Ndugu wanahabari,
Kufuatia hali tete
inayowakabili watetezi wa haki nchini Tanzania, mtandao wa Watetezi wa
Haki za Bidamu Tanzania (THRD) umeamua kuwakutanisha wadau muhimu katika
utetezi wa haki za binadamu, asasi mbali mbali za kiraia na viongozi wa
dini ilikujadili namna ya kuzuia wimbi la vitendo vya kikatili na
ugandamizaji wa haki za binadamu kwa ujumla.
Ni kwa kuzingatia muktadha huu Mtandao wa Watetezi umeandaa kongamano la siku moja litakalojadili
hali ya haki za binadamu nchini Tanzania, uhuru wa kupata habari na
tishio la usalama kwa watetezi wa haki za bindamu litakalofanyika katika
viwanja vya Mtandao wa Jinsia (TGNP) Mabibo Dar
es Salaam siku ya Jumatano tarehe 12 Septemba, 2012 kuanzia saa 4:00
mpaka saa 7:00 mchana.
Kongamano hilo linakuja
wakati familia nyingi wakiwamo akina mama na watoto wakiwa hawajui
maisha yao ya baadaye yatakuwaje baada ya kufiwa na wapendwa wao
wakiwamo wazazi ambao bado walikuwa wanahitajika katika malezi ya
familia zao.
Matukio ya hivi karibuni kabisa yamewahusisha
mashabiki na wapenzi wa chama kikuu cha upinzani kwa sasa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo kwa upande mmoja na Jeshi la Polisi kwa upande
mwingine.
Ipo hatari ya wazazi kuanza kuwazuia watoto wao
wasihudhurie kabisa mikutano ya chama hicho, lakini kwa upande mwingine
ipo hatari ya wanachi kupoteza imani na Jeshi la Polisi ambalo kimsingi
linawajibu mkubwa wa kulinda usalama wa raia na mali zao. Na zaidi ya
hayo iwapo watu wataanza kuamini kwamba jeshi hilo linatumika kisiasa
basi ipo hatari ya kuibuka kwa vyombo vingine vitakavyojivisha jukumu la
kuwalinda Watanzania na mali zao.
Kwa lengo jema la kurudisha
imani ya wananchi kwa jeshi lao, kwa wanaharakati za binadamu kuendelea
kufanya kazi bila vitisho na kwa waandishi wa habari kuhakikishiwa
usalama wao kazini, wadau wote wakiwa ni wanazuoni katika fani za
habari, sheria, haki za bainadamu na walaji wote wa kazi za habari
wanaombwa kuhudhuria na kutoa michango ya mawazo yao.
Historia
inaonyesha kwamba kumekuwapo na mauaji yanayohusiha wanasiasa kama
ifuatvyo; Arusha katika sakata la kumpinga meya wa mji huo ambapo watu
watatu waliuawa, Igunga, Singida, Morogoro na tukio la hivi karibuni
kabisa la mauaji ya kinyama ya mwandishi wa habari wa televisheni ya
Channel Ten, Daudi Mwangosi.
Matukio mengine ni lile la kutekwa
kuteswa na kIsha kutelekezwa porini kwa Daktari Stephen Ulimboka
aliyekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za wagonjwa na madaktari,
na pia lipo tukio la kufungiwa kwa gazeti huru la uchunguzi la
Mwanahalisi.
Wote mnakaribishwa.
Imetolewa na sekretariati ya THRD,
ELIAS MHEGERA- 0754-826272
KAIMU MRATIBU.
WASEMAJI
1. MISA-TAN
2. TGNP
3. MCT
4. TEF
5. MOAT
6. LHRC
7. UTPC
8. Jenerali Ulimwengu (bado anatafutwa kwa hilo haja-confirm)
9. Prof Issa Shivji (bado anatafutwa haja-confirm)
Post a Comment