Na Mwandishi Wetu 

January Makamba ambaye ni mbunge wa jimbo la Bumbuli na Naibu Waziri wa Sayansi na Mawasiliano ni kijana aliyepata bahati ya mtende hata kufikia hatua ya kumuondoa Mzee Shelukindo na kuwa Mbunge wa jimbo la Bumbuli, lakini leo kutoka sakafu ya moyo wangu, ninamuombea huyu mdogo wangu kheri ‘labda’ afanikiwe kuwa Rais wa Tanzania kwa hao waliozoea kumpa vyeo, lakini hawezi tena kuchagulika kuwa mbunge wa jimbo la Bumbuli.
 
January Yusuf Makamba, Naibu Waziri wa Sayansi na Mawasiliano na Mbunge wa Bumbuli CCM
Kilichomfikisha January mpaka kwenye hatua hiyo sio uwezo wa kufanya kazi sana bali ni kwa sababu ya promosheni ya kubebwa na Jk kutokana na uswahiba wa Baba yake Makamba, Mzee Yusuph Makamba na Jakaya Kikwete ambapo nyakati zote amekuwa akisikika akisema amemweka Rais Kikwete mfukoni wakati mwingine kiganjani. 

Hizo ndio tambo za kijana January azungumzazo awapo baa ama katika vijiwe vya kahawa na matusi kwa JK yamekuwa ni kawaida sana kwa January.

Haya maneno ya kijana January yanaweza yakawa na ukweli kwani hata ukiangalia uwezo wake kichwani hamna kitu, kwani hakuna hata mtihani mmoja wa hapa Duniani aliowahi kuufanya na kufaulu. 

Mathalani alifanya mtihani wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Galanos Tanga ambayo ilikuwa shule ya boarding, akafeli kabisa kwa kupata alama sifuri ambapo alionyesha kulalamika kufanyiwa hujuma za kisiasa kutokana na siasa zinazomuhusu Mzee wake (Yusuph Makamba) lakini ukweli unabaki pale pale January kichwani hamna kitu.

Kuna siku nikakutana na ndugu wa Makamba (jina namuhifadhi kwasababu namuheshimu na ni mtu mstaarabu lakini kwa nia njema kabisa ) katika bar ya friend’s corner ambapo alikuwa anajisifia uraia wa Marekani wa January na familia yake, na kudiriki kusema kwamba January amelelewa na ‘system’ ya wa Marekani kupitia kwa Rais Mstaafu Jimmy Carter na baada ya kurudi Tanzania na kukosa zile sifa za kuifanya familia yake kuwa raia wa Marekani, aliamua kwamba mke wake akifikisha ujauzito wa miezi nane akimbilie Marekani na watoto wake wawe raia wa Marekani. 

Hivi ndivyo tunaambiwa imetokea kwa wake wawili wa January, ambao wote wana vyeti vya kuzaliwa Marekani na moja kwa moja ni raia wa Marekani.

Ni dhahiri January haupendi Utanzania ndio maana ameamua kuwaambukiza watoto wake tabia ya kilichopo moyoni mwake cha kuukana Utanzania. Uzalendo wa January Makamba kwa Taifa la Tanzania upo wapi hapa?

Najiuliza, kijana huyu ambaye hakuwahi kupata tatizo la ajira na wala kujiajiri tangu amerudi Tanzania, na ambaye amelelewa kwa pesa za walipa kodi za Watanzania miaka yote, leo hii anaonea aibu Uraia na Utaifa wa Tanzania? 

Kumbe ndiyo maana hajui na wala hajali matatizo ya mama wajawazito na watoto wadogo huku wodini Bumbuli kwani mke wake anaenda kujifungulia Marekani. Wajawazito wanalala watatu kitanda kimoja, wengine wanajifungulia chini hili wala January halijui wala hana mpango wa kulifahamu kwani yeye yupo bize na kuusaka urais, Kweli tunamkumbuka Mzee William Shelukindo, Mbunge aliyetoka kabla ya kuingia kijana January Makamba.

Tangu January ateuliwe kwenye wizara hii ya Sayansi na Teknolojia ameshindwa kabisa kusimamia unafuu wa gharama za mawasiliano, na wenye makampuni ya simu wamekuwa wakitumia mwanya wa ulegelege wa kiuongozi wa January kupandisha gharama kila uchwao.

Mathalani, mwaka jana bei ya GB kwa mwezi ilikuwa Tsh. 1,500/- tu. Yaani ulikuwa unalipa Tshs. 30,000/- unapata GB 20 kwa mwezi. Lakini kwa mwaka huu bei ya GB imepanda hadi kufikia Tshs. 5,000/-. Yaani unalipa Tshs. 25,000/- unapata GB 5 tu kwa mwezi.

 Hili ni ongezeko la zaidi ya asilimia 233, wala hakuna maelezo yoyote yale ya msingi yanayotolewa kwa sie wateja kuhusu ongezeko hili. Na wala hakuna mjadala wowote ule bungeni uliowasilishwa na akina January ama kuwashawishi wabunge kupinga dhambi hii ya unyonyaji inayotendwa na makampuni ya simu kwa Watanzania na badala yake January amekuwa kimya kumaanisha anafurahishwa na Watanzania wanavyonyonywa.
January ameshindwa kututetea Watanzania akiwa kama kiongozi mwenye dhamana ya mawasiliano kwa makampuni ya simu kupitia suala hili dogo tu la gharama za mawasiliano na badala yake amekuwa bubu kwa maslahi ya Wananchi na amekuwa domokaya kuutaka urais. Nani akupe Urais endapo matendo yako yanaonyesha dhahiri kushindwa kuwatetea Watanzania?!
Ni shida kwa kweli. Shida hiyo ameiendeleza hadi kumfanya kutopapenda kwao kiasi cha kufikia kutokujenga hata chumba kimoja kwao na wala hajawahi kulala kijijini kwao hata siku moja na siku zote anapoenda Bumbuli hurudi kulala Hotel ya Highland iliyopo Lushoto mjini na anachumba binafsi anachokilipia kwa gharama kubwa na huko kazi yake kubwa ni kufanya ufuska, jambo lililomfanya awe maarufu Lushoto nzima.
Huyo ndiyo January Makamba kiboko ua anasa pale LushotoKutoka rohoni, mimi simpendi January, lakini nakubali ni mwandishi mzuri sana na uzuri kupitiliza hata kumwandikia Rais Kikwete hotuba zilizomgombanisha na Wananchi. 

Mathalani ile hotuba ya Kikwete aliwatukana TUCTA mwaka 2009 na kuzua mgogoro mkubwa kati ya serikali na TUCTA lakini Rais Kikwete ameendelea kumkumbatia mpaka kesho jambo linalomfanya ajitape mitaani kuwa amweka Rais Kikwete mfukoni na ndio maana anamsema vibaya Kikwete waziwazi akiamini hawezi kufanywa lolote.

Hii ni dharau ya hali ya juu anayoionyesha January Makamba kwa Rais wetu wa nchi.

Makala kwa msaada wa Jamii Forum 

Mwisho





















































Labels:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.