RAIS na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Jakaya
Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ) kuanzia Septemba 21.
Katika vyeo vipya hivyo ni pamoja na cheo kimoja cha Luteni Jenerali, Meja Jenerali 15 na Brigedia Jenerali 33.
Akizungumza
Makao Makuu ya Jeshi muda mfupi kabla ya kuwavisha cheo kipya maofisa
hao, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange alisema:
“Rais amempandisha cheo Meja Jenerali Samuel Ndomba kuwa Luteni
Jenerali”.
Rais pia amemteua Luteni Jenerali Ndomba kuwa Mnadhimu
Mkuu wa JWTZ kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali
Abdulrahman Shimbo aliyestaafu utumishi jeshini kwa umri Septemba 21.
Kwa
mujibu wa kanuni na sheria za Majeshi katika Juzuu la kwanza (Utawala)
Jenerali Mwamunyange alimvisha cheo cha Luteni Jenerali, Ndomba kwa
niaba ya Rais na Amir Jeshi Mkuu. Kabla ya uteuzi huo mpya, Luteni
Jenerali Ndomba alikuwa Mkuu wa Jeshi la KujengaTaifa (JKT).
Katika
hafla hiyo fupi, Jenerali Mwamunyange alisema kuwa Rais Kikwete
alimpandisha cheo Brigedia Jenerali Rafael Muhuga kuwa Meja Jenerali
kuanzia Septemba 21 na kumteua kuwa Mkuu mpya wa JKT.
Kabla ya
madaraka hayo mapya, Meja Jenerali Muhuga alikuwa Mkuu wa Utawala wa JKT
na amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Ndomba. Jenerali
Mwamunyange alimvisha cheo hicho kipya kwa niaba ya Rais na Amir Jeshi
Mkuu.
Wakati huo huo, makamanda wengine waliopandishwa vyeo
kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali wakiwamo maofisa
wanawake; Grace Mwakipunda ambaye kwa sasa ni Kaimu Mkuu wa Utumishi
Jeshini na Lilian Kingazi ambaye ni Mkurugenzi wa Utumishi Jeshini.
Wengine ni Farah Mohamed, Kevin Msemwa, Patrick Mlowezi, Charles
Jitenga, Charles Mzanila na Daniel Igoti.
Makamanda wengine ni Vincent Mritaba, Ipanda Ipanda, Adam Mwabulanga, Ezekiel Kyunga, Projest Rwegasira na Juma Kapwani.
Aidha,
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi aliwavisha vyeo vipya makamanda 33 waliokuwa
na cheo cha Kanali kuwa Brigedia Jenerali ambao ni Pellegrin Mrope,
Ryakitimbo Ryakitimbo, Mimy Abdallah, John Chacha, Ezira Ndimbwambo na
Augostino Gailanga.
Wengine ni Gaudence Milanzi, Masumbuko
Mndeme, Daniel Laswai, Sarah Rwambali, Mathew Sukambi, Narcis Lubamba,
Mwapipo Kyalaliko, O. S. Mateka na Jairo Mwaseba.
Mabrigedia
Jenerali wengine ni Abdullah Mwenjudi, Cosmas Kayombo, Honoratus Lyamba,
Ramadhani Kimweri, Nicodem Mwangela, Abbas Mnyani, R.A. Rukyaa, Elias
Athanas, Fabiani Mangore, George Mashamba, Zoma Kongo, Harison
Masebo, Paul Masao, Clemence Kahama, Jacob Mohamed, Mbazi
Msuya, Alfred Kapinga na George Ingrim.
Akitoa neno la shukurani
kwa niaba ya makamanda wenzake wa ngazi za juu waliopandishwa vyeo,
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Ndomba alimweleza Mkuu wa Majeshi
kuwa kwa pamoja walitambua majukumu yaliyo mbele yao na aliahidi kuwa
watayatekeleza kikamilifu.
Post a Comment