Picture
picha: uuldesign.com
Enzi zetu sisi ndoa zilikuwa hazivunjiki! Mimi na bibi yako tumekuwa tunagombana lakini usiku ilikuwa lazima tupatane! Tukiamka asubuhi tu wapya mapenzi yanaendelea kama vile hakuna lililotokea jana.

Pamoja na mapenzi ya dhati yasiyo angalia kitu kama yenu kitanda chetu cha kamba cha futi tatu kwa tano kimetufanya tumekuwa karibu sana! Tunagusana hata kama tumeudhiana, bibi yako anasikia harufu ya jasho langu na mimi nasikia la kwake, akiguna namskia akigeuka ananigusa, usiku kucha joto lake joto langu. Maisha yamekuwa ya raha mustarehe.

Nyie ndoa zenu hazidumu kwa sababu ya vitanda na sio wavumilivu, lakini wengi wenu mnaingia kwenye ndoa mkiwa tayari mmesha wahi kupenda sana watu wengine kuliko mlio waoa na hivyo inawawia vigumu kuwasahau kirahisi.

BABU HAPA KWENYE VITANDA PAKOJE?!

Nyie vitanda vyenu ni sita kwa sita, ama tano kwa sita! Hivi vinamkaribisha shetani! Mwenyezi mungu anasema "wawili wakishikamana yeye anakuwa kati yenu" vitanda vyenu vinavunja ndoa zenu!

Unakuta mmeudhiana, vitanda vyenu vya sita kwa sita wakati wa kulala mmoja yuko kule mwingine yuko huku katikati nafasi! Hapo katikati analala "shetani" upande wa kule mke anamuwaza mtu wake (john/ally) upande wa kule mume ana muwaza mtu wake (maria/asha), hawagusani, hawapeani joto, hawapeani harufu za kimahaba maana nafasi ya kitanda inawapa jeuri. Hata wakati wa kugeuka una weza kugeuka bila hata ya kumgusa mwenzako! Hili ni tatizo kwa ndoa, ndio maana mnaachana maana hamko pamoja na Mungu mnapo kuwa vitandani. Mnamruhusu shetani katikati yenu! (Hapa nikakumbuka kale ka mstari ka umombo kanako sema 'nearest is dearest')

Nakushauri mjukuu wangu! Kama unataka kuendelea kuishi na mkeo hadi uzee kama wangu achana na uleo! Haraka sana fanya hima ubadirishe kitanda.

** Haya yalikuwa ni masimulizi ya babu yangu mmoja niliyekwenda kumtembelea kijijjini kwetu Lushoto, pamoja na hayo nikagawa neno la mabadiliko, ameniambia hana hamu tena na ccm, ilibidi nimpatie kadi ya chadema na bendera atundike sehemu anayo otea jua**
ONYO: KITANDA CHA SITA KWA SITA NI HATARI KWA NDOA YAKO.

SHabari kwa msaada wa tovutiya wavuti
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.