Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kuendelea kwa ajali za barabarani. Picha na Venance Nestory |
Akizungumza jijini leo Mbatia amesema ajali hiyo
ilipangwa na watendaji wa serikali kwa sababu ajali hiyo ilisababishwa
na shimo kubwa ambalo limekaa kwa muda mrefu eneo hilo pasipo juhudi
zozote za Serikali kulikarabati.
Mbatia amesema hawezi kukaa kimya ni lazima
awasilishe suala hili bungeni ili wahusika wachukuliwe hatua kwa kuacha
shimo kubwa barabarani kwa muda mrefu bila kuliziba.
Amesema shimo hilo ambalo ndio hasa lilikuwa
chanzo cha ajali hiyo ni la muda mrefu lakini viongozi wa serikali
wanaliangalia tu bila kuchukua hatua ya kuliziba.
‘’Jamani watanzania waliopoteza maisha kwenye
ajali hiyo ni wengi na ni aibu kwa taifa, ukizingatia chanzo cha ajali
hiyo ni shimo la muda mrefu ambalo linaangaliwa na viongozi wetu kila
siku bila kuliziba’’alisema Mbatia
Amesema ajali hudokeza kwa ujumla matokeo mabaya
ambayo labda yangeweza kuepukwa au kukingwa ikiwa matukio
yaliyosababisha ajali hiyo yangetambuliwa na kurekebishwa kabla ya
tukio.
Amesema madereva wanaoendesha magari ya abiria
wanatakiwa kupelekwa shule angalau kwa miezi sita ikiwa ni pamoja na
kupimwa afya mara kwa mara.
Aidha ameitaka serikali kutoa tamko kuhusu ajali
hiyo na sio kukaa kimya mpaka waanze kupigiwa makelele na wananchi
kupitia vyombo vya habari.
Watu zaidi ya 40 waliokuwa kwenye basi la
kampuni ya Majinjah Express lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es
Salaam, walifariki papo hapo katika ajali hiyo iliyotokea jana wengine
23 wakijeruhiwa.
Chanzo cha habari na gazeti la kila la mwananchi
Chanzo cha habari na gazeti la kila la mwananchi
Post a Comment