Kwa mara ya kwanza serikali ya Kenya imekubali kutoa nyongeza ya asili
mia 300 kwa mishahara ya walimu ambao wamekuwa katika mgomo wa kitaifa
kwa wiki tatu sasa.
Kutokana
na maafikiano hayo kati ya serikali na chama cha walimu nchini KNUT,
sasa walimu wanatarajiwa kurejea kazini Jumatatu. Hatua hiyo sasa
itawapa afueni maelfu ya wanafunzi hususan wa shule za msingi na upili
za umma ambao hawajafunzwa wakati huu walimu walipokuwa mgomoni.
Vyama
vya walimu nchini Kenya KNUT na Kuppet vilikuwa vikishinikiza serikali
kuwalipa walimu nyongeza hiyo kwa awamu moja. Awali serikali ya Kenya
ilikuwa imekataa kutekeleza matakwa hayo na kuwataka walimu kukubali
kulipwa kwa awamu tatu, awamu ya kwanza ikitekelezwa Oktoba mwaka huu.
Mwalimu
wa chini aliyekuwa akipata shilingi 13,000 sasa atapata shilingi
39.000. Serikali ya Kenya imetenga zaidi ya dola 159 milioni kuwalipa
zaidi ya walimu 250,000 ambao walikuwa wakigoma kulalamikia mishahara
duni na mazingira mabaya ya kazi.
Post a Comment