Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Katiba,Sheria na Utawala wamefanya ziara katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya
kuona utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) na kukutana
na walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya Masikini unaotekelezwa na mfuko huo.
Wakizungumza na walengwa hao katika kijiji cha
Madabaga wabunge hao wameonyesha kuridhishwa na mafanikio makubwa yaliyoanza
kupatikana baada ya walengwa kupata fedha chini ya utaratibu wa uhawilishaji
fedha unaotekelezwa na Tasaf.
Wakizungumza katika ziara hiyo baadhi ya walengwa
wameeleza namna walivyonufaika na fedha zilizokwishatolewa ikiwa ni pamoja na
kusomesha watoto,kuboresha makazi yao na kuwa na uhakika wa huduma ya afya na
lishe.
Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika kijijini
Madabaga,mwenyekiti wa kamati hiyo Vedastus Rweyikiza amewahimiza wananchi hao
kutumia fursa hiyo kwa ukamilifu ikiwa ni pamoja na kubuni miradi
itakayowafanya wawe katika mazingira mazuri hata baada ya mpango huo
kumalizika.
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa
Tasaf Ladslaus Mananga,mkurugenzi wa ukaguzi wa mfuko huo,Christopher Sanga
alibainisha kuwa jitihada za kuwafikia walengwa wote wa mpango huo zinaendelea
ambapo ifikapo katikati ya mwaka huu zaidi ya kaya milioni moja zitanufaika na
utaratibu wa uhawilishaji fedha nchini kote.
Mkuu wa
mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro(wa tatu kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya wajumbe
wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala kabala ya wajumbe hao
kutembelea walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko
wa Maendeleo ya jamii(TASAF) wilayani Mbarani mkoani humo.Kulia ni mkurugenzi
wa ukaguzi wa Tasaf Christopher Sanga.
MKuu wa wilaya ya Mbarali Gulamhussein Kifu(wa
nne kulia) akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya
Katiba,Sheria na Utawala kabla ya wajumbe hao kutembelea walengwa wa Mpango wa
kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF)
wilayani Mbarani mkoani humo.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya
Katiba,Sheria na UtawalaVedastus Rweyikiza akizungumza jambo baada ya kamati
hiyo kukutana na wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na
Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika kijiji cha Madabaga wilayani Mbarani
mkoani Mbeya.
Wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini
unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika kijiji cha Madabaga
wilayani Mbarani mkoani Mbeya wakimsikiliza mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya
Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala Vedastus Rweyikiza kabla ya kuanza kugawiwa
fedha kwenye mkutano uliofanyika kijijini hapo jana.
Mmoja wa wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya
Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika kijiji cha Madabaga
wilayani Mbarani Hellena Bamba akikabidhiwa fedha kutoka kwa kamati ya mradi ya
wilaya(CMC).
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya
Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala wakiangalia namna wanufaika wa Mpango wa
kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya jamii(TASAF) katika
kijiji cha Madabaga wilayani Mbarani wanavyokabidhiwa fedha.Katikati ni
Mwenyekiti wa kamati hiyo Vedastus Rweyikiza kushoto kwake akifuatiwa na Felix
Mkosamali na Willium Ngeleja.
Post a Comment