Mkurugenzi wa Kampuni ya Serengeti Brewers Ltd, Steve Gannon (kushoto) akimpa mkono wa pongezi Linah (katikati) baada ya kukubali kusaini mkataba wa kuwa Balozi wa Jebel. Kulia ni meneja wa Linah, Tonny Akwesa, akishuhudia makabidhiano hayo |
Akizungumza wakati wa makubaliano ya mkataba huo, mkurugenzi wa kampuni hiyo, Steve Gannon, alisema wameamua kumpatia ubalozi wa kinywaji hicho Linah kufuatia uwezo wake mkubwa katika kuwashawishi wateja wao, na pia hiyo ni njia mojawapo ya kusapoti kipaji chake na itakuwa pia njia ya kushirikiana na wasanii wa Tanzania kwa kila kitu.
“Kampuni yetu imeingia mkataba wa mwaka mmoja na Linah ikiwa njia ya kutambua sanaa ya muziki Tanzania. Serengeti Brewers Ltd kupitia kinywaji chetu cha Jebel, tumefurahishwa na uwezo wa Linah hivyo tunaamini kupitia kwake tutaweza kupata manufaa makubwa ya kutangaza kinywaji chetu cha Jebel,” alisema na kuongeza:
“Tunatarajia kuanza naye kazi rasmi kwa kutengeneza video ya wimbo wake mpya ambayo ataifanyia katika nchi ya Kenya na Afrika Kusini. Video hiyo itakuwa chini yetu, ila mkataba huu utambulike kwamba tunaanza na mwaka mmoja ingawa utakuwa endelevu zaidi.
Linah (kulia) akisaini mkataba huo na Mkurugenzi wa Serengeti, Steve Gannon, ndani ya ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi kuu za kampuni hiyo Temeke, Chang’ombe, jijini Dar es Salaam. |
Linah na Mkurugenzi wa Serengeti Gannon wakionyesha kinywaji cha Jebel.(P.T) |
Steve Gannon akiangalia T-shirt yenye nembo ya kinywaji hicho mara baada ya kusainiwa na Lina |
Akionyesha T-shirt hiyo baada ya kusainiwa na Linah |
Linah akiongea jambo kwa waandishi wa habari baada ya kusaini mkataba |
Mkurugenzi Masoko wa Serengeti, Cescar Mloka (wa pili kulia), akifurahia jambo akiwa ameshikilia kinywaji hicho na Linah. Wengine ni Tonny Akwesa na Steve Gannon |
Linah akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Serengeti. |
Linah akiwa na wafanyakazi wa Serengeti.MSANII kutoka nyumba ya kukuza vipaji Tanzania (THT) Estelinah Sanga ‘Linah’, leo ameingia mkataba na Kampuni ya Serengeti Breweries Ltd, kupitia kinywaji chake cha Jebel. |
”(Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)
Post a Comment