Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam 
                
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la pili la Uwezeshaji  wananchi kiuchumi litakalofanyika Juni 10, 2017 mjini Dodoma ambalo litazileta pamoja sekta ya umma na binafsi kujadili suala la uwezeshaji kama njia ya kuongeza chachu ya uwezeshaji na kufikia uchumi wa viwanda.
Image result for majaliwa kassim majaliwa
Mh. Waziri Mkuu Ndugu, Kassim Majaliwa Kassim
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’I Issa alisema hayo wakati akizungumza na wanandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuwa kongamano hilo litawaleta pamoja sekta ya umma na binafsi kujadili masuala ya uwezeshaji kama njia ya kuongeza chachu ya u wezeshaji wananchi kiuchumi na kufikia uchumi wa viwanda.

“Kongamano hili linalenga kupata michango kutoka kwa wadau sekta hizo na hii itasaidia katika kuongeza chachu ya utekelezaji masuala ya uwezeshaji wananchi Kiuchumi,”.Kongamano hilo ni la siku moja lenye kauli mbiu isemayo Wezesha Watanzania Kushiriki Uchumi wa Viwanda, aliongeza kusema ,Bi.Issa.

Alisema kongamano hilo la pili lina malengo mbalimbali yakiwemo ya kukutanisha wadau wa sekta ya umma na binafsi kujadili masuala hayo, kupokea ripoti ya utekelezaji wa uratibu wa masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ngazi ya taifa na pia waziri Mkuu atakuwa Mwenyekiti wa Kongamano hilo.

Malengo mengine ni kutambua wizara, Idara, Taasisi, Serikali za Mikoa na Wilaya nchini zilizofanya vizuri katika kuratibu masuala ya uwezeshaji katika maeneo yao, kuchochea kasi ya utekelezaji wa mikakati ya uwezeshaji wananchi kiuchumi na kujifunza kutoka kwa wadau mbalimbali namna bora zaidi ya kusukuma mbele gurudumu la uwezeshaji. 

Kongamano hilo pia litawezesha wananchi kujifunza na kujitambua kupitia wengine waliofanya vizuri, na pia  Waziri Mkuu atazindua taarifa ya uwezeshaji ya mwaka ambayo inatokana na tathimini ya utekelezaji uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Bi. Beng’I alifafanua kwamba taarifa hiyo inatekelezwa na wadau mbalimbali na atatoa zawadi kwa washindi waliofanya vizuri katika kupeleka mbele ajenda ya uwezeshaji kutoka makundi ya wizara, Idara, na taasisi za umma, mikoa, sekta binafsi na mifuko ya uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

Pia alisema baraza limealika wadau 300 toka sekta ya umma na binafsi, wadau wa maendeleo, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, tasisi za utafiti na elimu ya juu kushiriki kongamano hilo.

Bi. Issa pia alisaini Makubaliano na Kampuni ya Magazeti ya Tanzania Standard Newspaper (TSN) katika kuhamasisha na uelimishaji umma kuhusu uwezeshaji wananchi kiuchumi na katika kongamano hilo watafanya kazi pamoja.

Naye Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya TSN, Dk. Jim Yonazi alisema magazeti ya serikali yatafanya kazi kubwa ya kuelimisha wananchi katika kushiriki  uchumi unaokusudiwa na serikali ya awamu ya tano yenye dhamira uchumi wa viwanda.

”Tumejipanga kuhakikisha shughuli hii inafanikiwa na hii ni fursa nzuri kwetu kuwafikishia wananchi taarifa sahihi na kwa wakati ili wazitumie,” na kwa kufanya hiyo itasaidia kukuza uchumi wao na uchumi wa taifa,aliongeza kusema,Dk. Yonazi.

 Kongamano hilo hufanyika kila mwaka mara moja chini ya baraza hilo na limetokana na mwongozo wa uratibu wa masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi katika Wizara, idara za umma, serikali za mikoa na wilaya na sekta binafsi nchini. Pia ulizinduliwa rasmi Feburuary 9, 2016 na waziri Mkuu Kassim Majawaliwa.

Mwongozo huu umekuwa kichocheo cha uratibu utekelezaji wa sera ya Taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi katika sekta ya umma kwa kuwezesha kuundwa kamati ya uwezeshaji na uteuzi wa waratibu katika wizara mikoa 26 na halmashauri zote 185 nchini.
Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.