengerema (Sengerema) na Redio Mazingira (Bunda) zilipata misaada mbalimbali kwa ajili ya kujiendesha,” alisema Dk. Kida. Mafunzo hayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii kutoka wilaya tano nchini ambazo ni Ileje, Bukoba Vijijini, Bunda, Nyasa na Sengerema pamoja na wawakilishi wa halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.


Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Bi. Margareth Nzuki akitoa taarifa kwa washiriki wa mafunzo kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Sehemu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya umma –SJMC), Dotto Kuhenga akitoa mafunzo kwa washiriki kuhusu redio jamii na jinsi zinavyotakiwa kufanya kazi.

Picha juu na chini ni Mtaalamu wamasuala ya Tehama kutoka ESRF, Joseph Ngonyani akitoa mafunzo kwa washiriki jinsi wanavyoweza kutumia mitandao kuapata taarifa ambazo wanaweza kuzitumia kwenye redio zao.




Baadhi ya washiriki wa mafunzo kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini.

 



Washiriki wa mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini wakiwa kwenye picha ya pamoja.[/caption]

Wasichana 8,000 waliopo shuleni na 600 ambao hawako shuleni watanufaika na mradi mkubwa wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupata elimu. Mradi huo wa miaka minne wenye gharama ya dola za Marekani milioni 5 utafanyika katika wilaya tano nchini. Wilaya hizo ni Ngorongoro, Kasulu, Sengerema, Micheweni na Mkoani. Mradi huo ambao upo hatua ya pili umeanza kwa kongamano lililofunguliwa jana na Katibu Mkuu wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dk Leonard Akwilapo.


Mgeni rasmi kwenye kongamano hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt Leonard Akwilapo akifungua rasmi kongamano la viongozi mbalimbali wa wizara na wilaya tano nchini kujadili na kupanga mikakati ya namna bora ya kuwawezesha wasichana na wanawake vijana katika wilaya husika kupata elimu katika kipindi cha miaka minne ijayo. 

Mradi huo mkubwa kwa mujibu wa Katibu mkuu huyo umelenga kuwaokoa wanafunzi kabla hawajakumbwa na matatizo yanayokatisha masomo yao. Aidha utawapa fursa za kuboresha zaidi mafunzo mbalimbali waliyonayo ambao utawafanya kuwa watu wazuri zaidi katika jamii na hivyo kuchangia maendeleo ya taifa na jamii walizopo. Katibu mkuu huyo ambaye alifungua kongamano na kuzindua mradi huoi awamu ya pili alisema kwamba ni matumaini yake kwamba jamii itaukumbatia mradi huo ili kuwa na taifa lenye mafanikio makubwa katika malengo ya maendeleo endelevu ya dunia kwa kuzingatia lengo namba tano.
  Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akitoa neno la ufunguzi katika kongamano la viongozi mbalimbali wa wizara na wilaya tano nchini kujadili na kupanga mikakati ya namna bora ya kuwawezesha wasichana na wanawake vijana katika wilaya husika kupata elimu katika kipindi cha miaka minne ijayo.

 Amewataka wazazi na vijana kutimiza wajibu wao kwa kubadilika kitabia na kutambua umuhimu wa elimu katika kufanikisha wanachotaka ambacho ni maendeleo binafsi , familia na taifa kwa ujumla. Katika hotuba yake alisema ni matumaini kwamba wadau katika mradi huo watafaikisha katika kipindi cha miaka minne mipango yote iliyolenga kuboresha huduma kwa wasichana na wanawake vijana, kushawishi jamii kubadilika na kuachana na tamaduni mbaya kama ndoa za utotoni na ukeketaji. Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na utamaduni UNESCO, Zulmira Rodrigues alisema mradi huo ulioanza mwaka jana na kufanyiwa tathmini umeonesha changamoto kubwa ya watoto wa kike ikiwamo mimba za utotoni,ukeketaji na kushindwa masomo.


Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la misaada Korea International Cooperation Agency (KOICA) nchini, Joonsung Park akitoa neon kuhusu ufadhili wa KOICA ambao imeutoa katika mradi huo na mipango yao ya kusaidia Tanzania.

Alisema lengo la mradi ni kuhakikisha kwamba mwanamke anapata fursa za kupambana katika mazingira yake kama anavyofanya mwanaume kwa kuwezeshwa na kuzuia mila, tabia na tamaduniu mbaya ambazo zinakwamisha uwezo wake wa kuhudhuria masomo. Aidha alisema mradi huo utatoa nafasi kwa wanawake vijana ambao wamekosa masomo au wameacha masomo au hawakwenda shule kabisa kupata nafasi ya kusoma. Mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la kimataifa la misaada la Korea (KOICA) kupitia UNESCO na kufanyiwa kazi pia na mashirika ya UN Women na UNFPA unaangalia namna bora ya kukabiliana na changamoto za mabinti wanaokwenda shule katika wilaya hizo ili kuwawezesha kuwa watu bora katika jamii siku za usoni.


Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA) nchini, Dk. Hashina Begum akitoa neno kwa niaba ya UNFPA.

Mradi huo ni sehemu ya mradi wa Global Initiative unaoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, sayansi na Utamaduni (UNESCO), Shirika la Mpango wa watu (UNFPA) na Shirika la Umoja wa mataifa la wanawake(UN Women) wa kuwawezesha wanawake kupitia elimu uliozinduliwa katika nchi sita duniani. Awamu ya kwanza ya mradi huo umelenga kufanywa katika nchi tatu za Mali, Nepal na Tanzania na ulitiwa saini mwaka jana, 2016. Katika mradi huo serikali ya Tanzania inawakilishwa na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi; Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; na Wizara ya Katiba na Sheria ambayo ikiratibu mradi kwa niaba ya serikali ya Tanzania.

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) Tanzania, Bi. Hodan Addou akitoa neno kwa niaba ya UN Women.

Aidha UNESCO inatekeleza mradi huo kwa kushirikiana na UNFPA na UN Women. Katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa KOICA Tanzania, Joosung Park pia alizungumza umuhimu wa kufundisha watoto wa kike na kuwapa fursa na kusema kwamba unapofunza wanawake unafunza taifa huku akisema kwamba wazazi wanahusika sana katika hilo akitolea mfano waziri wa mambo ya nje wa Korea wa sasa ambaye ni mwanamke kwa mara ya kwanza katika miaka mingi ya historia ya nchi hiyo. Mzungumzaji mwingine ni ambaye alikuwa Mwakilishi wa UNFPA Tanzania, Dk Hashina Begum alitaka jamii kuhakikisha kwamba inatoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana ili kuzuia uzazi usiokuwa na mpango ambao unakwamisha maendeleo.


Anna Holmström kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) akitoa maelezo kuhusu mradi huo kwa washiriki waliohudhuria kongamano hilo.


Picha juu na chini ni Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo.




Washiriki wa kongamano la viongozi mbalimbali wa wizara na wilaya tano nchini kujadili na kupanga mikakati ya namna bora ya kuwawezesha wasichana na wanawake vijana katika wilaya husika kupata elimu katika kipindi cha miaka minne ijayo wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.