KAMATI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi imeyaondoa majina ya wabunge wote
waliokuwa wanawania nafasi mbalimbali za uongozi katika chama hicho
waliokuwa wameunga mkono azimio la kumng’oa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
kama mawaziri wasingejiuzulu.
Chanzo
cha habari kilichoomba kutoandikwa jina kilisema kazi kubwa ambayo
imefanywa na Kamati ya Usalama na Maadili ya Chama hicho iliungwa mkono
na CC huku wajumbe wa vikao hivyo viwili wakimpongeza Rais Kikwete kwa
kufanya uamuzi mgumu.
Inadaiwa Kamati
ilikata majina yote ya wabunge waliowania nafasi hiyo, ambao walihusika
katika utiaji saini “Azimio la kumn’goa Waziri Mkuu”, Mizengo Pinda
lililoanzishwa katika kikao kilichopita cha Bunge na Mbunge wa Kigoma
Kaskazini Kabwe Zitto, endapo hakungefanyika marekebisho ya Baraza
Mawaziri.
Wabunge hao walisaini fomu
maalumu iliyolenga Pinda kuwaondoa mawaziri ambao wizara zao zilitajwa
katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na
Kamati za Bunge ambapo ilikuwa ikihitajika sahihi za wabunge 70.
Wabunge
hao ni Nimrod Mkono ambaye ni Mbunge wa Musoma Vijijini ambaye anawania
nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa; Mbunge wa Ludewa, Deo
Filikunjombe ambaye anagombea ujumbe wa NEC kupitia Wilaya ya Ludewa.
Kwa
mujibu wa wabunge hao, walikuwa wakishinikiza kuondolewa kwa Waziri wa
Uchukuzi, Omari Nundu, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Mkuchika, Naibu Waziri
wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu na Waziri wa Viwanda na
biashara, Cyril Chami.
Habari hizo
zilidai kuwa walioenguliwa na Kamati Kuu ambao pia Kamati ya Maadili
ilipendekeza waenguliwe, yumo Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina aliyekuwa
akiwania uenyekiti wa Mkoa wa Simiyu, Mbunge wa Kahama, James Lembeli na
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja ambao wote walikuwa
wakiwania uenyekiti wa mkoa wa Shinyanga.
Wengine
walioenguliwa na CC ni Mbunge wa Nzega, Dkt. Khamis Kigwangallah na
kada maarufu wa CCM, Hussein Bashe, ambao wote walikuwa wakiwania ujumbe
wa NEC kupitia wilaya ya Nzega. Pia Mbunge wa Viti Maalum, Sara Msafiri
ambaye alikuwa akiwania ujumbe wa NEC na Mbunge wa Viti Maalumu, Munde
Tambwe ambaye alikuwa akiwania uenyekiti wa Umoja wa Wanawake, mkoa wa
Tabora.
Habari
hizo zilisema sababu ya kuondolewa kwa wabunge Munde na Sara ni kutokana
na kashfa ya rushwa kwa wabunge inayoendelea kuchunguzwa na Kamati ya
Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Vick Swai ambaye alikuwa akitetea nafasi yake. Katika
Jumuiya ya Vijana (UVCCM), walioenguliwa ni pamoja na Mwenyekiti wa
UVCCM Mkoa wa Dodoma, Anthony Mavunde, Mbunge wa Ilala Musa Azzan
‘Zungu’ aliyekuwa akiwania uenyekiti Wazazi.
“Wengi
walioondolewa kwa kuwa wengi wao ni mizizi ya ufisadi, na kwa kuwa
ukishaondoa mizizi unabaki mti lazima mti ukauke, tuliona hakuna haja ya
kuleta kishindo kikubwa kwa kuondoa waliotajwa sana kwa ufisadi, ila
matokeo mtayaona baadaye,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo via wavuti
Post a Comment